Rungwe -Tukuyu pazuri kuishi 100%

Rungwe -Tukuyu pazuri kuishi 100%

Tukuyu town rungwe
Screenshot_2020-05-03-21-54-23.jpg
images%20(6).jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo la rungwe ni linasifika kwa unafuu wa maisha na mzunguko mzuri wa pesa
hapa tanzania.

Tuangalie sifa zake :

-Rungwe ni sehem nzuri kwa kilimo mfano ndizi, viaz mahind,maharage njugu,karanga nk

-Kiukweli Rungwe biashara yoyote inalipa we anzisha tu chochote utaona mafanikio.

-Watu wake ni wakarimu sana ila hawapend dharau.
-Hali ya hewa ni nzuri muda wote kutokana na miti ya matunda na mazao ya kilimo eneo zima la hapo.

-Rungwe hakuna kunyimana misosi ukimtembelea mtu kwake unapewa kamzigo

-Usafiri upo wa kumwaga noah,coster pamoja na hiace.

-Huduma za afya zipo za kutosha

-Ukiwa mtumishi wa umma unaweza ukajisahau hata kujenga maana vyumba ni bei chee sana. Mfano mji wa kibiashara wa Kiwira nyumba nzima elfu 70 kwa mwezi.

-Nauli mpaka Mbeya mjini ni buku 3 gari zake dk 45 tu umeingia mjini zinapaa mwendokasi.

-Wadada wa hapo ni kitonga sana hawaogopi kutoa mzigo nadhan ni kwasababu ya baridi ya kule lakini ukimkuta mlokole inabidi uokoke kwanza then ukajitambulishe kwa wazazi na mahali utoe ndio utakula mzigo.

-Ni vizuri uwe umeoa maana ukimwi upo nje nje.
-Watumishi wa Serikali mfano walimu walioanza kazi kule hawatakagi kuhama hiyo ni kutokana na unafuu wa maisha ukiwa na elfu kumi ukiingia sokoni unarudi na kiloba cha mazaga zaga.
-Ni sehemu ambayo watu wake jioni wanapiga pamba kali lakini asubuhi unawakuta mashambani wanachezea udongo.
-Watu wake wapo smart sana wanajua kuvaa
-Watu wake wanapenda sana dini, elimu na kilimo.
-Kama unapenda pombe hapa ndio penyewe
-Kama umeolewa halafu umehamia Rungwe unashinda ndani tu hujishughulishi na chochote utakoma na maneno ya wamama wa kinyakyusa sifa ya mwanamke wanajua ni kupiga kazi kusaidia familia.
-Watu wake wamechangamka muda wote


Mwisho::,,,,, kupanga ni kuchagua.






Sent using Jamii Forums mobile app
Du nahamia huko...!
 
Watu wa Tukuyu wamejazana hapa Dar, wamekuja kuendesha boda boda.

Eneo lolote la machakani hapa Tanzania utalipa maksi kama una kipato cha ajira. Kama unategemea ukaishi kama wanavyoishi, basi maisha sio mepesi huko. Kama ukiwa na kumi unarudi na full mazagazaga from sokoni ni wazi kuwa mkulima wa huko hali mbaya
Hii kitu ni uhalisia kabisa. Huko mikoani maisha ni mepesi ukiwa una ajira rasmi tofauti na bongo. Bongo mshahara tu hauwezi tosha ila kwa wafanyabiashara ni neema maana unakusanya hela nyingi kiwepesi zaidi tofauti na mkoani japo matumizi yako juu pia.
 
Wa huko watujuze huku ni wapi na viwanja vinapatikana maeneo haya

1588535611030.png





1588535752379.png


1588535840295.png
 
Wanyaki wanavinasaba the same na wahaya maana wanajisifia sana ila tukuyu baridi kama lote maparachichi, ndizi na mazagazaga
 


Rungwe/Tukuyu ikitulia halafu una wazee walotulia wakipiga mziki wa maana kama hawa basi tena wataka nini tena, na juu ya nini?
 
Nataka kwenda tukuyu kuanza maisha jamani,tupeane connection za michongo

Sent using Jamii Forums mobile app

Uwe na pesa ya kutosha kwa mwaka mzima.

Uwe na mwenyeji ambae atakuhifadhi kwa angalau mwezi 1

Uwe na plan ya maana kwa aina ya shughuli ukusudiayo kuifanya ukiwa Tukuyu.

Uwe na kazi yako au biashara yakoingine ya kukuingizia kipato wakati ukiwa watafuta venture ingine huko Tukuyu

Kwa mfano, haiwezekani mtu aje kutoka nje ya nchi na afanye shughuli za logistics kwa bidhaa kama parachichi na sisi watanzania tupo haoopo eneo la tukio.
 
Andiko lako limekuja kiumbeambea, kama sivyo ungeonyesha picha maneno matupu ya nini
 
Back
Top Bottom