Rtd General Mboma, Mhando wa TANESCO na Mh. Mbunge - ni Hatari!!

Matatizo hayo ya TANESCO hayataisha kutokana na kulazimisha njia ya msongo kubwawa umeme kutoka Ubungo hadi Mwenge mpaka mabango mliyoyabomoa kanisani myarudishe na kutubu. Wote waliohusika wameendelea kushughulikiwa Jairo, Ngereja na wengine unaweza kuongezea orodha. Kumbukeni zile fulana ziliwaonya kuwa mwogopeni Mungu.
 
Tanzania bila ukimwi haiwezekani
kabisa!Mbunge anatoa rushwa ya
Ngono!
Hadi dhaifu amalize hii game tutasikia mengi sana!
 
Walakini katika hoja zako:
Kulipiwa chakula ni jambo dogo
Bei ya mafuta sokoni (filling station?) 1500???
Lack of managerial skills basing on what?
Tupe sababu za kuikataa hiyo budget ya wazira kama ulivyohamasishwa

Mleta mada, ingekuwa vyema pia ungetuambia
1) uzalishaji na mahitaji yako vipi kwasasa?
2) Tangu Mhando, Eng. aingie madarakani, performance ya TANESCO iko vipi?

Kama kuna mdau mwenye CV ya Mhando, Eng. basi aitupe hapa tupime kilichowasilishwa jamvini
Tumia akili kidogo,mafuta wanaonunua kuendeshea mitambo makampuni haya makubwa yanapuunguzwa aina fulani ya kodi kama sio kuondolewa kwa kiwango kikubwa hivyo bei kuwa 1500/- Tshs/per lt ama chini ya hapo sio jambo la ajabu.
 
Na declare interest kuwa mimi ni Mbunge na nimeamua kuanzisha hii therad ili tuwekane sawa hapa baada ya kukamilisha uchunguzi wangu.

· Kuna Mbunge mmoja wa kike juzi aliniomba tupate naye chakula na tulipokaa alianza kunishawishi kwa kwa nguvu nyingi sana kuwa tuikatae kwa nguvu zote bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itakapowasilishwa na tukiweza tumseme sana na kumkataa Katibu wa Wizara hiyo kuwa hafai. Aidha alikuwa ananisisitizia niwambie na wengine hivyo na kwamba tumpongeze MD William Mhando maana anafaa sana. Mwisho wa chakula alikataa nisilipe na akanilipia na pia kutaka kunipa fedha za mafuta kwa ajili ya gari langu kitu nilichomkatalia.

· Jana na leo baada ya hili la kuwasimamisha watumishi wa TANESCO nikaona niingie ndani kutafiti undani wa kinachoendelea na nikaunganisha zile juhudi za Mbunge mwenzangu ambaye alikuwa na mwenzake (Mh. wa kike ambaye ni shoga yake ) ikanibidi kuanza upelelezi wangu ambao sasa matokeo yake nimeamua kuyamwaga hapa wazi baada ya kupata ukweli toka vyanzo vyangu vinavyoaminika toka ndani ya TANESCO na Taasisi zingine husika za umma .
·
I. Uwezo mdogo sana wa ndg. Mhando katika kuongoza Shirika
Huyu jamaa ameshindwa kuongoza TANESCO KABISA. He lacks managerial skills and his interpersonal communication is very weak and questionable. Toka ameingia amejenga makundi kwa misingi ya ukabila, urafiki na wizi. Ushahidi pia mnaweza kuuliza yale maoni ya watumishi wa TANESCO yaliyokusanywa na Katibu Mkuu wa Wizara. Nimefuatilia hata shule yake ni ya kuungaunga na hakika ilikuwa mbovu sana aliposoma huko Cuba.
Hakika habari za ndani kabisa zinasema uteuzi wake kuwa MD alichukuliwa toka namba tatu katika ranking wakati kulikuwa na mtu wa kwanza na wa pili walioachwa wenye uwezo kwenye vetting yao.

II. Kushiriki wizi ndani ya Shirika
Huyu ni mwizi moja kwa moja kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Bodi yake Rtd. General Robert Mboma na Makamu wake. Yaani huyu Mwenyekiti wa Bodi, Afande yeye anawauzia mafuta ya kuendesha mitambo TANESCO tena kwa bei ya juu Tshs. 2000/= kwa lita wakati sokoni ni 1500/=. Kwanini Mwenyekiti wa bodi huyu mzee mstaafu wa jeshi afanye biashara na chombo anachokisimamia akisababisha a conflict of interests and zero accountability?
TANESCO wanakusanya yapata Tsh. Billioni 100 kwa kila mwezi na hakuna ajuaye hizo fedha zinafanya kazi gani zaidi yake MD, Incarge wa idara ya fedha na Gererali Mboma. Kwa sasa TANESCO wameshindwa hata kulipa madeni anayodaiwa na wako mbioni kuuza mitambo yake. Kimkakati, sasa wamemega fedha nyingi mno (nasema tena mno) na wanazisabaza kwa kuanzia kwa baadhi tu (si wote) ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge na wao bila kufikiri wameamua kichwa kichwa eti kwenda kuonana na Wizara kesho kusimamisha hatua zilizochukuliwa na Wizara juu ya huyu MD. Na kwa kudhihirisha mahusiano yake na Generali , kama mwenyekiti wa Bodi amekataa kusaini barua ya kumsimamisha MD na watuhumiwa wengine kitu cha ajabu sana kwa sababu tu ya kulinda maslahi yake ya biashara anayofanya hapo TANESCO. Mzee huyu hatosheki na pensheni na marupurupu apewayo kama posho za vikao na kutembelea Shirika n.k kila mara.

III. Hujuma kwa Taifa kwa lugha za ‘ kiufundi’ .
Leo nimeambiwa na Injinia mmoja mwandamizi wa Tanesco ninayemwamini sana kuwa hakika ugomvi umeanza kwa sababu kama kawaida yao, MD na kundi lake walitaka kutangaza kuwepo na mgao (kwa kubumba) wa umeme kwa lugha za kiufundi ili waendelee kufaidi kutokana na biashara zao za majenereta na mafuta. Sasa Wizara kwa kutaka kupigania maslahi ya wananchi wakawakatalia na hapo ndipo huyu kilaza anaamua kukata umeme mwenyewe kwa kiburi cha mwenyekiti wake anayetengeneza mamilioni ya fedha za nje (USD) kwa kila mwezi kupitia mgao wa kubumba.
Kilichoniuma kuliko vyote ni kwamba huyu Mh. Mwenzangu mwanadada kwa nini alinifuata na kunilisha nami chakula kichafu kama zilivyo fedha chafu bila mimi kujua, nitamshughulikia kibinafsi . Nimepata ukweli kuwa huyu mwanamama ni Mpenzi wake huyo MD na watu kibao wanalijua hili na yeye anatumia nafasi yake ya ujumbe kwenye kamati husika ya Bunge kuendelea kumfanya huyu MD buzi lake la kudumu. Tanesco . Na kwamba haikuwa tu kwangu bali kawatembelea wengi akiwa na fuko la fedha akijaribu kugawa kwa usiri sana na kushawishi eti tukatae bajeti ya Wizara na pia wamfukuze Katibu Mkuu wa Wizara (eti wanasema anajifanya kuleta ulokole wa kisabato, kitu ambacho ni kweli huyu jamaa ni wa SDA lakini kosa lake sasa nalifahamu kuwa ni kwamba amekuta ameingia katika anga za TANESCO- mradi wa watu wachache na sio wa umma.

Hitimisho:
1. Wabunge tuweni macho (Independent Committee iundwe kama ya Mwakyembe ) tuone nani anasema ukweli na awajibishwe. Suala laBajetu hatuhitaji kufundishwa sisi tunawasubiri wao waiwasilishe tutaipima na kuuliza maswali yanayopaswa.

2. Mamlaka husika, vunja hiyo Bodi ya TANESCO kabisa sasa hivi na wawekwe watu wasiohusika na mahusiano ya kimaslahi na watumishi wa TANESCO na wawe wenye uwezo wa kuisimamia vyema. Why always taking retired people? Tanzania ni kubwa sana na ina wasomi kibao na wenye uwezo wa kuongoza Bodi kibao!!

MD na Mh. mpenzi wako na shoga wako na hii Kamati ya Bunge inayosimamia Wizara ya Nishati kuweni macho na kila mnachotaka kukifanya sasa maana media, wala kusambaza barua kwa Rais, PM na kwa Waziri mhusika haitawasaidia. Umma wa watanzania leo umesha wamulika kuwa ninyi ni wahujumu wa uchumi.

Sisi wabunge wenye akili na wananchi tutawaangukia ninyi na yeyote ambaye anataka kuwaunga mkono katika upuuzi wa kuihujumu TANESCO, kutumia mhusiano ya kimapenzi kujaribu kutuhadaa na zaidi ya yote kushindwa kuongoza shirika hili la TANESCO NA KUJITUNGIA MIGAO YA UMEME ILI MFAHIDI !

Ndugu mbunge kwa kuwa umesha onesha nia safi kabisa tunakuomba huyo mbunge umuumbue bungeni siku ya kuchangia hiyo bajeti. Umuumbue kama vile alivyoumbuliwa jairo live. madada kama hao wanaotumiwa ni virus, yaani kwa jinsi alivyokuwa anakomaa kukushawishi it means hata kama ungemwambia utakubaliana nae lakini mpaka umgonge angekubali kwani yeye ni kibaraka wa mafisadi. Mheshimiwa mbunge endelea kukusanya data ili umwage.
Pia utaniulizia, kama tanesco inauwezo wa kuleta mita za luku toka nje kwanini tanesco yenyewe isiweze kuwakopesha wateja kwa kuwaingizia deni kwenye akaunti zao za luku badala ya mchongo walioutengeneza na benk?
 
Jamani naomba kueleimishwa..Kunapokuwepo mgao hawa jamaa wanafaidika vipi kifedha?.

Wanatumia hivi vigenerator vya megawat 100, na hapo wanapiga kwa mafuta na mauzo ya umeme. ni kutengeneza udharula wa kila kitu watu wana make.
 
wana JF nchi hii ni ya kwetu wote tusiwaachie wabunge ndio watusemee. hawa waheshimiwa wananunuliwa tena kirahisi kabisa hata kwa gharama za chakula hotelini.wanahabari watusaidie kwa kulipua haya mambo kwenye magazeti yao.
 
kichwa kimestuck ghafla (no further intergration) kwa sababu nilikuwa natafakari ya kwamba huu WIZI na uhujumu uchumi utakwisha lini???? lakin tusilaumu sana kwa sababu tuliwaweka sisi wenyewe pasipo kuwajua!! remember that ""NO ONE CAN RIDE YOUR BACK UNLESS IT IS BENT"""
 
Sasa naelewa kwa nini kwenye kila nguzo huwa kuna HATARI/DANGER plate!!! Siasa kila mahali.... Na lile shirika halitaendelea koz of POLITICIANS!!! But I know the guy (Mhando) Jamaa anaujua Umeme na kiongozi mzuri tu, Ameanzia kama Engineer wa kawaida, Regional manager, Zonal Manager na mpaka U MD!!! tatizo cheo alichokipata kinaingilia maslahi yenu wanasiasa pia!!! hata mie usienijua siku nikipewa hicho cheo utasema kuwa "ooooh Nina elimu ya kuunga unga, Sina Communication Skills nk" majungu na fitina tu ndo kilichobaki....

Otherwise toa a way forward kwa nini tuna shida ya umeme!!!! Tuna mjua Adui ila tunazunguka mbuyu na kuendelea kutengeneza akina ULIMBOKA wengine.....

Kama bajeti ya wizara ina madudu na mnaiandalia mkakati ili ipite then msitumie migongo ya watu wengine kuwaharibia sifa ili mfiche madudu yenu!!!!!
 
Sisi wabunge [COLOR=#FF0000 said:
wenye akili [/COLOR]na wananchi tutawaangukia ninyi na yeyote ambaye anataka kuwaunga mkono katika upuuzi wa kuihujumu TANESCO, kutumia mhusiano ya kimapenzi kujaribu kutuhadaa na zaidi ya yote kushindwa kuongoza shirika hili la TANESCO NA KUJITUNGIA MIGAO YA UMEME ILI MFAHIDI !

Nimesoma kwa kurudiarudia na kwa umakini sana andiko lako. Na kwa kuwa uko huru ku-air mawazo yako kwa mujibu wa sheria, hilo sina tatizo nalo. Kinachonisikitisha ni maudhui ya lugha uliyotumia, imekaa kimajungu sana na kwa mtu wa capacity yako sidhani kama andiko hili linampa hadhi ya "UHESHIMIWA".

Nilidhani kwa kuwa uko na uchungu basi ungemtaja hata huyo muheshimiwa mwenzio aliyekuhonga chakula coz hela ya mafuta ulikataa sa kwa nini hukumrudishia hiyo pesa ya chakula! Maana general mstaafu umemtaja unashindwaje kumtaja na huyo mbunge mwenzio! Pia me nadhani kama unaushahidi basi peleka hoja binafsi bungeni na nadhani hapo ndo palikuwa mahala sahihi na kulishawishi Bunge liunde kamati kam ya Mwakyembe.

Unaposema kusambaza barua kwa media hakuwasaidii kitu, mbona na wewe umeleta hii mada hapa kwa media! Au JF siyo media! Lakini hapo kwenye red, hivi unafikiri andiko lako hili linaweza kukutafsiri kama ulivyojiita! Mwisho nisema, una hoja nzuri ila umeileta kimajungumajungu...Maana inaonyesha una hasira sana ambayo iko motivated beyond TANESCO, naomba kuwasilisha, niko tayari kukosolewa...
 
Nijibu kidogo kwa haraka kabla hatujarudi kwenye session.

1. Avatar & Jina: An avatar is a personalized graphic that a computer user has chosen to use for identification. I have chosen the one that exhibits a beautiful lady's legs in exquisite high heels. This is what I see and interpret. Kwangu hii ni alama ya jinsia inayopaswa kuheshimiwa. Je wewe unaona alama gani inayokwijia katika ubongo wako juu ya hiyo avatar yangu. Hapo kuna kitu gani cha ajabu, uhuni uko wapo kama si kilichoko katika mawazo yako finyu. Je, wale ambao hawana avatar, kwa hiyo tuwatafsiri kuwa hawana chaguo lolote duniani au kwamba hawana sense of symbolism katika vichwa vyao? Hakuna anaye weza kulazimisha kuwa kila Mbunge au Waziri au hata Rais ambaye ni mwanachama hapa basi atumie jina halisi. Hiyo si sehemu ya kanuni za JF. Na kwa wenye mawazo mapana wanaelewa the role of anonymity in the world of freedom of expression na saikolojia ya uelekeo wa kukubali (without questioning) au kudharau maoni ya mtu simply kwa sababu mnafahamiana! Wake up! si kila mtu lazima afuate style za Mnyika au Zito na wengineo hapa.

2. Genereta za TANESCO zinatumia mafuta ya aina kadhaa, sasa wachovu wachache hapa wanaona tu diesel au petrol na hivyo kukurupuka na bei za perol / diesel sokoni. 3. Leo hii mtu anaweza kuwa na Bsc. Degree in Electronics hata PhD, lakini mwenendo mzima wa usomaji na uwezo wake kwenye exams & papers akiwa chuoni kama vilikuwa ni vya kusua-sua, elimu yake bado itasemekana kuwa ya kuunga-unga. Hakuna ubishi hapa watu tunafahamiana sana wenye uelewa wa CV ya huyu MD wetu wanamfahamu sana kila chuo alikopita. 4. Moja ya Managerial Skills za muhimu kwa mtu kama MD ni uwezo wa KUSHAWISHI WADAU WOTE HUSIKA KATIKA TAASISI YAKE ili kuongeza tija kwa watumishi, kuboresha huduma na uwajibikaji na na ufanisi kazini kwa kufuata misingi na maadili ya mifumo ya menejiment ya kisasa.
Hivi MD kama ana sifa hizo angeendeleaje kutumiwa na Mwenyekiti wake wa Bodi ambaye anafanya biashara na TANESCO (anayebisha aje hapa akane) na tena kwa gharama ambazo si za lazima tena baadaye aendelee kumsimamia na kumdhibiti? Haijalishi nani anamiliki au ana hisa katika hayo majenereta (kama kanuni na sheria ya manunuzi ya umma vingefuatwa), lakini, kama hata MD anaruhusu migao ya umeme isiyo ya lazima ili majenereta na mafuta yake yawaingizie mamilioni katika mifuko yao hatuwezi kuyaacha haya.

Je, mnajua hii ina athari gani katika tija kwa watumishi wengine ambao wanataka kufanya kazi kwa moyo ili migao ya umeme ipungue au isiwepo kabisa lakini kiongozi wao na mwenyekiti wake wa Bodi wanalazimisha mambo hayo huku mitaani wananchi wanawatukana watumishi wote wa TANESCO kuwa ni wazembe au hawafai? Nani asiye jua kuwa gharama za kuendesha mitambo zinapokuwa kubwa ndivyo hata malipo ya units in various tariffs zinamfuata mlaji ambaye ni mwananchi wangu?

5. Mimi kupewa chakula na huyu Mh. Mwenzetu mwanamke unaweza kuona ni jambo dogo sana lakini Kusudio la ukarimu wake na ushawishi wake kwetu Wabunge ni kitu kibaya sana maana ni jaribio la kutufanya sisi kuwa muhuri wa wapenzi hawa (MD, yeye (Mb) na shoga yake(Mb) ) ambao wanapanga kuendelea kujinufaisha huku wakiidhoofisha TANESCO kwa kuihujumu. Sina haja na wala hatuongelei hapa mahusiano yao ya mapenzi (ambayo yanafahamika na wengi sana pale TANESCO na kwa Wabunge wengi maana hayafichiki haya kama kikohozi), bali nasema mtu asitumie mapenzi yake kutuibia na kutufikiri kuwa sote tunaweza kuhongwa kama ambavyo amefanikiwa kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge na Bodi pia. Msiwe na presha, twende hatua kwa hatua kila kitu kitakuwa wazi na majina yao wahusika wote yatakuwa wazi. Hadi nimeamua kuwalipua hapa, tayari riporti hii imeshafika TAKUKURU na hata Bungeni mtasikia!

6. Kuhusu Bajeti ya Wizara: Suala si kuwa naunga mkono au suingi mkono hiyo bajeti maana bado haijawasilishwa. Kazi yetu ni kusubiri iletwe, tutaisoma kwa makini na tuulize maswali ya msingi na kuikosoa au kuunga mkono pale inapobidi ambapo pana maslahi ya Wizara, idara zake, tasisi zilizo chini yake kwa faida ya nchi yetu. Hivyo mtu hawezi kuja kunishawishi sasa kuwa niikatae bajeti au nimshambulie Katibu Mkuu wa Wizara bila sababu zozote za msingi, isipokuwa eti kwa kuwa amemuumbua na kumtaka MD (mpenziwe mwenzetu) asiruhusu migao ya umeme bila sababu ya msingi na kwamba afuate taratibu za mawasiliano walizokubaliana kati ya Shirika na Wizara ambazo ziko kwa mujibu wa sheria inayounda shirika hili la ugavi wa umeme.

Hatukubali kuendelea kuwa na Watendaji wenye uwezo mdogo wa kuongoza na tena wanaoshiriki ubadhilifu tukanyamaza. Maana hawa ndio hakika wanafanya Serikali yetu na Chama Tawala inatukanwa na kudharauliwa.
 
Nje ya Mada kwa muda.

"Na declare interest kuwa mimi ni Mbunge na nimeamua kuanzisha hii therad ili tuwekane sawa hapa baada ya kukamilisha uchunguzi wangu".

Au na wewe huwa humlipi dereva wako na unaendeshwa na mpz wko?

Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
 
Yaani bachelor of scince in electronics ni elimu ya kuungaunga wewe mbunge darasa la ngapi? usilete udaku udaku hapa kama huna taarifa za uhahika kajipange.

Kwanza sitaki kukubishia kuwa BSc in electronics sio elimu ya kuungaunga!Ila kusema kweli imenishangaza kuona kuwa shirika la umeme linaongozwa na mtu aliyesomea electronics na sio Electrical Engineering, nadhani kwa wahandisi tofauti ya taaluma hizi mbili inaeleweka!Ndio maana hatuwezi kuzalisha umeme wa kututosha nchi hii kwani huyu uhando anwaza kuwasha redio,tv na computer na sio mitambo mikubwa iliyoko viwandani!Uwezxo wake mdogo ndiom uliomfanya akate umeme (mgomo bila taarifa) kinyume na taratibu kabisa za utumishi wa umma!Anatakiwa kufukuzwa kazi!
 
Na declare interest kuwa mimi ni Mbunge na nimeamua kuanzisha hii therad ili tuwekane sawa hapa baada ya kukamilisha uchunguzi wangu.

· Kuna Mbunge mmoja wa kike juzi aliniomba tupate naye chakula na tulipokaa alianza kunishawishi kwa kwa nguvu nyingi sana kuwa tuikatae kwa nguvu zote bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itakapowasilishwa na tukiweza tumseme sana na kumkataa Katibu wa Wizara hiyo kuwa hafai. Aidha alikuwa ananisisitizia niwambie na wengine hivyo na kwamba tumpongeze MD William Mhando maana anafaa sana. Mwisho wa chakula alikataa nisilipe na akanilipia na pia kutaka kunipa fedha za mafuta kwa ajili ya gari langu kitu nilichomkatalia.

· Jana na leo baada ya hili la kuwasimamisha watumishi wa TANESCO nikaona niingie ndani kutafiti undani wa kinachoendelea na nikaunganisha zile juhudi za Mbunge mwenzangu ambaye alikuwa na mwenzake (Mh. wa kike ambaye ni shoga yake ) ikanibidi kuanza upelelezi wangu ambao sasa matokeo yake nimeamua kuyamwaga hapa wazi baada ya kupata ukweli toka vyanzo vyangu vinavyoaminika toka ndani ya TANESCO na Taasisi zingine husika za umma .
·
I. Uwezo mdogo sana wa ndg. Mhando katika kuongoza Shirika
Huyu jamaa ameshindwa kuongoza TANESCO KABISA. He lacks managerial skills and his interpersonal communication is very weak and questionable. Toka ameingia amejenga makundi kwa misingi ya ukabila, urafiki na wizi. Ushahidi pia mnaweza kuuliza yale maoni ya watumishi wa TANESCO yaliyokusanywa na Katibu Mkuu wa Wizara. Nimefuatilia hata shule yake ni ya kuungaunga na hakika ilikuwa mbovu sana aliposoma huko Cuba.
Hakika habari za ndani kabisa zinasema uteuzi wake kuwa MD alichukuliwa toka namba tatu katika ranking wakati kulikuwa na mtu wa kwanza na wa pili walioachwa wenye uwezo kwenye vetting yao.

II. Kushiriki wizi ndani ya Shirika
Huyu ni mwizi moja kwa moja kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Bodi yake Rtd. General Robert Mboma na Makamu wake. Yaani huyu Mwenyekiti wa Bodi, Afande yeye anawauzia mafuta ya kuendesha mitambo TANESCO tena kwa bei ya juu Tshs. 2000/= kwa lita wakati sokoni ni 1500/=. Kwanini Mwenyekiti wa bodi huyu mzee mstaafu wa jeshi afanye biashara na chombo anachokisimamia akisababisha a conflict of interests and zero accountability?
TANESCO wanakusanya yapata Tsh. Billioni 100 kwa kila mwezi na hakuna ajuaye hizo fedha zinafanya kazi gani zaidi yake MD, Incarge wa idara ya fedha na Gererali Mboma. Kwa sasa TANESCO wameshindwa hata kulipa madeni anayodaiwa na wako mbioni kuuza mitambo yake. Kimkakati, sasa wamemega fedha nyingi mno (nasema tena mno) na wanazisabaza kwa kuanzia kwa baadhi tu (si wote) ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge na wao bila kufikiri wameamua kichwa kichwa eti kwenda kuonana na Wizara kesho kusimamisha hatua zilizochukuliwa na Wizara juu ya huyu MD. Na kwa kudhihirisha mahusiano yake na Generali , kama mwenyekiti wa Bodi amekataa kusaini barua ya kumsimamisha MD na watuhumiwa wengine kitu cha ajabu sana kwa sababu tu ya kulinda maslahi yake ya biashara anayofanya hapo TANESCO. Mzee huyu hatosheki na pensheni na marupurupu apewayo kama posho za vikao na kutembelea Shirika n.k kila mara.

III. Hujuma kwa Taifa kwa lugha za ‘ kiufundi’ .
Leo nimeambiwa na Injinia mmoja mwandamizi wa Tanesco ninayemwamini sana kuwa hakika ugomvi umeanza kwa sababu kama kawaida yao, MD na kundi lake walitaka kutangaza kuwepo na mgao (kwa kubumba) wa umeme kwa lugha za kiufundi ili waendelee kufaidi kutokana na biashara zao za majenereta na mafuta. Sasa Wizara kwa kutaka kupigania maslahi ya wananchi wakawakatalia na hapo ndipo huyu kilaza anaamua kukata umeme mwenyewe kwa kiburi cha mwenyekiti wake anayetengeneza mamilioni ya fedha za nje (USD) kwa kila mwezi kupitia mgao wa kubumba.
Kilichoniuma kuliko vyote ni kwamba huyu Mh. Mwenzangu mwanadada kwa nini alinifuata na kunilisha nami chakula kichafu kama zilivyo fedha chafu bila mimi kujua, nitamshughulikia kibinafsi . Nimepata ukweli kuwa huyu mwanamama ni Mpenzi wake huyo MD na watu kibao wanalijua hili na yeye anatumia nafasi yake ya ujumbe kwenye kamati husika ya Bunge kuendelea kumfanya huyu MD buzi lake la kudumu. Tanesco . Na kwamba haikuwa tu kwangu bali kawatembelea wengi akiwa na fuko la fedha akijaribu kugawa kwa usiri sana na kushawishi eti tukatae bajeti ya Wizara na pia wamfukuze Katibu Mkuu wa Wizara (eti wanasema anajifanya kuleta ulokole wa kisabato, kitu ambacho ni kweli huyu jamaa ni wa SDA lakini kosa lake sasa nalifahamu kuwa ni kwamba amekuta ameingia katika anga za TANESCO- mradi wa watu wachache na sio wa umma.

Hitimisho:
1. Wabunge tuweni macho (Independent Committee iundwe kama ya Mwakyembe ) tuone nani anasema ukweli na awajibishwe. Suala laBajetu hatuhitaji kufundishwa sisi tunawasubiri wao waiwasilishe tutaipima na kuuliza maswali yanayopaswa.

2. Mamlaka husika, vunja hiyo Bodi ya TANESCO kabisa sasa hivi na wawekwe watu wasiohusika na mahusiano ya kimaslahi na watumishi wa TANESCO na wawe wenye uwezo wa kuisimamia vyema. Why always taking retired people? Tanzania ni kubwa sana na ina wasomi kibao na wenye uwezo wa kuongoza Bodi kibao!!

MD na Mh. mpenzi wako na shoga wako na hii Kamati ya Bunge inayosimamia Wizara ya Nishati kuweni macho na kila mnachotaka kukifanya sasa maana media, wala kusambaza barua kwa Rais, PM na kwa Waziri mhusika haitawasaidia. Umma wa watanzania leo umesha wamulika kuwa ninyi ni wahujumu wa uchumi.

Sisi wabunge wenye akili na wananchi tutawaangukia ninyi na yeyote ambaye anataka kuwaunga mkono katika upuuzi wa kuihujumu TANESCO, kutumia mhusiano ya kimapenzi kujaribu kutuhadaa na zaidi ya yote kushindwa kuongoza shirika hili la TANESCO NA KUJITUNGIA MIGAO YA UMEME ILI MFAHIDI !
Safi sana Tanzania inakombolewa na Mungu tu, Hao wanaodhani wataendelea kuihujumu hawamjui Mungu kabisa
 
Tanesco was doing fine under former director Dr Idrisa Rashid,na tunajua sababu za kuondolewa ni kwa kuwa alikataa tanesco kuwa shamba la bibi la viongozi wa CCM.Everybody knows kwamba Mhando aliwekwa hapo ili fedha zichotwe kwa ajili ya kampeni za CCM kwenye uchaguzi and that has been done.He has played his role in that so They don need him anymore,na serikali ndio imefilisi Tanesco only that time has changed and some one must bare the cost.They knew this when they appointed him that post.They dont have to play us like fools.
 
Could sound well if supporting evidence attached!
 
Mkandara Hivi unawajua wenye dowans,ipptl,songas na wauza mafuta mazito ?
Siwajui isipokuwa swali langu nataka kujua wanafaidika vipi kifedha kila Tanesco wanapoweka mgao?. Nijuavyo mafuta mazito yatauzwa zaidi kama umeme unatumika na haya mashirika yatapata faida kubwa kwa kila ongezeko la matumizi. Je, wanapofanya mgao (kukata matumizi) wanafaidika vipi?..
 
Back
Top Bottom