"Rudi huko huko" au "Kalale huko unakotoka"... wanatarajia nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Rudi huko huko" au "Kalale huko unakotoka"... wanatarajia nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 11, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Hivi mpenzi wako au mwenza wako anapokasiria umekuwa ukichelewa chelewa nyumbani na hivyo anakujia juu na kukuambia rudi huko huko kweli anafikiria nini? Hivi ukiamua kugeuza mlangoni na kwenda "huko huko" hadi kesho yake au mtondogoo anaweza kukulaumu? Lakini pia kwaninii tufike mahali mtu atamani usilale nyumbani kwako mwenyewe? Nini kitamfanya mtu awe anachelewa nyumbani namna hiyo hadi kumfanya mwenzie atamani arudi "huko huko".

  Hivi kweli wanaume wakirudi huko "wanakotoka" familia zitasalimika? Hivi wapo wanaume wanaowaambia wake zao au wenza wao "wakalale huko huko"?

  Vipi wale wanaowaambia watoto wao hivyo?
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hizo huwa zina sababishwa na hasira ambapo akikaa muda kidogo anakuwa mpole..na kwa upande wa mtoto akiambiwa hivyo basi baada ya muda utamuona mzazi anaanza tena kumtafuta hiyo yote ni sababu ya hasira tu
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Anasema hivyo akipata moto tu...hakuna awezae maanisha maneno hayo.
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180

  IMO nafikiri ni hasira mara nyingi... na mwanaume akikuta kua Mkewe anamuambia hivo ajue kabisa hamtendei haki for yaonesha wazi huyo mwanamke bado anampenda... For angekua hampendi angefungua mlango kimya kimya bila hata lawama... na lawama yaweza kua more of kumsumbua kumtoa kitandani kuliko sababu ya kuchelewa... hapa mume asishangae mkewe akichongesha funguo na kumkabidhi ili walau asisumbuliwe usiku....

  Kuhusu why wanaume wanachelewa siku zoote kurudi... hapa sababu ni lukuki kwa kweli tokana na kwamba matatizo ya ndoa hu-vary from one to another... sababu ya kuchelewa yaweza kua sababu ya Mke ama Mme ama Wooote.
   
 5. RR

  RR JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama wanamaanisha hayo....
  Sawa na yule amtukanae mtoto wake 'mbwa', 'farasi' nk

   
 6. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,ngoja nikupe kisa cha ukweli.Jamaa yangu kuna siku alirudi usiku sana,mkewe akaleta hizo 'kalale huko huko'akagoma kufungua mlango.Jamaa alikuwa na landrover,all he did alichukua mnyororo akafunga kwenye mlango wa mbele akatia gia,vruuuuuuuu akaung'oa,mama akashtuka kishindo kutoka chumbani mlango wa mbele aliukuta barazani.Kilichofuata ni kibondo.Kesho yake namuuliza jamaa kulikoni,akasema 'nyumba yangu unifungie nje?'
   
 7. Poetik Justice

  Poetik Justice Member

  #7
  Oct 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi mpenzi wako au mwenza wako anapokasiria umekuwa ukichelewa chelewa nyumbani na hivyo anakujia juu na kukuambia rudi huko huko kweli anafikiria nini?
  Ni hasira hizo. Tabia imemkera kiasi kwamba anaona uende "hukohuko"!


  Hivi ukiamua kugeuza mlangoni na kwenda "huko huko" hadi kesho yake au mtondogoo anaweza kukulaumu?
  Yes. Atakulaumu kwa kuendeleza "irresponsibility"!


  Lakini pia kwaninii tufike mahali mtu atamani usilale nyumbani kwako mwenyewe?
  Very good question. Amependa tu kulala nje bila kujali consequences zake.

  Nini kitamfanya mtu awe anachelewa nyumbani namna hiyo hadi kumfanya mwenzie atamani arudi "huko huko".
  Affair....pombe....marafiki....labda ni watchman au muuguzi. Ana kazi za usiku...

  Hivi kweli wanaume wakirudi huko "wanakotoka" familia zitasalimika?
  Nope!

  Hivi wapo wanaume wanaowaambia wake zao au wenza wao "wakalale huko huko"?
  Yes! Tofauti ni ....pengine wengine wanarudi "huko huko" kama bado pako wazi. Wengine wanarudi kwa ndugu lawama ipungue nguvu.

  Vipi wale wanaowaambia watoto wao hivyo?
  Hasira pia! Tabia inakua imekithiri!
   
 8. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,944
  Trophy Points: 280
  Nafikiri haya hii ni dhana hasi ambayo kama haimaanishi kuwa ulikotoka si pahala adilifu basi dhana hii haipo mbali na nadharia hii...na hii cancer ya mtu kukinai nyumbani kwake mwenyewe inachangiwa na mambo mengi..mojawapo ikiwa ni mhusika mojawapo(aliyebaki/anayetoka)...ila yatosha kabisa kusema hasira haina staha,hivyo lolote laweza kumtoka mtu pindi hasira ikimpata!
   
 9. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Bi Asha acha kutetea ukorofi,utamfungiaje nje mmeo eti ni mapenzi? What if anafukuzwa na majambazi,wakimuulia mlangoni utasemaje? unakumbuka kisa cha jamaa mmoja maarufu kwenye michezo aliyevunjika mguu akafa kisa anaruka ukuta aingie ndani baada ya mkewe kumfungia nje?ilitokea kimara mwaka juzi,do you remember that? Jamaa alikuwa mnyamwezi,last respects tulifanyia national stadium.
   
 10. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  huwa wanakurupuka au wanajaribu kutumia udhaifu wake kwa kumfukuza au kumrudisha mtui alikotoka japo ni hatari zaidi kwani yatanengeneza mianya mingine isiyo na ulazima
   
 11. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ukishaambiwa hivyo, dhubutu kuondoka ndo utakapojua kama anamaanisha au la!
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180

  Wanaume bana!!!!!!! Hamkosi sababu... Usiku wa manane unarudi nyumbani kwako... cha ajabu nini kukimbizwa na majambazi?? lol
   
 13. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nadhani unamaanisha Charles Masanja..ryte??...Sikuwa najua kama alifungiwa nje na mkewe!!!
   
 14. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  haya ndugu naona uliipania hii mada
   
 15. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  hahahahaaa Bishanga bana! Kwa hiyo akivamiwa akiwa njiani ndo itapendeza? Halafu huyo aliyeruka ukuta alijitakia mwenyewe for alijitia kuyaweza manyanga (sad), angepungukiwa nini endapo angejifanya mpole ili afunguliwe mlango? Au kwa nini asingeenda kulala hata kwa ndugu??
   
 16. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mmmmmmhhh cha ajabu nini kufukuzwa na majambazi........hii kali ya 2011!.....yaani mke wangu aniache nichinjiwe getini? Kisa mapenzi? Lol aanze yeye kuondoka kabla sijavunja mlango.
   
 17. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,653
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Wewe ukiambiwa hivyo utafanyaje MM?
   
 18. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dah! Hii kitu imenikumbusha habari ya mkuu mmoja hivi (RIP).
  Alichelewa kurudi home (sina hakika kama ilikuwa ndo kawaida yake). Mama akagoma kufungua mlango. Jamaa akaamua kupanga matofali ili adandie ukuta. Kwa bahati mbaya akaporomoka, akapelekwa hospitali, akapoteza maisha siku ya pili yake.
  Sijui mkewe alifanyaje maskini!
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  tafazali Kipipi,nyumba nijenge mimi kulala nilale kwa jirani? Arrrrrrrrooooo tena usirudie kusema maneno hayo!
   
 20. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  ni kumfumngulia halafu mnamalizana huko huko ndani
   
Loading...