Rwanda yalegea, malori ya TZ yaruhusiwa

Rwanda yalegea, malori ya TZ yaruhusiwa

Tumezungumza na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Tzeba, amethibitisha kuwa Serikali ya Rwanda imeruhusu malori ya Tanzania yaendelee na safari kwa kulipa dola 152 badala ya 500 zilizoanza kutozwa jana. Kasema Waziri wa Fedha wa Rwanda, aitwaye Gatete, na wa Uchukuzi, Rwakabamba, wameridhia tozo ya dola 152 iendelee.

Source: mimi mwenyewe-dodoma

kagame aache kiburi, atawaumiza watu wake!
 
Tanzania yalegea kwanza.

Bado nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda, kwa habari ambazo ni rasmi Serekali ya Rwanda imefuta ongezeko la ushuru wa barabara ( Road Toll) la USD 500 kwa kila gari lenye usajili wa Tanzania na kuanzia leo kila gari litavuka kwa ushuru wa zamani wa USD 152. Uamuzi huu umefikiwa baada ya Mamlaka Ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kupunguza ushuru wa barabara ( Road Toll) kwa magari yenye plate numbers za Rwanda kutoka USD 500 mpaka USD 150. Hatua hii inaoenakana ni ushindi mkubwa kwa Rwanda ikizingatiwa kuwa umbali kutoka Dar mpaka Rusumo sio sawa na umbali kutoka Rusumo mpaka Kigali....kwahiyo ushuru wa barabara hauwezi kuwa sawa kwa simple basics za economics.....

Jackton Manyerere tunaomba uulizie na hili jambo jamaa kaliweka hapa ili story nzima iwe balanced
 
Hee kumbe hawa mawaziri wa pande zote wanapiga stori fresh tu? Bado jk na pk tu
 
Kichwa cha habari kimekaa kishabiki!

Pia unajua makubaliano yamefikiwaje? fuatilia vyema utajua TZ imepiga magoti na kupoteza baadhi ya haki zake kufikia maamuzi hayo.

Hivi ni wewe mwenyewe au kuna mtu anatumia ID yako?
 
Sarakasi zimeanza upya, lkn lzm tuwarudishe kwao, nasi tuaki kwetu
 
Kichwa cha habari kimekaa kishabiki!

Pia unajua makubaliano yamefikiwaje? fuatilia vyema utajua TZ imepiga magoti na kupoteza baadhi ya haki zake kufikia maamuzi hayo.

He!! kumbe hapa tunajadili maslai ya Taifa.........!!

hongera sana, hakuna kitu kizuri kama kutoa mawazo huru.!
 
.......hata hivyo.......wazungu husema ni "warning shot"........tusibweteke.........
 
Jackton Manyerere tunaomba uulizie na hili jambo jamaa kaliweka hapa ili story nzima iwe balanced

Waziri Tzeba kazungumza vizuri tu kasema viwango vya Tanzania viko juu. Kwa kila kilometa 100, tanzania inatoza dola 6 kwa gari la axels mbili hadi tatu, na dola 16 kwa gari lenye axels zaidi ya nne. Lakini kwa Rwanda kiwango
ni kimoja tu, yaani dola 152 kwa popote unakoenda ndani ya Rwanda. Kwa maaana hii, na kwa urefu wa barabara za Tanzania, utaona Wanyarwanda na wengine wanalipa zaidi. Kasema Tanzania ndiyo yenye viwango tofauti, na kwamba sasa kunafanyika mchakato kwa EAC na SADC kuwa na kiwango kimoja.

Nawasilisha
 
Badilisha kichwa cha habari kiwe, 'TANZANIA YALEGEA, YAPUNGUZA USHURU WA MAGARI YA RWANDA'. Ushabiki wa kipuuzi hautusaidii. Kumbe tatizo lilikuwa ni la Tanzania kuweka ushuru mkubwa wa dola 500 kwa malori ya Rwanda, nao wakajibu mapigo. Tanzania ikasalimu amri.

Wanyarwanda kwenye hilo nitawapongeza, wana akili. Siyo kama sisi hapa serikali inajiongezea ushuru kwa kila kitu sisi tupo kimya.
 
Adui muombee mjaa, FDRL wakiwatwanga tena hakuna kupokea wakimbizi maana wameaharibu sana mazingira.
 
Ni mda wa kujenga umoja na mshikamano na si kutengenezeana visa na kulipizana visasi. Mda huu ni mda wa kutambua umoja wa Afrika na mwafrika. Haya yote ni kutokana na uelewa finyu wa baadhi ya viongozi.Nashukuru kwa kuweka sawa bei hiyo.
 
Muziki wa wahamiaji haramu upo pale pale! Rwanda hana ujanja wa kuitenga Tanzania. Rwanda kwa Tanzania ni sawa na kichwa na bega. Rwanda ni bega-kamwe haliwezi kukivuka kichwa!

Sheikh ponda alipopiga risasi ya begani kichwa ilivurugika na hakukumbuka yaliyoendelea..... hahahaha umenikumbusha mbani sanaaa kichwa na begaaa.... kama hujui uliza kwa waliowahi patwa na matatizo ya begaaa.
 
Tumezungumza na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Tzeba, amethibitisha kuwa Serikali ya Rwanda imeruhusu malori ya Tanzania yaendelee na safari kwa kulipa dola 152 badala ya 500 zilizoanza kutozwa jana. Kasema Waziri wa Fedha wa Rwanda, aitwaye Gatete, na wa Uchukuzi, Rwakabamba, wameridhia tozo ya dola 152 iendelee.

Source: mimi mwenyewe-dodoma
"accord treatment to nationals of other Partner States, not less favourable than the treatment accorded to third parties;"

Hii ni moja ya Principles zilizoko kwenye Itifaki ya Soko la Pamoja. Ilinishngaza kusikia Kigali wanaweka viwango vya tozo za magari kwa kuangalia yanatokea nchi gani!
 
Tumezungumza na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Tzeba, amethibitisha kuwa Serikali ya Rwanda imeruhusu malori ya Tanzania yaendelee na safari kwa kulipa dola 152 badala ya 500 zilizoanza kutozwa jana. Kasema Waziri wa Fedha wa Rwanda, aitwaye Gatete, na wa Uchukuzi, Rwakabamba, wameridhia tozo ya dola 152 iendelee.

Source: mimi mwenyewe-dodoma
Wahenga walisema"Ukijamba kwa hasira ni kujinyea" Wao hawana bandari kama sisi. Wangeathirika wanyarwanda na sio wa tanzania.
 
Mi nadhani wengine wasipeleke tena mizigo Na hao wakifikisha hiyo mizigo wasirudi tena hadi suluhu ya kudumu ipatikane

kwahiyo watu waache biashara zao zinazowapatia kipato? serikali inaweza kuwafidia?

Sio wazo zuri hata kidogo tuendeleze biashara na jirani zetu hawa
 
Tanzania yalegea kwanza.

Bado nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda, kwa habari ambazo ni rasmi Serekali ya Rwanda imefuta ongezeko la ushuru wa barabara ( Road Toll) la USD 500 kwa kila gari lenye usajili wa Tanzania na kuanzia leo kila gari litavuka kwa ushuru wa zamani wa USD 152. Uamuzi huu umefikiwa baada ya Mamlaka Ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kupunguza ushuru wa barabara ( Road Toll) kwa magari yenye plate numbers za Rwanda kutoka USD 500 mpaka USD 150. Hatua hii inaoenakana ni ushindi mkubwa kwa Rwanda ikizingatiwa kuwa umbali kutoka Dar mpaka Rusumo sio sawa na umbali kutoka Rusumo mpaka Kigali....kwahiyo ushuru wa barabara hauwezi kuwa sawa kwa simple basics za economics.....
Kwa kutumia hizohizo basics za economics, hilo laweza kuwa win-win au win-lose in favor of Tanzania. Kwa kuwa idadi ya magari ya Rwanda yanayoingia Tanzania ni negligible, maana yake hata athari za mapato pia negligible. Vilevile hata uharibifu wa Barabara pia utakuwa negligible. Lakini pia iwapo TRA imechukua hatua hiyo kweli, imesaidia kuongeza/kudumsha ushindani kwa bidhaa za Tanzania kwani hiyo Dola 500 ambayo magari yangelipia ingesababisha kuongezeka kwa bei kwa bidhaa zinazovuka kutoka Tanzania na hiyo ingepunguza demand ya bidhaa za Tanzania.

Hata hivyo, hii Jumuiya haina budi kujifunza kutoka EU; hamna maana yyte ya kuwa na tozo tofauti kwa vitu vinavyochochea biashara kama road toll iwapo mko ndani ya Jumuiya tena inayofikiria kuingia kwenye hatua kama za sarafu ya pamoja. Kuna haja kubwa ya kuijenga haraka Reli ya kati (tena ilitakiwa ianze mwanzo kabla ya Bandari ya Bagamoyo) ili barabara tuwaachie wenye mabasi tu.
 
Ni vyema kama wametoa uamuzi huo kwani ni hatari huko tunakoelekea kati yetu na hawa warandwa. Ila zaidi wangeumia warandwa sidhani kama tunachakupoteza sisi tukivunja uhusiana na Rwanda.
 
Back
Top Bottom