Hivi nitakuwa nimekosea?

Hivi nitakuwa nimekosea?

Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
3,756
Reaction score
5,298
Habari zenu wakuu, natumai mpo sawa kiafya. Nisiwapotezee sana muda, tuingie kwenye lengo la kuandika chapisho hili.

Wadau nimekaa nikawaza kuhusu huu muziki wa Bongo flava, nikaona kuna kitu ambacho sisi ambao tulianza kuufuatilia muziki zamani tunakikosa.

Bongo flava ya kipindi kile na ya sasa, midundo hadi namna ya uimbaji imebadilika kwa kiasi kikubwa. Unakuta sisi ambao tulizoea muziki ule wa mwanzo wa miaka ya 2000 na mwishoni mwa miaka ya 1990, tunajiona tunakosa burudani ile.

Hivi wadau hawa wanamuziki wakongwe wakikaa na kuanza kutumia Old school Bongo flava ni vibaya? Iwe kama alama kama reggae na muundo wake uleule miaka nenda rudi.

Tupate burudani ileile ya zamani kwa kizazi hichi na wapenzi wa kizazi cha sasa wabaki na waimbaji ambao wanaupenda.

Iwe kama Ottu jazz (Msongo Ngoma), DDC Mlimani park na bendi zingine ambao hawakuacha aina yao ya uimbaji hata katika ujio wa muziki wa kizazi kipya. Waliendelea kusikika na kuwaimbia mashabiki wao.

Bongo flava ile ya zamami Producers wake wapo na wengine bado wanafanya kazi mpaka, composers waliyowasaidia kuongeza vionjo kwenye beats bado wapo.

Hivi inashindikana kweli kuurudia muziki ule wa mwanzo? Wapenzi wa huu mpya wabaki nao bila kuathiri na wa zamani wabaki nao pia.

Wakongwe waache kukazania muziki aina ya mpya warudi kwenye ule ambao uliwatoa na kuwapa jina na heshima. Soko lao lilenge mashabiki wa kipindi kile, ambao hivi sasa ni watu wazima na familia zao
 
Tatizo wanaofatilia sana mziki kwasasa ni hao gen Z, ambao kwa hizo old school bongo flava wanaona ni nyimbo za kizee hawazipendi zimepitwa na wakat, na wanaopenda hiyo miziki ni watu ambao wapo busy na maisha yao, mziki tena sio jambo la maana sana kwao hawafatilii kivile (ufatiliaj ni mdogo). Mziki kwa sasa ni biashara na wateja wakubwa wanaofatilia sana mziki huko youtube na kwenye platfom mbalimbali ni hao gen Z kizazi ambacho hakipend hizo bongo za zaman! Ushapata jibu kwann hao wakongwe wanajitahd kubadr stail ya uimbaj kuendana na soko la wahtaj
 
Nadhani ifanyike hamasa na wakongwe wasimame kwenye kuweka nyimbo zao hizo platforms za kusikiliza walipwe. Kama albamu za zamani kwenye hizo platforms zinaingiza hela hadi leo hii. Sidhani kama watashindwa wakifanya hamasa.

Ule muziki wa kusubiri upigwe redioni na auze kanda haupo, hivi sasa ni kuupigania muziki wenyewe. Si kutoa wimbo usubiri wausikie redioni

Hao hao wasikilizaji wao wakubwa wanaweza pata kwenye simu wakawasiliza kupitia hizo app kama Boomplay, Sportify na zinginezo. Wawe wanapata burudani wakiwa nyumbani au kwenye shughuli zao. Pia tamasha wakiandaa waangalie maeneo ambayo yana mashabiki wao kwa wingi sio kisa ni mjini tu
 
Back
Top Bottom