Rtd General Mboma, Mhando wa TANESCO na Mh. Mbunge - ni Hatari!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rtd General Mboma, Mhando wa TANESCO na Mh. Mbunge - ni Hatari!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Jul 16, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na declare interest kuwa mimi ni Mbunge na nimeamua kuanzisha hii therad ili tuwekane sawa hapa baada ya kukamilisha uchunguzi wangu.

  Kuna Mbunge mmoja wa kike juzi aliniomba tupate naye chakula na tulipokaa alianza kunishawishi kwa kwa nguvu nyingi sana kuwa tuikatae kwa nguvu zote bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itakapowasilishwa na tukiweza tumseme sana na kumkataa Katibu wa Wizara hiyo kuwa hafai. Aidha alikuwa ananisisitizia niwambie na wengine hivyo na kwamba tumpongeze MD William Mhando maana anafaa sana. Mwisho wa chakula alikataa nisilipe na akanilipia na pia kutaka kunipa fedha za mafuta kwa ajili ya gari langu kitu nilichomkatalia.

  Jana na leo baada ya hili la kuwasimamisha watumishi wa TANESCO nikaona niingie ndani kutafiti undani wa kinachoendelea na nikaunganisha zile juhudi za Mbunge mwenzangu ambaye alikuwa na mwenzake (Mh. wa kike ambaye ni shoga yake ) ikanibidi kuanza upelelezi wangu ambao sasa matokeo yake nimeamua kuyamwaga hapa wazi baada ya kupata ukweli toka vyanzo vyangu vinavyoaminika toka ndani ya TANESCO na Taasisi zingine husika za umma .

  I. Uwezo mdogo sana wa ndg. Mhando katika kuongoza Shirika
  Huyu jamaa ameshindwa kuongoza TANESCO KABISA. He lacks managerial skills and his interpersonal communication is very weak and questionable. Toka ameingia amejenga makundi kwa misingi ya ukabila, urafiki na wizi. Ushahidi pia mnaweza kuuliza yale maoni ya watumishi wa TANESCO yaliyokusanywa na Katibu Mkuu wa Wizara. Nimefuatilia hata shule yake ni ya kuungaunga na hakika ilikuwa mbovu sana aliposoma huko Cuba.

  Hakika habari za ndani kabisa zinasema uteuzi wake kuwa MD alichukuliwa toka namba tatu katika ranking wakati kulikuwa na mtu wa kwanza na wa pili walioachwa wenye uwezo kwenye vetting yao.


  II. Kushiriki wizi ndani ya Shirika
  Huyu ni mwizi moja kwa moja kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Bodi yake Rtd. General Robert Mboma na Makamu wake. Yaani huyu Mwenyekiti wa Bodi, Afande yeye anawauzia mafuta ya kuendesha mitambo TANESCO tena kwa bei ya juu Tshs. 2000/= kwa lita wakati sokoni ni 1500/=. Kwanini Mwenyekiti wa bodi huyu mzee mstaafu wa jeshi afanye biashara na chombo anachokisimamia akisababisha a conflict of interests and zero accountability?

  TANESCO wanakusanya yapata Tsh. Billioni 100 kwa kila mwezi na hakuna ajuaye hizo fedha zinafanya kazi gani zaidi yake MD, Incarge wa idara ya fedha na Gererali Mboma. Kwa sasa TANESCO wameshindwa hata kulipa madeni anayodaiwa na wako mbioni kuuza mitambo yake.

  Kimkakati, sasa wamemega fedha nyingi mno (nasema tena mno) na wanazisabaza kwa kuanzia kwa baadhi tu (si wote) ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge na wao bila kufikiri wameamua kichwa kichwa eti kwenda kuonana na Wizara kesho kusimamisha hatua zilizochukuliwa na Wizara juu ya huyu MD.

  Na kwa kudhihirisha mahusiano yake na Generali , kama mwenyekiti wa Bodi amekataa kusaini barua ya kumsimamisha MD na watuhumiwa wengine kitu cha ajabu sana kwa sababu tu ya kulinda maslahi yake ya biashara anayofanya hapo TANESCO. Mzee huyu hatosheki na pensheni na marupurupu apewayo kama posho za vikao na kutembelea Shirika n.k kila mara.


  III. Hujuma kwa Taifa kwa lugha za ' kiufundi' .
  Leo nimeambiwa na Injinia mmoja mwandamizi wa Tanesco ninayemwamini sana kuwa hakika ugomvi umeanza kwa sababu kama kawaida yao, MD na kundi lake walitaka kutangaza kuwepo na mgao (kwa kubumba) wa umeme kwa lugha za kiufundi ili waendelee kufaidi kutokana na biashara zao za majenereta na mafuta. Sasa Wizara kwa kutaka kupigania maslahi ya wananchi wakawakatalia na hapo ndipo huyu kilaza anaamua kukata umeme mwenyewe kwa kiburi cha mwenyekiti wake anayetengeneza mamilioni ya fedha za nje (USD) kwa kila mwezi kupitia mgao wa kubumba.

  Kilichoniuma kuliko vyote ni kwamba huyu Mh. Mwenzangu mwanadada kwa nini alinifuata na kunilisha nami chakula kichafu kama zilivyo fedha chafu bila mimi kujua, nitamshughulikia kibinafsi . Nimepata ukweli kuwa huyu mwanamama ni Mpenzi wake huyo MD na watu kibao wanalijua hili na yeye anatumia nafasi yake ya ujumbe kwenye kamati husika ya Bunge kuendelea kumfanya huyu MD buzi lake la kudumu. Tanesco.

  Na kwamba haikuwa tu kwangu bali kawatembelea wengi akiwa na fuko la fedha akijaribu kugawa kwa usiri sana na kushawishi eti tukatae bajeti ya Wizara na pia wamfukuze Katibu Mkuu wa Wizara (eti wanasema anajifanya kuleta ulokole wa kisabato, kitu ambacho ni kweli huyu jamaa ni wa SDA lakini kosa lake sasa nalifahamu kuwa ni kwamba amekuta ameingia katika anga za TANESCO- mradi wa watu wachache na sio wa umma.


  Hitimisho:
  1. Wabunge tuweni macho (Independent Committee iundwe kama ya Mwakyembe ) tuone nani anasema ukweli na awajibishwe. Suala laBajetu hatuhitaji kufundishwa sisi tunawasubiri wao waiwasilishe tutaipima na kuuliza maswali yanayopaswa.

  2. Mamlaka husika, vunja hiyo Bodi ya TANESCO kabisa sasa hivi na wawekwe watu wasiohusika na mahusiano ya kimaslahi na watumishi wa TANESCO na wawe wenye uwezo wa kuisimamia vyema. Why always taking retired people? Tanzania ni kubwa sana na ina wasomi kibao na wenye uwezo wa kuongoza Bodi kibao!!

  [FONT=&amp]MD na Mh. mpenzi wako na shoga wako na hii Kamati ya Bunge inayosimamia Wizara ya Nishati kuweni macho na kila mnachotaka kukifanya sasa maana media, wala kusambaza barua kwa Rais, PM na kwa Waziri mhusika haitawasaidia. Umma wa watanzania leo umesha wamulika kuwa ninyi ni wahujumu wa uchumi.

  Sisi wabunge wenye akili na wananchi tutawaangukia ninyi na yeyote ambaye anataka kuwaunga mkono katika upuuzi wa kuihujumu TANESCO, kutumia mhusiano ya kimapenzi kujaribu kutuhadaa na zaidi ya yote kushindwa kuongoza shirika hili la TANESCO NA KUJITUNGIA MIGAO YA UMEME ILI MFAHIDI !
  [/FONT]
   
 2. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh! Balaa!
   
 3. fmlyimo

  fmlyimo JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Tanesco janga la Taifa
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  nshakujua wewe ni nani, hongera kwa fikra huru.
   
 5. N

  Njaare JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Matatizo ya Tanesco ni ya kutengeneza ili watu wachache wajipatie miradi kutokana na mipango ya dharura. Toka mwaka 2006 migawo kila mara na kila mwaka tunasema afadhali ya mwaka jana. Kuna mijitu inaomba Mungu Tanzania iwe kame kabisa ili iendelee kuuuza majenereta na mafuta. Yashindwe kwa jina la Yesu.
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wabunge wanatoa rushwa ya ngono? Wabunge wanahongwa kutetea au kupinga jambo?

  Nasikia siku hizi rushwa ya Wabunge imekua hadi inawajali madiwani wenye njaa wa Kigamboni
   
 7. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Fichueni tu, sie tunayahifadhi ili 2015, tuwasute halafu tuwawajibishe.
   
 8. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wewe nawe inaelekea ni wale wale- kama unajua yote haya na ni mbunge kama unavyojitapa mahali sahihi pa kuwaumbua hao unaowatuhumu ni ndani ya ukumbi wa bunge-Kumbuka alivyofanya Kafulila kwa wale aliowakuta wakiomba rushwa. Hizi habari zenu za kuchafuana kwa visingizio vya uzalendo vimezidi. Tulisoma barua walizoandikiana wizara na Mhando, kutokana na mawasiliano hayo bado sijaliona tatizo la Mhando liko wapi unless utoe ushahidi kuthibitisha vinginevyo
   
 9. N

  Ngarenaro JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kukikucha nitachangia
   
 10. Miya

  Miya JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 817
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 180
  Hapa unatusumbua tu mara mboma cjui mbunge mara muhando mara watendaji..unazunguka bure tatizo ni ccm basi
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kiongozi ukisoma vizuri hii habari utaona imekaa ki-propaganda sana na sio kweli kwamba imetoka kwa mbunge, sana sana itakuwa imetoa kwa mpambe wa mbunge - tena wa mt wa Lumumba.

  Kwanza, ni mbunge gani alikuwa na uchaguzi eneo analowakilisha? Mbeya Mjini ndiko kumefanyika uchaguzi, sasa unaweza kuona hii propaganda inalenga nini. Na hapa anataka kusema kuwa upande mmoja wa bunge unashawishi wabunge ili wasiunge mkono budget ya Nishati na madini! Mwishoni watasema upinzani kuna watu subbotage serikali.

  Siiukubali hii taarifa.
   
 12. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mheshimiwa mbunge naomba tutajie jina la huyo mbunge mwanamama ile hapa JF wengine wamwage mavituuzi wanayoyafahamu.
   
 13. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Who is to be blamed kwenye hii saga? Nakumbuka huyu MD watu walioiga kelele sana kuwa hana SIDS za kuongoza Hilo shirika alipoteuliwa. Kuna udhaifu mkubwa sana kwenye ngazi za uteuzi wa watumishi wa mashirika haya ya umma.
   
 14. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Sijakujua wewe ni nani ila huyo Mbunge aliyekulisha namfahamu na Shoga yake ila pia mambo ya NMC waache Mkwasa alishindwa vumilia.
  Hivi hata Simbachawene keshaingia kwenye Ulaji Du tumekwisha umeme hata Kongwa na Kibakwe Finitio
   
 15. k

  kajima JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 866
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Walakini katika hoja zako:
  Kulipiwa chakula ni jambo dogo
  Bei ya mafuta sokoni (filling station?) 1500???
  Lack of managerial skills basing on what?
  Tupe sababu za kuikataa hiyo budget ya wazira kama ulivyohamasishwa

  Mleta mada, ingekuwa vyema pia ungetuambia
  1) uzalishaji na mahitaji yako vipi kwasasa?
  2) Tangu Mhando, Eng. aingie madarakani, performance ya TANESCO iko vipi?


  Kama kuna mdau mwenye CV ya Mhando, Eng. basi aitupe hapa tupime kilichowasilishwa jamvini
   
 16. Miya

  Miya JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 817
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 180
  Na we unataka mambo ya NMC kama Mkwasa?we utaweza lkn?
   
 17. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Unapoona wezi wetu wanafarakana chukua jembe ukalime, kumbuka kubeba panga ukombozi unakaribia watakaokimbilia upande wako fyeka miguu!
   
 18. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hii propaganda inatoka ktk kundi moja hasimu kati ya yanayotaka kuimiliki Tanesco. Kama ilivyokua ATCL,ndivyo sasa Tanesco. Mzizi wa fitina hapa ni Katibu Mkuu wa Wizara, yaonyesha anaandaa watu wake,ili wakamue! Waziri inabidi ajipange lasivyo ataondoka kwa aibu.
   
 19. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  hebu tumwangie mpunga huo hapa mkuu
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...ama kweli, nchi hii ni wengi waliotema mate chini mara tu baada ya kula viapo vya kiuongozi!!
   
Loading...