Kenney
JF-Expert Member
- Dec 8, 2013
- 294
- 165
maranyingi story kama hizi ndizo zinapelekea watu kupigwa, maana watahusishwa waganga na watu wakila aina ili kumvutia mlengwa. ukisikia mzungu anaulizia rupia ni kwa ajili ya kumbukumbu tu na si vinginevyo!Nimechelewa kuisoma hii mada ila sio mbaya kutokana na mda na siku yenyewe ilivyokaa leo ntaomba niwambie kifupi tu na mim nayojua kuhusu hii topic. Baada ya vita ya kwanza kuisha mjeruman alinyang'anywa makolon yake yote na baada ya kunyang'anywa wakat anaondoka kurud kwao muingereza aliwaambia hamna kuondoka na kitu zaid ya beg lako tu na alikuwa anawasachi wakat wakipanda mel au ndege kurud kwao, hii ndio ilopelekea wajeruman kuficha vitu vyao. Bas nije kwenye mada binafsi rupia nimeiona na maajabu yake ingawa sijaishika kakaangu alitumia miaka 3 kuchimba hiyo rupia ukerewe mwanza na baada ya kurud nyumban akil yake ilikuwa sio sawa na hii ilitufanya tujue ni kwel anayosema? Nilienda had ukerewe kwa rafik zake aliposema kuna hivyo vitu na wanatafta mteja. Walipata rupia nying ila wanazo nane ambazo zina nguvu ya ajabu. Hizo rupia mojawapo nimeiona kwenye picha hapo ya huyo mjeruman mwenye kofia yenye ndege. Hiyo rupia ni nyekundu kama shaba na pia ina sumaku na ina vuta coin nyingne na vitu chuma vidogo dogo na pia hiyo coin ukichukua blastic uweke maji na yenyewe ikae chin bas ukiweka coin yoyote juu yake haizam inaelea na bdae inatupwa nje ya kibakul. Na sio kila mtu anaweza kushika hiyo rupia huwa inapotea na kuna makabidhiano wakat inavyotoka kwa mtu kwenda kwa mwingne kuna kafara lazima zifanyike ndo uimilki. Ukiachana na rupia kuna pas kama ya mkaa ambayo ni nzito na hii inafanya kaz inaweekwa juan tu unanyooshea, taa ya chemry hii ipo kama iyo pas nayo, saa ya ukutan na pia walipata bunduki (rifle) na risas zake nying. Kwaiyo sio kitu ambacho ni imagination ila kweli kipo. Inasemekana kwel rupia imechanganywa na damu na mifupa ya watu ila sio zote ni hizo chache ambazo nimesema hapo juu. Watu wamekuwa wakitapelewa kwel sababu rupia ni hela ya kawaida ukiachana na hiyo maajabu. Kaka angu ameniambia walienda had kigoma kupewa dawa kwa waganga ili waweze kuingia kwenye ilo shimo. Na kwel baada ya kupata hivo vitu walisumbuka sana ni kama waliiba ile mizimu iliyoachwa pale iliendelea kuwasumbua had walipoenda tena kufanyiwa matambako kibao. Hivyo vitu wanavyo kabisa ila hadi sasa nakwambia hamna mteja ambaye wamepata na vitu wanavyo tu. Sasa ukija kiundan hivyo sio vitu vya kufuatilia hata kidogo vimezungukwa na nguvu ya giza ambayo sio nzur. Tutafute ela kwa njia halal na sio had kwa waganga au vitu vyenye nguvu ys giza sababu tunapita tu hapa dunian. Bro tulimkalisha chin tukamwelekeza ila hakuelewa na yupo bdo anaangaika na wenzake kutafuta wateja wengi mashart na bei wanayouza vimewashinda.