Rungwe tuna wabunge bubu!

Rungwe tuna wabunge bubu!

Ngoja niwaache Wahaya, niwaongelee Wanyakyusa. Wanyakyusa ni watu wa kusaidiana ila si watu wa kunyanyuana. Wanyakyusa (wanaoishi nje ya kwao) husaidiana kwa tahadhari sana, anayekusaidia huwa makini kuhakikisha hauji kumzidi hapo baadaye na ikitokea ukaonyesha mwekekeo wa kumzidi basi anaweza akakuanzishia tifu from no where, mara upo Pol8si mara Mahakamani. Hao ndiyo Wanyakyusa wa ugenini.
Na wanaposaidiana huwa wanahakikisha anakufahamu na kawaida kuna ubaguzi miongoni mwao.
Wanapokuwa na vikao vyao usitarajie utamkuta wa Keko Magurumbasi amechanganyikana na wa Upanga.
Kuhusu kunyanyuana huwa hawajadili mipango ya maendeleo ya kwao bali huibua mijadala ya majungu tu na kupingana kusiko na tija. Hawawezi kufikiria kwenda kusaidia shule, barabara au hospital, hawajadili mazingira ya elimu, afya n.k wanayopitia watu wa kwao sababu tu watoto au familia zao haziishi huko. Walio kwenye nafasi hawawezi kujenga ushawishi wa mipango kadhaa ya kimaendeleo ikafanyike kwao sababu hawai fikirii jamii ya kwao na watu wao, bali huwaza na kuishia katika level ya familia au ndugu tu.
Wanapenda sana sifa kwa kujisifia maendeleo ya kwao yaliyoletwa wakati wa mkoloni wakati wao hawajachangia hata moja. Akina Mwandosya ndiyo hao wanazeeka na sasa wanahitaji kupumzika. Lakini kwa bahati mbaya sana hakuna aliyeiga na kufuata mfano wake, mbaya zaidi walikua busy kujifanya wapo karibu na Mwandosya na wanamfahamu sana. Moyo wake na intelligence yake anazeeka nayo.
Kuna wakati Wanyakyusa likikua ni kabila la kujivunia, lakini siyo hawa Wanyakyusa wa hivi sasa, sijui wametengenezwa maabara!! Wamepausha na kuupoteza kabisa unyakyusa asilia.
Duuuh, mkuu kweli wewe unaifahamu sana Rungwe. Hongera kwa hili....
 
🙂
Mkuu nafikiri siasa siku hizi ni pesa zaidi. Mfano mbunge wa Rungwe(Saul) ni mtu Tajiri, wa Busokelo huko naye si haba. Kingine we mwenyewe kuna siku ulisemaa umeacha kujihangaisha na matatizo ya Tanzania🙂, system sucks
Wala hujakosea mkuu, mimi siasa za Tanzania nimekataa kabisa kujuhusisha nazo. Hata kazi serikalini nako nilishaondoka kitambo sana. Tanzania ni nchi ngumu sana, sema naamini tutafika tu...
 
Wala hujakosea mkuu, mimi siasa za Tanzania nimekataa kabisa kujuhusisha nazo. Hata kazi serikalini nako nilishaondoka kitambo sana. Tanzania ni nchi ngumu sana, sema naamini tutafika tu...
You're damn right, mkuu! Siasa za Tanzania is a wastage of time!
 
Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya inadorora kimaendeleo.

Kwa zaidi ya miaka 35 wilaya hii haina mradi mkubwa wa maendeleo, HATA MMOJA. Wananchi wanaishi kwa kudra tu za Mwenyezi Mungu.

Kibaya zaidi nimetoka huko vijijini kwetu, watu wana hisia mbaya kuwa uongozi uliopo unawachukia. Sababu hazijulikani!

Mbaya zaidi wilaya ina wabunge ambao hawana weledi wala umahiri wa kuongelea matatizo ya wananchi katika hadhiri za kitaifa.

Mbunge wa Rungwe Mashariki(ambaye hata jina silikumbuki) na Mbunge wa Rungwe Magharibi, maarufu kama SH Amon, sijawahi kuwasikia wakipiga makelele yasiyo ya kawaida katika kuomba miradi toka serikalini, iwe viwanda, utalii au barabara.

Hawa wabunge ni mabubu kisiasa.

Mkuu kama wameingia madarakani kwa kubebwa na vyombo vya dola watahoji nini, wao kazi yao ni kuunga mkono itakacho serekali kama sehemu ya kulipa fadhila.
 
Mie ni CCM lakini hawa wabunge ni jiwe la shingoni, linazamisha maendeleo ya Rungwe.
Mimi ninawachallenge, katika muhula wao wananchi wamepata nafuu gani katika kuwepo kwao?

Mkuu inaonekana kama umenasa kwenye uongo kwamba mbunge analeta maendeleo. Hakuna mbunge anayeleta maendeleo hilo ufahamu, sana sana anaenda kuomba serikali ilete maendeleo, na kama ni mtu wa kujipendekeza sio rahisi hata asikilizwe. Chagueni mpinzani kisha awe anaipaka serekali shombo, lazima wataleta maendeleo ili kumnyang'anya jimbo.
 
Baadhi ya MP ni ni shida pale CCM na makasuku tu hivyo basi bora ya hao effect yao ni ndogo. Japo wapuuzi ila upuuzi wao unasaidia kidogo. Kuna wengine wanauliza ndege iko wapi? Sasa hawa na wenyewe vipi ila laana iende kwa wote 🐜 CAG kwa maana wa***ge sana Bungeni
 
Kuhamasisha maendeleo siyo kazi ya wabunge. Kama mnasubiri masihi ashuke awahamasishe basi mtasubiri sana sana. Rungwe na Tukuyu kwa nilivyoona haraka mbali na kilimo, mnaweza kuanzisha shughuli za viwanda vidogo vidogo kama alivyosema mkuu kapalamsenga.
Jaribuni kuiga mfano wa Mufindi kule Iringa, ambako hali yake ya hewa inafanana kwa asilimia kubwa na Rungwe na Kyela. Wao pale wana viwanda vingi na hivyo bidhaa zinatoka mashambani na kuuzwa moja kwa moja viwandani hapo hapo. Bidhaa kama chai inaenda Chai Bora, magogo yanaenda kule Sao-Hill au kiwanda cha mgololo.
Hili limepelekea wakulima kupata sana nafuu, na Mafinga kuwa soko kubwa sana ambalo wafanyabiashara wa Afrika Mashariki wanafurika hasa kwenye biashara ya magogo. Rungwe kama mtaamua kutengeneza viwanda vya kusindika chakula mbona mtafika mbali sana na kutakuwa na soko kubwa sana maana badala ya kupata kadhia ya usafirishaji basi mtakuwa mnauza viwandani huko huko. Hili inabidi liende sambamba na kujitahidi kuanzisha mazao mapya ya chakula.
Pili, Rungwe na Kyela kuna vivutio vingi sana vya utalii, kule Arusha wazawa wengi wamejikita sana kwenye biashara ya utalii kwanini ninyi hamuangalii hizi fursa ?? Ukitoka lake Ngosi na useme ulale Tukuyu huwezi kupata hata hoteli na lodge nzuri. Nini tatizo ?? Mkuu Consigliere kasema mindset inabidi zibadilike....
Ni kweli unenayo mkuu. kuanzisha SACCOS za wauza maziwa au walima ndizi, chai, parachichi na baadaye kuwa na viwanda vyenu huhitaji mbunge.
 
Hayo ndiyo mawazo ya kimaendeleo tunayoyataka siyo kukaa unaponda tu viongozi mitandaoni. Mimi nina hekari mbili za miparachichi ya kisasa Kule next season naanza kuvuna rasmi na soko ni la uhakika, kuna halmashauri zina hali mbaya hapa nchini hata huduma za kawaida za kijamii ni kitendawili
Kuponda ni moja ya njia ya kukumbushana tu

Mkuu soko la parachichi la uhakika linapatikana huko huko au mpaka tupeleke mikoa jirani
 
Poti, nilikuwa nyumbani Kyimbila ningejua ningekutafuta. Na kuhusu hoja yako, Ni wabunge au Ilani ya Chama chao chakavu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Malafyale nami nilikuwa nyumbani wiki2 zilizopita na nakuwa frustrated sana na miundombinu.
Barabara za mizunguko wilayani ili kuendeleza wananchi zimeachwa zilivyo toka enzi ya ukoloni.
 
Mkuu inaonekana kama umenasa kwenye uongo kwamba mbunge analeta maendeleo. Hakuna mbunge anayeleta maendeleo hilo ufahamu, sana sana anaenda kuomba serikali ilete maendeleo, na kama ni mtu wa kujipendekeza sio rahisi hata asikilizwe. Chagueni mpinzani kisha awe anaipaka serekali shombo, lazima wataleta maendeleo ili kumnyang'anya jimbo.
Unajenga hoja na kuji side step kuelekea kule unako amini.
Nani kasema mbunge ndo analeta maendeleo?
Maendeleo ni matokeo ya uhamasishaji na kuipigia kelele serikai juu ya matatizo ya wananchi.

Ni ujinga kutegemea Sauli akajenge barabara za lami Rungwe, akini akipiga kelele bungeni, kwenye asasi tofauti, hata na waandishi wa habari tu, watu wana sikia na kuchukua hatua.

Pamoja na matatizo yake, Mbowe ameweza ku lobby mradi wa barabara ya lami 11km kule Machame.

Hapo sijui nini tusichoelewa, hasa wabunge wetu.
 
Kwanza jifunze kuwa mstaarabu neno fala linakupunguzia credit! Hiyo barabara ipo miaka mingi kabla ya atupele tena kipindi hicho busokelo inazalisha kahawa atupele ana miaka mingapi bungeni? Waliopita akina Mwandosya tena waziri mwandamizi hakuiona hiyo barabara? Kwenda na noah umependa mwenyewe kuna bodaboda nyingi tu.Pia elewa ile ni rough road huwezi kuifananisha na lami lazima nauli iwe juu! Huduma muhimu Kama afya maji na elimu busokelo haipo nyuma nakushauri nenda Isange angalia kituo cha afya kinachojengwa halafu leta mrejesho
Nimekuita hivyo maana una akili mfu sana ,kwahiyo kama hiyo Barabara ni rough road tokea enzi za mkoloni iendelee tu kuwa rough road haya nitajie main road ya kukufikisha kandete unapotokea katumba,pia unataka nipande pikipiki toka katumba had mwakalel km 33 kweli upo serious na je unaijua bei ya pikipik katumba to mwakalel labda nikwambie tu nauli kwa piki pik ni elfu kumi na hiyo ni km 33 tu ,je ni wangapi wanaweza kumudu hiyo gharama?.Siku zote maendeleo ni miundombinu kwanza mengine yanajiset yenyew,haiwezekan kila cku wabebe gesi ya kyejo miaka nenda rudi washindwe kutujengea barabara ya maana hata kama sio ya rami ila wangetujengea hata ile ya makapi ya rami angalau tungeona unafuu.pia unadai maendeleo ni umeme na maji sawa sikatai lakin hivyo vitu vinawafaidisha kivipi watu wa busokelo bila kuwa na miundo mbinu iliyo mizur?Busokelo ipi unayosema ina maendeleo tuache kujidanganya kuwa tuna maendeleo ni kwel tunajitahid kwa swala la elimu maana wazaz wa kule waliowengi wanajituma kusomesha ila sasa watoto wakishasoma wanaenda kuendeleza mikoa mingine wanasahau kwao kabisa ,yaan MTU anaweza kuwa na mansion dar ila nenda kwao hadi aibu ,wanyakyusa tubadirike tuwe kama wachage tukumbuke kujenga kwetu na kuendeleza mji wetu hasa jimbo la busokelo ni hayo tu hujaelewa kaa pembeni ,.

Asante mkuu!
Kwa sasa hivi wimbo wa wananchi Rungwe uwe mmoja, BARABARA, barabara, barabara!

Mbunge asiyeuimba wimbo huu, tumchinjilie mbali!
 
Back
Top Bottom