RPC apiga marufuku mahafali ya CHASO Morogoro

RPC apiga marufuku mahafali ya CHASO Morogoro

Inaonekana ni marufuku kufanya graduu za Chuo chini ya Chaso.

Ila chini ya CCM ni ruksa, Halafu anatokea mtu anatuambia marufuku kufanya siasa mpaka 2020. Only in Africa.
Inashangaza. Anaye piga marufuku anastahili kupimwa!
 
Hawa watu wanaofanya tanzania kama ni nchi yao peke yao,miaka ijayo Mungu akitusaidia tukapata uhuru naomba Mungu waje watafutwe popote pale walipo washitakiwe kwa udharimu huu wanatufanyia watanzania hata kama watakuwa ni wazee vikongwe wajibu mashitaka bila huruma.
 
Sasa wewe bwana Jafary, umepata nafasi ya kuongea na Kamanda kwa nini hukumuaeleza hayo yote unakuja kulalamika mitandaoni? Ili iweje?
Nna uhakikanungemwuliza maswali yako hayo yote angekupatia majibu.....
 
Kumbe chaso ni chama cha siasa. Duh!! Hawa wapuuzi kweli. So kama wanaona wameonewa waingie mitaani bila ruhusa. Watajuta kuzaliwa.

Kumbe walikuwa sahihi kukuweka kwenye ile list!
 
Mr. Ndege usirudi nyuma, do the occupy movement.
Redirect timu yako, hakikisha hayo ya CCM hayafanyiki.
This is an opportunity for you sacrifice Mr. Ndege.
Ushinde uoga walau mara hii moja, wasaidie makamanda wako kuushinda woga.
I count for you brother, make us proud.
 
Yaani Lowassa amewatoa jasho vile bado utaki kuamini kuwa nyie Ni wepesi. Haki haipotei Bali inachelewa.

Lowasa kawaharibia kabisaaa.Mahafali gani mtu anaenda kuongelea kuwa hatambui ripoti ya watazamaji wa kimataifa wa uchaguzi,Mahafali gani mtu anaenda kuongelea kuwa hatambui matokeo ya uchaguzi ,mahafali gani mtu anaongelea mambo ya uchochezi wa kisiasa? CHASO ni chama cha kisiasa kinachofanya kazi kinyume cha sheria kwa kuwa vyuoni haviruhusiwi vyama vya kisiasa vya wanafunzi.Kama kimesajiliwa kinabidi kifutwe sababu kinakiuka masharti ya vyuo ambavyo haviruhusu ukada vyuoni kwa wanavyuo
 
Duuuu!!CHASO,naikumbuka sana siku tunaianzisha CHASO tukia nje ya canteen ya Mabibo Hostel.Mwanzo tuliita CHASA jina ambalo hata hivyo lilidumu kwa juma moja tu ndipo baadae tukalibadilisha na kuwa CHASO.Mwenyekiti wa kwanza kbsa wa CHASO ni Mdada na kada wa CCM kwa sasa Juliana Shonza.

Haikuwa rahisi sana kuuanzisha huo umoja lakini tulipata support kubwa kutoka Chadema makao makuu hadi leo hii CHASO inawatoa watala jasho.Najisika fahari kila nionapo jina CHASO.
 
Kungangania mahafali ni kulazimisha kutengeneza forums kwa ukawa baada ya kujinyima haki ya kusema bungeni...vile vile ni kutanua wigo wa lowasa kupata media coverage....
 
Kesho nenden hapo Polisi kwa RPC mumpe taarifa kuwa CCM wamekusanyika mahal flan, asipowatawanya, Bas na nyie fanyeni mahafal yenu keshokutwa hapo hapo wanapofanyia CCM.
 
Na: Jafary Ndege:
Mratibu Chaso Mkoa~Morogoro

Leo nimebahatika kwenda kwenye Ofisi ya Kamanda wa Mkoa Polisi Morogoro baada ya kutuita Viongozi wa Chadema Mkoa na Wilaya kuzungumzia Mahafali ya Chaso Mkoa yaliyokuwa yafanyike kesho tarehe 25/06/2016 ambapo Mgeni Rasmi ni Mhe. Edward Lowassa.

Cha kunishangaza tulipokuwa tunazungumza na RPC akasema yafuatayo:

1. Siwezi kuwaruhusu kufanya mahafali yoyote kwa kuwa Sasa hivi Haturuhusu mikusanyiko ya aina yoyote.

2. Hivi msipofanya mahafali mtapungukiwa nini..mahafali yana faida gani kwenu??

3. Mnafanyeje Mahafali bila wanafunzi kufanya mitihani yao??

Lakini wakati RPC anasema hayo kesho Jumamosi tar 25/06/2016..Shirikisho la CCM wanafanya Mahafali yao pale SAVOY HOTEL.

Sasa najiuliza;

1.Mahafali ya CCM yanayofanyika kesho sio mkusanyiko?? Tena kwa mujibu wa RPC wa Morogoro inaonesha CCM wanafanya mahafali yao bila kibali chochote.

2.Naendelea kujiuliza hivi RPC hakusoma sekondari wala Chuo kujua umuhimu Mahafali au hata kama hakusoma hakuwahi kusikia mahafali kwa jirani ili atambue umuhimu wake.

3. Naendelea kujiuliza kuwa RPC hajui kuwa wengi wetu na utaratibu tangu sekondari tumekuwa tukifanya mahafali kabla ya mitihani? Amekariri kuwa mahafali yanafanyika tu baada ya mitihani...kumbe yote yanawezekana.

USHAURI: Ni lazma ifike sehemu tuache kulalamika kila siku tufanye maamuzi kwa vitendo ili Dunia yote ijue...Haiwezekani Nchi wapo wenye haki zaidi kuliko wengne...Nchi hii ni ya kwetu sisi sote..Kama mikutano inazuiwa, Vikao vinazuiwa, mahafali yanazuiwa, tutatafuta njia nyingine..HAKI HAIOMBWI..

Jafary Ndege,
Mratibu CHASO~MKOA MOROGORO.
kwani hamjafanya mahafali ya chuo?
 
Naona kwenye huu uzi wamejaa wapuuzi,wanajadili kwa kutumia viuno badala ya kichwa,shwain!Hamtambui katiba inavyotoa haki kwa vyama vya siasa!JF imejaa majuha siku hizi
 
Hizi graduation za kichama ni aina mpya ya graduation....yaani hivyo vyuo vyenu kwa miaka minne vimewafundisha siasa?

Mbona mnadhihaki mahafali kiasi hiki?

eti bwana! hawa UVCCM na chaso bwana wanashangaza kwa hizi graduation
 
Polisiccm katika ubora wao wa kuimarisha udikteta nchini dhidi ya vyama vya upinzani na wafuasi wao.
 
Naona kwenye huu uzi wamejaa wapuuzi,wanajadili kwa kutumia viuno badala ya kichwa,shwain!Hamtambui katiba inavyotoa haki kwa vyama vya siasa!JF imejaa majuha siku hizi
Nyie ongeeni tu,uzuri wote tutalipa gharama ya hiki mnachopanda leo hii maana wote tuko kwenye boti moja na tutazama pamoja.
 
Hivi kwanini dunia inajua tunavyama vingi ile hali uhuru wa vyama vingi umeminywa
 
mtu anayeongoza iv n huyu huyu alisema atakuwa rais wa wote na n huyuhuyu kila siku anasema tumuombee,,,,,hiz double standard za waz kuna siku zitatukost
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mtu anayeongoza iv n huyu huyu alisema atakuwa rais wa wote na n huyuhuyu kila siku anasema tumuombee,,,,,hiz double standard za waz kuna siku zitatukost
Ndugu, ombea wagonjwa na wenye shida hata kwa mungu utapata thawabu lakini sio hao unaowafikiria.
 
Back
Top Bottom