SoC01 Brainwashing kwenye Dini. Kushamiri kwa Madhehebu, Na muelekeo unaofaa kufatwa na Jamii kwa ustawi wa Afya ya akili.

Stories of Change - 2021 Competition

ngatungas

New Member
Sep 16, 2021
2
12
Utangulizi.
Nadhani sisi sote ni wafuasi wa imani fulani maishani.Either iwe ya kidini ama ya kifikra zaidi(scientific). Na hizi Beliefs system ndizo sana sana zinatuongoza maishani mwetu juu ya kile kipi tunafanya kila siku.

Mada.
Kwa Africa Uislamu-uliletwa na waarabu kipindi cha ukoloni na biashara ya watumwa.
Ukristo- uliletwa na Wamisionari kipindi cha ukoloni pia.
Wakati wanakuja kutuletea imani hizo, sisi tulikua tupo na mila na desturi zetu ambazo zilituongoza katika mambo kadhaa kama ya kijamii, kiafya na tabia nchi.
Mkanganyiko.
sote tunajua kwamba sayansi inasema binadamu wa kwanza alitokana na Nyani/sokwe. Ila vitabu vya imani vinasema binadamu aliumbwa akiwa mkamilifu. Je yupi yu sahihi?!

•Tunaambiwa binadamu wa kwanza aliishi Tanzania-Olduvai Gorge. Na vitabu vya kidini vinasema binadamu aliishi katika bustani moja pamoja na wanyama wote. Je itakua sio sahihi kusema Bonde la Hifadhi la Ngorongoro ndiyo Bustani ya Eden?
Maana ni sehemu pekee ulimwenguni ya Crater- penye wanyama wa kila aina na ambapo binadamu huishi na wanyama pori wakali bila kudhuriana.
•Na pia itakua sio sahihi kusema Mlima Kilimanjaro ni Mlima Sayuni?!?
•Maana ndio Mlima pekee uliosimama thabiti bila kufungamana{safu} na milima mengine. [ world highest free standing Mountain].
• sababu ya kuongea haya yote ni sayansi imeonyesha binadamu wa kale zaidi aliishi hapa nchini. Kwanini tusiwe na Maswali juu ya uhalisia wa vitu kama hivi?!
MADHEHEBU.
Mimi ni mkristo toka utoto wangu. Na Nadhani sote tu mashahidi juu ya wimbi kubwa la ongezeko la Madhehebu na kila kiongozi kujiita Mtume,Nabii etc. je ni sahihi?!
Kama si sahihi wahanga wa yote haya ni kina nani?
Naamini kabisa imani ni kitu nyeti sana.na kinachoweza leta watu pamoja. Lakini too much is Harmful.
Kuna baadhi ya viongozi wa kidini hutumia shida za watu kuwahadaa na kuwateka kisaikilojia.
Tunakumbuka habari za ‘kibwetere’ wa Uganda.alivyowachoma waumini kwa kuwaaminisha siku za mwisho zimefika.
Japo hatuwezi kataa kuwa wapo viongozi wa dini wenye nia dhabiti kabisa kuwasaidia waumini wao.
Ila wapo watumiavyo vibaya majukwaa ya kiimani kwa kujijenga kisiasa, kiuchumi na hata kujisafisha kijamii.
BRAINWASHING.
• kila siku tunasikia habari za watu kujitoa mhanga na kuwaua watu wasio na hatia. Kwa kile kwamba watafika Mbinguni moja kwa moja.
Je ni sahihi kuua binadamu mwenzako aliyeumbwa ili ufike mbinguni?!
•Pia tunasikia habari za watu kuhama hama nyumba zao za ibada kwa kile cha kutafuta “Muujiza”.
JE tumekua na desturi ya kumtafuta Mwenyezi Mungu ama kutafuta Muujiza?!
•Tunaabudu watu badala ya kuwa na Imani na kumjua huyu aliyetuumba kwa kuwa ana uwezo zaidi ya vyote hivyo.
Tumekua brainwashed kwa kufata mikumbo pasipo kuwa na misingi thabiti ya kiimani.
Ukweli uko wapi?
NINI KIFANYIKE.
~• somo la “Theology” lingepaswa kuanza fundishwa toka madarasa ya chini. Ili vijana waweze kujua misingi ya imani zao na za majirani.
Religion with Science ni watoto pacha wasioachana daima.
Tunakumbuka hapo kale Mnajimu “Galileo Galilei’ aliwahi fungwa na kanisa huko Italy kwa kupotosha jamii kuwa “Dunia ndiyo inayozunguka jua”.
Ilihali kanisa liliamini Jua ndilo linalozunguka dunia.[Nabii Eliya alisimamisha jua].
Lakini miaka mingi baadae walikuja kuamini maneno ya Mnajimu huyo kuwa ni ukweli.

~•Vitabu vingi va kiimani vinasema Dunia na Ulimwengu kwa ujumla viumbe hai wapo Duniani pekee.
Ila tunajua ya kwamba dunia na sayari zote pamoja na Jua, tupo kwenye sehemu ndogo ya Galaxy yetu.
Na zipo mamia ya Galaxy ulimwenguni zilizojaa sayari na Nyota zake Mamilioni.
Je tutakua selfish kusema “We are Alone”?!?
Maana ulimwengu ni Endless. Nini kipo huko tusipoweza fika?
Ukifatilia Documentaries nyingi utaona kuna kitabu cha “Book of Enoch” ambacho hakikuwekwa kwenye biblia.
Kitabu hiki kinazungumzia mambo yaliyotokea, na yajayo.
Kinaongelea wageni[watchers] walioshuka toka juu hapo zamani sana.na kinasema hao wageni “Annunakis” ndio waliwapa mbinu wamisri kujenga zile pyramids.
mimi na wewe hatuna budi kuujua ukweli. Tusiwe wasindikizaji.
Wanasema Vatican kuna the world biggest Library underground yenye historia za toka uumbaji wa dunia.

~•tusiwe watumwa wa imani zetu na kuanza kubaguana kisa imani.
Tujitambue, tujue chimbuko letu ni lipi.
Mostly mimi na wewe tupo na imani zetu hizi ambazo tuliaminishwa/rithishwa toka kwa wazazi wetu.
Iweje tuanze kubaguana?
Tuwe wadadisi kujua mambo kiundani. Tusiishi kwa Mazoea.
Ahsanteni.
 
Point of correction:

Aliyesimamisha jua na mwezi siyo Nabii Eliya ni Yoshua.
Yoshua.10:14 Ndipo Yoshua akanena na Bwana katika siku hiyo ambayo Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
13 Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao.
14 Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizoandama baada yake, hata ikawa yeye Bwana kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa Bwana alipiga vita kwa ajili ya Israeli.

Ushauri:
Siku zote ili upate muktadha na mantiki ya usomaji wa Biblia, usiridhike na kusoma Biblia moja, utapotea, siku zote tafuta kuhakiki andiko (scripture) kwa kurejea Biblia mbili kwa uchache. Hivi sasa kuna versions za Biblia takriban 25. Aidha, tafsiri ya lugha zilizotumika kuandika Biblia nayo inaleta changamoto. Mfano Biblia ya KJV Kitabu cha Kutoka.32:7-14 kinamtaja MUNGU kama Musa alimwambia "tubu" "Repent" wakati tafsiri ya Kiswahili inasema Musa alimwambia MUNGU geuka yaani "ghairi" mpango wa kuua wana wa Israeli. Je, MUNGU awezakutubu? Dhambi ipi aliyonayo? Je, yeye siyo Mtakatifu asiye na dhambi? Ili uuwe na uelewa mzuri wa maandiko jaribu kuwa unasoma Biblia ya Kiebrania ndipo ulinganishe na aina ya Biblia unayomiliki. Biblia OG iliandikwa kwa lugha za Kiebrani na Kiyunani (Dead language/lugha iliyotoweka duniani).

Biblia ya KJV ina jumla ya maneno 783,137, ina juzuu (versions) mbili, ya kwanza ya mwaka 1611 AD na ya pili ya mwaka 1616 AD, zina tofauti kwenye mstari mmoja tu wa Ruthu.3:15 ambapo juzuu ya kwanza inamtaja Ruthu kama mwaume "he went into the city" na juzuu ya pili inamtaja Ruthu kama mwanamke "she went into the city". Hata hivyo hakuna ubishi kwamba Agano la Kale liliandikwa kati ya mwaka 1200 BC & 165 BC na Agano Jipya 50 AD & 100 AD.

Ufananisho wa Maeneo:
Kutafuta kufananisha maeneo ya Nyakati za Biblia na Nyakati za leo.

Hili nalo ni mtambuka na kuna uelewa mbalimbali tofauti kama ifuatavyo:-
Wazungu wanaamini kwamba Zinjanthropus siyo binadamu wa kwanza kwa sababu wamegundua mafuvu kadhaa ya binadamu ambao walitangulia kundi la akina Zinjanthropus la Homo habilis. Hii inamuondoa Zinja kuwa binadamu wa kwanza na ikumbukwe kumtambua Zinja kuwa wa kwanza kulihitajika kutumia teknolojia ya wazungu hao hao, waafrika hatuna teknolojia hiyo, Carbon 14 ni ya Mzungu pia. So watachosema inabidi tukubaliane nao kwa sababu hatuna teknolojia yetu.

Kuna maarifa yanasambaa kwamba palikuwa na kisiwa kinaitwa Atlantis, kilikuwa kwenye bahari ya Atlantiki kikapigwa na kimwondo na kukizamisha chini ya bahari, kisiwa hiki kilikuwa na binadamu wa aina yetu Homo Sapien na kilikuwa na maendeleo yote haya ya karne hii miaka hiyo. Wataalam wa mambo-kale artifacts (Objet d'art) walizamia huko na kukuta magofu ya maghorofa marefu sana, hii ikithibitisha kuwa binadamu hawa walifikia hatua kubwa ya maendeleo ya binadamu kuliko tuliyofikia leo.

Wana historia wanaamini evolution of man inaendelea kwamba baada ya Homo Sapien ambao ndiyo sisi, binadamu ata evolve kuwa na sura nyingine mpya kabisa na akili ambayo ni advanced kuliko tulizo nazo leo. Yawezekana binadamu atayefuata Homo Sapien atakuwa na sura ya zombie sijui!, miguu minne na mikono minne sijui! kama robot sijui! Tuwaachie wao wanahistoria.
OIP.s_TSEGBshsCsL4z7MTKCRAHaHa

Homo Karn
(sijui mie)
Taswira kwa hisani ya Google
 
Neno Repent ambalo kwa kiyunani ni Metanoia maana yake ni 'Change of mind' this means that its not necessarily TUBU.Ingawa tumezoea kulitumia sana kwenye agano jipya ambalo kimsingi limeandikwa kwa kiyunani likitumika kama kubadilika kwa mtazamo.Sijajua bado exactly ni neno gani lilitumika kupresent neno Repent kwa kiebrania pengine tungelifahamu lingetupa mwanga zaidi but in this point i don't see any contradiction.
 
Pia Biblia imeandikwa kwa lugha tatu Kiebrania( agano la kale),Kigiriki ambacho ndo kinaitwa kiyunani (agano jipya) na Aramaic language baadhi ya scripture za agano la kale na baadhi verses za agano jipya.
 
Haiwezekani kuitumia Biblia na Sayansi kwa pamoja kuexplain origion of man and universe,biblia inazungumzia life on earth mpaka muda huu ni takribani miaka elfu 6 na kitu lakini sayansi inazungumzia some millions years.So this two theories cannot explain the same thing.Sayansi imeshindwa kueplain maswali mengi sana ambayo story ya uumbaji imejaribu kutoa majibu yake.Tatizo ni kwamba wengi tunajaribu kutumia sayansi hiyo hiyo iliyoshindwa kutoa majibu kuprove yaliyoandikwa kwenye Biblia.Kamwe haiwezekani.
 
Umezungumzia Book of Enoch lakini vipo vingi hujavitaja.So kila ancient manscript inaweza kutumika kama sehemu ya kitabu kitakatifu,vipo vingi sana ambavyo vimekataliwa kwa kuwa vinacontradict na mafumdisho mengine mengi yaliyowahi kuandikwa na kukubaliwa kutumika. Waliokwenye imani kwa sababu ni imani walizorithi kwa wazazi hawawezi kutumia hiyo kama excuse kwa sababu nafasi ya kujifunza habari za imani nyingine na kuchukua hatua kila mtu anayo kwa hiyo tusijifiche humo.Mimi nipo kwenye imani niliyonayo kwa sababu ya choice,i took my time to study and made a choice.
 
Back
Top Bottom