Ruto: Mtu wa kwanza duniani aliishi Kenya... imekaaje?

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Wakuu,

Ninafuatilia kuapishwa kwa Rais wa nne wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Cha ajabu nimemsikia Makamu wa Rais William Ruto akisema ya kuwa mtu wa kwanza kuishi duniani aliishi Kenya.
Nimejiuliza, mwalimu wangu wa historia alinifundisha ya kuwa Olduvai Gorge (Bonde la Olduvai) liko Tanzania.
Ama historia imeandikwa upya?

Chonde chonde, Ziwa Nyasa tumeshanyang'anywa na Malawi, Mlima Kilimanjaro karibu sana tutasikia pia uko Kenya.
Nimeshawahi kuona tangazo wakinadi ya kuwa njoo Kenya upande Mlima kilimanjaro, na lingine linasema Mlima Kilimanjaro uko

Tanzania, lakini ukitaka kuuona vizuri, njoo Kenya!

Ama ndiyo fastjet kashawauzia wakenya kila kitu?

http://www.pbs.org/wgbh/aso/databank/entries/do59le.html
 
kwani mkuu historia inayofundishwa tanzania ndo inayofundishwa kenya? sidhani kama hata ulaya na sehemu nyingine duniani wanalijua hili la kuwa binadamu wa kwanza aliishi tanzania.

Umesema kweli mkuu. Bahati mbaya ninaishi ughaibuni kuna siku niligombana sana na mwalimu wa watoto wangu alipowafundisha hivi:

'Africa is a continent without history'.

Nilihamaki ikabidi aombe msamaha...
 
nilishangaa juzi kabla hajaapishwa huyu bwana alitembelea tz na kukutana na mkulu lakini cha ajabu walikutana Serengeti/Olduvai Gorge badala ya makao makuu ya nchi na alikuwa anafurahi sana tena sana.
Huwezi jua ndio labda makabidhiano yalikuwa yanafanyika na leo nasikia tumepewa heshima kubwa zaidi ya waalikwa wote waliohudhuria sherehe za kuapishwa.
Likini pia kuna mkakati wa kuandika upya historia, watu wanaweza kuamua kubadilisha hata hilo ili ionekane kuwa binadamu wa kwanza aliishi kenye na wa pili akaishi mikoa ya pwani mwa tz
. ngoja tusubiri kusikia kama wakuu watalitolea maelezo.
 
Wakuu,

Ninafuatilia kuapishwa kwa Rais wa nne wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Cha ajabu nimemsikia Makamu wa Rais William Ruto akisema ya kuwa mtu wa kwanza kuishi duniani aliishi Kenya.
Nimejiuliza, mwalimu wangu wa historia alinifundisha ya kuwa Olduvai Gorge (Bonde la Olduvai) liko Tanzania.
Ama historia imeandikwa upya?
Chonde chonde, Ziwa Nyasa tumeshanyang'anywa na Malawi, Mlima Kilimanjaro karibu sana tutasikia pia uko Kenya.
Nimeshawahi kuona tangazo wakinadi ya kuwa njoo Kenya upande Mlima kilimanjaro, na lingine linasema Mlima Kilimanjaro uko Tanzania, lakini ukitaka kuuona vizuri, njoo Kenya!
Ama ndiyo fastjet kashawauzia wakenya kila kitu?

A Science Odyssey: People and Discoveries: Leakey family discovers human ancestors

Hujui kama kila nchi ina historia yake! na sisi tuanzishe yetu dunia ilianza kuumbwa kutokea TZ, I mean ardhi ya kwanza ni TZ!
 
Nafikiri hakuna cha kushangaza hapa kwani Hotel(you can say Hospitality industry)zote za nchi hii 80% ya staffs ni Kenyans,so what do you expect Mkuu!?
 
Hata Marehemu John Garang alisema bustani ya Eden ilikuwa Sudan Kusini. Juzi Babu wa Loliondo kaibuka na madai ya kwamba Eden yenyewe ni Ngorongoro.
Hata hivyo sayansi inaweza ikasema kilicho karibu na ukweli zaidi. Baada ya kile kilichogundulika Olduvai Gorge na kuonesha ni mabaki ya mtu wa kale zaidi, sio kwamba ugunduzi uliishia pale. Alichosema Ruto ni ugunduzi mwingine uliofuatia. Haya yote yanaweza kuthibitishwa kwa credible archolological finds.
Labda ukapimwe ule unyayo wa Babu wa Loliondo aliosema ni wa mtu wa 182 baada ya Adam, tuone una umri gani.
 
Anafaa kuwa marketing manager,amewanadi nyumbu na mzunguko wao bila kuitaja Tz kana kwamba wanazunguka ndani ya Kenya tu.
 
ndio watu tunaoshirikiana nao ''kimaendeleo'' kwa karibu katika EAC. Mungu turehemu utusaidie.
 
Hapo ndipo history inapochanganya.
Siajabu tukisoma vitabu vya Nigeria,South, Malawi na nchi nyingine tukaelezwa kuwa mtu wa kwanza anatoka kwenye nchi husika kulingana na kitabu cha nchi husika.
 
Back
Top Bottom