Rushwa Bungeni: Kamati ya bunge ya Nishati na Madini yavunjwa

cartura for god sake nitake radhi. Hivi nitakitoa kwa watu wangapi, mara ngapi ili nipate nini?
Basi ni heri nikitoe bure tu kwa yeyote yule ninayejiskia kuliko kukitoa kwa gharama ya uongozi, ama cheo ama pesa. Hivi my my professional excellency and competency can not sell me???
Kweli Mkuu gfsonwin
manake ukitoe kwa Walimu O'& A-Level, kwa ma lecturers na baadae kwa mwajiri na viongozi kitalegea 'nut' zake.

Ukichukulia kuwa watumiaji wengine wanakuwa na ile "nitakipata lini tena"

Kisiwe kigezo cha mafanikio!. Sifa na Jhudi za mtu ndiyo viwe vigezo!, mh...! lakini kwa viongozi wetu nina wasiwasi.
 
Mkuu soma posts zilizotangulia. ZZK sio mwenyekiti wala mjumbe wa kamati ya nishati. Ya kwake ni POAC (mashirika ya umma), ambayo kikanuni ni oversight, na lazima mwenyekiti wake atoke opposition

kwani tanesco sio shirika la umma?? au ni shirika la nini...i thought pia lilikua chini ya uangalizi wake ndo maana wakawa wanamhisi na yeye yuko involved...anyways!!
 
kwani tanesco sio shirika la umma?? au ni shirika la nini...i thought pia lilikua chini ya uangalizi wake ndo maana wakawa wanamhisi na yeye yuko involved...anyways!!

Hesabu za Tanesco hukaguliwa na Kamati ya Zitto. Suala la misumari na mbao za kichina toka kwa Chief mkwawa zinatakiwa zihojiwe na kamati ya Zitto. Zito hachomoi hapa, ameliibia taifa vya kutosha. Huwa anatumia tactic ya kuwa MBOGO ili aonwe kwa uharaka. Zinaanza kumtokea puani sasa. Lazima azitapike
 
January Makamba anahusika kwa kuwa yeye ndio aliasisi utaratibu wa kuiingilia Wizara ya Madini na Nishati iliyokuwa chini ya Mhe Wiliama Ngeleja pamoja na menejimenti ya Tanesco na madudu haya yamefanyika wakati wa kipindi chake. Ikizingatiwa kuwa Mhando ni homeboy wa Makamba ililazimika Zitto ambaye ni rafiki yake January Makamba kimaslahi kubebeshwa zigo la kumtetea Mhando blindly. kama kweli Bunge limataka kujisafisha ni lazima uchunguzi huo umhusishe Janaury Makamba. Inafahamika kuwa wote wawili walikuwa katika mradi wa kutafuta fedha kwa ajili ya harakati za kugombea urais katika vyama vyao

Wewe WATANABE lazima umetumwa, naona unajaribu sana kumuunganisha January Makamba kwenye hii issue lakini hautafanikiwa.

Wengine someni maelezo haya:
---------------------------------------------------------------------------------------

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambaye awali alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, alisema ni sahihi kamati hiyo kuvunjwa, kwa sababu imekithiri vitendo vya rushwa.

“Wakati mimi nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, vilikuwapo vitendo vya rushwa, si kwa wajumbe wote ila baadhi yao walikuwa vinara, kutokana na hali hiyo nilivipigia kelele na nimepata shida sana kupambana navyo,” alisema na kuongeza:

“Tuliweka msimamo ndani ya Kamati kwamba vitendo hivyo havikubaliki hata kidogo na ilifikia hatua nilienda kuwashitaki kwa Spika, Anne Makinda, kuhusu tabia ya baadhi ya wajumbe kupokea rushwa na alikubaliana na mimi kisha naye alikemea vitendo hivyo.

“Kusema ukweli tulifanikiwa kuvidhibiti kutokana na msimamo wa pamoja tuliokuwa nao. Baadhi ya wajumbe wa kamati wakalalamika kwanini nimeenda kusema kwa Spika, unajua ni wabunge wachache ndiyo wanaoharibu sifa ya wabunge wengine.

“Kwa hiyo, wananchi wasidhani wajumbe wote wa Kamati ya Nishati na Madini ni wala rushwa, hapana, wanaofanya vitendo hivyo ni wachache kama nilivyosema hapo mwanzo.

“Mimi nataka uchunguzi huo ufanywe haraka na wote wanaohusika wajulikane.”

Katika hatua nyingine, alisema wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, kuna baadhi ya watu walikwenda kwa baba yake, Yusuph Makamba kwa ajili ya kumshawishi alegeze msimamo wake.

“Unajua Kamati hii ina ‘deal’ na mambo makubwa na yenye maslahi ya watu, kwa hiyo usipokuwa makini kama kiongozi wa kamati au mjumbe wa kamati, watu wengi watakufuata na kukushawishi kwa fedha,” alisema na kuongeza:

“Mimi nilikuwa na msimamo wangu na ndio maana hata watu wengine wakawa wanaogopa kuanza kunifuata na kunieleza wanayotaka niyafanye.

“Nakumbuka siku moja, kabla ya kwenda katika mdahalo wa Star Tv kuna watu walimfuata mzee Makamba na kutaka anishawishi nisizungumzie mradi mmoja wa umeme ambao ulikuwa na walakini.

“Lakini Mzee Makamba akawajibu kwamba mimi sikai kwake na nimehama tangu nikiwa na umri wa miaka 18, kwa hiyo hana namna yoyote ya kufanya. Kwa hiyo mtu unatakiwa uwe na msimamo na ifikie hatua wakuogope.”


Source: Spika Makinda ang
 
Walijidai kupinga posho kumbe wanachukua rushwa! Safi sana mambo hadharani sasa, movie ndo imeanza.... Where is my popcorn bag!!!
zitto niambie Range Rover Vogue huku tabata uliipata wapi??kumbe umeipatia huku eeeh
mkuu usininyime na mimi hizo popcon,,hahaha
 
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameivunja Kamati ya Nishati na Madini kutokana na tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo.

Uamuzi huo aliutangaza jana bungeni muda mfupi baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini na kusema kuwa pia kamati nyingine za bunge ambazo zinatuhuma mbalimbali atazifanyia kazi na atachukua hatua ya kuzivunja.

Hatua hiyo ya Spika Makinda ilitokana na hoja iliyotolewa na Mbunge wa Namtumbo,Vita Kawawa (CCM), aliyetaka Kamati ya Nishati na Madini ivunjwe kutokana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kutuhumiwa masuala ya rushwa.

Pia Kawawa alitoa hoja kuwa licha ya Kamati hiyo ya Nishati na Madini, ambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Bukene, Suleiman Zedi (CCM), pia kamati nyingine ambazo zimepata kutuhumiwa masuala mbalimbali ya rushwa nazo pia zivunjwe.

Mbunge huyo alisema suala la kuwepo wabunge wanaotuhumiwa kuchukua rushwa limedhalilisha bunge, hivyo kuomba pia lifanyiwe kazi na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo, Hassan Ngwilizi, ili watakaobainika wachukuliwe hatua.

Akizungumza wakati akijibu hoja hiyo, Spika Makinda alisema hoja hiyo ipo wazi na ni tabia mbaya ambayo inalidhalilisha bunge na kuwaonya wabunge kuwa wasipokuwa makini wanakwenda kubaya, kwani hawawezi kuisimamia Serikali wakati wanaomba vitu mbalimbali.

Alisema unaweza kukuta Mbunge anachangia hoja huku jasho likimtoka kumbe anafanya kazi ya kutumwa na mtu kwa maslahi binafsi na kuwa ameagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kutengeneza kanuni za maadili na mtu yeyote atakayetuhumiwa katika mazingira ya rushwa lazima hatua kubwa zichukuliwe.

"Serikali yetu na nchi yetu inapita katika kipindi cha mpito na kama nyie wabunge hamtakuwa imara kuweza kuisimamia serikali kwa ukweli hatutaweza kwenda matumaini ya wananchi yako wapi kama si Bunge?

"Kitendo hiki kwa kweli hakikubaliki ndani ya Bunge, hatuwezi kuisimamia serikali huku tunapokea pokea, unaisimamiaje serikali kwa mtindo huu?

" Kwa hiyo minaamini wabunge mkikaa vizuri na kufanya kazi yetu vizuri mabadiliko makubwa katika serikali yatatokea, lakini wenzetu wanakwenda huko mara wajipendekeze mara waombe hiki hatuwezi kwenda hivyo," alisema na kuongeza kuwa kwa kutumia kanuni hiyo 53(3) amelipeleka suala hilop Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ili walifanyie uchunguzi na kuleta taarifa bungeni.

"Mliokuwa mkitaka watajwe sasa hiyo kamati itafanya kazi hiyo, ya pili kwa kutumia kanuni 113(3) baada ya kuunga mkono hoja ya Mheshimiwa Kawawa, naridhia ombi hilo nitaivunja na nyingine ambazo zimeonekana zikilalamikiwa katika hili,"alisema.

Wajumbe wanaounda Kamati ya Nishati na Madini iliyotangazwa kuvunjwa jana licha ya Mwenyekiti Zedi ni Diana Chilolo ambaye ni Makamu Mwenyekiti, Yussuf Haji Khamis, Mariam Kisangi, Catherine Magige, Abia Nyabakari, Charles Mwijage, Yusuph Nassir,Chritopher Olesendeka na Dk. Festus Limbu.

Wengine ni Shafin Amedal Sumar, Athumani Mfutakamba, Lucy Mayenga, Josephine Chagulla, Mwanamrisho Abama, David Silinde, Suleiman Nchambis Suleiman, Kisyeri Chambiri, Ali Mbarouk Salim, Sarah Ali Msafiri, Munde Abdallah Tambwe, Vicky Kamata na John Mnyika.

Katika michango mbalimbali ya wabunge juzi na jana kwa wizara hiyo, zilitolewa tuhuma mbalimbali kwa baadhi ya wabunge na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kuhongwa na kampuni za mafuta kwa ajili ya kutaka wamshinikize Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Eliakim Maswi wang'oke katika nyadhifa zao.

Katika mjadala huo baadhi ya wabunge walipokuwa wakichangia, waliwatuhumu baadhi ya wabunge wenzao kwamba wanawaunga mkono mafisadi na kumtisha Waziri Muhongo na Katibu Mkuu Maswi kwa madai ya kukiuka sheria ya manunuzi ya umma na kuwa wabunge hao walikuwa wakifanya hivyo kwa shinikizo la baadhi ya kampuni za mafuta.

Ilidaiwa na baadhi ya wachangiaji kuwa baadhi ya wabunge wamekuwa wakiendesha kampeni kutaka watendaji hao wang'oke kwa madai walikiuka sheria ya manununuzi ya umma na kuipa zabuni Kampuni ya Puma Energy na kuwa baadhi ya wabunge walienda mbali zaidi kwa kumtumia ujumbe wa vitisho Maswi kwa simu yake ya kiganjani.


Chanzo: Habarileo
 
ndugu wanajukwaa nahitaji maelezo kidogo juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya hawa wabunge ambao ilithibitika kupokea rushwa ili kutumia kamati yao kuwaondoa madarakani waziri na katibu mkuu wake mwaka 2013.naona baadhi ya majina wamekuwa wasemaji wakubwa wa kupinga rushwa!
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameivunja Kamati ya Nishati na Madini kutokana na
tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo.
Uamuzi huo aliutangaza jana bungeni muda mfupi baada ya Bunge kupitisha bajeti ya
Wizara ya Nishati na Madini na kusema kuwa pia kamati nyingine za bunge ambazo
zinatuhuma mbalimbali atazifanyia kazi na atachukua hatua ya kuzivunja.
Hatua hiyo ya Spika Makinda ilitokana na hoja iliyotolewa na Mbunge wa Namtumbo,
Vita Kawawa (CCM), aliyetaka Kamati ya Nishati na Madini ivunjwe kutokana na baadhi
ya wajumbe wa kamati hiyo kutuhumiwa masuala ya rushwa.
Pia Kawawa alitoa hoja kuwa licha ya Kamati hiyo ya Nishati na Madini, ambayo
Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Bukene, Suleiman Zedi (CCM), pia kamati nyingine ambazo
zimepata kutuhumiwa masuala mbalimbali ya rushwa nazo pia zivunjwe.
Mbunge huyo alisema suala la kuwepo wabunge wanaotuhumiwa kuchukua rushwa
limedhalilisha bunge, hivyo kuomba pia lifanyiwe kazi na Kamati ya Haki, Maadili
na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo, Hassan Ngwilizi, ili
watakaobainika wachukuliwe hatua.
Akizungumza wakati akijibu hoja hiyo, Spika Makinda alisema hoja hiyo ipo wazi na ni
tabia mbaya ambayo inalidhalilisha bunge na kuwaonya wabunge kuwa wasipokuwa makini
wanakwenda kubaya, kwani hawawezi kuisimamia Serikali wakati wanaomba vitu
mbalimbali.
Alisema unaweza kukuta Mbunge anachangia hoja huku jasho likimtoka kumbe anafanya
kazi ya kutumwa na mtu kwa maslahi binafsi na kuwa ameagiza Kamati ya Haki, Maadili
na Madaraka ya Bunge, kutengeneza kanuni za maadili na mtu yeyote atakayetuhumiwa
katika mazingira ya rushwa lazima hatua kubwa zichukuliwe.
“Serikali yetu na nchi yetu inapita katika kipindi cha mpito na kama nyie wabunge
hamtakuwa imara kuweza kuisimamia serikali kwa ukweli hatutaweza kwenda matumaini ya
wananchi yako wapi kama si Bunge?
“Kitendo hiki kwa kweli hakikubaliki ndani ya Bunge, hatuwezi kuisimamia serikali
huku tunapokea pokea, unaisimamiaje serikali kwa mtindo huu?
“ Kwa hiyo minaamini wabunge mkikaa vizuri na kufanya kazi yetu vizuri mabadiliko
makubwa katika serikali yatatokea, lakini wenzetu wanakwenda huko mara wajipendekeze
mara waombe hiki hatuwezi kwenda hivyo,” alisema na kuongeza kuwa kwa kutumia kanuni
hiyo 53(3) amelipeleka suala hilop Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ili
walifanyie uchunguzi na kuleta taarifa bungeni.
“Mliokuwa mkitaka watajwe sasa hiyo kamati itafanya kazi hiyo, ya pili kwa kutumia
kanuni 113(3) baada ya kuunga mkono hoja ya Mheshimiwa Kawawa, naridhia ombi hilo
nitaivunja na nyingine ambazo zimeonekana zikilalamikiwa katika hili,”alisema.
Wajumbe wanaounda Kamati ya Nishati na Madini iliyotangazwa kuvunjwa jana licha ya
Mwenyekiti Zedi ni Diana Chilolo ambaye ni Makamu Mwenyekiti, Yussuf Haji Khamis,
Mariam Kisangi, Catherine Magige, Abia Nyabakari, Charles Mwijage, Yusuph Nassir,
Chritopher Olesendeka na Dk. Festus Limbu.
Wengine ni Shafin Amedal Sumar, Athumani Mfutakamba, Lucy Mayenga, Josephine
Chagulla, Mwanamrisho Abama, David Silinde, Suleiman Nchambis Suleiman, Kisyeri
Chambiri, Ali Mbarouk Salim, Sarah Ali Msafiri, Munde Abdallah Tambwe, Vicky Kamata
na John Mnyika.
Katika michango mbalimbali ya wabunge juzi na jana kwa wizara hiyo, zilitolewa
tuhuma mbalimbali kwa baadhi ya wabunge na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Nishati na Madini kuhongwa na kampuni za mafuta kwa ajili ya kutaka wamshinikize
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Eliakim Maswi wang’oke katika nyadhifa zao.
Katika mjadala huo baadhi ya wabunge walipokuwa wakichangia, waliwatuhumu baadhi ya
wabunge wenzao kwamba wanawaunga mkono mafisadi na kumtisha Waziri Muhongo na Katibu
Mkuu Maswi kwa madai ya kukiuka sheria ya manunuzi ya umma na kuwa wabunge hao
walikuwa wakifanya hivyo kwa shinikizo la baadhi ya kampuni za mafuta.
Ilidaiwa na baadhi ya wachangiaji kuwa baadhi ya wabunge wamekuwa wakiendesha
kampeni kutaka watendaji hao wang'oke kwa madai walikiuka sheria ya manununuzi ya
umma na kuipa zabuni Kampuni ya Puma Energy na kuwa baadhi ya wabunge walienda mbali
zaidi kwa kumtumia ujumbe wa vitisho Maswi kwa simu yake ya kiganjani.

Habarileo
 
Kumbe akina Ole Sendeka kupiga mzigo kwao ni kawaida! Ndo maana wamelamba fedha za akina Mengi ili wawashughulikie akina Muhongo na Maswi
 
MAR
15
KAMATI ZA BUNGE ZAVUNJWA KWA KUKITHIRI RUSHWA...

Ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
Kamati za Bunge zimetangazwa, ambapo wajumbe wa kamati mbili zilizowahi kutuhumiwa kwa rushwa, wamesambaratishwa.
Kwa mujibu wa orodha mpya ya wajumbe wa kamati hizo iliyotolewa jana na Ofisi ya Bunge, Kamati ya Hesabu za Serikali na ya Nishati na Madini zilizopata kutuhumiwa kwa rushwa, zimesambaratishwa.
Mbali na hatua hiyo, kwa maana ya wajumbe wake kusambazwa katika kamati zingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, amepangwa kupambana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, John Cheyo.
Kamati ya Nishati na Madini iliyokuwa na wajumbe 25 ambao baadhi walituhumiwa kupokea rushwa ili kukwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, imebakiwa na wajumbe watatu wa zamani.
Katika Kamati iliyopita, wajumbe walikuwa Selemani Zedi, aliyekuwa Mwenyekiti, Diana Chilolo, Makamu Mwenyekiti na John Mnyika.
Wengine walikuwa Yusuph Haji Khamis, Mariam Kisangi, Catherine Magige, Abia Nyabakari, Charles Mwijage, Yussuph Nassir, Christopher ole Sendeka, Dk Festus Limbu, Shaffin Sumar, Lucy Mayenga na Josephine Chagula.
Wengine ni Mwanamrisho Abama, David Silinde, Suleiman Nchambi Suleiman, Kisyeri Chambiri, Munde Abdallah, Sara Msafiri, Vicky Kamata, Mbarouk Ali, Athuman Mfutakamba na Pamela Palangyo.
Kwa sasa inaundwa na wajumbe wachache kuliko iliyopita akiwamo Victor Mwambalaswa, Saleh Pamba, David Silinde, Martha Mlata, Devotha Likokola, Raya Khamis,- Murtaza Mangungu na Juma Njwayo.
Wengine ni Jerome Bwanausi, Richard Ndassa, Anne Kilango,- Herbert Mntangi, Shaffin Sumar, Yussuf Haji Khamis na Riziki Lulida na wa zamani Chagula, Charles Mwijage na Mariam Kisangi.
Kamati nyingine iliyosambaratishwa ni ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ambapo- wajumbe walioteuliwa- ni- Deusderius Mipata, Filikunjombe, Asha Jecha na Lucy Owenya.
Wengine ni Esther Matiko, Cheyo, Zitto, Zainab Vulu, Ally Keissy, Zainab Kawawa, Kheri Ali Khamis, Faida Mohamed Bakari, Ismael Aden Rage, Modestus Kilufi, Abdul Marombwa, Gaudence- Kayombo, Kombo Khamis Kombo na Catherine Magige.
Wajumbe wa zamani walikuwa Augustine Mrema, aliyekuwa Mwenyekiti, Iddi Azzan, Makamu Mwenyekiti; Riziki Saidi Lulinda, Zabein Mhita na Godfrey Zambi.
Wengine ni Subira Mgalu, Hasnain Murji, Susan Kiwanga, David Kafulila, Omary Badwel, Abdul Mteketa, Tauhida Nyimbo, Joseph Selasini, Kuruthum Mchuchuli, Maida Abdalah, Dk Cyril Chami.
Kamati hiyo, katika mikutano ya Bunge iliyopita, wajumbe wake walituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa huku mjumbe wake ambaye ni Mbunge wa Bahi, Badwel, akipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kupokea rushwa na kesi yake bado inaendelea.
Aidha, katika orodha hiyo mpya, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto na Makamu wake, Filikunjombe, wameingizwa kwenye Kamati ya Hesabu za Serikali ambayo aliyekuwa Mwenyekiti wake, Cheyo anaendelea kuwa kwenye Kamati.
Kutokana na mabadiliko hayo, katika uchaguzi wa viongozi wa kamati hizo unaotarajiwa kufanyika leo, mchuano mkali utakuwa baina ya Zitto na Cheyo katika nafasi ya uenyekiti kutokana na taratibu zilizopo kuonesha kuwa Kamati hiyo, huongozwa na mbunge kutoka chama cha upinzani.
Aidha, katika orodha hiyo inaonesha kuwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Kilango, ameondolewa kwenye Kamati hiyo na kuingizwa Kamati ya Nishati na Madini ambayo wajumbe wake wa awali 25, takribani wote isipokuwa wanne wamehamishiwa kamati zingine.
 
Karata ni zile zile hata ukizichanga mara ngapi, usitegemee kutokea karata yenye alama tofauti.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom