Ruge wa Clouds yuko live kumjibu Jide

twatwatwa

JF-Expert Member
Sep 19, 2011
2,067
419
ile cinema ya jide dhidi ya ruge na wajanja wenzie inaendela sasa kwa ruge kumjibu jide tegeni sikio kwenye redio cloudsfm sasa


Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu,
hatimaye mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
ameamua kujibu shutuma za LadyJaydee dhidi yake.

Ruge amekitumia kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM, kujibu rasmi shutuma hizo.
Amesema anasikitishwa na jinsi Jaydee anavyoendesha harakati zake na kudai
kuwa anapigana kwenye vita isiyo sahihi.

"Jaydee akaze buti, anapigana na wrong war, vita yake ameidirect tofauti na
mizinga yake, bunduki zake amezielekeza kusiko. Skylight Band
inamsumbua, akubaliane na ukweli kwamba Skylight ndio iliyoisababishia
Nyumbani Lounge kushuka ilivyoshuka,sio Lady Jaydee kama msanii.

Vita yake na bunduki zake azielekezee Skylight Band. Hajazungumza hata mara moja
kwamba ndio kitu kinachosumbua. Mimi naamini kabisa akifanya hiyo kazi,
Jaydee bado ni msanii mzuri, ana nguvu, afanye kazi kubwa ya kuweza
kurudisha mapambano yake kisanii, kufanya kazi na aangalie tatizo
lililotokea Nyumbani Lounge labda anaweza akatatua matatizo lakini sio
kushambulia watu kwenye mitandao," amesema Ruge.

Hata hivyo amesema yupo tayari kukaa meza moja na Lady Jaydee kuzungumza
na kumaliza tofauti zao. "Mimi niko tayari, kesho, kesho kutwa,
kama yupo tayari na ana watu wengine wengi tu ambao wanahisi kuna matatizo
binafsi ya kuongea na Clouds, twende sehemu nyingine neutral tu, tukodishe,
tukae pale tusikie matatizo.

Haisaidii muziki wetu kuonekana Bongo Flava ni watu ambao kutwa ni kulalamika, kutwa
ni maneno na matusi tu pale panapokuwa na matatizo."
Ameongeza kuwa suala la wasanii wa Bongo Flava kupenda kutukana
limewafanya hata wasambaji wa muziki nchini kuacha kufanya kazi nao.

"GMC kampuni iliyowapa pesa nyingi wasanii kwenye biashara sio kuwapa tu
kwa kuwagawia, kwa kufanya nao biashara, sasa hivi huu ni mwaka wao
wa pili na nusu hawajatoa hata albam moja ya Bongo Flava. Wasanii wa Bongo
Flava wanafikiria kwa Mamu pamefungwa lakini Mamu anaendelea
na wasanii wa Gospel na wanauza vile vile.

Ruge amewaasa wasanii wa Tanzania akiwemo Lady Jaydee kuzitumia vizuri
fursa za kiuchumi zinazojitokeza na sio kupenda kulalamika.
"Turudi kwenye mstari wa kuziona opportunities, turudi kwenye mstari wa
kusema kwamba leo tunataka kumzungumzia Jaydee akiwa na
perfume, akiwa na lipstick kama jana iliyozinduliwa na Rihanna ambayo
nikaambiwa kwamba stock ya lipstick mpya ya Rihanna iliyozinduliwa ilikwisha
baada ya masaa matatu.

That's how bigger brand is supposed to be, and that's how powerful a brand is
supposed to be katika namna ya kuunganisha na fursa zilizopo.
Unapokuwa na jina tumia fursa, tumia opportunities zinazokuijia wewe
kujiendeleza na kujikuza.

Lakini suala la kulaumiana halitatukuza kwasababu sisi ni radio binafsi, tutafanya kile
tunachokifanya sisi kwa matakwa ya wasikilizaji wetu wengi zaidi, tukiiangalia
faida kama motivation, tukiiangalia social responsibility kama motivation
yetu ya pili, in the long run kuangalia tunakotaka kwenda kufikia strategy
ambayo kampuni yetu inajiwekea."

Ruge pia amewakumbusha wasanii kutojisahau kwakuwa hakuna msanii
anayeweza kuhit maisha yake yote. "Tuwaandae wasijisahau, na katika hili
simzungumzii Jaydee peke yake, nazungumzia wasanii wote wa Tanzania
nawazungumzia kuelewa kwamba tunajisahau sana.

Tunapata hela nyingi sana, sitashangaa miaka mitatu baada
ya leo, Ommy Dimpoz naye ukamsikia anaandika hivi hivi, au Diamond naye ni
kwasababu hakujipanga tu."

Kuhusu shutuma kuwa Clouds FM inaua
muziki wa Bongo Flava, Ruge amesema,
"inanishangaza kidogo kwasababu
Clouds inategemea matangazo ya
biashara kwa asilimia 95, ndio biashara
yake hiyo. Lakini inategemea muziki wa
Bongo Flava kama maudhui ya kipindi,
inaanzaje kuuua, inategema wasanii wa
Bongo Flava kama wasanii wa kwenda
kufanya shows mkoani."
Kuhusu msimamo wa kampuni Ruge
amesema:
Msimamo wa kampuni ni kwamba
tunaamini kabisa mwanadada kinara wa
muziki wa Tanzania naamini atakaa na
kutafakari la kufanya. Tunamtakia kila
lakheri kwenye show yake ya tarehe 31
afanye vizuri lakini atakapokuwa tayari
sisi tuko tayari kuendelea kufanya kazi,
anajua cha kufanya. Chanzo cha haabari Bongo 5.

Habari wanaJf,
Nimebahatika kusikia alichoongea Boss Ruge kama wanavyomuita wafanyakazi wa clouds Fm, eti leo hakuna kupiga bongo flava kwenye redio yao.Swali langu hii kama ni redio ya watu hizo bongo flava ambazo amesema zisipigwe na kwa ajili ya wanyama au viumbe wa sayari nyingine.Angefanya la maana asema kabisa kuanzia leo redio yao haitapiga Bongo fleva au imekua ni redio ya gospel hapo ningemkubali,but the way amesema ni kwa siku ya leo,tena kwa kuamrisha kabisa,"nimesema leo hakuna kupiga bongo fleva mpaka saa sita usiku" mi sielewi kwa kweli ,anafanya hivyo kumkomoa nani.Lady Jay dee au waskilizaji wao.Eti redio ya Watu.ama kweli kuwa mkurugenzi sio tu jina,hata kichwani nako kunahusika.Maneno aliyoongea kwa kweli sio ya kiutendaji.Halafu anailaumu serikali eti imeshindwa kufanya kazi yake kwa kuwakamata wanaowachafua na kuwatukana watu kwenye mitandao.Leo ndio ameona ? Tangu siku zote alikuwa wapi.? na anasema eti hataongea tena kuhusu hili suala la yeye na Lady Jay Dee,..Ningemuona wa busara kama angeenda kuongea naye kabla hajaja kwenye media yao na kuliongelea hili.Haya malumbano ya clouds na wasanii wetu wa hapa nchini yanaelekea kuipeka hii tasnia yetu ya mziki wapi?
 
Namsikia huyu mwizi...
anasema eti wamesajili TCRA n.k
anaendelea kutiririka
 
Kumbe ugomvi wao ulianza siku nyingi.
Clouds inasupport SKYLIGHT band badala ya MACHOZI band.
 
Ruge ametunza mpka meseji.lol.ugomvi skylight band chanzo moja wapo
huu ugomvi tununue pop corn na coca tutizame
:coffee::coffee:
 
Saida Kaloli njoo na wewe ulalamike usikae kimya...tunajua ulichofanywa but umekaa kimya
 
Back
Top Bottom