Rushwa NSSF Ilala imekithiri mnooo, Msaada wa Takukuru unahitajika

Rushwa NSSF Ilala imekithiri mnooo, Msaada wa Takukuru unahitajika

Jamani tunaomba msaada kwa mamlaka husika juu ya Uvundo huu uliokithiri Kwenye mfuko wa NSSF!Hali ni mbaya saana. Rushwa imekithiri mpaka imekuwa ndio sheria ya pale.

Ukienda kudai stahiki zako pale NSSF hakyamungu wale wafanyakazi pale kuanzia reception mpaka madirishani kote wanaomba rushwa waziwazi na ukisema huna utarudishwa mpaka utakata tamaa ya kufatilia stahiki zako!

Watu wanatoka mikoani ila kila siku wanazungushwa ili mradi utoe rushwa!!

Wale wahudumu pale dirishani anakuambia waziwazi umpatie pesa kidogo ili mambo yaende haraka [emoji27]!ukisema huna hela anakupa namba ya simu umtumie kwenye namba hiyo!hawajali jinsia!

Waliofanikiwa kupata mafao pale wana sema ukitaka kupata hela zako basi unagawana nao hela ndefu!kuna kijana wangu anafatilia million moja na nusu pale NSSF anaambiwa atoe Lakimoja 100,000/afanyiwe utaratibu!

Kila siku akifika pale na wenziwe wanaambiwa mtandao hamna!wiki ya 2 sasa anarudishwa bila sababu!

Waziri na mamlaka husika tunaomba kilio chetu wananchi kisikilizwe na kusaidiwa!hali ya rushwa NSSF inatishaaa!!
Sio hapo tu hata Benjamin Mkapa,wanatoa come back za wiki mbili mbili.Huku Ni kwa wale wa Pensheni.Kiukweli ukifatilia Sana na ukiwabana wanakupa vitisho.Katika Eneo ambalo Serikali ya Mama imefeli kabisa Ni NSSF au Kuna mafungu wanagawana huko juu.
Mama Samia fao la kujitoa lifanyie marekebisho,litakuchafulia serikali yako.
Mtu Hiari yake apewe pensheni au achukue hela yake .Hii sheria Ni uaji au sawa na ughaidi
 
Bora haTa huko Ilala Mwanza ndo kumeoza kabisaa,wafanyakazi wanakiburi sana, hawajali wateja NSSF inahitaji kufumuliwa.
 
Dada umeandika ukweli,niliombwa laki tano Mimi...bila Hela utasikia file sijui limefanya nini, sijui halijasigniwa wapuuzi Sana wale.
Sasa uliwapatia pesa hiyo? Ama zilipotoka ndio ukawapa? Nisaidie namie nasaka zangu
 
Zile zama zilikua ngumu mno na za kukatisha tamaa,halafu uzuri hiyo 6m nilitoka kwenye interest niliyopata kwenye pesa yangu kumbe unapolipwa unapewa na interest kulingana na pesa yako. Interest nilipata zaidi ya 7m so pesa yangu ilibaki kama haijaguswa na nikabaki na chenji ya interest juu
Kumbe kuna interest, so wanatoa 14.28% ya mafao unaongezewa.
 
Ni aibu kuongelea rushwa,Ila hamna namna ndio mifumo yetu,l mbinu niliyotumia Ni hii,niliwaomba Sana niwape zikitoka wakagoma,wanasema niwape250 nikawaomba nitangulize 150,wakakukubali kishingo upande,siku zimetoka wakanipigia simu oyaa kaangalie mzig,kuangali statement kweli zimo basi nikawajibu zimetoka nawatumia Sasa hivi,mpaka muda hi sijafika kwa wakala....wameshanipigia na kunitext na kunipa laana zote .....
Hahahahah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]...kumbe ukiwapa wanatoa aisee, na mie sijui nianze kwa nani nitoe tu rushwa maana hakuna namna, na chako ndio kinakuokoa, ila mie nikiwaahidi kuwapa nitawapa kweli. Sasa mie kila nikienda naambiwa status yangu inaonesha ipo kwenye michango. Hata sijui ndio wanamaanisha nini!
 
Hahahahah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]...kumbe ukiwapa wanatoa aisee, na mie sijui nianze kwa nani nitoe tu rushwa maana hakuna namna, na chako ndio kinakuokoa, ila mie nikiwaahidi kuwapa nitawapa kweli. Sasa mie kila nikienda naambiwa status yangu inaonesha ipo kwenye michango. Hata sijui ndio wanamaanisha nini!
Ukiwapa pesa haipiti miezi miwili mzigo inatoka kweli.....🤣🤣🤣150 nyingi bwana zinawatosha .....huyohuyo anaekupa majibu stutus yako Ipo kwenye michango muombe number ya Simu baadae mpange....Ila baada ya huu Uzi mtakuwa na Hali mbaya
 
Ukiwapa pesa haipiti miezi miwili mzigo inatoka kweli.....[emoji1787][emoji1787][emoji1787]150 nyingi bwana zinawatosha .....huyohuyo anaekupa majibu stutus yako Ipo kwenye michango muombe number ya Simu baadae mpange....Ila baada ya huu Uzi mtakuwa na Hali mbaya
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]150 na mafao yalikua ya kubamba au...asante kwa kunipa wazo, jumatatu nitaamka nae nimpange wallah
 
Kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba yake...nssf hata mimi nimejionea wana kamba ndefu sana! Kiukweli wanatesa sana kupata halali yako...kama umetoka mkoani lazima urudi nyumbani ukiwa huna hata ndala na hela huna...hili jambo liangaliwe kwa karibu sana...tofauti na hapo linatia doa kubwa kwa serikali yetu!!
 
Nilichojifunza mimi, NSSF ukiingia na majina yamepishana na jina la NIDA wakati usajili wa Nida Uliangalia vyeti na wewe usajili wa NSSF uliandika mwenyewe au kuandikiwa na majina kupishana hata herufi moja .ndio utahangaishwa sana.na utapeleka rushwa mahakamani ili urekebishiwe jina.
 
Na MAHAKAMANI kila mtu ana apa hata hawahakiki chichote ili mradi utoe pesa tu.
 
Kuna mtu alishawahi hoji hivi ile pesa za viapo mahakamani zinaenda wapi?
 
Wana huyo Mkurugenzi wao Mkuu Mshomba,ni mpumbavu na mjinga zaidi ya wapumbavu wote Duniani,ingekuwa vizuri kama Mh.Rais angeanza kulitumbua jinga kama hilo DG Mshomba
 
Mm naona hii taasisi tumudishie dr dau coz aliimudu sana hii
 
Huo ni ukweli kabisa haiwezekani watu wengi wanalalamika.
Kuna watu wamefuatilia mafao yao hadi wamekata tamaa wameamua kumwachia Mungu na wengine wamekufa bila kulipwa.
Yani huu ni wizi, mtu kaweka pesa yake inafika muda wa kumpa chake inakuwa kama anaomba msaada
Nchi imejaa wananchi mazuzu. Kazi kulalamika tu na kusubiri wengine wawatatulie shida zao. Sasa jamba kama hili ni la kumlalamikia rais wa nchi na kumuomba aingilie kati? Mawaziri na watu wa ngazi za chini wanafanya nini? Kwa nini kusiwepo na mfumo wa maalumu wenye mwongozo wa kulipa wahusika? Yaani wana-set time maalumu kuwa mtu kulipwa na ikizidi ule mda mfanyakazi aliyekuwa anashughulikia hayo mafao awajibike? Opps haya yote hayaji yenyewe bila wananachi kukinukisha!
 
Zile zama zilikua ngumu mno na za kukatisha tamaa,halafu uzuri hiyo 6m nilitoka kwenye interest niliyopata kwenye pesa yangu kumbe unapolipwa unapewa na interest kulingana na pesa yako. Interest nilipata zaidi ya 7m so pesa yangu ilibaki kama haijaguswa na nikabaki na chenji ya interest juu
Mkuu mbona umefunga Pm naomba tuzungumze Mkuu
 
Back
Top Bottom