Ni katika taarifa ya habari ya ITV ya jana Tar 28/08/2012, Shigela alisema kuwa haingii akilini kuona polisi wanasemwa kuwa ndio waliomuua mtu pale Morogoro asiyekuwa mhusika hata kidogo katika maandamano ya CHADEMA, wakati waliovaa magwanda walikuwa wanaonekana na wasidhurike na risasi hizo, Shigela akasema kuwa huo ni mchezo mchafu wa CHADEMA.
Kwa kauli hii ilinipa maswali mengi ya kujiuliza katika CD hii ya Shigela na mtazamo wake kuhusu Polisi na Serikali, kwani ailiingia akili kupigwa kwa Ulimboka ? na polisi kumleta mtu anayesemekana mkenya katika mazingira ya utata? iliingia akilini kuawa kwa mfuasi wa CHADEMA pale Igunga? iliingia akilini mauaji yaliyofanywa na Zombe? ilingia akilini kwa kupigwa kwa wabunge wa CHADEMA pale Mwanza? ilingia akilini kupigwa na kuawa kwa raia pale Songea waliokuwa wakienda kutaka kauli ya mkuu wa wilaya ? iliingia akilini kwa mauaji yaliyofanywa kule Arumeru.
Kwa mujibu wa SHIGELA ni mauaji ya Morogoro tuu ambayo hayaingii akilini na hivyo jibu rahisi kama mauaji hayaingii akilini mwa SHIGELA muhusika ni CHADEMA. Kwa kauli ile inadhihirisha kuwa mauaji yaliyopita yaliingia akilini mwa SHIGELA.