kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,426
- 7,213
Rwanda ni nchi ndogo ya milima na isiyo na bandari pia ina idadi kubwa ya watu kulinganisha na eneo lake. Ni tofauti na Tanzania ambayo ni nchi kubwa ardhi ya kutosha mali asili kibao na ukanda wa bahari mkubwa wenye bandari nyingi.
Rais Kagame ni mtu mwerevu sana kwenye kujenga uchumi wa nchi yake na kuwapatia maslahi tabaka la utawala huko Rwanda. Yuko tayari kutumia udhaifu wa nchi jirani kwa manufaa ya Rwanda.
Tumeona Rwanda wakivuna madini na mali asili za Congo na wala hawajali kusaidia vikundi vya kijeshi kwa kisingizio chochote mradi kuhakikisha wanadhibiti maeneo ya madini mashariki ya congo.
Nchi kama tanzania hatutakiwi kuigiza mkakati wa maendeleo wa rwanda. Hivi karibuni Rwanda wamewapa DP World kujenga bandari kavu kubwa Rwanda kwa hivyo bila shaka ni mkakati wa mjanja Kagame kuitumia DPworld kuhakikisha bandari ya Dar es Salaam inahamia Rwanda kwa bidhaa za Congo, Burundi Uganda na Sudan ya Kusini.
Mpango ni transit cargo kupelekwa Rwanda ambapo zitalipiwa kodi huko na kuongeza shughuli za kiuchumi kabla ya kusafirishwa nchini kwao Congo ya Mashariki, Uganda na Sudan ya Kusini.
Kabla ya sakata la DPW kuibuka tumeona ziara za mjanja kagame za kikazi chapchap bila shaka akimtia moyo mama asighairi mpango wa kuipa DPW bandari zetu licha jumba kutaka kumuangukia.
Tusisahau pamoja na kauli za mara kwa mara dhidi ya ubeberu kagame ni mshiriki wa karibu wa njama za kiuchumi za wamarekani dhidi ya Congo. Rwanda iko tayari kuidhuru nchi yoyote kiuchumi ili kupata makombo ya ngawira za mabeberu.
Watanzania tuchunge mali zetu asili tulizojaliwa kwa wivu vinginevyo zitatumika sio kwa manufaa ya wale mabeberu wa asili ila wajanja na mabeberu wapya wa uchumi kama rwanda na Dubai huku tukibakia masikini na kuonekana wajinga.