Ruling Kuhusu Kesi ya Lema ni Leo!!

more updates pls, tunafuatilia uzi kutoka mtambaswala (mpakani tz na msumbuji)
 
muanzisha thread pls uwe unaifanyia updates pale mwanzo kwa kila tukio litakalokuwa linatokea. wazalendo wengi wanaifuatilia habari hii through JF.
 

Afadhali umeweka sawa naona watu wanachanganya mambo hapa leo ni Rulling itatolewa aidha rufaa ya Lema iendelee kusikilizwa au la baada ya mlalamika kuweka pingamizi ya rufaa ya Lema.
 

Na kwa jinsi pingamizi lenyewe lilivyokaa kuna uwezekano mkubwa likakubaliwa ila tusubiri tuone.
 
Karani wa mahakama ameanza kusoma dondoo
-Mawakili wanatambulishwa
 
Wanabodi na wanaushirika.

Tujenge utamaduni wa kuheshimu uhuru wa mahakama tukubali hukumu yoyote itakayotolea na mahakama.
kabisa mkuu Ritz
 
Watu wanaendelea kuja.Foleni ilikua changamoto kwa wengi
 
Majaji wanahitaji busara ya kawaida tu kwani kwa namna yoyote Arusha haiwezi kwenda CCM. Wasipomrudishia ubunge wake, wananchi wa Arusha watafanya hivyo, tena kwa kishindo.
 
Karani wa mahakama ameanza kusoma dondoo
-Mawakili wanatambulishwa
Tupatie UPDATE mkuu, thanx, Please Mods tulekibishieni Title coz kuna watu wapo live....JF msituangushe..
 
Karani wa mahakama ameanza kusoma dondoo
-Mawakili wanatambulishwa

Ben tunashukuru ukitupa update sawia kadri mambo yatakavyokwenda vipi upande wa watu wamejitokaza kufuatilia kesi hiyo?
 

Point of correction, ni Court of Appeal of Tanzania, sio High court na sio majaji wa mahakama kuu ni majaji wa mahakama ya rufaa wakiongozwa na jaji mkuu.
 
Wanabodi na wanaushirika.

Tujenge utamaduni wa kuheshimu uhuru wa mahakama tukubali hukumu yoyote itakayotolea na mahakama.

Hacha kuwafunza watu ushupavu wa mende wewe,waikubali hukumu hata kama haikutenda haki? mara ngapi tunashuhudia muhimili huu huu wa dola ukiwapoka watu haki zao za msingi,eti kwa sababu tu wanahatarisha maslahi ya watu wengine ambayo mara nyingi huwa siyo haki zao.
 
Karibu sana.Tupo Mahakamani.Kamanda Lema ameshaingia amekaa kiti cha Mbele ........

Safi sana kamanda. Mtujuze kila kinachojiri huko mahakamani. Mkiweza kutiririka kama alivyofanya kamanda Mungi last time kutoka Arusha mtakuwa mmeitendea haki sana JF.
 
Naishukuru sana Jamiiforums ,nafuatilia hatma ya pingamizi la Hukumu ya kuvuliwa Ubunge wa Mh Lema kutoka Mikindani-Mtwara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…