Na: Jafary Ndege:
Mratibu Chaso Mkoa~Morogoro
Leo nimebahatika kwenda kwenye Ofisi ya Kamanda wa Mkoa Polisi Morogoro baada ya kutuita Viongozi wa CHADEMA Mkoa na Wilaya kuzungumzia Mahafali ya Chaso Mkoa yaliyokuwa yafanyike kesho tarehe 25/06/2016 ambapo Mgeni Rasmi ni Mhe. Edward Lowassa.
Cha kunishangaza tulipokuwa tunazungumza na RPC akasema yafuatayo:
1. Siwezi kuwaruhusu kufanya mahafali yoyote kwa kuwa Sasa hivi Haturuhusu mikusanyiko ya aina yoyote.
2. Hivi msipofanya mahafali mtapungukiwa nini..mahafali yana faida gani kwenu??
3. Mnafanyeje Mahafali bila wanafunzi kufanya mitihani yao??
Lakini wakati RPC anasema hayo kesho Jumamosi tar 25/06/2016..Shirikisho la CCM wanafanya Mahafali yao pale SAVOY HOTEL.
Sasa najiuliza;
1.Mahafali ya CCM yanayofanyika kesho sio mkusanyiko?? Tena kwa mujibu wa RPC wa Morogoro inaonesha CCM wanafanya mahafali yao bila kibali chochote.
2.Naendelea kujiuliza hivi RPC hakusoma sekondari wala Chuo kujua umuhimu Mahafali au hata kama hakusoma hakuwahi kusikia mahafali kwa jirani ili atambue umuhimu wake.
3. Naendelea kujiuliza kuwa RPC hajui kuwa wengi wetu na utaratibu tangu sekondari tumekuwa tukifanya mahafali kabla ya mitihani? Amekariri kuwa mahafali yanafanyika tu baada ya mitihani...kumbe yote yanawezekana.
USHAURI: Ni lazma ifike sehemu tuache kulalamika kila siku tufanye maamuzi kwa vitendo ili Dunia yote ijue...Haiwezekani Nchi wapo wenye haki zaidi kuliko wengne...Nchi hii ni ya kwetu sisi sote..Kama mikutano inazuiwa, Vikao vinazuiwa, mahafali yanazuiwa, tutatafuta njia nyingine..HAKI HAIOMBWI..
Jafary Ndege,
Mratibu CHASO~MKOA MOROGORO.