RPC na RC nani mkubwa?

Nick

Member
May 18, 2009
55
7
Hapa najatibu tuu kuangalia hawa watu wawili nashindwa kuelewa ni nani afanye nini. Kwamba ni nani anatoa ripoti kwa mwenzake.
Mifano midogo tuu ni hii hapa
1) Gari likipata ajali na kuua watu wengi nani atoe ripoti kimkoa
2) Shule au bweni la shule likiwaka moto na kuunguza/kuua wanafunzi nani msemaji mkuu
3) Majambazi/watu wameuawa na polisi nani awe msemaji
4) Maandamano ya wanafunzi/wanachama/wafanyakazi nani awe msemaji
Ninapokuwa najiuliza maswali haya yote nabakia kusema kwa kweli RC wetu hana kazi. Atasikika kwa kuongoa nini endapo kila kitu mkoani msemaji ni RPC?
Naomba mwana JF anifafanulie zaidi. Haya ni mawazo yangu tuu yananitatiza
 
Kwa mujibu wa utaratibu wa uongozi wetu, masuala ya ulinzi yanasimamiwa na jeshi la polisi, jeshi la wananchi, magereza na usalama wa Taifa. Mabossi wa taasisi hizo katika mkoa wanaunda Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo Mwenyekiti ni Mkuu wa Mkoa. Hivyo kama suala linatambuka ktk idara hizo RC ndo atakuwa msemaji. Hata hivyo RPC amepewa nafasi kubwa ya kusemea mambo yanayohusu usalama wa rai na mali kuliko RPO, RSO, Makamanda na majeshi kwa kuwa mambo yao ni nyeti zaidi hivyo kama yanatolewa kwa wananchi yatahitaji itafaki zaidi.

Hata hivyo, binafsi huwa sioni umuhimu wa kuwa na RC wakati RAS yupo. Majukumu anayoyafanya RC yanaweza kufanywa na RAS. Hali kadhalika DC, DAS anatosha.
 
RC ni Boss, ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, RPC anaripoti kwake. RC ndiye rais wa Mkoa.
 
Back
Top Bottom