Rushwa inayoendelea ktk eneo la ukaguzi wa magari (Transit Goods)Pale Vigwaza eneo la mzani ni ya kutisha!

Wenye magali nyie ni wakunyonywa tu....kuanzia bandarini,tra mpaka barabarani...maana nyie MNA mahela mingi mingi
 
Hii ni aibu kwa askari wa usalama barabarani!

Kwa nilichokishuhudia leo eneo tajwa ni jambo la hatari!Askari wetu wa usalama barabarani wamegeuza pale ni km kitega uchumi wao.

Kuna dereva mmoja wa kinyaRwandwa tatizo ilikuwa ni kreki tena ndogo tu ya kioo amepigwa 20000!Hii ni hatari!

Kosa la kuelekezwa mtu anadai rushwa tena kwa amri;AIBU!Mgeni yule aliishia kufyonza na kutamka kwamba anamuachia Mungu.

Zaidi ya yote kwa mda wote niliosimamishwa pale tena kwa kosa la kuelekezwa kabisa nilishuhudia maovu mengi!Askari wetu wanachukua rushwa pale tena kwa kufosi na hatmae hupongezana kwa kugongeana 5!

Takukuru hebu tembeleeni eneo lile tena shirikianeni na madereva wale wa masafa marefu hakika mtashuhudia ujinga huu niusemao hapa.

Nanyi askari wetu hata km ni pesa ya kiwi pale mmezidi!
Naamini kabisa kwamba hicho ulichoshuhudia ni sehemu ndogo sana ya rushwa inayoendeshwa na polisi barabarani.

Mwezi uliopita nilisafiri toka Arusha kuja Dar. Nimejionea rushwa ya wazi inayofanyika kati ya polisi na madereva. Njiani kuna vituo vingi vyenye askari na kila wanaposimamisha gari, utagundua kwamba wanafahamiana na madereva. Madereva wamekubaliana na hali hiyo bila kupenda.

Nilipomuuliza mmoja wa madereva kwa nini wanafnaya hivyo, jibu lake ni kwamba akigoma basi kila sehemu atacheleweshwa kwa makusudi. Watakagua tairi, watakagua buti, wataomba abia mwenye begi hili au lile, nk. yote hayo ni kuhakikisha kwamba unachelewa kufika uendako. Wakati unakaguliwa hayo, magari mengine yatapita kwa uhusiano wa aina hiyo. Kwa ujumla rushwa barabarani ni tatizo.
 
Madhara ya rushwa wanazodai Traffic Police barabarani ni makubwa kupita maelezo. Ni kitu kinachojenga taswira kwamba rushwa ni sehemu ya kawaida ya maisha Tanzania.

Kipimo cha kwanza cha mgeni cha kuona kama nchi ina utawala wa kisheria (rule of law) ni tabia za polisi barabarani. If law officers are corrupt then you can be sure the rest of the public service machinery is corrupt.

Ajabu kubwa ni kwamba hata watu wema wanaamini sasa ni sawa kuwapa Traffic Officers fedha kidogo wakuache uendelee na safari yako. Tabia chafu kama hizi zimekubalika na wengi.

Bahati mbaya sana hata Rais amewezesha tabia hii ya kutoa na kupokea rushwa kwa polisi ikubalike. Ameiita ni kutoa fedha za kubrashi viatu. That is most unfortunate.

Ukichekee nyani utavuna mabua.
 
Nimempa trafic karatasi nimeikunja vizur nikamfinyia nikamwambia afande kamata kumi hiyo nawai wala hajakagua' mimi ndio mchezo wangu huo naandaa makaratas mekundu ndio naanza safar wakinipiga mkono nawawai kabla hawajaanza kukagua gari
 
Nimempa trafic karatasi nimeikunja vizur nikamfinyia nikamwambia afande kamata kumi hiyo nawai wala hajakagua' mimi ndio mchezo wangu huo naandaa makaratas mekundu ndio naanza safar wakinipiga mkono nawawai kabla hawajaanza kukagua gari

Ila inabidi tujenge taswira kwamba rushwa ni haramu. Hatuwezi kuigeuza mchezo. Kila anayempa Traffic Officer hata elfu mbili tu afahamu anashiriki kudidimiza taifa. Hizi tabia za rushwa na udokozi zinafanya tudharauliwe sana.

Kidini pia tukumbuke ni dhambi ya mauti kutoa au kupokea rushwa. Poorly formed consciences might not realize this but it is objectively evil to receive or give a bribe.
 
Traffic wanahusika vipi na mizani?Labda tuanzie hapo
Traffic wanakuwepo kwenye mzani ili kumuelekeza driver husika kuweka gari sawasawa inavyotakiwa kukaa kupimwa,madereva wengine ni wahuni{hasa hawa wa malori}huwa wanaichezesha gari jinsi wanavyojua wao yule msomaji wa weight mule ndani hawezi kujua kama chombo imechezezwa ama lah...pia mbele kidogo unapotoka ktk kila mzani unakuta kizuizi cha askari nadhani hawa ndiyo wanaozungumziwa hapa,nimesafiri leo kutoka Moshi to Dar nimeona live konda wa kike wa bus nililopanda akimkunjia askari elf10 japo sikuona mistake yoyote iliyofanywa na dereva ila kwanini alimpa?sijui!!
 
Mara nyingine rushwa inatokana na sisi wananchi wenyewe.
Mtu anafanya kosa halafu hataki kuwajibika kwa kosa lake.
Kama trafiki akikuonyeha kosa ambalo lipo kisheria kwa nini mtu anatoa rushwa badala ya kulipa faini?

Nadhani ifikie mahali kama makosa ya barabarani ni kwa ajili ya kusamehewa basi sheria itamke wazi kuwa kosa hili lisamehewe jambo ambalo litakua sio kosa tena. Siamini kuwa serikali iliweka askari barabarani kwa ajili ya kukamata na kusamehe.Watasehe wangapi mana kila mtu anatamani asamehewe.
Wale nao ni binadamu.
Haiwezekani mtu afanye kosa kwa makusudi halafu amtupie lawama trafiki.
Pamoja na madhaifu yao trafiki lakini wananchi tuwajibike na kama tuna makosa basi tuwajibike ili kuwaondolea lawama.

Mh. Rais anaakili sana , aliposema pesa ya brashi watu walifikiri kuwa anahalalisha rushwa lakini kwa aliongeza morali wa kukamata wa trafiki. Na aliona pia kuwa haiwezekani ukaanza kuwawinda trafiki kwa sababu ya makosa ya makusudi ya watu ambayo anapaswa alipe faini kwa kosa lake na sio kuomba kusamehewa.
Mana hapo linapokuja suala la kuomba omba ndipo panapotokea suala la kuanza kubageini rushwa.
Kumbe mtu angelipa faini angekua amepunguza matukio ya rushwa.

Rushwa itaisha pale ambapo watenda makosa watakapoisha au watakapoamua kuwajibika kwa makosa yao.

Wananchi tunatakiwa tupambane na wale wenzetu wanaofanya makosa barabarani na kuwakemea kwa nguvu zote. Trafiki wakikosa makosa patakua hakuna huo ushawishi wanaoshawishiwa kupokea.

Siku zote mvunja sheria anashawishi kusamehewa kwa rushwa.

Mimi kwa kweli kama nina kosa basi ama nitalipa faini au nitaomba radhi au brashi.
Siwezi kufanya kosa halafu nimfukuzishe baba au mtoto wa mtu kazi kwa kosa langu mwenyewe. Hii ni dhambi kubwa.
Kosa langu halafu nilifanye liwe jambo la kutafuta umaarufu. No kila mtu apambane na hali yake.

Nadhani rushwa anayoikemea sana mkuu wa nchi ni ile ya kubambikia watu makosa.
Aloo wale wanaobambikia watu kosa ni jambo lisilovumilika mbinguni na duniani.
Lakini kuambiwa kuwa una kosa hili na unatakiwa kulipa faini elfu 40 ,halafu kwa hekima ukashawishi na kukubaliwa kutoa elfu tano utakua mtu wa ajabu kama utalalamika. Kusamehewa bure kabisa nako ni aibu mana wazee wa watu wanaungua jua ,na moshi wa magari unasababosha kansa na kifua kikuu.

Kwa ufupi tujikite kwenye kuwakemea na kuwalaumu zaidi wale wanaotenda makosa ili kupunguza rushwa.
Mfano mwendo kasi dunia nzima ndio chanzo kikuu cha ajali lakini tunashindwa kuwakemea madereva wanaoendesha mwendo kasi badala yake tunawatetea na kutaka wasiadhibiwe ila wasamehewe tu huku tukiwaona wale wanaowadhibiti kuwa ni wabaya kwa sababu tu kuna kuwaza pesa zinazowatoka kwa faini au hata kumaliza juu kwa juu.
Pesa ni pesa tu ikimtoka mtu inamuuma sio sawa na kutoka bure.

Kama trafiki atambambikiza mtu kosa kwa lengo la kupata rushwa kwa kweli hiyo ni dhambi kuu.
Biblia na mkuu wa nchi wanasema juu ya askari kuwa wasiwashtaki watu kwa uongo.
 
Solution ya hilo swala na mambo mengine ya hovyo yanayoendelea hapa nchini ni moja tu, kila baada ya miaka mitano tuwe tunabadili utawala.
 
Back
Top Bottom