Rtd General Mboma, Mhando wa TANESCO na Mh. Mbunge - ni Hatari!!

Hii habari ni utata mtupu kwani itawezekana vipi kwa Mboma kama mwenyekiti wa bodi kukataa kusaini hiyo barua wakati uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando ulifanywa na hiyo bodi yenyewe ambayo Mboma ndio mwenyekiti.Labda ungesema alisaini kwa shingo upande na uamuzi wa bodi ni shinikizo kutoka wizarani.
 
Kama ni kweli wapandishwe kizimbani kwa kosa la kuhujumu uchumi,maisha ya Watanzania wa kawaida yamekuwa magumu mno kutokana na gharama za umeue ili kufaidisha matumbo ya watu wachache na jamaa zao. TISS, PCCB mko wapi madudu yanafanyika kiasi hicho na wananchi wanaumia sana?

Mjomba, wewe tuko wote hapa tanzania kweli!?? hivi bado una imani na hizo taasisi ulizozitaja?
 
Sarakasi! sarakasi! sarakasi!
Katika ukumbi wa Bunge la JMT kutakuwa na maonesho ya sarakasi.............
 
Guys, acheni ushabiki wa makundi kwa mrengo wa jinsi yoyote ile.

Maswali ya msingi:
- Je ni kweli usimamizi wa bodi una mgongano wa ki-maslahi? Yes or No is a question of Uchunguzi
- Wizi: Upo unaoweza kudhihirishwa kwa jinsi alivyoeleza aliyetoa maneno haya? Yes or No is a question of Uchunguzi
- Any other allegation ...; Yes or No is a question of Uchunguzi

Ushabiki utaangamiza taifa, and mind you mchangiaji hebu tuwe makini kuangalia maslahi ya nchi.

Mtu akisimamishwa kupisha uchunguzi ni vema wadau muone iko sawa ili tukuze uwajibikaji.

Kama haya ni ya kweli jueni kuwa ipo siku mambo mengi yata - COLLAPSE. Wewe unaejiona unatanua sasa, hicho ulichoiba utakosa pa kukitumia.

Tuchunguze na kutoa majibu, kama yasemwayo ni uongo, waongo waadhibiwe.
 
Duh, ama kweli fedha mwanaharamu yaani mtu anaamua kutulaza kwenye giza ili apate hela na vibaka watuibie sisi mtaani
 
2. Mamlaka husika, vunja hiyo Bodi ya TANESCO kabisa sasa hivi na wawekwe watu wasiohusika na mahusiano ya kimaslahi na watumishi wa TANESCO na wawe wenye uwezo wa kuisimamia vyema. Why always taking retired people? Tanzania ni kubwa sana na ina wasomi kibao na wenye uwezo wa kuongoza Bodi kibao!!

Hapo kwenye red ndo nimekukubali... Madhara ya kuwaweka hawa watu ni makubwa sana coz mtu anakua anafanya kazi bora cku ziishe coz ana mafao na kadhalika

Lakini Tukiweka Professional na anayeipenda kazi yako kwa kuzingatia umri kabla ya kustaafu nadhani mtu huyu ataogopa kazi yake na atafanya kwa utiifu huku akijua Termination yako itampoteza kwenye ramani.
 
Sie wabongo ni watu wa ajabu. Nilitegemea mleta mada apongezwe kwa kufichua madhambi yanayoendelea ndani ya TANESCO, matokeo yake tunamponda mleta thread.Kwa hiyo mtu akipata issue asiilete janvini?

humu hatujadili vitu visivyo na mantiki na wala mambo au maisha binafsi ya mtu....humu tunajadili issues ...soma kwa makini uzi wa huyo mleta mada utagundua una mapungufu mengi!! ni mafuta gani yanauzwa tsh 1500?
 
Na declare interest kuwa mimi ni Mbunge na nimeamua kuanzisha hii therad ili tuwekane sawa hapa baada ya kukamilisha uchunguzi wangu.

· Kuna Mbunge mmoja wa kike juzi aliniomba tupate naye chakula na tulipokaa alianza kunishawishi kwa kwa nguvu nyingi sana kuwa tuikatae kwa nguvu zote bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itakapowasilishwa na tukiweza tumseme sana na kumkataa Katibu wa Wizara hiyo kuwa hafai. Aidha alikuwa ananisisitizia niwambie na wengine hivyo na kwamba tumpongeze MD William Mhando maana anafaa sana. Mwisho wa chakula alikataa nisilipe na akanilipia na pia kutaka kunipa fedha za mafuta kwa ajili ya gari langu kitu nilichomkatalia.

· Jana na leo baada ya hili la kuwasimamisha watumishi wa TANESCO nikaona niingie ndani kutafiti undani wa kinachoendelea na nikaunganisha zile juhudi za Mbunge mwenzangu ambaye alikuwa na mwenzake (Mh. wa kike ambaye ni shoga yake ) ikanibidi kuanza upelelezi wangu ambao sasa matokeo yake nimeamua kuyamwaga hapa wazi baada ya kupata ukweli toka vyanzo vyangu vinavyoaminika toka ndani ya TANESCO na Taasisi zingine husika za umma .
·
I. Uwezo mdogo sana wa ndg. Mhando katika kuongoza Shirika
Huyu jamaa ameshindwa kuongoza TANESCO KABISA. He lacks managerial skills and his interpersonal communication is very weak and questionable. Toka ameingia amejenga makundi kwa misingi ya ukabila, urafiki na wizi. Ushahidi pia mnaweza kuuliza yale maoni ya watumishi wa TANESCO yaliyokusanywa na Katibu Mkuu wa Wizara. Nimefuatilia hata shule yake ni ya kuungaunga na hakika ilikuwa mbovu sana aliposoma huko Cuba.
Hakika habari za ndani kabisa zinasema uteuzi wake kuwa MD alichukuliwa toka namba tatu katika ranking wakati kulikuwa na mtu wa kwanza na wa pili walioachwa wenye uwezo kwenye vetting yao.

II. Kushiriki wizi ndani ya Shirika
Huyu ni mwizi moja kwa moja kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Bodi yake Rtd. General Robert Mboma na Makamu wake. Yaani huyu Mwenyekiti wa Bodi, Afande yeye anawauzia mafuta ya kuendesha mitambo TANESCO tena kwa bei ya juu Tshs. 2000/= kwa lita wakati sokoni ni 1500/=. Kwanini Mwenyekiti wa bodi huyu mzee mstaafu wa jeshi afanye biashara na chombo anachokisimamia akisababisha a conflict of interests and zero accountability?
TANESCO wanakusanya yapata Tsh. Billioni 100 kwa kila mwezi na hakuna ajuaye hizo fedha zinafanya kazi gani zaidi yake MD, Incarge wa idara ya fedha na Gererali Mboma. Kwa sasa TANESCO wameshindwa hata kulipa madeni anayodaiwa na wako mbioni kuuza mitambo yake. Kimkakati, sasa wamemega fedha nyingi mno (nasema tena mno) na wanazisabaza kwa kuanzia kwa baadhi tu (si wote) ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge na wao bila kufikiri wameamua kichwa kichwa eti kwenda kuonana na Wizara kesho kusimamisha hatua zilizochukuliwa na Wizara juu ya huyu MD. Na kwa kudhihirisha mahusiano yake na Generali , kama mwenyekiti wa Bodi amekataa kusaini barua ya kumsimamisha MD na watuhumiwa wengine kitu cha ajabu sana kwa sababu tu ya kulinda maslahi yake ya biashara anayofanya hapo TANESCO. Mzee huyu hatosheki na pensheni na marupurupu apewayo kama posho za vikao na kutembelea Shirika n.k kila mara.

III. Hujuma kwa Taifa kwa lugha za ‘ kiufundi’ .
Leo nimeambiwa na Injinia mmoja mwandamizi wa Tanesco ninayemwamini sana kuwa hakika ugomvi umeanza kwa sababu kama kawaida yao, MD na kundi lake walitaka kutangaza kuwepo na mgao (kwa kubumba) wa umeme kwa lugha za kiufundi ili waendelee kufaidi kutokana na biashara zao za majenereta na mafuta. Sasa Wizara kwa kutaka kupigania maslahi ya wananchi wakawakatalia na hapo ndipo huyu kilaza anaamua kukata umeme mwenyewe kwa kiburi cha mwenyekiti wake anayetengeneza mamilioni ya fedha za nje (USD) kwa kila mwezi kupitia mgao wa kubumba.
Kilichoniuma kuliko vyote ni kwamba huyu Mh. Mwenzangu mwanadada kwa nini alinifuata na kunilisha nami chakula kichafu kama zilivyo fedha chafu bila mimi kujua, nitamshughulikia kibinafsi . Nimepata ukweli kuwa huyu mwanamama ni Mpenzi wake huyo MD na watu kibao wanalijua hili na yeye anatumia nafasi yake ya ujumbe kwenye kamati husika ya Bunge kuendelea kumfanya huyu MD buzi lake la kudumu. Tanesco . Na kwamba haikuwa tu kwangu bali kawatembelea wengi akiwa na fuko la fedha akijaribu kugawa kwa usiri sana na kushawishi eti tukatae bajeti ya Wizara na pia wamfukuze Katibu Mkuu wa Wizara (eti wanasema anajifanya kuleta ulokole wa kisabato, kitu ambacho ni kweli huyu jamaa ni wa SDA lakini kosa lake sasa nalifahamu kuwa ni kwamba amekuta ameingia katika anga za TANESCO- mradi wa watu wachache na sio wa umma.

Hitimisho:
1. Wabunge tuweni macho (Independent Committee iundwe kama ya Mwakyembe ) tuone nani anasema ukweli na awajibishwe. Suala laBajetu hatuhitaji kufundishwa sisi tunawasubiri wao waiwasilishe tutaipima na kuuliza maswali yanayopaswa.

2. Mamlaka husika, vunja hiyo Bodi ya TANESCO kabisa sasa hivi na wawekwe watu wasiohusika na mahusiano ya kimaslahi na watumishi wa TANESCO na wawe wenye uwezo wa kuisimamia vyema. Why always taking retired people? Tanzania ni kubwa sana na ina wasomi kibao na wenye uwezo wa kuongoza Bodi kibao!!

MD na Mh. mpenzi wako na shoga wako na hii Kamati ya Bunge inayosimamia Wizara ya Nishati kuweni macho na kila mnachotaka kukifanya sasa maana media, wala kusambaza barua kwa Rais, PM na kwa Waziri mhusika haitawasaidia. Umma wa watanzania leo umesha wamulika kuwa ninyi ni wahujumu wa uchumi.

Sisi wabunge wenye akili na wananchi tutawaangukia ninyi na yeyote ambaye anataka kuwaunga mkono katika upuuzi wa kuihujumu TANESCO, kutumia mhusiano ya kimapenzi kujaribu kutuhadaa na zaidi ya yote kushindwa kuongoza shirika hili la TANESCO NA KUJITUNGIA MIGAO YA UMEME ILI MFAHIDI !

TUMA SALAMU!!!!!!!:israel:
 
humu hatujadili vitu visivyo na mantiki na wala mambo au maisha binafsi ya mtu....humu tunajadili issues ...soma kwa makini uzi wa huyo mleta mada utagundua una mapungufu mengi!! ni mafuta gani yanauzwa tsh 1500?
Mkuu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo mikubwa ndio yalishuhwa bei kununua kwa bei kubwa ni ufisadi !!!

Huyo mbunge anaezungumzwa ni mh SARA MSAFIRI mbunge wa viti maalum mkoa wa morogoro na mbunge mwingine anaetumiwa na Mhando ni Mh MUNDE mbunge wa viti maalum Tabora.

waheshimiwa wana JF Naomba niwajulishe tu kidogo kuhusu uchafu na hujuma anazofanya Mhando dhidi ya nchi hii.
siku ya jtatu iliopita Mhando alienda mtera na kuamuru maji yafunguliwe kwenye Bwawa la mtera ili maji yapungue na wapate nafasi ya kutangaza mgawo wa umeme. alipotoka mtera ndipo akaanzisha mgawo bila kufuata utaratibu.

Mhe SARA MSAFIRI na Mhe Munde wamekuwa wapambe wakubwa sana wa Mhando ndani ya mjengo ili watumike kumsafisha yeye na kuchafua majina ya viongozi wa wizara ili ionekane anaonewa.kazi hii wamekuwa wakifanya kwa kwa kuwashawishi baadhi ya wabunge waikatae bajeti ya wizara ya Niashati na Madini ili ionekane wameshindwa kazi.
waheshiwa hawa wamekuwa wakipewa na mhando US Dolla 10,000 kila mmoja kila mwezi.hawa waheshiwa wamekuwa wakipewa kazi za kusupply bidhaa mbalimbali pale makao makuu. na kazi waliyopewa ni kupeka matairi ambayo yalikuwa chini ya viwango na havikutumika.kazi hii walipewa na Mhando kama sehemu ya mkakati wa kuwatumia kwa malengo yake mhando
M'kiti wa bodi Mboma ni mmoja wa watu wanaoiuzia Tanesco mafuta tena kwa bei mbaya.hapa kuna comflict of interest maana hana nguvu tena ya kukemea uovu ndani ya shirika.kwa nini bodi hii isivunjwe na kuteuliwa mkiti ambae atatetea maslahi ya nchi badala kujinufaisha binafsi na kutetea uovu kama wa mhando.
Tunamwomba Mheshiwa Rais alifanyie kazi na ikiwezekana Mhando ashitawe kwa uhujumu wa uchumi na matumizi mabaya ya madaraka.kwa wale waheshiwa wabunge wa viti maalum tunawaonya waheshimu miiko yao na kufanya kile kilichowapeleka ndani ya mjengo.waache kuchanganya mapenzi na kazi.wanawatia aibu wabunge wengine wa viti maalum waliowastarabu tena wanaoipenda nchi yao.wakiendelea nguvu ya umma itawashughulikia.

waziri wa nishati na Madini na Katibu mkuu wake ndugu Maswi fanyeni kazi bila woga umma wa watanzania uko nyuma yenu na Mungu atawalinda shughulikieni wabadhirifu wote ndani ya wizara na ndani ya Tanesco na kwenye mashirika yote yaliochini ya wizara yenu.MHE Rais amewaamini na kuwapa wizara nyeti msimwangushe .

Mheshiwa Rais Tunakupongeza kwa kuchagua wachapa kazi katika wizara ya nishati.kwa kipindi kifupi wamefanya mengi na ya manufaa makubwa kwa nchi,endelea kuwapa support yako ili wakuondolee aibu iliokuwepo ndani ya wizara hii ya nishati kwa muda mrefu
 
Mhando na Mboma wote mafisadi.
Wizara ya nishati nayo imeoza, bajeti haina sababu ya kupita.
Serikali nayo mbofu, dhaifu inatakiwa kujiandaa kuleta bajeti ya maana.
Imeleta bajeti mbofu mmeipitisha, wacha iendelee kufanya blanda
 
Nchi ya Tanzania ni ina uchafu mwingi sana.ila mkuu apa ni tatizo moja tu kwa udhaifu wa baba mwenye nyumba ndio chanzo cha uchafu wa aina hiyo maana wanafanya wananavyo taka kwani baba atasema nini?
 
Huyo mbunge anaezungumzwa ni mh SARA MSAFIRI mbunge wa viti maalum mkoa wa morogoro na mbunge mwingine anaetumiwa na Mhando ni Mh MUNDE mbunge wa viti maalum Tabora.

waheshimiwa wana JF Naomba niwajulishe tu kidogo kuhusu uchafu na hujuma anazofanya Mhando dhidi ya nchi hii.
siku ya jtatu iliopita Mhando alienda mtera na kuamuru maji yafunguliwe kwenye Bwawa la mtera ili maji yapungue na wapate nafasi ya kutangaza mgawo wa umeme. alipotoka mtera ndipo akaanzisha mgawo bila kufuata utaratibu.

Mhe SARA MSAFIRI na Mhe Munde wamekuwa wapambe wakubwa sana wa Mhando ndani ya mjengo ili watumike kumsafisha yeye na kuchafua majina ya viongozi wa wizara ili ionekane anaonewa.kazi hii wamekuwa wakifanya kwa kwa kuwashawishi baadhi ya wabunge waikatae bajeti ya wizara ya Niashati na Madini ili ionekane wameshindwa kazi.
waheshiwa hawa wamekuwa wakipewa na mhando US Dolla 10,000 kila mmoja kila mwezi.hawa waheshiwa wamekuwa wakipewa kazi za kusupply bidhaa mbalimbali pale makao makuu. na kazi waliyopewa ni kupeka matairi ambayo yalikuwa chini ya viwango na havikutumika.kazi hii walipewa na Mhando kama sehemu ya mkakati wa kuwatumia kwa malengo yake mhando
M'kiti wa bodi Mboma ni mmoja wa watu wanaoiuzia Tanesco mafuta tena kwa bei mbaya.hapa kuna comflict of interest maana hana nguvu tena ya kukemea uovu ndani ya shirika.kwa nini bodi hii isivunjwe na kuteuliwa mkiti ambae atatetea maslahi ya nchi badala kujinufaisha binafsi na kutetea uovu kama wa mhando.
Tunamwomba Mheshiwa Rais alifanyie kazi na ikiwezekana Mhando ashitawe kwa uhujumu wa uchumi na matumizi mabaya ya madaraka.kwa wale waheshiwa wabunge wa viti maalum tunawaonya waheshimu miiko yao na kufanya kile kilichowapeleka ndani ya mjengo.waache kuchanganya mapenzi na kazi.wanawatia aibu wabunge wengine wa viti maalum waliowastarabu tena wanaoipenda nchi yao.wakiendelea nguvu ya umma itawashughulikia.

waziri wa nishati na Madini na Katibu mkuu wake ndugu Maswi fanyeni kazi bila woga umma wa watanzania uko nyuma yenu na Mungu atawalinda shughulikieni wabadhirifu wote ndani ya wizara na ndani ya Tanesco na kwenye mashirika yote yaliochini ya wizara yenu.MHE Rais amewaamini na kuwapa wizara nyeti msimwangushe .

Mheshiwa Rais Tunakupongeza kwa kuchagua wachapa kazi katika wizara ya nishati.kwa kipindi kifupi wamefanya mengi na ya manufaa makubwa kwa nchi,endelea kuwapa support yako ili wakuondolee aibu iliokuwepo ndani ya wizara hii ya nishati kwa muda mrefu

Hivi waheshimiwa wabunge,hamna mamlaka ya kusema haya Bungeni? Hizi tuhuma ni nzito,mbona kule ndani mnagonga meza tu? Hamuaminiani tena kiasi hiki? Tuna nchi kweli namna hii mkuu? wote mnakuja na majina bandia kama wewe hii ni ya leo muda huu!
 
Jamaa (Mhando) akaamrisha maji yafunguliwe, kina cha maji kipungue na mgao uanze, teh,teh,teh!
 
Hivi waheshimiwa wabunge,hamna mamlaka ya kusema haya Bungeni? Hizi tuhuma ni nzito,mbona kule ndani mnagonga meza tu? Hamuaminiani tena kiasi hiki? Tuna nchi kweli namna hii mkuu? wote mnakuja na majina bandia kama wewe hii ni ya leo muda huu!

Yaani mimi ndo huwa nashindwa kuelewa hawa Wabunge sijui hata tuliwachagua wa nini??
Wao wanalalamika, sisi wananchi tunalalamika, Rais analalamika..sasa jamani Nchi itakwenda kweli kwa stahili hii??..Hebu kama mnazo facts zilipueni huko huko bungeni bana..wangapi wanasoma JF??..humu mwisho wetu ni kwenye monitor za computer na screen za simu zetu tu..ebo???
 
Back
Top Bottom