Kwa madereva na watumiaji wa IT (IN transit)

wakukurupuka1

JF-Expert Member
Feb 17, 2023
525
1,187
IT, hili neno linaweza kuwa na maana nyingi lakini hapa nataka kumaanisha IN TRANSIT kwa maana ya zile gari zinazopelekwa nchi za jirani kupitia bandari yetu ya Dar es salaam nk.

Hizi gari zimekuwa moja ya usafiri wa tuliowengi pale tunapopata safari za dharura kwenda makwetu, huwa zinatusaidia sana japo wengi wetu hatujajua hatari yake.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye point kuwa baadhi ya hizi gari au usafiri huu ni moja kati ya vyanzo VIZURI vya ajali za barabarani na hasa nyakati za usiku na askari hawatangazi sana matukio ya ajali za hizo gari kwani zinakuwa zimepita kwenye check points wanazozisimami.

Iko hivi, utakuta dereva au madereva hao baadhi (natumia neno baadhi kwa makusudi ili kuepuka kushambuliwa) huwa wanapata tenda hiyo let say kupeleka hizo gari kwenye exit points kwa maana ya mipakani, sasa ukute madereva wa 3 wamepata tenda ya kupeleka gari kumi au kumi na tano hivi pengine zaidi au pungufu, wanachofanya wanazitoa hizo gari wanazipaki majali hapa hapa tuseme Dar wanachukua mbili au tatu kulingana na idadi yao wanaanza kuzikimbiza kwenda nazo mpakani let say Tunduma Kasumulu Rusumo nk.

Na mara nyingi huwa wanapenda kusafiri nyakati za usiku kukwepa askari na tochi za mchana, na lengo lao kwa mfano wakienda Tunduma wana target wafike asubuhi kunapambazuka halafu waache hizo gari wadandie usafiri mwingine tena wa kurudi Dar waje wachukue gari nyingine tena hivyo mpaka wamalize, ili mradi tu wapate pesa nyingi, lakini ujiulize hivi dereva wa namna hiyo akipata ajali pengine kutokana na uchovu wa safari za mfululizo atasema ajali hazina kinga!?

Kama haitoshi madereva hawa baadhi yao huwa wanapenda sana kutumia vinywaji fulani kama enejaiza au booster wenyewe wanaita ,je kuna usalama kweli hapo, lakini kama haitoshi baadhi ya madereva wa hizo IT ni wale ambao hawana UZOEFU wa kutosha hata kidogo its ok ndo wanaanza kupata UZOEFU lakini ilitakiwa wawe chini ya usimamizi wa wenye uzoefu.

Hizi IT zinasababisha sana ajali lakini polisi au hata niseme serikali kama vile hawalioni wao wanangoja tu kutangaza matokeo, utasikia uzembe wa dereva, MWENDO KASI, KUTAKA KULIPITA GARI LINGINE BILA KUCHUKUA TAHADHARI na mengi ya namna hiyo.

Askari wa usalama barabarani anaweza asione kitu chochote lakini sio gari la IT, hata liwe mbali kiasi gani na liwe na rangi ya aina gani atalitambua tu maana akishaiona tu IT anajua chambichambi tayari.

Wito wangu, tujitahidi kubaini vyanzo vya ajali badala ya kusubiri tutangaze matokeo, kwanini pasiwe na utaratibu kuwa it zote zitengewe siku ya kusafirishwa mfano inaweza kuwa mara mbili au mara tatu kwa wiki na kwa kuripoti kwenye check points maalumu na kwa muda maalum,kwa kifupi lazima ziwe controlled ,ziwe na muda wa kusafiri kutoka point moja hadi nyingine na si vinginevyo, nawaza tu.

Angalizo: Baadhi ya IT
Onyo: Unayetumia IT kama usafiri wa kuaminika hukatazwi lakini kuwa makini

Credit: Thomas Mwamfupe
 
Solution wa hili ni kuanzishwe route za usiku,MTU unakuwa unapata emergency unatakiwa kusafiri muda huo huo unakwenda stendi hamna gari-utafanyaje sasa.
 
Nimewahi kusafiri na magari ya IT mara mbili na nakubaliana na wewe kuwa wana mwendo wa kutisha.

Nilichogundua ni kuwa, hawa madereva wa IT ni watu wazoefu kwenye hizo fani na wanafanya kazi zao kwa malengo! Ajali kama zilivyo ajali nyingine hutokea na sababu zake ni zile zile tu za kibinadamu kwa asilimia 80.
Mara ya kwanza nilisafiri na IT moja kutoka Dodoma hadi Kahama, Kutoka saa sita usiku, asubuhi saa moja niko Kahama.
Safari ya pili nilipata IT kwenye border ya Rusumo saa sita mchana saa tisa na nusu niko Kigali na bado niliwahi niunganisha safari.
Kwa ujumla IT zinasaidia sana pale usafiri wa umma unapozingua na mtu una safari ya haraka. 😆
 
IT, hili neno linaweza kuwa na maana nyingi lakini hapa nataka kumaanisha IN TRANSIT kwa maana ya zile gari zinazopelekwa nchi za jirani kupitia bandari yetu ya Dar es salaam nk.

Hizi gari zimekuwa moja ya usafiri wa tuliowengi pale tunapopata safari za dharura kwenda makwetu, huwa zinatusaidia sana japo wengi wetu hatujajua hatari yake.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye point kuwa baadhi ya hizi gari au usafiri huu ni moja kati ya vyanzo VIZURI vya ajali za barabarani na hasa nyakati za usiku na askari hawatangazi sana matukio ya ajali za hizo gari kwani zinakuwa zimepita kwenye check points wanazozisimami.

Iko hivi, utakuta dereva au madereva hao baadhi (natumia neno baadhi kwa makusudi ili kuepuka kushambuliwa) huwa wanapata tenda hiyo let say kupeleka hizo gari kwenye exit points kwa maana ya mipakani, sasa ukute madereva wa 3 wamepata tenda ya kupeleka gari kumi au kumi na tano hivi pengine zaidi au pungufu, wanachofanya wanazitoa hizo gari wanazipaki majali hapa hapa tuseme Dar wanachukua mbili au tatu kulingana na idadi yao wanaanza kuzikimbiza kwenda nazo mpakani let say Tunduma Kasumulu Rusumo nk.

Na mara nyingi huwa wanapenda kusafiri nyakati za usiku kukwepa askari na tochi za mchana, na lengo lao kwa mfano wakienda Tunduma wana target wafike asubuhi kunapambazuka halafu waache hizo gari wadandie usafiri mwingine tena wa kurudi Dar waje wachukue gari nyingine tena hivyo mpaka wamalize, ili mradi tu wapate pesa nyingi, lakini ujiulize hivi dereva wa namna hiyo akipata ajali pengine kutokana na uchovu wa safari za mfululizo atasema ajali hazina kinga!?

Kama haitoshi madereva hawa baadhi yao huwa wanapenda sana kutumia vinywaji fulani kama enejaiza au booster wenyewe wanaita ,je kuna usalama kweli hapo, lakini kama haitoshi baadhi ya madereva wa hizo IT ni wale ambao hawana UZOEFU wa kutosha hata kidogo its ok ndo wanaanza kupata UZOEFU lakini ilitakiwa wawe chini ya usimamizi wa wenye uzoefu.

Hizi IT zinasababisha sana ajali lakini polisi au hata niseme serikali kama vile hawalioni wao wanangoja tu kutangaza matokeo, utasikia uzembe wa dereva, MWENDO KASI, KUTAKA KULIPITA GARI LINGINE BILA KUCHUKUA TAHADHARI na mengi ya namna hiyo.

Askari wa usalama barabarani anaweza asione kitu chochote lakini sio gari la IT, hata liwe mbali kiasi gani na liwe na rangi ya aina gani atalitambua tu maana akishaiona tu IT anajua chambichambi tayari.

Wito wangu, tujitahidi kubaini vyanzo vya ajali badala ya kusubiri tutangaze matokeo, kwanini pasiwe na utaratibu kuwa it zote zitengewe siku ya kusafirishwa mfano inaweza kuwa mara mbili au mara tatu kwa wiki na kwa kuripoti kwenye check points maalumu na kwa muda maalum,kwa kifupi lazima ziwe controlled ,ziwe na muda wa kusafiri kutoka point moja hadi nyingine na si vinginevyo, nawaza tu.

Angalizo: Baadhi ya IT
Onyo: Unayetumia IT kama usafiri wa kuaminika hukatazwi lakini kuwa makini

Credit: Thomas Mwamfupe
Umeandika kuhusu IT na ukweli wake, sasa kapande magari ya magazeti tuone kama haujafuta hiyo Post ya IT endapo utafika salama.
 
Ha haa. Acha uoga.
Hakuna raha kama kusafiri usiku. Hasa wewe ndio ukiwa kwenye usukani. Muhimu kama uwezo wako ni mdogo, tafuta dereva mzoefu ukae nyuma yake umfuatishe...
 
Nilijua hao madereva huwa wa kampuni na tenda zinapitia kwa kampuni.

Sijawahi kukutana na trekta la IT nafikiri hata hizo gari ndogo ni heri kubeba kwenye malori tu.
 
Nina uzoefu wa kuendesha gari za IT huu ni mwaka wa 6. huwa tuna kimbia speed ila njia tuna ijua ipasavyo.

Pia huwa hatukimbii tu ili mradi tuna kimbia.

speed 140 au 160 kph kwenye sehemu tunazo zijua zimekaaje kimiundo mbinu. Achana na stori za watu wana kudanganya ajali sijui nini... Ajali ni kweli huwa zina tokea lakini ni kama ajali zingine tu kawaida.

Pia wanao pata jali wengi ni wale wa levi, wasio wazoefu wa high way, wanao lazimisha kusafirisha gari mpaka 5 kwa week yaani aende Tunduma leo kesho ageuke jioni arudi na gari tena hii ni hatari lazima ulale kesho uanze mdogo mdogo.
 
Back
Top Bottom