Tanzania DAIMa ..........Takwimu za kisiasa nchini tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi Julai 1992, zinaonesha kuwa vyama vyote vikubwa vimesambaratishwa kwa nguvu ya virungu, mabomu ya machozi, maji ya kuwasha, risasi za moto za polisi vilivyoelekezwa ama kwa viongozi wa vyama hivyo au wafuasi wao ............ kumbuka NCCR-Mageuzi (1995-1998) chini ya Augustine Mrema na baadaye TLP. Makeke ya mwanasiasa huyu na wafuasi wake yalimalizwa na polisi waliowaandama kila kona kuhakikisha hawaandamani kwa amani wala kufanya mikutano ya hadhara na shughuli zao nyingine za kisiasa.....Miaka ya 2000-2005 baada ya NCCR-Mageuzi na TLP kunyongonyeshwa, kiliibuka Chama cha Wananchi (CUF), enzi hizo kikijiita ngangari, lakini nacho kilishughulikiwa ipasavyo na polisi chini ya IGP yule yule, Omar Mahita......mauaji yalifanywa na polisi Januari 26 na 27 mwaka 2001 kwa wafuasi wa CUF kule visiwani Zanzibar kwa wananchi zaidi ya 33, wengine kubakia vilema hadi leo, huku mamia wakiikimbia nchi na kwenda kuishi maisha ya ukimbizi eneo la Shimoni Mombasa nchini Kenya......unyama waliotendewa viongozi wa CUF na wafuasi wao Bara na Visiwani, .....kituko cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, ambapo IGP Mahita alijitokeza kwenye vyombo vya habari akiwa na visu na kudai ni vya chama hicho.......Ngwe hiyo imepita, mwaka 2010 CHADEMA ndicho kimeshika usukani wa upinzani nchini, lakini tayari polisi wamekiandama kwa mizengwe ya kila aina ambayo sasa inaelekea kushindikana kabisa japo hawajakubali. ............... kule jijini Mwanza, polisi walipowapiga virungu, mabomu na kuwamwagia maji ya kuwasha wafuasi wa CHADEMA, .................Mkoani Singida hivi karibuni mkutano wa chama hicho ulivamiwa kwa mawe hadi kijana mmoja anayedaiwa kuwa mfuasi wa CCM kuuawa..........mkoani Morogoro risasi za polisi zimemuua kijana Ally Nzona na kuwajeruhi wengine wawili, Frank Mbalimba na Hashim Seifu katika harakati za kusambaratisha maandamano ya amani ya CHADEMA.. Tafakari!...