RPC: Hakuna wa kuzuia mkutano wa CCM

RPC: Hakuna wa kuzuia mkutano wa CCM

Unwezaje kufananisha kutaniko kuu la Chama kinachounda serikali na mkutano wa kampeni zenye matusi?

JIONGEZENI !

KAMA VIPI NA CHADEMA IITISHE MKUTANO MKUU AMBAPO MBOWE ATAKABIDHI KITI MUONE KAMA HAMTARUHUSIWA KUFANYA.
Daah hiyo ID inakupendeza kweli
 
Umetisha mkuu...Hivi jiji la Mbeya na Manispaa ya Iringa wao wapo upande gani...
Ni vizuri watanzania tukaongea siasa za hoja zenye nguvu badala ya kuanza kuongea hoja zenye chembechembe za ukanda, ukabila na udini..hizo hoja zako hazina nafasi kwa Tanzania ya leo..


Asante kwa kunikumbusha nilisahau Mbeya City pia ambako hata hivyo Sugu alishinda kwa sababu vijana wanapenda Hip Hop hivyo walichagua Hip hop na siyo Sugu, lkn hiyo ni mada nyingine hata hivyo!
 
Hakuna haja ya BAVICHA kujipanga na kwenda kujaribu kuuzuia mkutano wa CCM. Hii ni kuingia ''vitani'' huku unajua fika utashindwa vibaya. Dawa sasa ni UKAWA kujipanga kuendelea na ile mikutano waliyoipanga kuanzia siku hiyo ambapo CCM wanafanya mkutano wao maana by default lile tangazo la police la kuzuia mikutano litakuwa limeexpire (Intelijensia imegundua mambo yako OK)
Ndio maaana Msumbiji wanaangaika na Dhlakama mpaka Leo kwa watu kujiona wao ndio wao
 
Hakuna lisilokuwa na mwisho,ila mara nyingi mwisho huwa ni mbaya sana.Hakuna aliyewahi baki salama kwa kukandamiza demokrasia milele ila ni kwa muda tu.When you're on top,there's no way you can go but down.
 
wakati wao wanafanya na nyie fanyeni mkutano wenu tuone nani atamkolofisha mwenzake
 
nimemiss maisha ya shule, hasa kusoma vitabu kama cha KUSADIKIKA NA MFALME JUHA. vilikuwa na story nzuri na za kuelimisha.
 
Kuzuia ccm ni sawa sawa kuzuia yanga kuchukua ubingwa vijana wa mwendo kasi
 
Ni kweli kabisa. Inatakiwa na wao CHADEMA waanze mikutano siku hiyo hiyo badala ya kuzuia ule wa CCM. Tena na wao wangefanya mkutano wao huko huko Dodoma na sehemu nyingine nyingi
Wangefanya mahafali yaliyokatazwa!!
 
Kwan mkutano wa ccm ni mkutano wa hadhara au imekaaje hii
Nina hakika pia cdm, cuf, act nk wakiamua kufanya mikatano yao kweny majengo ya ofis zao polis hawatawazuia
Tatizo ni kuishi kwa kuangalia mwenzako anakosea wapi na kulipizana visasi
#Hatari
 
Nimesikia sasa Polisi wanatawanya Mikutano, Sherehe, na hata Misiba ya Wanasiasa Ati kulinda amani. Sasa Hiyo inaitwa Kulinada amani au Ni Kuvuruga amani, Watu wako kwenye sherehe, au msiba au ibada, au mkutano wa Chama Unawapiga Mabomu, Je Ni Kulinda amani huko? au ni Kuvuruga amani?

Kama Kulinda amani ndio huko, Kama Niaa yao ni ya kweli, Kama hawafanyi hivi kwa Kutumwa na Serikali Kuwasaidia Wanaccm Kisiasa kwa Njia ya Uharamia, Basi wanithibitishie hili, naomba Polisi Tanzania Muandae Mabomu ya Kutosha na Maji ya Washawasha Muwapige Mkutano Mkuu wa CCM Unaanza Dodoma nadhani ni Mwezi wa saba ili kuwe na Amani. Na Mtaonekana 1) Mnapowapiga wengine Mabomu hamtumwi na CCM 2) Kuwa Kweli huo ndio Mtindo wenu wa kulinda amani.

Vinginevo Wakuu wote wa Polisi Tanzani, Pamoja na Kuwa Kweli Mnafanya kazi ya Kweli ya Kulinda amani, Lakini Katika hili Mtatufanya Kuendelea Kuamini Kuwa Mmekuwa Vibaraka na Wanyapara wa CCM Tendo ambalo ni Kinyume na sheria ya Vyama Vingi, Na Ni fedheha Kwa Mtu anayejiheshimu Tena Polisi Kutumwa Kukandamiza haki.

Yupo wapi Mkuu wa Polisi Mmoja atakayejitolea Muhanga Kujiuzulu, Watanzania Tutamchangia Mamilioni aishi Kwa raha na heshima na Awe ni Mfano wa Historia.Haki ya Mama hata Mimi Nitauza ikiwezekana, Mbusi, Kuku, mbwa, hata Paka na Gari yangu na mimi nivurutishie kamchango!

Vinginevyo Zoezi haramu wanalolifanya Polisi la Kuzuia Mikutano, sherehe na hata Mazishi ilimradi tu sherehe hizo ziwe na harufu ya Zitto wa ACT, au Chadema au CUF. POLISI MKOME NA MNAOWATUMA MKOME.
 
Kwan mkutano wa ccm ni mkutano wa hadhara au imekaaje hii
Nina hakika pia cdm, cuf, act nk wakiamua kufanya mikatano yao kweny majengo ya ofis zao polis hawatawazuia
Tatizo ni kuishi kwa kuangalia mwenzako anakosea wapi na kulipizana visasi
#Hatari
kwanza fahamu kwamba CCM haijawahi kuwa na jengo.
 
Back
Top Bottom