Rungu la mabadiliko laja kufyeka Majimbo ya Uchaguzi 84 na nafasi za Viti Maalum 44: Serikali kuokoa Tsh. 122,000,000,000.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
IMG_6454.JPG


Panga la mabadiliko katika Majimbo ya Uchaguzi, linaweza kuyakumba Majimbo ya Uchaguzi nchini yapatayo 264 endapo Mapendekezo yanayotolewa na wadau, yatakubaliwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

Kulingana na taarifa zilizoandikwa na Jamhuri, kuna Mapendekezo kuwa, Majimbo ya Uchaguzi yaendane na Halmashauri zilizopo Tanzania Bara ambazo ni 186 (plus 16 wa kuteuliwa). Vilevile, nafasi ya viti maalum inapendekezwa kuwa asilimia 35% ambazo zitakuwa sawa na Viti 69. Hivyo, Bunge litakuwa na Wabunge 271 badala ya 393 na hivyo tofauti kuwa 122.

Mishahara, posho, marupurupu na kiiinua mgongo cha Wabunge hao 122, kwa kipindi cha miaka mitano, ni sawa na Tsh. bilioni 122.

IMG_6453.JPG

IMG_6455.JPG
 
Duh! Hii itasaidia kupunguza matumizi ya serikali lakini pia ni njia makini sana ya kumaliza vyama vya upinzani kwa kufuta majimbo yaliyo chini ya upinzani na kurahisisha 'goli la mkono'!

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu kma animeelewa ni kuwa watafuata mfumo wa Halmashahuri Moja Mbunge Mmoja, sioni ttaizo hapo mbona?
 
Kuthibiti majimbo yote nchi nzima ni kazi hivyo ni lazima yapunguzwe maana hata askari watakuwa ni wachache.

Hawa wanaonunua wanasiasa na kusababisha nchi iimgie kwenye uchaguzi kila siku msidhani wana uchungu na hela za watanzania.

Uzuri wa maamuzi haya ni hata CCM wataathrika ila panga linaweza kupitishwa zaidi katika maeneo ambako upinzani una nguvu.


Hata hivyo, kwakuwa Bunge lenyewe halina nguvu, wacha tu wawapunguze maana kodi zetu zinapotea bure tu kulipa wabunge wa ndio.
 
Duh! Hii itasaidia kupunguza matumizi ya serikali lakini pia ni njia makini sana ya kumaliza vyama vya upinzani kwa kufuta majimbo yaliyo chini ya upinzani na kurahisisha 'goli la mkono'!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini uone kwamba ni njia ya kuua upinzani na si kukata matumizi ambayo si ya lazima?

Katika hili naiunga mkono serikali kwa asilimia zote. Kama hoja ni kupeleka madaraka na uwakilishi mkubwa wa wananchi katika usimamizi wa rasimali na matatizo yao, basi ni bora uongezwaji wa Wilaya na sio utitizi wa majimbo!

Isipokuwa kwamba katika mfumo huo mpya ambao Wilaya zitageuzwa kuwa eneo jimbo, basi ni vema Ofis ya Mbunge itanuliwe kutoa nafasi ya kuwa shirikishi zaidi kwa kuongeza watumishi ofini hapo.
 
Kuthibiti majimbo yote nchi nzima ni kazi hivyo ni lazima yapunguzwe maana hata askari watakuwa ni wachache.

Hawa wanaonunua wanasiasa na kupelekea nchi kuingia katika uchaguzi tangu lini wakawa na uchungu na hela za walipa kodi wa nchi hii?!

Uzuri wa maamuzi haya yataathiri pia wana-CCM ingawa panga la kupunguza majimbo linaweza kuelekezwa zaidi katika maeneo ambayo upinzani una ngyvu.
 
Hawaoni kuwa gharama wanayotumia kununua wapinzani ni hatari zaidi kuliko gharama ya kuhudumia majimbo?kwa kuwa gharama zinazokwenda kwenye majimbo zinawafaidisha wananchi moja kwa moja.
 
Watanganyika kila kitu tunaingiza siasa na uchama. Sasa hivi kuna wabunge kama utitiri na hawana maslah yoyote kuwepo kwao bungen. Mfano dar tu kuna wabunge zaid ya saba wote hao wa nn? Na kwa mwez kila mmoja anapata hela zaid ya dc,DAS na mkurugenzi kwa pamoja. Hii itapunguza sana gharama za uendeshaji wa serikali na kufanya kupatikana wabunge bora na sio bora mbunge
 
Back
Top Bottom