Rungu la mabadiliko laja kufyeka Majimbo ya Uchaguzi 84 na nafasi za Viti Maalum 44: Serikali kuokoa Tsh. 122,000,000,000.

Edit habari yako; kwenye idadi ya viti vipya vya ubunge baada ya hayo mabadiliko
 
Kama itakuwa fair hakuna shida hata hivyo uwingi wa wabunge haujaleta tija ni bora hata kuwe na mbunge mmoja kila wilaya na kusiwe na wa viti maalumu na wa kuteuliwa. Mawaziri wasiwe wabunge ili kuimarisha uwajibikaji na utendaji. Hakuna haja ya kuwa na majimbo mawili au matatu katika wilaya moja wakati wilaya hiyo hiyo inaongozwa na mkuu mmoja wa wilaya. Kwa upande wa Zanzibar wabunge kule wawe watano tu siyo mtu anakuja katika bunge la jamhuri akiwakilisha watu elfu tatu au nne ambao ni wachache kuliko hata wanafunzi wa shule au chuo kimoja. Wabunge wa Zanzibar katika bunge la jamhuri ni wengi mno tofauti na idati ya watu kule. Napendekeza pia wabunge wa Zanzibar wahudhurie bunge wakati wa mijadala ya bajeti za wizara za muungano baada ya hapo warudi zao Zanzibar wakati wa mijadala ya bajeti za wizara za Tanganyika hiyo itasaidia kupunguza matumizi sana na kwa kiwango kikubwa
 
tapatalk_1534791584816.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na pia vile viti vya mkuu vipunguzwe maana sio halmashauri............. vibaki 0000.
 
View attachment 842818

Panga la mabadiliko katika Majimbo ya Uchaguzi, linaweza kuyakumba Majimbo ya Uchaguzi nchini yapatayo 264 endapo Mapendekezo yanayotolewa na wadau, yatakubaliwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).
Kulingana na taarifa zilizoandikwa na Jamhuri, kuna Mapendekezo kuwa, Majimbo ya Uchaguzi yaendane na Halmashauri zilizopo Tanzania Bara ambazo ni 186 (plus 16 wa kuteuliwa). Vilevile, nafasi ya viti maalum inapendekezwa kuwa asilimia 35% ambazo zitakuwa sawa na Viti 69. Hivyo, Bunge litakuwa na Wabunge 271 badala ya 264 na hivyo tofauti kuwa 122.
Mishahara, posho, marupurupu na kiiinua mgongo cha Wabunge hao 122, kwa kipindi cha miaka mitano, ni sawa na Tsh. bilioni 122.
View attachment 842814View attachment 842822
GPA ya 32 SUA Dodoma, hesabu zako ngumu.
 
Baada ya kazi ya kutunga sheria kukamilika, bunge lilitakiwa libaki na wabunge 31 tu, kila mbunge 1 akiwakilisha mkoa. Ok, basi tufanye twice as much so wangekuwa wabunge 62, wawili kila mkoa. Au basi hata tufanye mbunge mmoja kwa kila wilaya, maximum bunge lilitakiwa liwe na wabunge 150 tu.
 
Nani aliyeyaongeza majimbo?
Nadhani tuanzie hapo.Kama aliyeyaongeza
ameamua kuyapunguza binafsi sioni tabu.
ukiangalia majimbo mengi,kata na halmashauri
nyingi zimeongezwa kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Lengo kubwa analijua aliyeamua kuyaongeza,labda ameona
lengo lake limetimia hivyo anayapunguza.
mimi kama mtanzania mlipa kodi ni heri yapunguzwe
maana kazi ya kusema ndiyooo haihitaji watu wengi sana.
 
Nami naunga mkono hoja ya kupunguza wabunge. La kwanza kabisa waondoe viti maalum. Pili wapunguze majimbo
Good idea. Nchi nyingi idadi ya wabunge iko constant. Lakini TZ kila kipindi cha uchaguzi majimbo yanaongezeka for NO REASON.Mara nyingi huwa ni kwaajili ya kulinda masilahi wa watu fulani. Itafika kipindi itabidi wajenge ukumbi mpya wa bunge au pengine mikutano ya bunge kufanyika uwanja wa Jamhuri kutokana na uwingi wa wabunge. Nonsense. Idadi ya wabunge LAZIMA ITHIBITIWE NA IWE CONSTANT KULINGANA NA WILAYA HUSIKA. WILAYA MOJA MBUNGE MMOJA. IT IS ENOUGH.
 
Panga la mabadiliko katika Majimbo ya Uchaguzi, linaweza kuyakumba Majimbo ya Uchaguzi nchini yapatayo 264 endapo Mapendekezo yanayotolewa na wadau, yatakubaliwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).
Sioni wapi kwenye hiyo taarifa mapendekezo hayo yametolewa na wadau. Haya nielewavyo hiyo taarifa ya Jamhuri ni mapendekezo yanayo toka na yanafanyiwa kazi na serikali. Nafikiri ni muhimu tukajua hao wadau ni wepi au mkuu una source nyingine?
 
Watanganyika kila kitu tunaingiza siasa na uchama. Sasa hivi kuna wabunge kama utitiri na hawana maslah yoyote kuwepo kwao bungen. Mfano dar tu kuna wabunge zaid ya saba wote hao wa nn? Na kwa mwez kila mmoja anapata hela zaid ya dc,DAS na mkurugenzi kwa pamoja. Hii itapunguza sana gharama za uendeshaji wa serikali na kufanya kupatikana wabunge bora na sio bora mbunge
Kama una uchungu kwanini usipendekeze tufute wakuu wa wilaya type ya jery muro na jokate hawana faida yoyote no hasara tu.
 
Back
Top Bottom