Rushwa Bungeni: Kamati ya bunge ya Nishati na Madini yavunjwa

January Makamba anahusika kwa kuwa yeye ndio aliasisi utaratibu wa kuiingilia Wizara ya Madini na Nishati iliyokuwa chini ya Mhe Wiliama Ngeleja pamoja na menejimenti ya Tanesco na madudu haya yamefanyika wakati wa kipindi chake. Ikizingatiwa kuwa Mhando ni homeboy wa Makamba ililazimika Zitto ambaye ni rafiki yake January Makamba kimaslahi kubebeshwa zigo la kumtetea Mhando blindly. kama kweli Bunge limataka kujisafisha ni lazima uchunguzi huo umhusishe Janaury Makamba. Inafahamika kuwa wote wawili walikuwa katika mradi wa kutafuta fedha kwa ajili ya harakati za kugombea urais katika vyama vyao
kaazi kweli kweli...
 
Kuvunja kamati haitoshi, ni lazima tunajue wasaliti kwa majina yao. Spika asitake kutuaminisha kuwa kundi zima la kamati limeshirikiana kufanya makosa. Atajwe huyo, tumshughulikie.
 
Mwenyekiti wa hii kamati ni Seleman Zedi, miongoni mwa wajumbe wa hii kamati ni Sara Msafiri (mbunge Viti maalum UVCCM) Munde Tambwe (viti maalum CCM), Chirstopher ole Sendeka, John Mnyika (CDM). Hii kamati ilikuwa inaongozwa na Naibu waziri wa sayansi na Technolojia Januari Makamba kabla ya reshufle ndogo iliyofanywa na JK Mwanzoni mwa mwezi June

Selemani Zeddy atawajibika kisiasa kwa sababu yeye ndie Mwenyekiti wa hii kamati, Wanaodaiwa kuivuruga TANESCO ni Zitto Kabwe na January Makamba, wakishirikiana na Munde Tambwe na Sara Msafiri. Sina nia ya Kumsafisha Zeddy but jamaa ni Clean, namfahamu since akiwa ZAIN. Haya madudu aliyoyasema Prof. Mulongo yalifanyika January Makamba akiwa ni Mwenyekiti.

Munde ni fisadi mkubwa aliwahi kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na Manispaa ya Tabora kwa ubadhirifu wa Shs 987,214,000/= akiwa ni karani idara ya uhasibu manispaa ya Tabora.

Nashauri ni vizuri kamati ya uongozi ya bunge uwe unawafanyia wajumbe wa kamati vetting kabla ya uteuzi
vetting wapi?bongo?tena hata kusaidia haitasaidia,kwasababu pesa aliyoipata huko ndo imemsaidia kupata cheo kingine cha juu,kama wanavyosema,wengine wanakusanya kwa madaraka ya juu zaidi,wengine urais nk,tegemea na level yako.Ndo bongo hiyo yenye kuendeshwa kisanii,yani mabaya ya ubepari yakitekelezwa bila wasiwasi huku kwenye makaratasi ni ujamaa.Halafu ngoma inaenda tu kama kawa na watu wanajadili.Kuendelea kujadili haya mambo sometimes ni kumwunga mkono chizi na kucheza naye kwenye matope ukitegemea utaweza kumwondoa kwenye hilo tope kwa njia hiyo.Dawa ni kuanza upya,sioni kabisa ni kivipi tutaondoka kwenye haya matatizo kwa njia hizi.2015 is a most important year yet on our nation's calender.
 
Nafikiri January aanze kujiudhuru huo unaibu ili achunguzwe hili la kamati aliyoiacha na mauchafu. Inaonekana yeye ndio aliyaacha haya yote
 
Duh tutapona kweli sisi Watanzania wa Mungu? Tunawatuma wakatuwakilishe na kukemea vitendo viovu wao wanaenda kula! Bongo kweli kama sifongo na chemsha bongo kabla hujapagawa. Bongo Dar es Salaam kila mtu mjanja aliyeuziwa dhahabu feki yeye katoa noti feki ngoma droo. Bongo watu wanapenda hela wanatamani wangezaliwa Burunei kila mtu anataka vijisenti. Wawakilishi wanakula toka kwa waliotumwa wawasimamie na pia wanakula toka kwa waliowatuma.

Naona tumefika patamu sasa kilichobaki ni bunge lote kuvunjiliwa mbali manake tetesi za rushwa ndani ya BUNGE LETU TUKUFU ZIMEZIDI. Kwa hali hii sipendi kusikia mtu akisimama na kusema Mh. SPIKA NAPENDA KULIAMBIA BUNGE LAKO TUKUFU.....Wamejivua utukufu!
 
Nafikiri January aanze kujiudhuru huo unaibu ili achunguzwe hili la kamati aliyoiacha na mauchafu. Inaonekana yeye ndio aliyaacha haya yote

JF iko juu manake kuna mambo yanaibuka na tayari yalishasemwa humu kwa kina kinagaubaga bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno!
 
HAPA KUNA UBABAISHAJI KAMA ISSUE NI TUHUMA ZA RUSHWA VIPI KAMATI YA MREMA AU KWA KUWA HOJA ILITOLEWA NA KAFULILA WA UPINZANI Bi KIROBOTO AKAIPOTEZEA?
 
mkuu nina hofu sana na vitisho ambavyo amekuwa akipata hata leo humu bungeni jamani prof ni kichwa aisee hata simba chawene na mwenzie wako vizuri hofu wasije tu waka mfanya kama mwakyembe walivyo mfanya.
usemacho ni kweli,lakini nini nafasi ya January kwa sasa,ambapo mengi yametokea yeye akiwa mwenyekiti,,,,nishati na madini ni JINAMIZI:A S-baby:
 
Prof Muhongo na timu yake wamefanya kazi nzuri sana kwa niaba wa Watanzania wote.
 
Kwa wenye akili,maneno yako ni kweli. Kama alivyosema mkuu Mkandara hii ni vita baina ya makundi hasimu kuimiliki wizara hii,sababu kubwa ikiwa ni uchaguzi wa 2015.
kweli?????????????????me siamin,mi naamini sababu ni UROHO,KUMBUKA URANIUM MAFUTA NA GAS VIPO NJIANI
 
Hivi huoyo khalfani aeshi aliyekuwa mbunge wa sumbawanga alichaguliwaje?
Huyu jamaa mie ninavyojua utajiri wake wa malori aliupata baada ya kupiga dili na kuiba pembejeo za kilimo za wananchi wa sumbawanga lakini walivyo wapumbavu wakamchagua kuwa mbunge kwa sababu aliwahonga baiskeli.
Jmaa alienda london mwezi wa tano kununua vifaa vya kupigia kampenio kama vile maspika na vitu vinginevyo ili akiruhusiwa kugombea ajaribu tena. wote tunajua asingekuwa pinda huyu alikishindwa kwa chadema lakini matokeo yalichakachuliwa.
jamaa ni muhuni muhuni tu nashngaa sana kuona mtu wa mitaani leo anakuwa mjumbe wa kamati ya nishati??? kweli nchi yetu imekwisha. Hebu kama kweli serikali inaakili timamu ichunguze utajiri wa aeshi na kupotea kwa pembejeo za wakulima sumbawanga
 
Back
Top Bottom