RPC Morogoro akana polisi kutumia risasi za moto

Kweli CCM ina viumbe wa ajabu!.. Kwa namna hii ndo mnadhani mnarudisha imani kwa wananchi?. Pole ccm!
 
Nahitimisha kwa kusema CDM ni sawa na kuku wa kuchora ambae hawiki, hadonoi, hali na hafai kwa nyama wala kwa mayai....[/QUOTE]

Hujui nini maana ya haki za kiraia, na uongozi huujui.

Wamezuiwa wasiandamane,lakini wananchi waliandamana, wakapigwa mabomu, wakazidi kuandamana, polisi ikaona iachane nao, wakaandamana mpaka eneo la mkutano.

Hawakuharibu kitu pamoja na kuwa walikuwa wameshapigwa mabomu. Je, kama wangeachiwa wakaandamana, nani angeumizwa? nani angeuwawa? unatumika vibaya wewe, inawezekana NI SHILOGILE
.
 
kwani mabomu ya machozh yanaua. Kwanini asiende kukagua mwili wa marehemu ili ajiridhishe kama ni bom au risasi.?

Bomu la machozi linajieleza wazi ni bomu linalo sababisha mtu kutoa machozi sio kupasua kichwa cha mtu...RPC aibu.
 
Hawakuharibu kitu pamoja na kuwa walikuwa wameshapigwa mabomu. Je, kama wangeachiwa wakaandamana, nani angeumizwa? nani angeuwawa? unatumika vibaya wewe, inawezekana NI SHILOGILE
........[/QUOTE]

Taratibu za kuandamana ziko wazi kabisa, lazima wapate kibali cha polisi na siku zote wamekuwa wakifanya hivyo , sasa jana kibali walikuwa nacho ?
 
- sasa ni kwa nini anakanusha wakati ndilo lililotokea!?
- kama wanajua kuwa sio vizuri kuwaua binanamu wenzao, Waafrika wezao, Watanzania wenzao, Wana Morogoro wenzao ni kwa nini sasa wanawaua!????

Mara zote kwa binadamu kamili huwa kuna haja ya kufikiri kabla ya kutenda
 
Katika hatua ya kushangaza, RPC wa Morogoro amekana askari wake kutumia silaha za moto wakati wa kuzima maandamano ya chadema yaliyofanyika mkoani Morogoro leo.Alisisitiza polisi kupiga mabomu ya machozi tu.

Source:Mahojiana ya kamanda huyo na kituo cha TV cha chanel ten wakati wa taarifa ya habari ya saa moja usiku huu.
Hii ni kweli tupu, mimi naweza kuamini kwamba kutokana na ushahidi wa Slaa kukutwa na silahaa kule arusha kwenye maandamano, na huku morogoro inawezekana kabisa watu hawa wakawa wanaua ili kuisingizia polisi, hilo polisi mnatakiwa kuwa makini nalo, na maandamano yao wanayofanya sio ya heri kabisa kutokana na kulazimisha hata pale wanapoambiwa wasifanye hivyo. na hao waliokamatwa wanatakiwa kueleza vizuri kuhusu kifo cha huyo muuza magazeti.
 
Ndio wale wale wafuasi wa magamba
 
....[/QUOTE]

Hizi taratibu unazozungumzia ziko tofauti Mkoa hadi Mkoa? Je kila RPC anaunda zake? Chadema wanafanya mikutano nchi nzima, wanayohabari kuhusu vibali hivi kila wanapoenda na si mara ya kwanza kukumbana na dhoruba hizi, tungependa kufahamu kama kibali hakikuwepo kwanini hakikutolewa?
Na kama hakikutolewa uamuzi sahihi siyo kuua mwananchi asiye na hatia. Wangewachukulia hatua viongozi wa Chadema.

Walikuwepo wa ngazi za juu na wenye ufahamu wa sheria kama Tundu Lisu. Hakuna anayeweza kuamini haya maneno yako kirahisi labda utuletee uthibibisho sahihi hapa.
Je kama ilikuwa hakuna kibali kwanini RPC mwenyewe alisemekana kuwepo mbele kabisa kwenye ule mkutano? Alifuata nini badala ya aidha kuwaita viongozi wa Chedama baada ya Mkutano na kuwahoji kama walivyozewea??

G/Brain nadhani hukuangalia ITV, ungeangalia usingeuliza maswali haya maana hata kama hapakuwa na kibali Kamanda mwenye akili nzuri, kamanda mwenye nia njema ya kulinda raia na anaeelewa kuwa huo ndiyo wajibu wake asingetenda kama ilivyoonekana kwenye yale matukio.

Ilionekana wazi kuwa Polisi walitumwa kwenda kufanya uchokozi ili wananchi waliokuwa hawakushika chochote mkononi waanze labda kuokota mawe ili iwe ni kisingizio cha kufyatua risasi. Kilichoshangaza sana hakuna hata aliyeinama sasa baadhi ya Polisi baada ya kuona nia yao haikutimia wakaanza fujo wao wenyewe.

Nilishangaa kuona gari ya Polisi ilikwenda mpaka karibu kabisa na kundi la waendesha pikipiki wala hawakusogea wala hawakukimbia, na hiyo ndiyo ilikuwa salama yao maana ndipo Polisi wangezidi kuwavuruga wananchi.

Kitendo cha wananchi wale kusimama kwa utulivu na kungoja wapigwe mabomu ya machozi na kuendelea kutembea kuelekea kwenye mkutano kisichukuliwe kirahisi namna hiyo. Serikali inabidi sasa ifahamu kuwa hao ma RPC hawatakiwi tena kuwa ndiyo watoa vibali vya mikutano, wanatakiwa badala yake waelekezwe kwenda kuwalinda wananchi kwenye hiyo Mikutano.

Kinyume chake nchi inaplekwa pabaya. Maneno ya kiajana mmoja aliyosema "Wao wanajifunza kutuuwa na sisi tunajifunza kuuwawa".

Serikali itumie busara zaidi kuulewa ujumbe huu wa huyu kijana.
 
Hivi nchi hii tunaelekea wapi hivi inaposemekana polisi hawajasoma ndo hivi? mtu ameuawa kwa risasi yeye anakana hivi hata kama akili zako ni ndogo ndo zinakuwa ndogo kupitiliza. Mungu atawahukumu wote mliotenda udhalimu huu na wote waliowatuma na wanaoshabikia uhovu huu.

nguvu iliyotumika ni kuzea na matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi, ukitathmini, unaona jeshi la polisi litumika kisiasa, je hayo maandamano yalikuwa na athari gani kusababisha uvunjifu wa amani ukilinganisha na kuwaache waandamane waende kwenye mkutano wao?nimeona kwnye vyombo vya habari wakati wanazuia maandamano hayo kulikuwa na vurugu kubwa ukilinganisha na walipozidiwa nguvu, vijana wakajikusanya wakaandaman wakaenda mkutanoni hakukuwa na uvunjifu wowote wa amani.hakuna matukio yaliyoripotiwa baadaya ya kuzidiwa nguvu na vijana kujiunga tena kwenda kwenye mkutano.Pia watu wote waliohojiwa waliokuwa karibu na mtu aliyeuawa, wanasema, ilikuja defenda yenyeupe ya polisi ikaanza kufyatua mabomu na risasi za moto, huyo mtu alikuwa kwenye magazeti yake anasoma, ndo wakamfyatuli risasi kichwani na kuua.Kwahiyo maanake risasi zilikuwa zinafyatuliwa hovyohovyo, na kusababisha vifo kinyume na inavyotakiwa kuwa hazitakiwi kulenga watu bali kupiga hewani.Shilogile, ni mjinga ndo askikari wachumia tumbo bila kujali haki na mienendo ya haki.polisi wameua asikwepe.
 
Katika hatua ya kushangaza, RPC wa Morogoro amekana askari wake kutumia silaha za moto wakati wa kuzima maandamano ya chadema yaliyofanyika mkoani Morogoro leo.Alisisitiza polisi kupiga mabomu ya machozi tu.

Source:Mahojiana ya kamanda huyo na kituo cha TV cha chanel ten wakati wa taarifa ya habari ya saa moja usiku huu.

Huyu Shilogile nilidhani ni mojawapo ya askari wasomi wenye busara, japo nilipewa visa vya matendo yake ya ajabu sana katika nyanja za mahusiano ya kijamii, yanayoonesha wazi kutokuwa kwake na busara katika jamaii yenye ustaarabu. Naona ni walewale tu polisi wetu ambao wanaona suluhisho kwa kila tatizo lililoko mbele yake ni kutumia nguvu ya silaha badala ya akili.
 
Katika hatua ya kushangaza, RPC wa Morogoro amekana askari wake kutumia silaha za moto wakati wa kuzima maandamano ya chadema yaliyofanyika mkoani Morogoro leo.Alisisitiza polisi kupiga mabomu ya machozi tu.

Source:Mahojiana ya kamanda huyo na kituo cha TV cha chanel ten wakati wa taarifa ya habari ya saa moja usiku huu.

What did you expect kutoka kwa Kova and Kompany! like father like son!

japo jeshi letu la Polisi ni dhaifu bado ninaamini tunao ballistic experts wanaoweza kutambua aina ya bunduki, callibre, range na velocity ya risasi iliyotumika kumuua mwanamapinduzi huyo!

Kwa hiyo wahusishwe kwenye postmorterm ya huyo shujaa sambamba na pathologist huru (not an embbedded one!!) ambaye kazi yake ni kutambua proximate cause of death ya shujaa huyo. uongozi wa CDM Morogoro lisimamieni hilo kama ilivyofanyika hapa Arusha.
 
Shilogile asilaumiwe jamani ni maelekezo ya wakubwa wake,hata yeye inamuuma sanalakini hana jinsi
 
Katika hatua ya kushangaza, RPC wa Morogoro amekana askari wake kutumia silaha za moto wakati wa kuzima maandamano ya chadema yaliyofanyika mkoani Morogoro leo.Alisisitiza polisi kupiga mabomu ya machozi tu.

Source:Mahojiana ya kamanda huyo na kituo cha TV cha chanel ten wakati wa taarifa ya habari ya saa moja usiku huu.

Mimi nafikiri huyu RPC Shilogile anakula unga au anavuta Bangi!

Asitake kuwafanya Watanzania hawana akili kama yeye. Hapa kuna mtu tayari amekufa kwa kupigwa risasi na wengine wamejeruhiwa. Anaposema kuwa askari polisi hawajatumia risasi za moto anamdanganya nani hasa???

Yawezeka huyu afande anashindwa kujieleza. Alitakiwa aseme kwamba yeye hakutoa amri ya askari wake kutumia risasi za moto na kwahiyo hatua za kisheria zichukuliwe haraka kwa askari wote waliohusika na mauaji kwa kutumia silaha za moto na ikiwezekana wafukuzwe kazi. Hii kukanusha tu kwenye media haimsadii RPC wala IGP wake na CCM yao.

Kwanza inasikitisha kuona kwamba si Rais Kikwete,IGP wala Waziri wa Internal Affairs Bwana Nchimbi hakuna ambaye ametoa tamko au kuzungumzia mauaji haya ya Morogoro. Baadaye pengine tutamsikia vuvuzela wao Nape Nauye akiropoka maneno yake ya kiwendawazimu. Tusubiri.
 
Shilogile asilaumiwe jamani ni maelekezo ya wakubwa wake,hata yeye inamuuma sanalakini hana jinsi

Thats why i don't like polisi"kwani yeye akili yake iko likizo mpaka aue binadamu wenzie
kwa maagizo ya wakuu wake?
 
Back
Top Bottom