Watu wengne mmejawa na chuki na unafki. Kwan hakuna mazuri aliyofanya huyo kamanda mnaliona la mawazo tu?
Acheni unafki na chuki binafsi dhidi ya maisha ya wenzenu
Sio unafiki .
Hata anachofanya Magufuli ni chuki kwa mtizamo wako dhaifu.
Mtumishi wa umma ni lazima awe mwadilifu sana na mwenye kutoa maamuzi sahihi kulingana na sheria na sio matakwa yake au shinikizo.
Haya majipu yanayotumbuliwa yalifanya kwa mashinikizo na kukiuka sheria.
Mahakama kama chombo chenye mamlaka ya mwisho cha kutoa haki imesema wazi Mkumbo alikiuka sheria. Hata mwezi haujaisha mtu huyo huyo anayevunja sheria ama kwa makusudi au kutokujua au kwa shinikizo anapandishwa cheo. Ni aibu kubwa. Hafanyi kazi ya ukoo wake au nyumbani kwake anafanya kazi ya umma. Umma sio CCM wala kanda ya ziwa au Mwanza pekee bali ni watanzania wote.
Alionyesha kukiuka sheria kwenye eneo dogo kwa tamaa ya cheo. Ni hatari sana. Kama mtaanza kushabikia haya mapungufu mwishowe Magufuli atashindwa kama watangulizi wake halafu mnaanza kuleta unafiki ooh waliomwangusha ni watendaji. Lakini mlipoambiwa mapema mlisema kuwa ni wivu na chuki. Hakuna chuki kama mtu anasimamia haki. Hata enzi za JK mlikua mnaambiwa haya ambayo mwanzo mlisema ni sawa na leo CCM hao hao na familia nufaika mnajifanya kumuunga mkono Magufuli.
Wapo Viongozi wengi wa Polisi wasio na tuhuma zilizothibitshwa na mahakama tofauti na Mkumbo.
Awekwe pembeni ajifunze kuwaheshimu watanzania. Sio lazima jeshi la polisi makao makuu lisimamiwe na wale waliofanya vibaya kwenye nafasi za Mikoa.
Nchi ikichafuka hata yeye hataishi kwa amani. Wapo wengi sana waadilifu na wanaofuata sheria.
Kazi ya polisi isiwe ni siasa tu watu watakosa imani na vyombo vya dola.
Mbona askari wadogo wakitenda kinyume na sheria wanafukuzwa na wote tunapongeza?
Ili Mh. Rais Magufuli afanikiwe ni lazima ajenge mfumo wa kila mtu kutii na kufuata sheria mahali alipo na majukumu aliyo nayo.
Mtu asivunje sheria kwa manufaa yake au kwa kumlinda mtu au kikundi cha watu.
Usivunje sheria ya mtu mmoja kwa sababu ya kumlinda mwingine ,kumbuka kuwa sisi wote ni watanzania bila kujali chama,hivyo kuvunja haki ya mwanachama kimoja kwa lengo la kufurahisha kingine au kupanda cheo ni makosa makubwa . Hapa ndipo majipu yanapoanzia.
Hata kama tuna nia ya kurudi kwenye chama kimoja lakini sheria ni lazima zifuatwa na haki itolewe kwa wote . Anayevunja sheria apishe wengine wamfundishe namna ya kuongoza umma na kazi zake.