Rwanda yalegea, malori ya TZ yaruhusiwa

Rwanda yalegea, malori ya TZ yaruhusiwa

Nina wasiwasi huyu anaweza kuwa murutongore au Balali.

Mkirua kaka mimi ni ndugu yako tena matanzania halisi, tunatofautina mitazamo tu.

Wakati wengine wanadhani vita ndiyo suluhisho, sisi wengine hatupendi kabisa kusikia neno vita.

Vita si lelemama wala mchezo, vita hupiganwa pale tu kunapokuwa na ulazima na kila njia kuiepusha imeshindikana

Njia sahihi ya kutatua matatizo yawe ya ndani au nje ya nchi ni majadiliano.
 
Last edited by a moderator:
na kasema ilikuwa imewekwa kwa sababu gani?

nilishasema karwanda hakana kitu chochote cha kututishia sisi wala hakuna sababu za kupigana eti na Rwanda tutaonekana sisi ndo wajinga,ni sawa na kumkuta et baunsa wa miaka 35 anapigana na katoto ka miaka miwili,sisi hatufaidiki na chochote kutoka Rwanda ila wao ndo wana utegemezi mkubwa kutoka TZ ni sawa na leo hii Rwanda izuie unga wa bakharessa usiingie Rwanda,ni wazi kutatokea gharika la njaa pale.
 
Hapa inaonekana wazi walikwishaongea lakini afisa aliongeza ushuru prematurely. Ipo siku watafanya hivyo, watanzania tujiandae tusibweteke
ukweli ndio huu.hapa wanatuandaa kisaikolojia.huenda hiyo 152USD mwisho wake ni mwezi huu.
 
Kasema ofisa mmoja katika Wizara ya Fedha ya Rwanda ndiye aliyezomoka na kutangaza mabadiliko hayo kwa mdomo. Waziri wa Fedha Rwanda alipoulizwa na mwenzake wa Tanzania, alishituka, na akaahidi kulipatia ufumbuzi. Tzeba kasema ndani ya dakika 30 jibu likawa limepatikana kuwa agizo la ofisa wa Rwanda halikuwa halali.

Muhimu: Nadhani Rwanda wanajua bila Tanzania hawana maisha. Huo ndiyo ukweli. Rais Kagame asituvuruge uhusiano wa nchi hizi mbili.

Kwa taarifa sahihi, Rwanda imetoa msamaha na si afisa aliyehusika kujitangazia. Wanasema wamekuwa wakiomba Tanzania kupunguza ushuru wa barabara kwa miaka minne sasa bila mafanikio ingawa ahadi zimekuwa zikitolewa na viongozi wetu kulishughulikia kila mwaka wa fedha unapoanza.
Inasemekana Rwanda imebadilisha msimamo wake kama kutoa nafasi kwa tanzania kupunguza ili watoze kwa gharama sawa nchi mbili.

Anjo
 
Mkirua kaka mimi ni ndugu yako tena matanzania halisi, tunatofautina mitazamo tu.

Wakati wengine wanadhani vita ndiyo suluhisho, sisi wengine hatupendi kabisa kusikia neno vita.

Vita si lelemama wala mchezo, vita hupiganwa pale tu kunapokuwa na ulazima na kila njia kuiepusha imeshindikana

Njia sahihi ya kutatua matatizo yawe ya ndani au nje ya nchi ni majadiliano.

unajuwa Balali hakuna anayependa vita hata siku moja na wengine hatujasahau mdhara ya vita vya kagera ambavyo vimekuwa kaburi la uchumi wetu hadi kesho ila inapobidi lazima state ioneshe autonomy yake kwa vitendo.

Fikiria jambo dogo tu la kuambiwa kaa chini upatane na adui yako kama alivyoambiwa PK....pengine JK kwa kujuwa ama kutokujua alikuwa akitekeleza mojawapo ya mafundisho ya Yesu Mlimani "Heri wapatanishi kwa maana wataitwa waana wa Mungu"....Ona Matusi aliyotoa PK na watu wake, ona kashfa na mikakati ya kuitenga TZ inayoendelea....Kwa hili hata kama simpendi JK, wala sijawahi kumpigia kura wala kushangilia ushindi wake, lakini nje ya Tanzania ni Rais Wetu, hivyo, nasimama naye na namuahidi tuko nyuma yake....Tanzania ni bora kuliko haya mengine...Ni hilo tu linalotusukuma wengine na kwakweli hata kama itatulazimu kupigana kulinda utu na heshima ya taifa letu tunaungana na pinda...Liwalo na liwe,.... tutawapiga tu...
 
hii habari imeletwa kiushabiki mnooooo, nina mashaka na malengo halisi ya aliye ileta
 
Taarifa nilizonazo nikuwa tozo hilo limetolewa kwa siku tano tu halafu mziki utaendelea huyu tizeba kaongea tu ukweli mgogoro huo wa road toll bado ni mbichi. Source mimi mwenyewe niko eneo la tukio
 
Kama wameruhusu malori ni vizuri. Nilijua lazima wangefanya hivyo. Rwanda hana ubavu wa kuweka bifu kiuchumi na Tz. Wangekufa na njaa ndani ya wiki tu. Basi tu jeuri za kitoto.
 
Huyo ndugu aliyeko Rusumo ametoa taarifa muhimu sana. Sasa mbona post yake mmeifuta? Au kwavile inasema ukweli unaoiumbua sirikali ya Tz..! Kasema awali road toll kwa magari ya kirwanda yanayoingua Tz yalitozwa dola 500 (Rusumo-Dar-Rusumo). Kagame alipopandisha wamekubali kushusha mpaka dola 150. Hivyo sasa ni dola 150 kwa 152. Linganisha umbali huu ndo utajua Tz wachumi hawapo bali wanasiasa. (Rusumo-Dar-Rusimo) na (Ruaumo-Kigali-Rusumo)
 
Waziri wa miundo mbinu wa Rwanda akihojiwa na VOA amesema utaratibu huo umesitishwa hadi tarehe 9 mwezi huu. Sababu ya kupandisha ni kulinganisha tozo sawa na lile la Tanzania amayo kwa muda mrefu imekuwa ni dola 500. Huyo ndiyo Prof. Silas Rwakabamba.
 
Tumezungumza na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Tzeba, amethibitisha kuwa Serikali ya Rwanda imeruhusu malori ya Tanzania yaendelee na safari kwa kulipa dola 152 badala ya 500 zilizoanza kutozwa jana. Kasema Waziri wa Fedha wa Rwanda, aitwaye Gatete, na wa Uchukuzi, Rwakabamba, wameridhia tozo ya dola 152 iendelee.

Source: mimi mwenyewe-dodoma

Huyu Profesa Silas Rwakabamba nilidhani kuwa ni mtanzania kwa vile alikuwa Dean wa FoE hapo UDSM kwa kipindi fulani mwanzoni mwa miaka ya 80 hadi mwishoni mwaka 1984 alipoondoka kwenda Nigeria. Hawa ndio waliokuwa maprofessa wa kwanza kwanza waafrika hapo Engineering. Sikujua kuwa naye alikuwa ni mnyarwanda ingawa niliwajua wengine pale FoE akina Lujara na Ndamage ambao wote leo hii ni maafisa wakubwa kwenye serikali ya Kagame. Wafuasi wa Kagame wanaweza kuwa ni wengi sana Tanzania kuliko tunavyoweza kuwa tunajua.
 
unajuwa Balali hakuna anayependa vita hata siku moja na wengine hatujasahau mdhara ya vita vya kagera ambavyo vimekuwa kaburi la uchumi wetu hadi kesho ila inapobidi lazima state ioneshe autonomy yake kwa vitendo.

Fikiria jambo dogo tu la kuambiwa kaa chini upatane na adui yako kama alivyoambiwa PK....pengine JK kwa kujuwa ama kutokujua alikuwa akitekeleza mojawapo ya mafundisho ya Yesu Mlimani "Heri wapatanishi kwa maana wataitwa waana wa Mungu"....Ona Matusi aliyotoa PK na watu wake, ona kashfa na mikakati ya kuitenga TZ inayoendelea....Kwa hili hata kama simpendi JK, wala sijawahi kumpigia kura wala kushangilia ushindi wake, lakini nje ya Tanzania ni Rais Wetu, hivyo, nasimama naye na namuahidi tuko nyuma yake....Tanzania ni bora kuliko haya mengine...Ni hilo tu linalotusukuma wengine na kwakweli hata kama itatulazimu kupigana kulinda utu na heshima ya taifa letu tunaungana na pinda...Liwalo na liwe,.... tutawapiga tu...

[MENTION]Mkrua[/MENTION]

Akikuomba kanzu, mpe na joho lake

akikupiga la kushoto mgeuzie na la kulia

Je nyinyi mnahokumu mu-wasafi kiasigani? nani kati yenu asietenda dhambi?, angalieni msijekulaum kwa kuhukumu nanyi mkaja hukumiwa.

Yesu hakuhubiri vita wala visasi bali alihubiri upendo na toba yakweli

Msijikweze kwa kujiweka viti vya mbele mkaja aibika. viongozi wa eneo moja ilikuwa lazima kusubiri makutano wa kimataifa ili wapeane ushauli?

Ushauli wa heri na amani hufanyika kwa busara na hekima kwa watu husika, mazingira na muda muafaka Hili halikuzingatiwa kwanini?
 
Huyu Profesa Silas Rwakabamba nilidhani kuwa ni mtanzania kwa vile alikuwa Dean wa FoE hapo UDSM kwa kipindi fulani mwanzoni mwa miaka ya 80 hadi mwishoni mwaka 1984 alipoondoka kwenda Nigeria. Hawa ndio waliokuwa maprofessa wa kwanza kwanza waafrika hapo Engineering. Sikujua kuwa naye alikuwa ni mnyarwanda ingawa niliwajua wengine pale FoE akina Lujara na Ndamage ambao wote leo hii ni maafisa wakubwa kwenye serikali ya Kagame. Wafuasi wa Kagame wanaweza kuwa ni wengi sana Tanzania kuliko tunavyoweza kuwa tunajua.

watu lazima wafikirie kwenye three dimension, na tukifikia hapo tutagundua wengi wa watanzania wanauhusino wa moja

kwa moja au vinginevo na hao tunaofarakana nao.
 
Non tariff barriers hizo jamani, EAC wamekubaliana zipunguzwe, TZ tumeng'ang'ania Tu, check point kibao,polisi wapige mabao, mizani zaidi ya kumi ucheleweshaji Tu, mf pale kibaha. Ushuru ufanane cc tulikazania iwe juu, saa zingine mnyonge mpeni haki yake
 
Hehee kumbe tishio letu limeigusa Rwanda,

Tukiwa kama taifa lenye kura ya Veto tunayo kila sababu ya kuwa na karipio kwa yeyote EAC

Tulitoa saa 24 za angamizo kwa Kagame

nakuheshimu sana boss sikuwedha kudhan unaweza ongea kiushabiki kiasi hiki!!!
 
Badilisha kichwa cha habari kiwe, 'TANZANIA YALEGEA, YAPUNGUZA USHURU WA MAGARI YA RWANDA'. Ushabiki wa kipuuzi hautusaidii. Kumbe tatizo lilikuwa ni la Tanzania kuweka ushuru mkubwa wa dola 500 kwa malori ya Rwanda, nao wakajibu mapigo. Tanzania ikasalimu amri.

Wanyarwanda kwenye hilo nitawapongeza, wana akili. Siyo kama sisi hapa serikali inajiongezea ushuru kwa kila kitu sisi tupo kimya.
Wewe nawe mbwiga kweli...sijui hata kama unajuwa kinachojadiliwa hapa. Rudia tena kusoma tangu mwanzo na kama huelewi anzisha thread yako tutachangia accordingly.
 
Back
Top Bottom