RPC wa Mwanza Charles Mkumbo, apandishwa cheo

Mkuu 1000 digits kazi ya polisi ni.
. Kuzuia
. Kupambana na hatimaye kukamata na kufikisha mbele ya sheria.

Unataka kuniambia kuwa mkoa wa mwanza hapakuwa na matukio mengne mabaya zaidi?

Unafikir hili tukio la kuzuia kuagwa mwili wa mawazo unadhan ndio tukio kubwa zaidi?

Mwanza ni mkoa mkubwa wenye matukio mengi sana ya ujambaz, mauaji n.k je umeona kuwa huyo kamanda wa polis ameeshindwa kuyazuia na kuyafanyia kazi?

Una ushahidi wowote wa kutoka mahakaman kuwa hakuna kabisa za kesi za robbery, mudder, ubakaji, unyang'anyi wa kutumia nguvu, ukiukwaji wa haki za binadamu mpaka useme hakuna alichokifanya?

Amefanya Mengi sana.
Lakini mtumishi wa umma anapotangazwa na mahakama kwamba amevunja sheria hakuna namna ya kumlinda kwa sababu ya aliyokuwa amefanya .
Sheria ni msumeno.
Jeshi la polisi halitabadilika kama wakubwa wao wanapewa promosion kwa kuvunja haki na sheria za nchi.
Kuna askari maskini ya Mungu walipiga tu picha wakiwa wamekumbatiana wakafukuzwa kazi mara moja na hakuna aliyejali utendaji wao wa huko nyuma. Sheria ilifuata mkondo bila ajizi. Wote tulishangilia askari wale maskini wasio na mshahara wa kuwafanya hata waishi mtaani kwa wiki mbili mbele.
Leo wakubwa wao wanatajwa na hukumu ya mahakama kuwa wamevunja sheria halafu wanapandishwa vyeo badala ya kukaa benchi bila kitengo.
Tena sijasema huyo mkumbo afukuzwe kazi bali aachie wengine hizo nafasi kubwa za kitaifa.

Hata haya majipu yanayotunbuliwa na Dr. Magufuli yamefanya mambo mengi tu katika utumishi wao lakini pale wakipokiuka wanatumbuliwa ,why wengine wanapokosea wanatumbuliwa na wengine wanapongezwa tena mahakama ikiwa imeshatoa na mwongozo wa kukiuka sheria.
Huoni kuwa hawa watendaji wanaofanya kazi kwa matakwa na malengo binafsi ya vyeo ni hatari kwa amani ya nchi?

Na pia mtu anayefanya kazi kwa maslahi binafsi hata hayo matukio mengine anaweza kupindusha ukweli pale anapoona atanufaika.
Kama tumeamua kujenga nchi yenye haki kwa wote na hasa wanyonge basi hatuna budi kuwa na viongozi watakaohakikisha wanyonge wanapata haki zao.
Unapovunja haki ya mnyonge kwa lengo la kumlinda mtawala ni uonevu na ndio dhulma inapoanzia.
Huyo kamanda anaonekana yuko kwa ajili ya kulinda maslahi ya watawala na yuko tayari kuvunja haki za wanyonge. Jambo ambalo linamuuma sana Mh. Rais Magufuli.

Sheria ikisimamiwa kwa haki kila mtu atamuheshimu mwenzake na nchi itakua na umoja.
Hata hao majipu wanaotumbuliwa wataridhika kwa kuona hawaonewi bali ni sheria lakini huyu anatumbuliwa halafu huyu anapandishwa cheo, tutaanza kuona kwamba kuna dalili ya kukomoana na sio kazi ya kusimamia haki.
 
Last edited by a moderator:
Watu wengne mmejawa na chuki na unafki. Kwan hakuna mazuri aliyofanya huyo kamanda mnaliona la mawazo tu?

Acheni unafki na chuki binafsi dhidi ya maisha ya wenzenu

Acha bangi kaka,
 
DCI ni Diwani Athumani
Hata mimi ninavyojua kuna Chombo kunaitwa Military Inteligence ambacho Mkuu wake alikuwa Liutenant General xxxxx wa TPDF
May be huenda now Mkuu wake akatokea Polisi.

wewe kweli hamnazo
 
Amefanya Mengi sana.
Lakini mtumishi wa umma anapotangazwa na mahakama kwamba amevunja sheria hakuna namna ya kumlinda kwa sababu ya aliyokuwa amefanya .
Sheria ni msumeno.
Jeshi la polisi halitabadilika kama wakubwa wao wanapewa promosion kwa kuvunja haki na sheria za nchi.
Kuna askari maskini ya Mungu walipiga tu picha wakiwa wamekumbatiana wakafukuzwa kazi mara moja na hakuna aliyejali utendaji wao wa huko nyuma. Sheria ilifuata mkondo bila ajizi. Wote tulishangilia askari wale maskini wasio na mshahara wa kuwafanya hata waishi mtaani kwa wiki mbili mbele.
Leo wakubwa wao wanatajwa na hukumu ya mahakama kuwa wamevunja sheria halafu wanapandishwa vyeo badala ya kukaa benchi bila kitengo.
Tena sijasema huyo mkumbo afukuzwe kazi bali aachie wengine hizo nafasi kubwa za kitaifa.

Hata haya majipu yanayotunbuliwa na Dr. Magufuli yamefanya mambo mengi tu katika utumishi wao lakini pale wakipokiuka wanatumbuliwa ,why wengine wanapokosea wanatumbuliwa na wengine wanapongezwa tena mahakama ikiwa imeshatoa na mwongozo wa kukiuka sheria.
Huoni kuwa hawa watendaji wanaofanya kazi kwa matakwa na malengo binafsi ya vyeo ni hatari kwa amani ya nchi?

Na pia mtu anayefanya kazi kwa maslahi binafsi hata hayo matukio mengine anaweza kupindusha ukweli pale anapoona atanufaika.
Kama tumeamua kujenga nchi yenye haki kwa wote na hasa wanyonge basi hatuna budi kuwa na viongozi watakaohakikisha wanyonge wanapata haki zao.
Unapovunja haki ya mnyonge kwa lengo la kumlinda mtawala ni uonevu na ndio dhulma inapoanzia.
Huyo kamanda anaonekana yuko kwa ajili ya kulinda maslahi ya watawala na yuko tayari kuvunja haki za wanyonge. Jambo ambalo linamuuma sana Mh. Rais Magufuli.

Sheria ikisimamiwa kwa haki kila mtu atamuheshimu mwenzake na nchi itakua na umoja.
Hata hao majipu wanaotumbuliwa wataridhika kwa kuona hawaonewi bali ni sheria lakini huyu anatumbuliwa halafu huyu anapandishwa cheo, tutaanza kuona kwamba kuna dalili ya kukomoana na sio kazi ya kusimamia haki.

Ni maoni yako, tunayaheshimu!!
 
kila rais huwa ana culture yake....hao walioteuliwa wapya na wazamani waliopandishwa cheo, wasipo enda na mfumo wa serikal ya maguful inayofata sheriakwa maslahi ya taifa bila kuweka itikad za chama mbele basi uongoz utakuwa mchungu kwao!!!!
 
Nje ya hii mada nilishangaa huyu jamaa alipoteuliwa kuwa rpc Mwanza sababu kuna mfanyabiashara alimtuhumu kutaka kumbambikizia kijana wake dawa za kulevya

hii ndio Tanzania mkuu wangu , vipi huyo mfanyabiashara yuko hai ?
 
Ulianza kwa kureport vizuri, mwishoni ukaharibu! Kumbe unaushabiki ndani yake
 
Taarifa nilizopata zinatanabaisha kuwa,aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza amepandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Intelijensia Nchini.

Ikumbukwe kuwa RPC huyu mwenye jina na Mkumbo, ndiye aliyezuia kuagwa kwa marehemu Alphonce Mawazo pale Mwanza.

Ni wazi kuwa ule utamaduni wa kuwapandisha cheo watendaji wa serikali wanaojaribu kudhibiti upinzani,unaendelea hata kwenye uongozi mpya wa Magufuli.

Fanya utafiti kabla ya kukurupuka, kubali kwanza kuwa wewe ni mjinga kwa habari hii. Mkumbo hajapandishwa cheo amebadilishwa kituo cha kazi.
 
huyo mtoa mada ni me au ke nakama kweli we mfuasi wa chadema bac mkapa hakukosea mkumbo hajapanda cheo bali kahamishwa kituo cha kazi acheni kuleta story za kwenye kahawa humu mmekosa hoja mnakurupuka tu msiba umeisha safari hii sijui mtamuua nani ilimpate tena kusikika
 
Shetani alikuwa ni malaika awezi kugeuka kuwa tena kuwa malaika !!!
 
Fanya utafiti kabla ya kukurupuka, kubali kwanza kuwa wewe ni mjinga kwa habari hii. Mkumbo hajapandishwa cheo amebadilishwa kituo cha kazi.
Mjinga ujitambue kua ni wewe! Fahamu huwezi kupewa kazi kubwa kama ile ukiwa ACP mpaka uupandishwe kwanza kutoka ACP Kwenda CP ndivyo ilivyo kiutaratibu. Fanya utafiti wewe kwanza b.w.e.ge wewe.
 
Hii ndio Tanzania vijana hawana uwezo wa kufikir tena, fikra zao znaendesha na wanasiasa. Mtu hawez kukaa na kulifikir jambo na kupata uamuzi badala yake anasubir mpaka mwanasiasa alalamike au aongee ndio na wao wanaanza kubwabwaja.

Inatia huruma sana.
 
Mjinga ujitambue kua ni wewe! Fahamu huwezi kupewa kazi kubwa kama ile ukiwa ACP mpaka uupandishwe kwanza kutoka ACP Kwenda CP ndivyo ilivyo kiutaratibu. Fanya utafiti wewe kwanza b.w.e.ge wewe.

Hivi kwanini unakua hivyo? kwani Mkumbo alikua ACP? Mkumbo ni SACP. Acheni watu wafanye kazi buana. Kitu kama hukijui tulia ueleweshwe sio kupotosha.
 
Mi nasubiri taarifa kamili ndio ntasema neno
 
Hivi kwanini unakua hivyo? kwani Mkumbo alikua ACP? Mkumbo ni SACP. Acheni watu wafanye kazi buana. Kitu kama hukijui tulia ueleweshwe sio kupotosha.
Kwani tofauti ya SACP na ACP ni nini mbona wewe ndiye hujui kitu ndugu yangu? Wengine tulisotea huko muda mrefu kama hujui unyamaze.Hapa tofauti ndogo kati ya SACP na ACP ni seniority! CP ni cheo baada ya SACP.
 
Back
Top Bottom