Rungwe tuna wabunge bubu!

Rungwe tuna wabunge bubu!

Wazo zuri sana, lakini wabunge wa kuhamashisha new ideas hatuna.

Nachokiona msiwalaumu wabunge tu, hata ninyi wananchi mnawaweza kuanza kwa kuandika wazolenu na kuliwasilisha kwa waziri husika, huwa napatwa simamanzi kununu mkungu wa ndu chini ya Tsh 5000 wakati Mkungu huohuo ukiuku Dar bei yake ni above 20K
 
Nachokiona msiwalaumu wabunge tu, hata ninyi wananchi mnawaweza kuanza kwa kuandika wazolenu na kuliwasilisha kwa waziri husika, huwa napatwa simamanzi kununu mkungu wa ndu chini ya Tsh 5000 wakati Mkungu huohuo ukiuku Dar bei yake ni above 20K
Unachosema ni kweli akini inaelekea hujafika Rungwe.
Miundombinu ya barabara ni balaa!
Watu wanamkumbuka Mwalimu Nyerere kwa barabara moja tu kueekea Malawi.

Hakuna kabisa al weather roads kuekekea kule waliko wananchi.
Sehemu kama Mwakaleli, Itete, Masebe, Ikuti, Mpuguso-Lutengano, Masoko-Mbambo, sehemu zote hizi hazijui barabara za lami.

Bila uwekezaji wa miundombinu ungehimizwa na wabunge wetu hawa, watu wasingehamia Mbeya kuwekeza.
 
Mbunge wenu kapangiwa kazi ya kusema ndioooooooooo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unasema mtu asafiri kwa bodaboda km 33, mbona ni mateso?
Kwanza jifunze kuwa mstaarabu neno fala linakupunguzia credit! Hiyo barabara ipo miaka mingi kabla ya atupele tena kipindi hicho busokelo inazalisha kahawa atupele ana miaka mingapi bungeni? Waliopita akina Mwandosya tena waziri mwandamizi hakuiona hiyo barabara? Kwenda na noah umependa mwenyewe kuna bodaboda nyingi tu.Pia elewa ile ni rough road huwezi kuifananisha na lami lazima nauli iwe juu! Huduma muhimu Kama afya maji na elimu busokelo haipo nyuma nakushauri nenda Isange angalia kituo cha afya kinachojengwa halafu leta mrejesho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nakuunga mkono ndugu Mimi kwetu ni busokelo pale kandete ,huyo fala anaposema hatuna shida namshangaa sana ,sijui ndio hao wanaohongwa elfu mbili kipindi cha uchaguz hata sielew,busokelo tuna matatizo kibao sema kwa majuha hawawez kujua matatizo maana wao wakishiba ugali na lyanyungu basi hakuna shida ,mfano barabara katumba to mwakalel ingeboreshwa nauli ilitakiwa iwe 2000,alafu usafir ni shida sana watu mnapangwa kwenye vinoa kama ndiz ,pia watumishi kufuata mshahara hadi rwangwa au tukuyu mjini ASA unasemeje kule hamna shida?wakulima wanalima SNA viazi ila shida Barbara zikiwa mbovu wanalazimika kuuza gunia had elfu kumi alafu fala mmoja unasema hatuna shida


Sent using Jamii Forums mobile app
Cha.muhimimu watu kupanga pamoja shughuli za maendeleo.
 
Mbeya nzima kuna wabunge wawili kam sio watatu

Rungwe hamna wabunge

Kyela hamna mbunge

Mbeya vijijini hamna mbunge

Mbalali hamna mbunge


Mkoa wa songwe angalau tunaona vijana wakijitahidi namna ya kuishi na jamii ila nao

Ileje hamna mbunge
 
Labda huko kwenu lakini kwetu busokelo mambo safi tunakunywa tunalala tunaamka tunachuma chai, tunauza maziwa kwa asas tunapata pesa wewe ulitaka tununue ndege?
Umesahau mananasi


Ila mkuu utajikiaje siku mbunge wako akitafuta mfadhili aweze kujenga kiwanda cha juisi ila tupandishe thamani ya matunda yetu hapo busokelo
 
Unajua mkuu, kabla ya kujitokeza kuwaongoza watu kuna kazi kubwa ya kufanya. Kazi hiyo si tu kujinadi ili kuwashawishi watu wakuchague bali ni kuwa shape aina ya watu ambao ningependa kuwaongoza.
Binafsi ninafahamu vizuri sana changamoto za kule na nini kifanyike, lakini ningependa kwanza watu wenyewe wayajue mahitaji na changamoto zao na vipaombele vyao. Sihitaji mimi eti ndiyo niende nika waambie kuwa nitawafanyoa hivi na vile bali wao wainuke na kuziorodhesha changamoto na mahitaji na waseme tunataka mtu atakayetufanyia haya. Hapo mimi ndiyo nitajitokeza kuiomba hiyo kazi kwa kuwaambia haya wayatakayo nitayafa vipi na kwa timeline ipi kwa support kutoka wapi, hiyo ndiyo jamii ninayotamani kuiongoza. Watu ambao watanihiji au watakuja kunihoji kama sitatimiza mahitaji yao, lakini si watu ambao wataishia kulalamika.
Lakini kwa mindset za sasa hivi za kutaka kuahidiwa watafanyiwa nini, kwa kweli sipo tayari kujitokeza kuwaongoza watu wa aina hii.
Kwa sasa acha niendelee kuwa shape namna ya kuzitambua chsngamoto zao na kuzi present pia namna ya kuondokana na tabia ya kusubiri kuahidiwa.
Nimekaa nimejiuliza sana hili swali kuhusu Wahaya na Wanyaki. Lakini kama ulivyoniambia Mind-Set ndiyo tatizo kubwa.
 
Umesahau mananasi


Ila mkuu utajikiaje siku mbunge wako akitafuta mfadhili aweze kujenga kiwanda cha juisi ila tupandishe thamani ya matunda yetu hapo busokelo
Hayo ndiyo mawazo ya kimaendeleo tunayoyataka siyo kukaa unaponda tu viongozi mitandaoni. Mimi nina hekari mbili za miparachichi ya kisasa Kule next season naanza kuvuna rasmi na soko ni la uhakika, kuna halmashauri zina hali mbaya hapa nchini hata huduma za kawaida za kijamii ni kitendawili
 
rungwe yote ifanywe jimbo moja kuanzia kyela mpaka busokelo halafu apewe Tulia Akson muone maendeleo ya kweli,
Si jimbo litakuwa kubwa sana ??
Halafu kuna hatari moja kubwa, kama mbunge atakuwa mzembe ina maanisha kuanzia Kyela hadi Rungwe kutakuwa na umasikini. Yabaki hivihivi tu.....
 
Hahaha, hii kali, hili lina ukweli wowote ule ?

Ukiishi mmkoa wa Mbeya utajua kwanini makabila mengine hayawapendi Wanyaki, ingawa wao hawakubali yani kama Wakoloni walivyowapendelea Wachaga na Wahaya wao wakajiona ndo wanajua kutawala makabila mengine, kiujumla Wanykyusa ni watu wenye kiburi na dharau awe mwanamke au mwanaume awe na pesa au asiwe na nazo kwao ni kawaida
 
Hayo ndiyo mawazo ya kimaendeleo tunayoyataka siyo kukaa unaponda tu viongozi mitandaoni. Mimi nina hekari mbili za miparachichi ya kisasa Kule next season naanza kuvuna rasmi na soko ni la uhakika, kuna halmashauri zina hali mbaya hapa nchini hata huduma za kawaida za kijamii ni kitendawili
Viongizi wetu bubu na mabomu ya mkono tutaendelea kuwananga popote pale kama hawafanyi kazi watarajiwayo kufanya.

La kwanza barabara ya kufungua wilaya kimaendeleo.
Katumba~Lwangwa ~Itete~Mbambo~Masoko~ Tukuyu barabara hii ni kilio cha miaka nenda rudi.
Wabunge wetu kimya utafikiri nao ni watazamaji tu.
 
Viongizi wetu bubu na mabomu ya mkono tutaendelea kuwananga popote pale kama hawafanyi kazi watarajiwayo kufanya.

La kwanza barabara ya kufungua wilaya kimaendeleo.
Katumba~Lwangwa ~Itete~Mbambo~Masoko~ Tukuyu barabara hii ni kilio cha miaka nenda rudi.
Wabunge wetu kimya utafikiri nao ni watazamaji tu.
Tukuyu-bujela-ijigha masukulu hadi kyela.. barabara na huduma zingine za jamii zina hali mbaya.
 
Wazo zuri sana, lakini wabunge wa kuhamashisha new ideas hatuna.
Kuhamasisha maendeleo siyo kazi ya wabunge. Kama mnasubiri masihi ashuke awahamasishe basi mtasubiri sana sana. Rungwe na Tukuyu kwa nilivyoona haraka mbali na kilimo, mnaweza kuanzisha shughuli za viwanda vidogo vidogo kama alivyosema mkuu kapalamsenga.
Jaribuni kuiga mfano wa Mufindi kule Iringa, ambako hali yake ya hewa inafanana kwa asilimia kubwa na Rungwe na Kyela. Wao pale wana viwanda vingi na hivyo bidhaa zinatoka mashambani na kuuzwa moja kwa moja viwandani hapo hapo. Bidhaa kama chai inaenda Chai Bora, magogo yanaenda kule Sao-Hill au kiwanda cha mgololo.
Hili limepelekea wakulima kupata sana nafuu, na Mafinga kuwa soko kubwa sana ambalo wafanyabiashara wa Afrika Mashariki wanafurika hasa kwenye biashara ya magogo. Rungwe kama mtaamua kutengeneza viwanda vya kusindika chakula mbona mtafika mbali sana na kutakuwa na soko kubwa sana maana badala ya kupata kadhia ya usafirishaji basi mtakuwa mnauza viwandani huko huko. Hili inabidi liende sambamba na kujitahidi kuanzisha mazao mapya ya chakula.
Pili, Rungwe na Kyela kuna vivutio vingi sana vya utalii, kule Arusha wazawa wengi wamejikita sana kwenye biashara ya utalii kwanini ninyi hamuangalii hizi fursa ?? Ukitoka lake Ngosi na useme ulale Tukuyu huwezi kupata hata hoteli na lodge nzuri. Nini tatizo ?? Mkuu Consigliere kasema mindset inabidi zibadilike....
 
Nimekaa nimejiuliza sana hili swali kuhusu Wahaya na Wanyaki. Lakini kama ulivyoniambia Mind-Set ndiyo tatizo kubwa.
Ngoja niwaache Wahaya, niwaongelee Wanyakyusa. Wanyakyusa ni watu wa kusaidiana ila si watu wa kunyanyuana. Wanyakyusa (wanaoishi nje ya kwao) husaidiana kwa tahadhari sana, anayekusaidia huwa makini kuhakikisha hauji kumzidi hapo baadaye na ikitokea ukaonyesha mwekekeo wa kumzidi basi anaweza akakuanzishia tifu from no where, mara upo Pol8si mara Mahakamani. Hao ndiyo Wanyakyusa wa ugenini.
Na wanaposaidiana huwa wanahakikisha anakufahamu na kawaida kuna ubaguzi miongoni mwao.
Wanapokuwa na vikao vyao usitarajie utamkuta wa Keko Magurumbasi amechanganyikana na wa Upanga.
Kuhusu kunyanyuana huwa hawajadili mipango ya maendeleo ya kwao bali huibua mijadala ya majungu tu na kupingana kusiko na tija. Hawawezi kufikiria kwenda kusaidia shule, barabara au hospital, hawajadili mazingira ya elimu, afya n.k wanayopitia watu wa kwao sababu tu watoto au familia zao haziishi huko. Walio kwenye nafasi hawawezi kujenga ushawishi wa mipango kadhaa ya kimaendeleo ikafanyike kwao sababu hawai fikirii jamii ya kwao na watu wao, bali huwaza na kuishia katika level ya familia au ndugu tu.
Wanapenda sana sifa kwa kujisifia maendeleo ya kwao yaliyoletwa wakati wa mkoloni wakati wao hawajachangia hata moja. Akina Mwandosya ndiyo hao wanazeeka na sasa wanahitaji kupumzika. Lakini kwa bahati mbaya sana hakuna aliyeiga na kufuata mfano wake, mbaya zaidi walikua busy kujifanya wapo karibu na Mwandosya na wanamfahamu sana. Moyo wake na intelligence yake anazeeka nayo.

Kuna wakati Wanyakyusa likikua ni kabila la kujivunia, lakini siyo hawa Wanyakyusa wa hivi sasa, sijui wametengenezwa maabara!! Wamepausha na kuupoteza kabisa unyakyusa asilia.
 
🙂
Sasa watu kama wewe, masopakyindi ,Red Giant kwanini msiende kufanya mambo huko kiongozi ?? Kama leo hii Wanyakyusa mkiamua kurudi kejenga kwenu, Rungwe itafika mbali mno maana kama kusoma wengi wenu mmesoma sana.
Mkuu nafikiri siasa siku hizi ni pesa zaidi. Mfano mbunge wa Rungwe(Saul) ni mtu Tajiri, wa Busokelo huko naye si haba. Kingine we mwenyewe kuna siku ulisemaa umeacha kujihangaisha na matatizo ya Tanzania🙂, system sucks
 
Back
Top Bottom