TUKUTUKU
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 11,765
- 4,033
Napenda kuchukua fursa hii, kumpongeza mr Rutashubanyuma kwa michango mingi aliyoitoa kwa kipindi kifupi,na mbali ya wingi wa michango hiyo,pia imekuwa michango ya muhimu katika kuelimisha jamii.Maana waswahili wanasema wingi si hoja,kinachohitajika zaidi ni ubora,lakini kwa Mr Rutashubanyuma, michango yake imekuwa na sifa zote mbili yaani ni mingi na yenye ubora wa kutosha.Sina uzoefu mkubwa sana hapa JF,lakini kwa kipindi kifupi nilichokuwepo hapa sijapata kuona mtu aliyeweza kuandika posti nyingi kwa siku kama mr Rutashubanyuma .Wastani wake wa kuandika posti kwa siku ni 97,hakika huu ni uwezo mkubwa sana.Hongera sana mkuu na endelea na juhudi zako katika kuelimisha jamii.
Nawasilisha
Nawasilisha