Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu,
hatimaye mmoja wa wakurugenzi wa
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
ameamua kujibu shutuma za Lady
Jaydee dhidi yake. Ruge amekitumia
kipindi cha Power Break Fast cha
Clouds FM, kujibu rasmi shutuma hizo.
Amesema anasikitishwa na jinsi Jaydee
anavyoendesha harakati zake na kudai
kuwa anapigana kwenye vita isiyo
sahihi.
"Jaydee akaze buti, anapigana na wrong
war, vita yake ameidirect tofauti na
mizinga yake, bunduki zake
amezielekeza kusiko. Skylight Band
inamsumbua, akubaliane na ukweli
kwamba Skylight ndio iliyoisababishia
Nyumbani Lounge kushuka ilivyoshuka,
sio Lady Jaydee kama msanii. Vita yake
na bunduki zake azielekezee Skylight
Band. Hajazungumza hata mara moja
kwamba ndio kitu kinachosumbua. Mimi
naamini kabisa akifanya hiyo kazi,
Jaydee bado ni msanii mzuri, ana
nguvu, afanye kazi kubwa ya kuweza
kurudisha mapambano yake kisanii,
kufanya kazi na aangalie tatizo
lililotokea Nyumbani Lounge labda
anaweza akatatua matatizo lakini sio
kushambulia watu kwenye mitandao,"
amesema Ruge.
Hata hivyo amesema yupo tayari kukaa
meza moja na Lady Jaydee kuzungumza
na kumaliza tofauti zao.
"Mimi niko tayari, kesho, kesho kutwa,
kama yupo tayari na ana watu wengine
wengi tu ambao wanahisi kuna matatizo
binafsi ya kuongea na Clouds, twende
sehemu nyingine neutral tu, tukodishe,
tukae pale tusikie matatizo. Haisaidii
muziki wetu kuonekana Bongo Flava ni
watu ambao kutwa ni kulalamika, kutwa
ni maneno na matusi tu pale
panapokuwa na matatizo."
Ameongeza kuwa suala la wasanii wa
Bongo Flava kupenda kutukana
limewafanya hata wasambaji wa muziki
nchini kuacha kufanya kazi nao.
"GMC kampuni iliyowapa pesa nyingi
wasanii kwenye biashara sio kuwapa tu
kwa kuwagawia, kwa kufanya nao
biashara, sasa hivi huu ni mwaka wao
wa pili na nusu hawajatoa hata albam
moja ya Bongo Flava. Wasanii wa Bongo
Flava wanafikiria kwa Mamu
pamefungwa lakini Mamu anaendelea
na wasanii wa Gospel na wanauza vile
vile.
Ruge amewaasa wasanii wa Tanzania
akiwemo Lady Jaydee kuzitumia vizuri
fursa za kiuchumi zinazojitokeza na sio
kupenda kulalamika.
"Turudi kwenye mstari wa kuziona
opportunities, turudi kwenye mstari wa
kusema kwamba leo tunataka
kumzungumzia Jaydee akiwa na
perfume, akiwa na lipstick kama jana
iliyozinduliwa na Rihanna ambayo
nikaambiwa kwamba stock ya lipstick
mpya ya Rihanna iliyozinduliwa ilikwisha
baada ya masaa matatu.
That's how bigger brand is supposed to
be, and that's how powerful a brand is
supposed to be katika namna ya
kuunganisha na fursa zilizopo.
Unapokuwa na jina tumia fursa, tumia
opportunities zinazokuijia wewe
kujiendeleza na kujikuza. Lakini suala la
kulaumiana halitatukuza kwasababu sisi
ni radio binafsi, tutafanya kile
tunachokifanya sisi kwa matakwa ya
wasikilizaji wetu wengi zaidi, tukiiangalia
faida kama motivation, tukiiangalia
social responsibility kama motivation
yetu ya pili, in the long run kuangalia
tunakotaka kwenda kufikia strategy
ambayo kampuni yetu inajiwekea."
Ruge pia amewakumbusha wasanii
kutojisahau kwakuwa hakuna msanii
anayeweza kuhit maisha yake yote.
"Tuwaandae wasijisahau, na katika hili
simzungumzii Jaydee peke yake,
nazungumzia wasanii wote wa Tanzania
nawazungumzia kuelewa kwamba
tunajisahau sana. Tunapata hela nyingi
sana, sitashangaa miaka mitatu baada
ya leo, Ommy Dimpoz naye ukamsikia
anaandika hivi hivi, au Diamond naye ni
kwasababu hakujipanga tu."
Kuhusu shutuma kuwa Clouds FM inaua
muziki wa Bongo Flava, Ruge amesema,
"inanishangaza kidogo kwasababu
Clouds inategemea matangazo ya
biashara kwa asilimia 95, ndio biashara
yake hiyo. Lakini inategemea muziki wa
Bongo Flava kama maudhui ya kipindi,
inaanzaje kuuua, inategema wasanii wa
Bongo Flava kama wasanii wa kwenda
kufanya shows mkoani."
Kuhusu msimamo wa kampuni Ruge
amesema:
Msimamo wa kampuni ni kwamba
tunaamini kabisa mwanadada kinara wa
muziki wa Tanzania naamini atakaa na
kutafakari la kufanya. Tunamtakia kila
lakheri kwenye show yake ya tarehe 31
afanye vizuri lakini atakapokuwa tayari
sisi tuko tayari kuendelea kufanya kazi,
anajua cha kufanya. Chanzo cha haabari Bongo 5.