Rushwa NSSF Ilala imekithiri mnooo, Msaada wa Takukuru unahitajika

Rushwa NSSF Ilala imekithiri mnooo, Msaada wa Takukuru unahitajika

Wezi sana wale jamaa mi kila siku ilikuwa wananikata hela nikiangalia salio hela inapungua walikuja kunipa nusu nyingine ikabaki nikawapotezea wana njaa wale.
 
NSSF iweje wafanyakazi wavune kwenye shamba ambalo hawajavuna. Taasisi zote kila inapofika suala la kwa mnufaikaji, lazima 10%.
 
Jamani tunaomba msaada kwa mamlaka husika juu ya Uvundo huu uliokithiri Kwenye mfuko wa NSSF!Hali ni mbaya saana. Rushwa imekithiri mpaka imekuwa ndio sheria ya pale.

Ukienda kudai stahiki zako pale NSSF hakyamungu wale wafanyakazi pale kuanzia reception mpaka madirishani kote wanaomba rushwa waziwazi na ukisema huna utarudishwa mpaka utakata tamaa ya kufatilia stahiki zako!

Watu wanatoka mikoani ila kila siku wanazungushwa ili mradi utoe rushwa!!

Wale wahudumu pale dirishani anakuambia waziwazi umpatie pesa kidogo ili mambo yaende haraka [emoji27]!ukisema huna hela anakupa namba ya simu umtumie kwenye namba hiyo!hawajali jinsia!

Waliofanikiwa kupata mafao pale wana sema ukitaka kupata hela zako basi unagawana nao hela ndefu!kuna kijana wangu anafatilia million moja na nusu pale NSSF anaambiwa atoe Lakimoja 100,000/afanyiwe utaratibu!

Kila siku akifika pale na wenziwe wanaambiwa mtandao hamna!wiki ya 2 sasa anarudishwa bila sababu!

Waziri na mamlaka husika tunaomba kilio chetu wananchi kisikilizwe na kusaidiwa!hali ya rushwa NSSF inatishaaa!!
Hapa ndipo mtu unapomkumbuka hayati Magufuli, Mama anafanya kazi lakini she's too lame anamtegemea sana rais aliyeshindwa kuongoza nchi (Kikwete).
 
Ndugu mdau inawezekana tuhuma zako ni za kweli Ila ungeweka na ushahidi ili aliyehusika ashughulikiwe maana Mimi ninaamini wapo wafanyakazi wengi wengine wa NSSF ambao hawafanyi vitendo hivyo.
 
Nauliza miaka na miaka contributions ya watu wanazichukua. Tukiomba HAKI zetu wanatutesa!!
There is something seriously wrong na hiyo scheme ya NSSF!!
Tatizo wale waajiriwa wa NSSF wanakuwa kama Hawajui zile pesa zimekatwa kutoka kwa mfanyakazi na mwajiri wa Mfanyakazi, wao wamepewa wakatumie kuzizalisha ili baadae wampe mfanyakazi muda utakapofika. Wao wanaona Kama zile pesa ni za NSSF. Inatakiwa NSSF watoe elimu kwa wafanyakazi wao, kuwa zile pesa sio za NSSF, ni za wafanyakazi waliowekeza pale. NSSF imepewa on TRUST tu.
 
Ilinilazimu kutoa 6m mafao yangu yaingizwe maana ilikua ndo kipindi wametunga sheria kuzuia fao la kujitoa. Kwa sababu hela yangu ilikua ndefu karibu 100m sikua na namna na kweli nilisaidika
 
Ndugu mdau inawezekana tuhuma zako ni za kweli Ila ungeweka na ushahidi ili aliyehusika ashughulikiwe maana Mimi ninaamini wapo wafanyakazi wengi wengine wa NSSF ambao hawafanyi vitendo hivyo.
Hayo mambo ya ushahidi ni mambo ya Polisi. Mtu ametoa Malalamiko, Kwa nini isifuatiliwe hiyo NSSF Temeke kuona kama ni kweli? Takukuru si wako kila Wilaya? Kwani NSSF hawana database kuona watu wamepeleka Lini maombi Yao ya kulipwa, kisha kuona ni Kwa nini yamechukua muda mrefu? Hiyo ni moja ya Kiashiria cha rushwa. Moja ya KPI ya NSSF inatakiwa iwe efficiency ya kuwalipa wastaafu. Sasa sijui KPI zao ni nini?
 
Ilinilazimu kutoa 6m mafao yangu yaingizwe maana ilikua ndo kipindi wametunga sheria kuzuia fao la kujitoa. Kwa sababu hela yangu ilikua ndefu karibu 100m sikua na namna na kweli nilisaidika

aisee!yaani wanaona kama ni msaada wanakupatia na sio haki yako kupata
 
Hayo mambo ya ushahidi ni mambo ya Polisi. Mtu ametoa Malalamiko, Kwa nini isifuatiliwe hiyo NSSF Temeke kuona kama ni kweli? Takukuru si wako kila Wilaya? Kwani NSSF hawana database kuona watu wamepeleka Lini maombi Yao ya kulipwa, kisha kuona ni Kwa nini yamechukua muda mrefu? Hiyo ni moja ya Kiashiria cha rushwa. Moja ya KPI ya NSSF inatakiwa iwe efficiency ya kuwalipa wastaafu. Sasa sijui KPI zao ni nini?

ukiona hivyo ujue na lenyewe ndio jizi la hukohuko NSSF hilo
 
Ilinilazimu kutoa 6m mafao yangu yaingizwe maana ilikua ndo kipindi wametunga sheria kuzuia fao la kujitoa. Kwa sababu hela yangu ilikua ndefu karibu 100m sikua na namna na kweli nilisaidika

Acha bana 6m??? 😡😡 Jasho lako??... ungewakamatisha Takukuru...
 
Duuh ngoja niwatonye wadau wangu wawe makini kwanzia sasa maana hio platform sio poa wapo pale kuna sister kaleta unoku huku kashamwaga mchele huku
 
Huo ni ukweli kabisa haiwezekani watu wengi wanalalamika.
Kuna watu wamefuatilia mafao yao hadi wamekata tamaa wameamua kumwachia Mungu na wengine wamekufa bila kulipwa.
Yani huu ni wizi, mtu kaweka pesa yake inafika muda wa kumpa chake inakuwa kama anaomba msaada
NARUDIA TENA MIMI NI MHANGA MWAKA WA PILI KUNA MTU NILIELEKEZWA KWAKE KWA KIMEMO. KUFIKA HANA CHA KUNIELEZA. ANAITWA ALLY MTOLEA LEO NIMEMTAJA KWA MARA YA PILI NDUGUZE KAMA WAPO HUMU WAKAMWAMBIE NA WAMKUMBUSHE SIJANYAMAZA KIMYA TU.
 
Yani pale kuna rushwa iliokomaa. Wakishakuoa rushwa wanaenda makanisani kutoa ushuhuda kuwa wameombewa maombi ya kajibu imekuja ela ambayo hawakuitegemea sasa wameanza ujenzi
 
Weka ushahi we dada
Af wewe@shinyangakwetu siku zako zinahesabika,siku usiyodhani utaangukia kwenye mikono ya sheria.
kuna uzi humu unamuomba mh.rais aangalie upya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii
umen'gaka kule utadhani umeombwa wewe.
Kilichokuwa kinaelezwa kule kimeletwa huku ila kwa njia nyingine bado unawahi na kejeli zako
tutawachukulia fedha za moto na usidhani utachomoka.
 
Back
Top Bottom