Russian invasion on Crimea is underway

Russian invasion on Crimea is underway

Mnaosema Malekani ni superpower siwaelew kwa kweli..
Yan RUSSIA pekeyake ana ichachafya malekani na washirika wake wotee.!
Hahaha..wakamtoe Putin kwa nguvu kama Gadaffi..
 
Msululu wa magari ya kijeshi ya russia,ukiingia crimea mapema leo.
Russian%20trucks_0.jpg
 
Vifaru vya kijeshi vya ukraine vikielekea crimea,hapo jana ,ndo kusema mambo yako karibu kuwa mambo?.
640x427.jpg
 
Putin anaweza kuwa anatumia mwanya uliopo kwenye political system ya Marekani kuhusu mgawanyiko wa Republican na Democrats; ila itakapofika kuwa enough is enough na jamaa wakawa Marekani moja kama ilivyokuwa 9/11 utashangaa kuona mabavu ya Marekani dhidi ya Putin na wafuasi wake. Cold War iliyokwishwa zaidi miaka 20 iliiypita na kuacxha superpower mmoja haiwezi kurudi tena leo. Sehemu kubwa sana ya teknolojia inayotumiwa na urusi leo imetoka marekani, na vile vile uchumi wote wa urusi leo unategema sana gesi wanayouza kwenye nchi za NATO.
Kichuguu,

Wewe kweli kichuguu cha mchwa hasa, wewe huo Upofu wa Yuda-kristo mweusi inakusumbua kama unavyowasumbua kwani hujui kama tofauti zote walonazo baina ya republicans na democrats lakini wanakutana kuwa kito kimoja kwenye foreign policy na kuikuza Empire na wao ndio hawa wanaishi katika era za zamani maana empire zote zimekufa wao wanaburuzwa kwa niaba mabepari na mayahudi wa AIPAC kupigana vita si vyao katika mashariki ya kati na Africa na kwengineko kwenye rasilmali kama mafuta gesi uranium na madini mengineyo.

911 ilikuwa kiini macho kwa wananchi wao walio wengi ambao si wanachama wa chama chochote. Sasa wameamka hata hao waliompigia kura Obama nao wamechoka nae kwani mpaka leo hajatimiza ahadi nyingi alizotoa katika kampeni. Vita walivyoingia Afghanistan na Iraq vimepandisha deni la taifa maradufu kwani China inashikilia robo tatu ya Hawala (Govt Bonds) za serikali ya Marekani. Katika maidani ya vita kihistoria wamarekani hakuna eneo wameshinda vita baada ya WW II kuanzia Korea, Vietnam, Iraq na Afghanistan wata waweza Russia?
 
Last edited by a moderator:
Kichuguu,

Wewe kweli kichuguu cha mchwa hasa, wewe huo Upofu wa Yuda-kristo mweusi inakusumbua kama unavyowasumbua kwani hujui kama tofauti zote walonazo baina ya republicans na democrats lakini wanakutana kuwa kimoja kwenye foreign policy na kuikuza Empire na wao ndio hawa wanaishi katikabera za zamani maana empire zote zimekufa wao wanaburuzwa kwa niaba mabepari na mayahudi wa AIPAC kupigana vita si vyao katika mashariki ya kati na Africa na kwengimeko kwenye rasilmali kama.mafuta gesi uranium na madini mengineyo.

911 ilikuwa kiini macho kwa wananchi wao walio wengi ambao si wanachama wa chama chochote. Sasa wameamka hata hao waliompigia kura Obama nao wamechoka nae kwani mpaka leo hajatimiza ahadi.nyingi alizotoa katika kampeni. Vita walivyoingia Afghanistan na Iraq vimepandisha deni.la taifa maradufu kwani China inashikilia robo tatu ya Hawala (Govt Bonds) za serikali ya Marekani. Katika maidani ya vita kihistoria wamarekani hakuna wameshinda vita baada ya WW II kuanzia Korea, Vietnam, Iraq na Afghanistan watwaweza Russia?

Mkuu Averoes heri umempasha huyo Kichuguu maana huko nyuma alikuwa akimj-underrate Putin akifikiri Russia is a third rate banana republic.

Nimesema huko nyuma , hapo Obama amegota kwa Putin.
Salama yake ni kukaa kimya wakati Urusi inamnyoosha Ukraine kwa kuweka kiburi ya kumwondoa Rais wake(mwenye mlengo wa kulalia Urusi).

Maandamano na fujo zote zile zilifadhiliwa na West, wakifikiri Urusi haijui hilo.
Sasa Urusi vile vile inafadhili Crimea kujitoa Ukraine.

Ni gemu la tit-for-tat.

Mkuu wewe huwafahamu Warusi.
They can be pig headed hasa wakati huu ambapo nchi za magharibi zimecheza rafu kando mwa nchi yake.
If anything to go by, Georgia ilibomondwa bila West kufanya lolote.

Katika hili licha ya Urusi kuahidi kuisaidia Ukraine wakaamua kumpindua rais kwa msaada wa West,

Ukraine ndo inavunjika hivo , Urusi imeamua kuisaidia Crimea,yenye warusi wengi.

Warusi ukiwachokoza tegemea kiburi, na West wameipata sasa.
Katika hili the west can only watch and they will do NOTHING.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Averoes heri umempasha huyo Kichuguu maana huko nyuma alikuwa akimj-underrate Putin akifikiri Russia is a third rate banana republic.

Nimesema huko nyuma , hapo Obama amegota kwa Putin.
Salama yake ni kukaa kimya wakati Urusi inamnyoosha Ukraine kwa kuweka kiburi ya kumwondoa Rais wake(mwenye mlengo wa kulalia Urusi).

Maandamano na fujo zote zile zilifadhiliwa na West, wakifikiri Urusi haijui hilo.
Sasa Urusi vile vile inafadhili Crimea kujitoa Ukraine.

Ni gemu la tit-for-tat.

Hawa nchi za Magharibi kwa karne walikuwa wakinyonya mataifa yaliokuwa makoloni yao na kujenga biashara kubwa kubwa na viwanda vizito hasa vya silaha. Ubepari umethibitika kuwa ni failure katika nchi zao since Greece riots za kupinga unyanyap na mwenendo hasi wa kiuchumi sasa Ulaya nzima inatetemeka na maandamano. Mfano Ufaransa haikaliki, Spain nayo hailaliki, Itali imebaki kubadilisha serikali tu katika mwaka mmoja wamebadili serikali tatu.

Sasa wanaunda migogoro na vielelzo vya kuashiria vita ili matajiri wa viwanda vya silaha wafaidike. Kwa mfano Uarabuni kila siku anatumiwa Iran indirectly kiwatisha waarabu eti atawashambulia ili wafanye order za silaha.

Wale the so called Pirates of the Horn of Africa si kuwa waliamka tu wakaamua kufanya vile. Hawa hawana tofauti na wale ISIL wa Syria. Weletwa.pale on purpose kabisa ili Wababe walete madude pale kwa kisingizio kulinda meli zao. Someni kitabu by Robert D kaplan "Monsoon - The Decline of American Power in the Indian Ocean" Lakini utaona hakuna aliebaki, wachina na wa Irani pia wameleta manowari zao.
 
Last edited by a moderator:
Kichuguu,

Wewe kweli kichuguu cha mchwa hasa, wewe huo Upofu wa Yuda-kristo mweusi inakusumbua kama unavyowasumbua kwani hujui kama tofauti zote walonazo baina ya republicans na democrats lakini wanakutana kuwa kito kimoja kwenye foreign policy na kuikuza Empire na wao ndio hawa wanaishi katika era za zamani maana empire zote zimekufa wao wanaburuzwa kwa niaba mabepari na mayahudi wa AIPAC kupigana vita si vyao katika mashariki ya kati na Africa na kwengineko kwenye rasilmali kama mafuta gesi uranium na madini mengineyo.

911 ilikuwa kiini macho kwa wananchi wao walio wengi ambao si wanachama wa chama chochote. Sasa wameamka hata hao waliompigia kura Obama nao wamechoka nae kwani mpaka leo hajatimiza ahadi nyingi alizotoa katika kampeni. Vita walivyoingia Afghanistan na Iraq vimepandisha deni la taifa maradufu kwani China inashikilia robo tatu ya Hawala (Govt Bonds) za serikali ya Marekani. Katika maidani ya vita kihistoria wamarekani hakuna eneo wameshinda vita baada ya WW II kuanzia Korea, Vietnam, Iraq na Afghanistan wata waweza Russia?

Hayo niliyo bold yanaonyesha upungufu wa mawazo yako:

(1) Ingekuwa Republicana na democrats wa leo wanakubaliana kuhusu foreign policy kama walivyokuwa wakati wa Cold War basi wasingekuwa wanayumba katika maamuzi yanayohusu nchi za nje. Ni wazi hujui siasa za Washington DC leo, at least usingesema wanakubaliana kuhusu mambo ya nchi za nje kwani ungekuwa unajua jinsi swala la Syria lilivyokuwa na mvutano. Usilaumu mwenzako bila kumfahamu. Wengine hutafuta habari zinazohusu pande zote mbili za mgogor na kufahamu unbiased halafu ndipo unatoa mawazo yako, wewe unaonekana kutoa mawazo yako kwa kutumia assumptions tu ambazo si za kweli.

(2) Imani yako kuwa 911 ni kiini macho ni upofu mkubwa sana wa mawazo ambayo siwezi kukusaidia, ni kuoinyesha zaid kuwa unaongea kitu kwa kutumia assumptiona za kufikirika.

(3) Halafu jitahidi uwe unasoma habari za uchumi wa dunia vizuri kwani habari hizo zinasaidia sana hata kujua jinsi ya kuendesha nchi yetu. Madai kuwa robo ya madeni ya marekani ni mkopo kutoka China ni ya kufikirika sana mabayo nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kukusahihisha Kiasi kama 66% cha government bonds za Marekani zinashikiliwa na Mutual Funds pamoja na investors wa Marekani. Nchi za nje zinashika kiasi cha kama 34% tu. Ingawa ni kweli China ndiyo nchi ya nje yenye government bonds nyingi za kimarekani ikifuatiwa kwa karibu na Japan, bado hazifikii robo kama unavyodai; angalia jedwali hili hapa. Ziliongezeka kidogo kwa asilimia kama moja hivi mwanzoni mwa mwaka huu lakini zikatelemka tena mwezi wa pili na kurudi namba ile ile ya zamani. Deni la Marekani leo ni trilioni $17.5 trilioni wakati kati hilo China inashikilia $1.3 trililion wakati Japan nayo ikiwa inashikilia $1.2 trlilion, je ni hesabau gani unayotumia kusema kuwa deni la China ni robo kama siyo mawazo yaliyopindika. Kutokana na kupindika mawazo unakuwa unashindwa kuongea mambo objectively bali kudhani kuwa tunaosema ukweli. Ndiyo maana unaamini kuwa 911 ilikuwa ni njama ya serikali. Kila gazeti la dunia huwa lina sehemu ya uchumi na magazeti mengi yanapatikana online, jitahidi uwe unasoma vitu hivyo.
 
Kuanguka kwa world powers.Mivutano hii inaua mataifa yote makubwa.Hata U.S yenyewe inatumika tu kama tool kufikia malengo,lakini mwishowe na yenyewe haitabaki salama!Making the way for something bigger than U.S,USSR,UN e.t.c
 
Hayo niliyo bold yanaonyesha upungufu wa mawazo yako:

(1) Ingekuwa Republicana na democrats wa leo wanakubaliana kuhusu foreign policy kama walivyokuwa wakati wa Cold War basi wasingekuwa wanayumba katika maamuzi yanayohusu nchi za nje. Ni wazi hujui siasa za Washington DC leo, at least usingesema wanakubaliana kuhusu mambo ya nchi za nje kwani ungekuwa unajua jinsi swala la Syria lilivyokuwa na mvutano. Usilaumu mwenzako bila kumfahamu. Wengine hutafuta habari zinazohusu pande zote mbili za mgogor na kufahamu unbiased halafu ndipo unatoa mawazo yako, wewe unaonekana kutoa mawazo yako kwa kutumia assumptions tu ambazo si za kweli.

(2) Imani yako kuwa 911 ni kiini macho ni upofu mkubwa sana wa mawazo ambayo siwezi kukusaidia, ni kuoinyesha zaid kuwa unaongea kitu kwa kutumia assumptiona za kufikirika.

(3) Halafu jitahidi uwe unasoma habari za uchumi wa dunia vizuri kwani habari hizo zinasaidia sana hata kujua jinsi ya kuendesha nchi yetu. Madai kuwa robo ya madeni ya marekani ni mkopo kutoka China ni ya kufikirika sana mabayo nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kukusahihisha Kiasi kama 66% cha government bonds za Marekani zinashikiliwa na Mutual Funds pamoja na investors wa Marekani. Nchi za nje zinashika kiasi cha kama 34% tu. Ingawa ni kweli China ndiyo nchi ya nje yenye government bonds nyingi za kimarekani ikifuatiwa kwa karibu na Japan, bado hazifikii robo kama unavyodai; angalia jedwali hili hapa. Ziliongezeka kidogo kwa asilimia kama moja hivi mwanzoni mwa mwaka huu lakini zikatelemka tena mwezi wa pili na kurudi namba ile ile ya zamani. Deni la Marekani leo ni trilioni $17.5 trilioni wakati kati hilo China inashikilia $1.3 trililion wakati Japan nayo ikiwa inashikilia $1.2 trlilion, je ni hesabau gani unayotumia kusema kuwa deni la China ni robo kama siyo mawazo yaliyopindika. Kutokana na kupindika mawazo unakuwa unashindwa kuongea mambo objectively bali kudhani kuwa tunaosema ukweli. Ndiyo maana unaamini kuwa 911 ilikuwa ni njama ya serikali. Kila gazeti la dunia huwa lina sehemu ya uchumi na magazeti mengi yanapatikana online, jitahidi uwe unasoma vitu hivyo.
Kichuguu,

Naona kichuguu kinamegwa na mchwa hicho, usinifundishe kutafuta habari mimi mimi mainstream media nina access nazo since miaka 1970 na nimebahatika kwa sababu nilijitegemea kuwa nje miaka mingi sana tenq kwa hela yangu mwenyewe! Access ya mtandao since the early 90s. Eti unaniletea figures hizo ziko all over the internet na tovuti za serikali, Treasury Bonds za US walizonazo China ni USD 2 Trillions. Hizo ni sawa na 11% lakini still ni deni kubwa kwani China ni mdau wa tatu kwa ukubwa katika deni lote la taifa la USA hata hizo hela 9.8 trillion ni za wadau (American people) yaani ni inveatments za wananchi kama vile pensions na mfuko wa ustawi wa jamii na vitu kama hivyo; takwimu za 2011-2012.

Hata hivyo haiondoi ile dhana kuwa Serikali ya Marekani haina ubavu wa kuingia vita vyengine vikubwa zaidi katika kipindi hiki.

On 911 usinifundishe kutafuta habari zake kama wewe ushazoea kusikiliza habari.za TBC ambazo ni copy and paste news from Reuters.

Tukirudi kwenye fitna yote ya Ukraine bila.shaka hapa.nchi.za magharibi wamechemsha.

Hakika historia ni kielelezo cha hikaya na historia hujirudia yenyewe.

Mel Gibson mara moja akiwa amelewa alisema "Vita vyote ni kwa sababu ya Wayahudi"

Hivyo ni jinsi gani hii inavyohusishwa na matukio katika Ukraine?

Mwaka 1956 Israel waliogopa kwamba Urusi hwenda ikangilia vita vya Suez upande wa Misri. Wakati huo huo wananchi wa Hungary walihadaiwa (duped) kupandikizwa chuki dhidi ya Urusi wafanye uasi (popular uprising). Hungarians kwa ujinga waliamini (na waliambiwa) kwamba kama wangeweza kuwatoa Warusi kutoka nchini mwao, Uingereza na washirika wao zingeweza kuzuia Urusi kuto kurudi tena Hungary. Game halisi ilikuwa imepangwa pembeni nyuma ya mgongo Urusi eti wata negotiate kukubaliana na nchi za Magharibi ziache kuingilia kati katika Hungary na badala yake Urusi isitake kuingilia kati katika Misri. Ni nini kilichotokea kwa Hungarians ni maovu tu baada ya Warusi kurudi ambayo sasa ni historia.

Historia mara kwa mara hujirudia yenyewe.

Ukrainians (sehemu kubwa ya Ukraine ya leo ilikuwa imemegwa kutoka Hungary katika makubaliano maarufu ya Versailles (scramble for the Balkans)) sasa hivi wamewekwa rehani katika mchezo huo huo. Bila shaka Warusi wangali ambiwa wasijishughulishe na wawe mbali na Syria na Iran nao mataifa ya magharibi waiache Ukraine peke yake. Putin na timu yake outflanked US allies kwa mshangao vikosi vyake vimeingia katika Crimea nayo Crimea kutangaza uchaguzi (kura ya maoni) kwa ajili ya Crimea kisheria iweze kujiunga na Urusi.

Katika michezo hii ya kisiasa Urusi haijali kama kwa maslahi ya raia maskini wa Kiukreni lakini bali ni maslahi yake ya kuweka na kudhibiti naval base yake katika Crimea. Uchokozi (uvamizi) uloanzishwa ns Israel kwa kuisaliti (blackmail) Urusi umeharibu maisha ya Ukrainians na hata kukaribia kuingiza dunia na dhana ya kutokea vita vya WW3. Kifupi ngoma imewakalia rohoni wamarekani na vibaraka vyao vya Ulaya.
 
\

Kama kweli umeishi nje kwa "miaka ishirini kwa hela yako" (ingawa sijui kama unaamini kuwa kuna wanaoishi nje kwa hela ya wenzao) halafu na hutumii TBC kupata taarifa zako inawezekana kabisa ukawa unaishi katika nchi ambamo umefundishwa kutokuangalia mambo positively hasa pale inapohusu nchi za magharibi. Kama utakuwa unaishi katika nchi ambamo pamoja na mambo mengine huwa unanunua stocks au mutual funds ni lazima utakuwa una habari up-todate kuhusu deni la serikali ya Marekani kwa vile ndilo linalotoa dira kwa wall street, pamoja na markets nyingine zote za dunia. Wall street inapoanduka na masoko ya dunia nzima pia yanaanguka, ndio ukweli huo. Mwaka 2008 wakati Riemann Brothers ilipoanguka pale Wall Street nadhani unajua kuwa uchumi wa dunia nzima ulianguka pia. Kwa hali hiyo usidhani sote ni wapiga porojo kama wewe. Deni la China ni asilimia ndogo sana katika madeni ya marekani, lilipanda kidogo Januari mwaka huu lakini mwezi February wakaliachia na likanunuliwa na Ubegiji, na hivyo kurudisha namba ile ya zamani; amini usiamani ni juu yako lakini siyo robo - 25% . Exagerrations na distrotions zako zinafanya maoni yako kwenye mada hii yawe ni maoni yako, lakini siyo ukweli.

Iwapo unataka yaliyotokea zamani ndiyo yaamue mwelekeo wa dunia ya leo basi huwezekaniki; mwishoni utataka Ujerumani ipigwe vita na nchi zote za Ulaya kwa sababu ya matendo yaliyofanywa na Hitler Zamani. Ni kushindwa kuwa na mawazo neutral.

Nafurahi kuwa unajua kwamba Urusi hawajali maisha ya watu wa Ukraine kwa hiyo wako tayari kufanya lolote kwa sababu ya kituo chao cha kijeshi walichokubaliana mwaka 1994 kuwa kibaki pale Crimea kwenye bahari nyeusi. Hapo ndipo watu tunapopigania kuwa binadamu wote pamoja na wale wa Ukraine wana haki ya kuishi kwa amani salama bila kuvurugwa ma mataifa ya nje, siyo maisha yao yavurugwe kwa sabau ya kikoksi cha jeshi la Urusi ambacho kilikuwa hakijaguswa kutokana na mvurugano wao wa ndani. Urusi ilikuwa na haki ya kulinda na kutetea kikosi chake lakini siyo kuvuruga na kutishia amani ya nchi nyingine.
 
Putin anajifariji tu, nchi za magharibi ni wajanja sana kwa kupiga propaganda za siasa wakikuchukia wao ukiwa Rais wa nchi fulani utashangaa hata raia wako wanakuchukia
You are dreaming, Ulaya na ujanja wao wote na Uktraine wanaitegemea Urusi kiuchumi kwa asilimia zaidi ya 45. Na katu hawawezi kufanya lolote kwa maana watakuwa wanajizima wenyewe. Ukraine project imeanzishwa na EU on same terms kama Georgia Project na zote Putin aliibuka mshindi ( Leo hii Georgia ni minus Ossetia), na Ukraine is minus Crimea and very soon minus Doneskh. Chezea Putin. Obama ndiyo kabisa ubavu kwa Putin.
 
Hapa tunaongelea uwezo na ubavu wa USA kupigana Urusi na in context ni global war katika medani tofauti zilizo katika maeneo tofauti katika dunia.

Mimi nikiishi nchi yoyote hakuhusu wewe wala haihusiani na mimi kukubalia kila unachosema kwa sababu you think kuishi na wamagaharibi nawe utakuwa westernized naishi na hao wamagharibi wenyewe lakini sina haja kuwa westernized kufuatilia ukweli na kujuwa mambo kwa uhakika.
Tukiachilia mbali ya weather robo au 1/8 ya deni la USA kwa China tuangalie hali halisi ya uwezo wa serikali ya Marekani kifedha.
Katika nchi zote ulimwenguni na.mfano maskini kama Tanzania hujasikia hata siku moja Serikali ya Tanzania kufilisika. Lakini tushaisikia mara mbili serikali ya Marekani kufilisika na kushindwa na madeni kiasi kushindwa kulipa mishahara na ada nyengine za lazima kama mfuko wa ustawi wa jamii.

Na huo ndio mfumo wa Uchumi nchi za Magharibi inawalazimisha nchi za 'Dunia ya Tatu' kupitia IMF na WB ili kufuata matakwa yao.
Tanzania ni nchi tajiri ilikuwa katika NAM ilijikuta inwekewa vikwazo kila aina na hayo mataifa ya magaharibi kwa kukataa sera za IMF leo karibu miaka 40 bado inategemea donors na mikopo kwa sababu imeshuingia huo mtego.

Tukirudi Ukraine ni wa Ukrania wenyewe ndio wanataka kujiunga na Urusi sababu wengi wao ni warusi. Angalia TV zinazoonyesha mambo yanayotokea live uwanjani sio CNN, Jazeera na Fox TV. Sasa hivi mashariki na magharibi ya Ukrania kuna maandamano kwa maelfu na bendera za Urusi zinapepea. MR. WEST
 
Last edited by a moderator:
Russia na marekani hawawezi kupigana kamwe kwani wana walitiliana mkataba wa kutokupigana miaka ya nyuma ambao una dumu mpaka leo.
SHIN BET,
Huo mkataba unaitwa START leo umeshafutwa na Urusi leo hii:thumbup::thumbup:
 
Last edited by a moderator:
russia hajawahi kushnda katka siasa za kimataifa. Hzo ni mbwembwe tu marekani ikiamua kumkomalia hataweza kufanya chochote
 
Kichuguu,

Hapa tunaongelea uwezo na ubavu wa USA kupigana Urusi na in context ni global war katika medani tofauti zilizo katika maeneo tofauti katika dunia.

Mimi nikiishi nchi yoyote hakuhusu wewe wala haihusiani na mimi kukubalia kila unachosema kwa sababu you think kuishi na wamagaharibi nawe utakuwa westernized naishi na hao wamagharibi wenyewe lakini sina haja kuwa westernized kufuatilia ukweli na kujuwa mambo kwa uhakika.
Tukiachilia mbali ya weather robo au 1/8 ya deni la USA kwa China tuangalie hali halisi ya uwezo wa serikali ya Marekani kifedha.
Katika nchi zote ulimwenguni na.mfano maskini kama Tanzania hujasikia hata siku moja Serikali ya Tanzania kufilisika. Lakini tushaisikia mara mbili serikali ya Marekani kufilisika na kushindwa na madeni kiasi kushindwa kulipa mishahara na ada nyengine za lazima kama mfuko wa ustawi wa jamii.
.............................................

Propaganda ndizo zinazokufanya usiwe na mantiki katika unayoongea. Unapodai kuwa serikali ilifilisika ikashindwa kulipa watu mishahara ni kuonyesha kuwa hujui jinsi fedha za serikali ya Marekani zinavotolewa. Goverenment sutdown uliyosikia ni kuwa Bunge halikuidhinisha matumizi ya fedha siyo kuwa serikali ilikosa fedha; pesa zote zinazotumiw na serikali ya Marekani zinaidhinishwa na bunge.

Majitambo ya kudai umekaa nje ya nchi ukadahani kuwa ndiyo warrant ya kujua mambo ni wewe umeyaleta hapa. Huko ulikokaaa miaka 20 hakukusaidia kujua mambo ya dunia.

Kupigana vita siyo sifa katika dunia ya kisasa, ni kupoteza maisha ya watu bure, tena wengi waowakiwa hawana faida ya mohja kwa moja na vita hiyo kwa pande zote mbili zainazohusika. Huwa hakuna ushindi wa kivita usionedana na kupoteza maisha ya watu. Ninakushangaa wewe wakati Marekani inaingia vitani huko Iraki watu tulipiga kelele sana dhidi ya uvamizi huo pamoja na kuwa walijidai kupeleka kesi yao umoja wa mataifa; halafu eti leo taifa jingine linavamia nchi nyingine unashangilia.

Haya mzee Mr RUSSIA, wewe shangilia vita; nasikia huko kwenu hata wanamuziki wanapoimba mambo yasiyomfurahisha Mtukufu wanafungwa kimya kimya!
 
Mimi sishangilii vita, ninacho kwambia wewe kuwa Empire era zimepitwa, Ukraine na Russia sio Libya. Iraq na Afghanistan zimewatoa kamasi. Marekani hawezi kuwa kijibwa maji wa Myahudi akaleta ujinga wake Russia. Tena huyo Myahudi ashukuru kwa sababu anaoshindana na Putin ni Neo- Nazis wanaotaka kufanya ubaguzi. This time litajulikana la kumenya na kuchinja.

Na wewe unaekaa huko uliko kama una ki green card chako uchwara cha magendo utarudi kwenu Bongo uje kulima mahindi.

Kuna ardhi ya kutosha huku ya kukuendeshea maisha usisubiri Chadema kushika madaraka ndio urudi maana utasubiri sana. Chadema ni Antichrist entity haiwezi kushinda uchaguzi kirahisi rahisi. Kwanza kisu cha kuimaliza Chadema kiko Zanzibar na tutaichinja dakika za mwisho kikose usajili. Teh teh teh

Samahani Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Russia hawana soko kubwa la ndani wanaitegemea Ulaya haswa kwa kuiuzia ges asilia na mbao, kumbuka tu kwasasa unaweza ukaiona Russia ya Putin ikiwa Imara haswa katika siasa za nchi jirani lakini usisahau kuwa Ulaya(EU) huwa wana log term planning hata kama wakibadilisha viongozi kwa miaka 50 ijayo. Jiulize Russia bila Putin in 10 or 20 years to come watakuwaje? Je yale majimbo yanayopigani kujitenga kutoka Russia ambayo yana gesi asilia na misitu kwa wingi yataendelea kuwa Russia?

Back
Top Bottom