Rushwa NSSF Ilala imekithiri mnooo, Msaada wa Takukuru unahitajika

Rushwa NSSF Ilala imekithiri mnooo, Msaada wa Takukuru unahitajika

Jamani tunaomba msaada kwa mamlaka husika juu ya Uvundo huu uliokithiri Kwenye mfuko wa NSSF!Hali ni mbaya saana. Rushwa imekithiri mpaka imekuwa ndio sheria ya pale.

Ukienda kudai stahiki zako pale NSSF hakyamungu wale wafanyakazi pale kuanzia reception mpaka madirishani kote wanaomba rushwa waziwazi na ukisema huna utarudishwa mpaka utakata tamaa ya kufatilia stahiki zako!

Watu wanatoka mikoani ila kila siku wanazungushwa ili mradi utoe rushwa!!

Wale wahudumu pale dirishani anakuambia waziwazi umpatie pesa kidogo ili mambo yaende haraka [emoji27]!ukisema huna hela anakupa namba ya simu umtumie kwenye namba hiyo!hawajali jinsia!

Waliofanikiwa kupata mafao pale wana sema ukitaka kupata hela zako basi unagawana nao hela ndefu!kuna kijana wangu anafatilia million moja na nusu pale NSSF anaambiwa atoe Lakimoja 100,000/afanyiwe utaratibu!

Kila siku akifika pale na wenziwe wanaambiwa mtandao hamna!wiki ya 2 sasa anarudishwa bila sababu!

Waziri na mamlaka husika tunaomba kilio chetu wananchi kisikilizwe na kusaidiwa!hali ya rushwa NSSF inatishaaa!!
piga 113 tafadhali toa taarifa
 
Acha bana 6m??? 😡😡 Jasho lako??... ungewakamatisha Takukuru...
Ukiwa na shida utaelewa mkuu...na wao waliona mzigo mkubwa ndo maana. Na ilikua imeshashindikana kulipwa hela zangu so nilisaidika
 
aisee!yaani wanaona kama ni msaada wanakupatia na sio haki yako kupata
Niliisotea sana aisee,halafu nilikua naishi mkoani kwa hiyo go and return zilikua nyingi na ilikua imeshashindikana kwa taratibu za kawaida. Nilivyojicommit kuwapa 6m hata sikusumbuka tena kusafiri kila kitu wakawa wanafanya wao wananipa tu update. Siku wameandika chq wakanambia kesho mzigo utaingia na kweli mzigo ukaingia. Halafu pesa ilivyoingia nikawaza niwazulumu au niwawekee...nikajisemea as long as nilikubaliana nao na sijawahi mzulumu mtu acha tu niwawekee. Nikaenda bank nikafanya transfer nikawawekea. Hawakuamini,walinipigia mara mbilimbili kunishukuru maana walihisi ntawazulumu
 
Ukiwa na shida utaelewa mkuu...na wao waliona mzigo mkubwa ndo maana. Na ilikua imeshashindikana kulipwa hela zangu so nilisaidika
Pole sana, imeniuma sana.. jasho lako wamekula wahuni.. ila kwa kipindi kile naweza elewa your decision kuwapa huo mzigo.
 
Undeni grupu la WhatsApp wote mnaodai mfahamiane na mnapoenda kudai mnaalikana na kuandamana kwa pamoja na msiondoke mpaka kieleweke,iteni na waandishi wa habari,umoja ni nguvu.

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Dawa ni mdogo, unatoa taarifa takukuru, unawashikisha pesa za moto.

Shida inakuja unapogundua takukuru na wao wanataka kitu kidogo ili wakusaidie. [emoji85][emoji85]
Tunakoelekea ,habari ya watz ni wapole naona inaelekea kuisha.maana nyodo unazokutana nazo
hali ukijua anayekujibu anakula kwa sababu wewe ndo mleta pesa,unaweza kuchukua maamuzi ya mabaya mkagawana majengo ya serikali.
 
Hawa wa nssf hawatumii kamba za katani, wanatumia mipira ya manati,na hivyo huwezi kudetermine urefu wa kamba zao
Haki ya Mungu nimecheka hadi nimemwaga kahawa yangu, kwa hiyo vijana wanajipimia tu watakavyo.

Ndio ipo hivyo scratch their back they scratch yours too.
 
Undeni grupu la WhatsApp wote mnaodai mfahamiane na mnapoenda kudai mnaalikana na kuandamana kwa pamoja na msiondoke mpaka kieleweke,iteni na waandishi wa habari,umoja ni nguvu.

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
Yani sio kwamba waandishi au serikali haijui inajua sana. Mimi kaka yangu mkubwa kadai miaka miwili mfululizo, ikafika mahali kaona maisha yanakuwa magumu maana anafuatilia kitu ambacho hakuna dalili za kukipata amegive up. Wakati anafuatilia alikutana na watu wengi wanamwambia wewe unalalamika mwaka wa pili, sisi tuna miaka zaidi.
Wengine wagonjwa wanasaka pesa ya matibabu.
Yani now kaachana nayo.
Tanzania acha kabisa...
 
Dawa ni mdogo, unatoa taarifa takukuru, unawashikisha pesa za moto.

Shida inakuja unapogundua takukuru na wao wanataka kitu kidogo ili wakusaidie. [emoji85][emoji85]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ndugu mdau inawezekana tuhuma zako ni za kweli Ila ungeweka na ushahidi ili aliyehusika ashughulikiwe maana Mimi ninaamini wapo wafanyakazi wengi wengine wa NSSF ambao hawafanyi vitendo hivyo.

Rushwa ya NSSF nayo unataka ushahidi wakati wanachukua rushwa na kusumbua wanachama wa mfuko nchi nzima
 
Ndugu mdau inawezekana tuhuma zako ni za kweli Ila ungeweka na ushahidi ili aliyehusika ashughulikiwe maana Mimi ninaamini wapo wafanyakazi wengi wengine wa NSSF ambao hawafanyi vitendo hivyo.
Hao wasiofanya vitendo hivyo wafuatilie ili kundi la ''wachache" lisiwachafue,
ikitokea ofisi yenu ikanyoshewa kidole,waliosafi wanafanya utafiti na kuwaonya wenzao kishikaji
ili wajirekebishe,kinyume na hapo formula ni ile ile samaki mmoja ikioza wote wameoza.

Nakubaliana na wewe to some extent, kuna ofisi moja niliingia ya nssf mkoani kijana niliyekutana naye alinifanyia uungwana sana nikashangaa
tofauti na tunayokutana nayo huku Dar.
 
Asiyejua Maana hataukimwambia Maana (Ataona haina Maana - atakejeli tu)
 
Ndugu mdau inawezekana tuhuma zako ni za kweli Ila ungeweka na ushahidi ili aliyehusika ashughulikiwe maana Mimi ninaamini wapo wafanyakazi wengi wengine wa NSSF ambao hawafanyi vitendo hivyo.
Upo tz kweli? Na ushawahi kwenda NSSF? Wala hata haihitaji ushahidi
 
Mama yenu si amewaambia kila mtu ale kwaurefu wa kamba yake & ndio haya watu wanakula kwa urefu huo sasa
Hivi huyu mama alikuwa ana maana gani kusema hivyo? Tuna msubili 2025 tu muulize kwenye kampeni labda atatu dadavulia.
 
Af wewe@shinyangakwetu siku zako zinahesabika,siku usiyodhani utaangukia kwenye mikono ya sheria.
kuna uzi humu unamuomba mh.rais aangalie upya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii
umen'gaka kule utadhani umeombwa wewe.
Kilichokuwa kinaelezwa kule kimeletwa huku ila kwa njia nyingine bado unawahi na kejeli zako
tutawachukulia fedha za moto na usidhani utachomoka.
Nyumbu
 
Sehemu yoyote ukiwa mzito, mambo hayaendi; ndivyo ulimwengu ulivyo....ndio maana hata madhabahuni tunahimizwa kutoa, ili kupata huduma ya kiroho
 
Ningepata hyo connection ningetoa pesa zangu TU.!!
Kuna Dada mmoja alipewa Namba na jamaa pale ndani nikamkimbilia Dada anipe Namba aligoma katakata.
Yani angenipa leo hii ningekuwa nimeshapandisha vyumba viwili vya kulala na sebule pia.
 
Back
Top Bottom