Russian invasion on Crimea is underway

Russian invasion on Crimea is underway

Hizi ndo akili zetu...sijui umetumia kigezo gani kusema Putin anatumia akili ya zamani sana,in short tutapiga kelele humu ila hatutajua chanzo chake hasa hadi wamefika/amefikia hapo......We are African lets solve our problem 1st before looking outside our boundary ambayo hata tungeachiwa changamoto zao hata robo tu tutakesha miaka mia mbili hatumalizi hata robo ya tatizo.

Kama una akili kuliko huyo Putin tusaidie kuondoa matatizo ya kiuchumi hapa Tanzania au jambo kubwa kuliko hilo dogo la huko Russia la msongamano wa magari Dar-Es-Salaam.

Hebu tulia ujadili hoja iliyoko mbele yetu, siyo kukurupuka na ku-question akili zangu. Kama unataka nitatua matatizo ya Dar es Salaama, niko tayari kufanya hivyo iwapo utanipa madaraka hayo. Siwezi kutatua matatizo ya Dar wakati umewapa madaraka watu wasiokuwa na akili.

Kama wewe unadhani kuwa tendo la Putin ni sawa basi tuambia uhalali wake ni nini. Huwezi kuchukua jeshi lako na kuliingiza nchi ya jirani yako wakati hamjagombana. Matatizo ya Ukraine yalikuwa yao ya ndani, yeye kuingilia ni kosa ambalo litakuwa ni hasara kwa urusi. Kuvamia nchi ya jirani kwa sababu tu rafiki yake kaondolewa madarakani na wabunge wa nchi hiyo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo ni kusa sana. Ni akili ya kizamani kudhani kuwa Ukraine bado ni sehemu ya USSR wakati ni wao Russia wakiongozwa na Yelstin ndio waliovunja muungano ule na kuacha kila nchi ijiendeshe yenyewe.

Amejenga mazinigira ambayo nchi nyingine zote zilizokuwa sehemu ya USSR kuanza kujijenga kijeshi kwa kuogopa kuvamiwa na urusi; waliwahi kuivamia Georgia, na sasa wamefanya hivyo kwa Ukraine kwa hiyo nchi nyingine zilizobaki zinajua kuwa wana bully jiranni yao. Kumbuka kuwa Ukraine ndiyo iliyokuwa na silaha nyingi sana za Nyuklia kuliko republic nyinginje yoyote huko USSR, wakaombwa sana waziharibu na hapo mwaka 1994 wakawekeana mkataba wa kuziharibu mradi tu usalama wao usitishiwe na urusi. Kwa vile Putin amekiuka mkataba huo, basi Ukraine inaweza kuanza tena kujilimbikiza silaha hzio, jambo ambalo linakuwa ni hatari siyo tu kwa usalama wa dunia bali kwa Urusi pia.

Nchi nyingi zilizokuwa za USSR na zile za Warsaw pact zinaanza kuhamia NATO haraka haraka kwa sababu ya matendo ya Putin; hilo halitakuwa jambo zuri kwa Urusi.
 
Kichuguu nmegundua kuwa kwa akili zako unadhan Putin alilala na kuamka akaamua tu apeleke majeshi UKRANE,na unadhan wabunge wa bunge la URUSI walikunywa mvinyo wakalewa kabla ya kumpa ruhusa putin ya kupeleka jeshi Ukrane..
KIUFUPI HAUJUI KINACHOENDELEA NA MVIVU WA KUJIFUNZA,HVO NA KUSHAURI KWA KULINDA HESHIMA YAKO TU KAA KIMYA..
 
Last edited by a moderator:

Hata ukinitukana matusi ya ngunoni, bado nina imani kuwa elewa wangu ni mpana sana zaidi ya mara kumi kuliko wa kwako. Hakuna international lawa ianyoruhus nchi moja kuvamia nchi nyingine bila kuwepo kwa azimio la umoja wa mataifa kuonyesha kuwa uvamizi huo ni wa muhimu ili kuzuia raia wa kawaida wasidhruike. Urusi bado wanalia sana kwa kuvunjika kwa USSR, na kile kisingizio alichotumia cha kuokoa maisha ya warusi walioko Ukraine ni NULL and VOID; warusi wako urusi, wale wote walioko Ukraine siyo warusi bali nmi raia wa Ukraine hata kama asili yao ni urusi. Huwezi kutegemea Serikali ya Tanzania ipeleke majeshi Kenya eti kwenda kuwatetea wajaluo na wamasai walioko Kenya kama kwamba wamasai na wajaruao wote ni raia wa Tanzania. Kama ana raia wa urusi ambao ni reguisted, jukumu lakie ni kufanya evacuation ya kuwaondoa hatarini siyo kuvamia nchi ya mwanzako. Putin huyu alipindisha katiba ya nchi kusudi arudi madarakani halafu na bunge hilo likamkubalia halafu wewe unadai wabunge wanatumia akili? Kama hujui siasa za dunia kaa kimya uache wanaojua kuzifuatilia wazijadili. Huwa nashindwa sana kubadilishana mawazo na watu wa aina yako wanaotanguliza matusi badala ya kujenga hoja. Inaonekana kama vile matusi ndiyo jadi yetu waswahili wengi.
 
Wote manotetea kitendo cha Putin mbona hamkumtetea Amin alipoingiza majeshi yake pale Kagera tena sehemu ndogo tu akiwa anatafauta mpaka aliouita wa asili, yaani mto? Kuna wahaya pande mbili za mpaka lakini tulitetea sana eneo letu tena kwa nguvu zote hadi uchumi wetu ukaharibia. Kitendo cha Putin ni uvamizi na uchokozi usiokuwa na maana; acheni ushabiki mwingine usiokuwa na mantiki. Mkishbikia kitendo cha taifa moja kuvamia taifa jingine kwa mapenzi ya kiongozi wake basi msishangae siku Tanzania nayo ikivamiwa na taifa moja kubwa sana. Kuna mataifa mengi yenye nguvu yanayoweza kuivamia Tanzania.

Watu mnashindwa kuelewa kwa nini marekani inapotaka kuivamia nchi yoyote hujenga sana ile coalition kupitia umoja wa mataifa na kujenga kesi yao kuwa kweli ni lazima uvamizi ufanyike. Hata kama tunaona kuwa uvamizi huo ni halali, at least huwa umeshapitia ngazi zote za kisheria katika UN: Putin kakurupuka.
 
"The process that put Aksyonov(newly elected crimenian PM by Crimean Parliament) in power violated

the Ukrainian constitution, since Kiev is supposed to appoint the regional prime minister. But

then again, so did the process through which Oleksandr Turchynov(newly elected - by the Ukranian

Parliament- PM) became acting president of Ukraine, because, as Daisy Sindelar, a senior

correspondent for Radio Free Europe/Radio Liberty, has pointed out, former President Viktor

Yanukovych’s ouster did not follow constitutional protocol. One can argue that the cases are

somewhat equivalent: In both, parliamentary majorities supported a new leader."

Mkuu Kichuguu, hakuna aliye madarakani kihalali hapo. Wote wana uhuru wa kuomba msaada wa kijeshi!
 
Tatizo marekani lengo lao ni kuizingira russia pande zote.baada ya kufanikiwa kuzishawishi nchi zilizokua chini ya WARSAW PACT kama poland,latvia,lithunia,check etc kujiunga na NATO ,walikua pia katika process za kuifanya ukraine ijiunge na EUROPEAN UNION na hatimae Nato ,lakini ugumu ni kwamba ukraine ni muhimu sana kwa usalama wa russia kwani katika crimea ndiko ilipo Russian black sea fleet ambayo ni bandari pekee ya warm water,kwamaana kwamba fleet zao zingine ziko kwenye bandari ambazo kipindi cha winter huganda na hivo military movement za warship zao huwa zinakua restricted.
Pia blacksea fleet ndo inawezesha njia ya mkato ya meli za russia kufika mediterania.sasa russia haiko tayari kuona ukraine ikiwa chini ya Nato kwa gharama yeyote ile.
Katika mazungumzo ya backchanel yanayoendelea hivi sasa kati ya russia na marekani ,russia imetoa masharti ambayo lazima yafuatwe ndipo waondoe majeshi yao hapo crimea.
 
Katika watu ambao si wapendi ni dizain yako.....Kuna aina ya watu humu duniani asipolisikia/kuona jambo yeye kwa masikio/macho yake anahalalisha kuwa jambo linalozungumziwa halipo au halijatokea.
MAWAZO UJENZI sijasikia kuwa hawa watu wameongea chochote coz sipo na media 24hrs ila aliyesema sio mpuuzi na walichoongea haviwezi kuwa wazi sana na mara nyingi habari ambazo huwa zinatolewa kwa wananchi ni zile zisizo kuwa na athari but am sure 85% ya mazungumzo ya aina hiyo huwa zinafichwa.

Nashukuru sana kwa kutopenda watu wa dizain kama yangu!!!
Kwanza naomba niseme huwezi nilazimisha kuamini maneno yako ni lazima we mwenyewe ujirizishe
Mbili hata chuon tunapofanya assignment,research,lazima uwe na Bibliography ya kuonyesha hizo data umezitoa wapi!! Ndo maana kila mtu hapa akikandamiza uzi lazima auwekee minofu ili watu waamini na kuchangia hoja,la sivyo,kuna hatari,siku mtu kama wewe mwenye mawazo finyi unaweza lidanganya taifa, kosa langu ni lipi kuhoji kwamba hizo taarifa kazitoa wapi??
Jaribu kua mwerevu na wenye long plan na sio short plan,na ndio maana viongozi wengi hufeli,hv leo hii kuna sababu gani ya serikari kubomoa nyumba za watu na kuwalipa fidia ili wajenge barabara au soko?? Je viongozi hawa hawakujua 100 years to come what will happened??
Leo hii mtu mwenye akili kama zako ndo aje kuomba kura zetu??
Kweli Tanzania tumelogwa, na aliyetuloga hatumjui
Kwa leo naomba niishie hapa, maana hujanitendea haki kusema watu wa dizaini kama yangu huwapendi!!
Usiwe kama yule Mwenyekiti wa opposition party, akihojiwa mapato na matumizi anang'aka
 
Last edited by a moderator:
"The process that put Aksyonov(newly elected crimenian PM by Crimean Parliament) in power violated

the Ukrainian constitution, since Kiev is supposed to appoint the regional prime minister. But

then again, so did the process through which Oleksandr Turchynov(newly elected - by the Ukranian

Parliament- PM) became acting president of Ukraine, because, as Daisy Sindelar, a senior

correspondent for Radio Free Europe/Radio Liberty, has pointed out, former President Viktor

Yanukovych's ouster did not follow constitutional protocol. One can argue that the cases are

somewhat equivalent: In both, parliamentary majorities supported a new leader."

Mkuu Kichuguu, hakuna aliye madarakani kihalali hapo. Wote wana uhuru wa kuomba msaada wa kijeshi!

OK,

Sasa Urusi inaingiaje kwenye mgogoro wa Ukraine mpaka kupeleka jeshi huko; hawajasema waliombwa na upande wowote wa mgogoro bali wamesema wanakwenda kulinda warusi wenzao. Huo ni mgogoro wa ndani ya Ukraine kuna sheria na taratibu zao zinahusu kutatua migogoro yao ya ndani. Hiyo quote yako ni single sided, kwani inasahau kuwa bunge la Ukraine lina mamlaka ya kumwondoa rais madarakani. Katiba za nchi nyingi ikiwamo hata ya Tanzania inatoa mamlaka kwa Bunge kumwondoa rais madarakani. Mgogoro wa Ukraine ulikuwa Kiev, na ndipo Bunge lilipomwondoa rais madarakani kihalali kabisa, Urusi ikatengeza mgororo mwingine huko Crimea kwa sababu zao binafsi. Tataizo kubwa ni kuwa hakupewa muda wa kujitetea lakini katiba hiyo pia inaruhusu bunge kuchukua hatua za dharura katika hali ya hatari. Yule alitolea kwa vile nchi ilishakuwa katika mgogor wa muda mrefu na watu wengi kuwa wampoteza maisha. Puti angeingia pale kama Big Brother kusaidia kumaliza mgogor angefanya vizuri lakini yeye anakwenda pale akiwa upande mmoja wa mgogor tena kwa kutumia mabavu, hiyo ni kutumia akili za ki-USSR ambazo ni za kizamani sana zilizowahi kutumika Czechslovakia na Afghanstan zamani sana.
 
jana kwenye UN security council,Russia walionyesha barua iliyoandikwa na rais victor kabla hajapinduliwa iliyokua ikiomba msaada wa kijeshi toka russia.
 
Aiseee!! Yaani hakuna na haitakuja kutokea forum ya watu wenye akili na upeo wa hoja kama jf. Yaani leo kwenye hii posti nimepata habari na uelewa mpana zaidi juu ya huu mgogoro wa Eastern na Western block from different angles.
Maana hapa kuna wengine bado tuna uwanda mdogo juu ya hii isue nzima na mwenendo wake.
Ahsanteni kwa wote mlochangia na mtakao kuja na michango mingine.
 
jaman,soma kwanza kilicho nyuma ya pazia ndo uanze kumlaumu putin,wakati ukrain inataka kuingia eu,russia walitumia resources nyingi sana kuzuia ikiwemo msaada wa dollar billion 15 na mengine mengi,na walipofanikisha hili warusi walifanya hadi party,politically hawana uhakika na akili ya ajae so wanahofia kupoteza nguvu zao bure..HAPA MAREKANI HATA AFANYEJE,RUSSIA LAZMA ATAINGIA UKRAIN
 
OK,

Sasa Urusi inaingiaje kwenye mgogoro wa Ukraine mpaka kupeleka jeshi huko; hawajasema waliombwa na upande wowote wa mgogoro bali wamesema wanakwenda kulinda warusi wenzao. Huo ni mgogoro wa ndani ya Ukraine kuna sheria na taratibu zao zinahusu kutatua migogoro yao ya ndani. Hiyo quote yako ni single sided, kwani inasahau kuwa bunge la Ukraine lina mamlaka ya kumwondoa rais madarakani. Katiba za nchi nyingi ikiwamo hata ya Tanzania inatoa mamlaka kwa Bunge kumwondoa rais madarakani. Mgogoro wa Ukraine ulikuwa Kiev, na ndipo Bunge lilipomwondoa rais madarakani kihalali kabisa, Urusi ikatengeza mgororo mwingine huko Crimea kwa sababu zao binafsi. Tataizo kubwa ni kuwa hakupewa muda wa kujitetea lakini katiba hiyo pia inaruhusu bunge kuchukua hatua za dharura katika hali ya hatari. Yule alitolea kwa vile nchi ilishakuwa katika mgogor wa muda mrefu na watu wengi kuwa wampoteza maisha. Puti angeingia pale kama Big Brother kusaidia kumaliza mgogor angefanya vizuri lakini yeye anakwenda pale akiwa upande mmoja wa mgogor tena kwa kutumia mabavu, hiyo ni kutumia akili za ki-USSR ambazo ni za kizamani sana zilizowahi kutumika Czechslovakia na Afghanstan zamani sana.

mkuu unachanganya madesa hapa, Hilo jeshi lilikuwepo Crimea, halijapelekwa. LIMEKUWA activated tu. Kila mwerevu anaelewa kuwa Arab Spring, Mgogoro wa Syria, Kina Dalai Lama na wengine ni Njia za Wamarekani kusukuma mbele ajenda zao.Ni vitu vilivyo wazi kabisa, havihitaji uishi Ulaya miaka 20 kuvifahamu, unless uamue kutochanganya na za kwako.

Crimea kuna asilimia 60 ya warusi, kuna naval bases zao, Kinachoendelea kule warusi wanakifahamu vizuri kuliko sisi ambao we are lost in translation. Kibiashara makampuni mengi ya CIS headquarters zao ziko moscow, lakini wanaserve Kiev, Kijamii kuna muingiliano mkubwa sana wa warusi na watu wa Crimea,na Ukraine,hata raisi wa Urusi aliwahi kutoka Ukraine hapo zamani, HUWEZI kusema kuwa kinachotokea UKRAINE URUSI hakiwahusu. Halafu hapohapo MAREKANI Inatunisha sharubu zake hovyo kila Izrael inapochokzwa na waarabu.

Putin is not any less a big brother than US, actually it's the opposite, Sijaona URUSI ikilazimisha Costarica ijitenge na Marekani, au ikilazimisha mapinduzi yatokee alaska au canada. Influence ya warusi kwa nchi zilizokuwa sehemu za USSR sio jambo la kinadharia.kama umeshawahi kuishi ULAYA Mashariki utagundua kuwa m-ukraine yoyote anaiita Russia, mother Russia.

kama huwafahamju hawa watu huwezi kuwatofautisha, na lugha zao zinaingilana mno. Ni watu ambao maisha yao yameingiliana kwa karne na karne, kwa mabaya na Mazuri.

Kinachotokea kwenye hizi nchi MAREKANI hakiwahusu.Kinachoendelea kwenye hizi nchi Marekani ni kiherehere chao. wasilete hadithi za haki za binadamu and all that yada yada, we all know what that pretext leads to.

Hapa hakuna mwema.
 
to Kichuguu when you lend someone $60B and you have naval bases in large patr of that country you are damn well entitled to have your say. hawa wamarekani wamewaahidi waganda a mere $90 that might never have seen the sun, lakini leo hii wanawachagulia hadi style ya kujamiiana.

It will take a lot of convincing kusema hawa watu wana afadhali.
 
Last edited by a moderator:
So far nimegundua kwamba kihalali urusi hana haki ya kuivamia ukraine ila kwa sababu maslahi yake binafsi yameguswa so anaingia kujilinda na kuweka maadui zake mbali,since duniani hakuna nchi wala mwanadamu ambae hatangulizi mbele maslahi yake binafsi(human being is selfish by nature) so russia ana haki ya kujihami ingawaje naona pia kazi itakuwa sio ndogo hasa katika kuweka utawala ambao atakuwa anautaka yeye na pindi wananchi watakapoukataa...
 
Duh..!!,nilidhani mambo yanaanza kutulia kumbe moto ndo unazidi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa russia amesema,russia will retaliate if US impose economic sanction on russia.
Pia kuna taarifa ya milio ya risasi kwenye kambi moja ya kijeshi huko crimea.
Not only that,but olso Interfax inaripoti kuwa,russia imefanya jaribia la kombora la INTERCONTINENTAL BALLIST MISSILE usiku huu.
 
Kombora la Topol limefyatuliwa toka astrakhan ,russia na kuhit target huko kazakhstan.
 
We mjinga kweli,kwa hiyo unataka western ndo waendelee kuandika historia ya himaya yao?
Jaribu kufikiri kabla ya kuandika.Si kila unapopata mbs basi unaleta nonsense kwenye jukwaa.
Eti kuandika historia mpya.Hivi wew hujui kuwa kila taifa linataka kujijenga?
 
Back
Top Bottom