RPC wa Mwanza Charles Mkumbo, apandishwa cheo

RPC wa Mwanza Charles Mkumbo, apandishwa cheo

Mkuu 1000 digits kazi ya polisi ni.
. Kuzuia
. Kupambana na hatimaye kukamata na kufikisha mbele ya sheria.

Unataka kuniambia kuwa mkoa wa mwanza hapakuwa na matukio mengne mabaya zaidi?

Unafikir hili tukio la kuzuia kuagwa mwili wa mawazo unadhan ndio tukio kubwa zaidi?

Mwanza ni mkoa mkubwa wenye matukio mengi sana ya ujambaz, mauaji n.k je umeona kuwa huyo kamanda wa polis ameeshindwa kuyazuia na kuyafanyia kazi?

Una ushahidi wowote wa kutoka mahakaman kuwa hakuna kabisa za kesi za robbery, mudder, ubakaji, unyang'anyi wa kutumia nguvu, ukiukwaji wa haki za binadamu mpaka useme hakuna alichokifanya?
 
Last edited by a moderator:
ukiona kamanda wa polisi kapelekwa Mwanza Au Mbeya huyo cheokikubwa kinamsubiri
mfano
Ernest Mangu
Valentino Mlowola
Diwani Athumani
Said Mwema
Charles Mkumbo

Uko sahihi!!! Hata Kova alishakua Mbeya na sasa ni kamanda wa kanda maalum (Dar es salaam), huyu yuko juu huwezi kulinganisha na maRPC wengine.
 
pia alisaidia ushindi wa kishindo kanda ya ziwa....nimesikia
 
Taarifa nilizopata zinatanabaisha kuwa,aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza amepandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Intelijensia Nchini.

Ikumbukwe kuwa RPC huyu mwenye jina na Mkumbo, ndiye aliyezuia kuagwa kwa marehemu Alphonce Mawazo pale Mwanza.

Ni wazi kuwa ule utamaduni wa kuwapandisha cheo watendaji wa serikali wanaojaribu kudhibiti upinzani,unaendelea hata kwenye uongozi mpya wa Magufuli.

Hiko kitengo cha Intelijensia kiko chini ya Idara gani ?
Maana kuna Idara inaitwa Military Intelligence na Mkuu wake alikuwa Liutenant General xxxxx
 
Kwa hiyo ulitaka asipande cheo kwa kigezo cha kuzuia kuagwa kwa mwili wa Mawazo?. Wewe ulitakaje kwani
 
Hicho cheo hakipo jeshi la polisi ....mbona mnashusha hadhi ya hili jukwaa? Labda mleta mada amemaanisha DCI ...

DCI ni Diwani Athumani
Hata mimi ninavyojua kuna Chombo kunaitwa Military Inteligence ambacho Mkuu wake alikuwa Liutenant General xxxxx wa TPDF
May be huenda now Mkuu wake akatokea Polisi.
 
Hii intelijensia ni kitengo kipya au kilikuwepo toka mwanzo, na kama kilikuwepo, aliyekua kwenye hiyo nafasi amepelekwa wapi au kapangiwa kazi gani?
 
Huu uzi muda si mrefu utabadilika na kuwa wa kisiasa ngoja nitoke haraka kabla hawajaanza kutukanana
 
A negative mind will always think negatively but as long as it makes you happy just go on.....
 
Taarifa nilizopata zinatanabaisha kuwa,aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza amepandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Intelijensia Nchini.

Ikumbukwe kuwa RPC huyu mwenye jina na Mkumbo, ndiye aliyezuia kuagwa kwa marehemu Alphonce Mawazo pale Mwanza.

Ni wazi kuwa ule utamaduni wa kuwapandisha cheo watendaji wa serikali wanaojaribu kudhibiti upinzani,unaendelea hata kwenye uongozi mpya wa Magufuli.
damu ya mawazo imtafune kila aliyehusika na makandokando yoyote .
 
Hiki cheo naona kitakuwa ni katika Idara ya Itelijensia ya Jinai - kipo Jeshi la Polisi Makao Makuu na huongozwa na Naibu Kamishna wa Polisi..mwanzo alikuwa CP Diwani Athumani na baadaye DCP Mlowola.
Kumbuka kuwa mfumo wa Jeshi la Polisi umejengwa na Kamisheni - Operesheni na Mafunzo, Intelijensia, Utawala, Fedha na Ugavi, Upelelezi, Uchunguzi wa Kisayansi wa Kesi za Jinai na Polisi jamii.
Kama ni kweli hayo mabadiliko yametokea basi Afande Mkubwa atakuwa ameamua kumsogeza karibu wanyumbani..
 
Nje ya hii mada nilishangaa huyu jamaa alipoteuliwa kuwa rpc Mwanza sababu kuna mfanyabiashara alimtuhumu kutaka kumbambikizia kijana wake dawa za kulevya
 
Back
Top Bottom