Royal Tour: Wacheni Tuseme Ukweli

Royal Tour: Wacheni Tuseme Ukweli

Wazo lilikuwa zuri, lakini mleta wazo katuzidi ujanja.

Unapotengeneza filamu ambayo ni andishi la kitaaluma na kibiashara,tulipaswa kutanguliza taaluma zaidi kuliko siasa.

Mwanasiasa anaweza kukumbwa na kashfa au dosari za kiuongozi na kupelekea kupoteza soko kusudiwa baada ya kususiwa kote ilikotangawzwa na kuvuma. Huo ndio utamaduni wa wazungu.

Tulipaswa pia kuzilenga taasisi kubwa zilizobobea katika taaluma hiyo Duniani kama vile National Geographic au Animal Planet ambazo tayari zinajiendesha kupitia Vituo vyao binafsi vya kurushia Documentary zao Dunia nzima. Na zinaangaliwa na mamilioni ya watu Duniani kila siku.

Huyu Peter Greenbag hana Impact kubwa Duniani kama ambavyo ametuingiza mkenge kumdhania. Unaweza kutafakari hilo kwa kujiuliza aina ya watu ambao wamehudhuria uzinduzi wake huko Marekani.

Pia jiulizeni kwamba,inakuwaje utengeneze filamu ya kukutangangaza kibiashara,halafu unaiingiza Sokoni Amazon kuiuza.

Badala ya wewe Mtangazaji wa biashara yako ndio uwalipe wao ili wakutangaze.eti wewe ndio unaliuza tangazo lako kwa wateja.

Lengo likiwa kujulikana zaidi na hivyo kuvutia wateja kuja kuyaona yale uliyoyatangaza kupitia filamu yako.

Unapoanza kwa kuiuza bila kujua kama ita hit kwenye mauzo au la! Hii inaleta maswali mengi kuliko majibu.

Pia ingekuwa vema Rais angeambatana na wataalamu wa fani ya utalii pamoja na wabobezi wa African Wildlife Management.
Ambao tungewaona bega kwa bega na Rais wetu,wakimsaidia kujibu maswali na kukidhi kiu ya waulizaji. Kwa kujikita zaidi kitaaluma na kitakwimu sahihi. Hususan kwenye hafla za uzinduzi.

Ambapo majibu yao ya kitaaluma yangeongeza chachu ya watu kuitamani zaidi filamu ili wajionee uzuri wa Tanzania.

Tofauti na kilichofanyika kwa kwenda kumpambanisha Rais wetu,ambaye kitaaluma sio fani yake.

Hapo tayari umemchezesha Bahati Nasibu rais na watanzania bila kujua wala kupenda.

Hapo ni wazi kwamba waandaaji wameutumia muda wa Rais kwa manufaa yao zaidi.

Boston ndio mji ambao ni kitovu cha utalii na taasisi za utalii na wadau wake nchini Marekani.hasa kuhusu utalii wa nje ya Marekani kama Afrika na kwingineko.
Kuliko New York au Los Angeles

Hivyo ingekuwa vema uzinduzi ule ukafanywa katika mji huo,kuliko kwenye jiji la New York ambalo halina sifa ya utalii zaidi ya kujaa watoto wa mjini.

Kwa nini hata hawakupata wazo la kuingia mkataba na mmojawapo wa wasanii maarufu nchini Marekani,ili waweze kurekodi pamoja na Rais wetu ili kuiongezea chachu na umaarufu kimataifa?

Rais Samia ni Maarufu Tanzania ndiyo.
Lakini hajawa maarufu kimataifa kwa kiwango cha kuwashawishi watu kumiminika kuinunua filamu yake kwa sasa.
Kama waandaaji na wapiga debe mnavyotaka kuiaminisha Dunia.

Will Smith ametengeneza filamu ndogo tu ya jinsi alivyotembelea Afrika na Tanzania ikiwemo na inaweza kuipiku kwa mbali sana hii ya kwetu.kulingana na jinsi inavyoshambuliwa huko Marekani kwa mauzo.

Tujaribu kidogo kumuangalia Kagame wa Rwanda jinsi anavyoitangaza nchi yake bila kuingiza sura yake hata kidogo na Rwanda inapaa kimataifa.

Madhara ya kumtumia Rais moja kwa moja,
Na kuihusisha serikali yake kwenye masuala ya matangazo hasa haya ya kitalii. Ni kwamba soko lake pia litategemea rekodi yake pamoja na serikali yake kiutawala.
Wazungu huwa wanapiga chini kila kitu pindi mhusika anapokumbwa na kashfa yoyote ile.

Nimalizie kwa kuitaka serikali isikie maombi ya watanzania kutaka watuweke wazi kuhusu gharama na umiliki wa filamu ya Tanzania Royal Tour.

Nimemaliza kuutumia uhuru wangu kikatiba.
View attachment 2200347
Tufanyeje?
 
Unahamisha magoli.Rostam Aziz hahusiki lolote na Royal Tour Tanzania.
Kama tatizo kuhusu yeye anzisha mada mpya kuhusu yeye.
Kama hahusiki anafanya nini huko na mama huku akisaini mikataba pembeni ya mama.
Wakati yeye si afisa wa serikali?
 
Hivi mleta mada ushawahi kuiangalia Royal Tour film ya Rwanda? Je Kagame hakuwepo kwenye filamu? Tatizo lenu dada zetu wa siku hizi kila kitu mnakichukua kimipasho mipasho ilimradi na nyie muonekane kuwa mnajua kusuta.

Unaweza kukuta mleta mada ni raia wa nchi nyingine hivyo maendeleo yoyote kwa Tanzania ni sawa na msumali wa moto katikati ya makalio yake. Shem on you poor girl. JF imeingiliwa na mabinti wa mipasho na wanaharakati koko.
Wivu tu na ujuaji umemjaa mtoa mada.
Ni wa kawaida sana ukiangalia guests/clients wake wa the royal tour.

He also produces and hosts a television series called The Royal Tour which airs on PBS. The series features various heads of state giving Greenberg and viewers a personal tour of their country. It has featured a number of world leaders including New Zealand's Helen Clark, Israel's Benjamin Netanyahu, Abdullah II of Jordan, Peru's Alejandro Toledo, Mexico's Felipe Calderón, Rwanda's Paul Kagame, Poland's Mateusz Morawiecki and Tanzania's Samia Suluhu Hassan. Greenberg was previously the Travel Channel's chief correspondent.
..👆..

Soma hapo mtoa mada.
 
Achana na film industry hapa tunaongelea sekta ya utalii na gharama za kutengeneza hiyo film pamoja na umiliki wake?

Masuala ya vyeti Tanzania vimejaa ila havina thamani wala Soko.

Kama unabisha beba vyeti vyako uimgie Kenya kutafuta kazi!
Qualification sio vyeti ila vyeti vinaweza kuwa sehemu ya qualification. Basi tuseme leta personal profile yake kuhusu filamu na utalii.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Umejieleza, ingawa inaweza kuwa ngumu kueleweka kwa baadhi ya wasomaji. Umetumia uwasiliaji mgumu kidogo, hasa kwa wasomaji wako ambao hawapo kwenye hiyo fani yako.
Kwa mfano, unapochanganua hapa haya maeneo matatu: Kitaaluma, Kibiashara, Kisiasa...

Inakuwa vigumu kuelewa hasa ni maeneo yapi ya 'movie' hiyo yamelenga biashara, siasa au taaluma.

Lakini kiujumla, ninakubaliana nawe kwamba kilichofanyika hapa ni mwendelezo ule ule wa "kiujanja ujanja" unaotumiwa na serikali hii na hasa huyo kiongozi wake mkuu. Nadhani anaamini kwamba maneno matamu matamu na sauti nyororo ndio nyenzo muhimu zaidi kwake katika kuwahadaa watu, huku matendo yakiwa yanalenga manufaa binafsi zaidi kuliko manufaa ya nchi.

'Movie' hii ni sehemu ya Kampeni ya kujijenga kuelekea 2025. Hawa watu wanaookotezwa kama hawa akina Rostam na hao akina Greenberg, ni mpango ule ule wa kujijenga wao na huyo anayewapa ulaji wa 'free range'.

Tanzania itapigwa sana kupitia kwenye siasa hizi za janja janja za kuwalaza watu akili zinazotumika wakati huu. Hakuna tena kuburuzana na polisi, au vyombo vingine vya mabavu, kama kuulizwa uraia, lakini kuburuzwa kunabaki palepale kwa kutumia njia mbadala.
Mwenzako amejenga hoja ya msingi wewe unaleta blaa blaa za kitoto hapa.
 
Ni kweli mhusika anajulikana kwenye ulingo wa filamu, lakini tujiulize lengo kuu la filamu ni nini? Lengo halikuwakutengeneza pesa kupitia hiyo filamu, bali kutangaza biashara ya utalii Tanzania. Itakuwa ajabu tangazo la biashara kulipiwa kuliona. Naunga mkono kama hii ingewahusiaha National Geographic ingepata coverage kubwa, sasa hivi itaoozea Amazon. Juu ya yote filamu iliyotengenezwa na pesa ya mlipa kodi inatumika kumtajrisha SSH, Greenberg, na Amazon.
Acha utoto,Rais kaongea mara nyingi na hata msemaji wa Serikali aneongea mara nyingi tuu kwamba pesa ni waliwachangisha wadau wa Utalii na ndio hasa walikuja na wazo..

Na kasema bil.11 zilipatikana ila wameshatumia bil.7

Sasa upotoshaji mwingine unamsukumo wa chuki binafsi kutoka kwenye kundi la wapuuzi wa Sukuma gang na Umoja Party yao.
 
Wabongo hata leo NEWTON AKIFUFUKA watabishana naye kwenye zile laws of motion au Archmedes na the law of floatation yake...

Sisi ndio sisi hata ile S400 ya Russia tunaweza kusema Mrusi fala tu ile teknolojia amejifunzia pale matimila Songea...
Ukiwasikiliza hao watu hakuna kitu utafanya..

Samia anawafahamu vizuri ndio maana huwa hawapi attention 👇

2935085_FB_IMG_16307140795615105 (1).jpg
 
Mkuu hapo tumeliwa kekundu. Hili wazo Mama alipewa na PK alipoenda kupiga nae picha kwenye kiwanda cha VW pale Kigali.
Yeye akakariri badala ya kuelewa kilichopo sasa tunapuyanga na kumpuyangisha HoS wetu huko.

PGg ni mpigaji na mfanyabiashara na si mtangaza utalii. Halafu wasaidizi sijui hawasaidii, ni kama RT inamtangaza SSH badala ya utalii wa TZ na vivutio vyake. Ni kama vile anatafuta appeal sijui akigombea kura atapigiwa na NY, LA ect ect USA badala ya TZ.

Ukiwaambia ukweli wanakasirika wanaona unapinga, this project is a big time failure. It adds little to No vale.
Chuki binafsi 😂😂😂😂😂..

Tueleze na wewe ulichofanya cha maana kwenye Nchi
 
Samia hana budi kujifunza yale yaliyomtokea Zuma kula Afrika Kusini na uhusiano wake na wafanyabiashara wa kihindi wakina GUPTA!! Asije akajikuta kupitia huo uhusiano wake na so called PRIVARE sector akajichanganya na kukuta the STATE IS CAPTURED!!!
Watanzania hawajali kuhusu hili, ila wanajali maisha yao binafsi na familia zao tu.

Kikwete alikuwa muhanga wa STATE CAPTURE through HOME SHOPPING CENTRE lakini bahati yake kuwa wakati ule watu walikuwa hawana muamko na katiba haikuruhusu apelekwe mahakamani kwa ufisadi alioufanya!!! Hivyo Samia must be very careful where she treads with her solicitation of the private
Katiba haijawahi kuruhusu hilo na haitakaa iruhusu hilo maana wenye-nchi yao hawapo tayari kwa hilo.
 
Kumbukeni pia kuwa huyu mfanyabiashara Rostam Azizi ndiye aliyekuwa architect wa wizi wa fedha kule BOT enzi ya marehemu Mkapa na gavana Balali!!!
Huyu mburushi mwanzoni mwa kipindi cha JPM alibakia kimya kama hayupo japo baadae alirejea na kuzindua 'taifa gas' kwa mbwembwe.

Huyo jamaa amejua sana kucheza na siasa za hii nchi.
 
Hakuwepo U.S , alituma watoto wake.
Ebu acha upumbavu hii ni JF, jukwaa la watu wenye akili kubwa tofauti, usifikiri upo Fb kwa wendawazimu wenzako. Kwenye uzinduzi wa Royal Tour film ya Rwanda Kagame alikuwepo kama kawaida. Tatizo wengi wenu mmekuwa mkishikiwa akili na wanasiasa koko waliofilisika kiakili na kimawazo. Matokeo yake ndo mnakuja kuumbuka kama hivi.

images (64).jpeg

39876622880_75ab92ae28_b.jpg
 
Watanzania hawajali kuhusu hili, ila wanajali maisha yao binafsi na familia zao tu.

Katiba haijawahi kuruhusu hilo na haitakaa iruhusu hilo maana wenye-nchi yao hawapo tayari kwa hilo.

Huko nyuma katiba haikuruhusu lakini kumbuka katiba sio msahafu huweza kubadirika kadiri nchi inavyobadirika!!! Na yatu hivyo hivyo , generation ya kupigania uhuru sio generation ya leo; things change!!
 
Hata ukiwawekea ushahidi ni kazi bure kwa sababu wameamua kupinga na kukosoa tu.
Mkuu hao ni problem make up gang sio problem solvers.
Wao hata siku moja hawajengi kazi yao ni kukosoa tu.
 
Huyu mburushi mwanzoni mwa kipindi cha JPM alibakia kimya kama hayupo japo baadae alirejea na kuzindua 'taifa gas' kwa mbwembwe.

Huyo jamaa amejua sana kucheza na siasa za hii nchi.

Na hivi sasa kwa kupita kwa Kikwete watamchezea sana huyu mama ; kwa kumdanganya kwamba wanamtafutia hela za kumuweka madarakani 2025 kumbe ndio wanaifirisi nchi!! Kuna muhimu kwa Wananchi wenyewe kuwa macho hasa kupigania kupata katiba mpya kwa udi na uvumba ingawa hawa wezi watapigana pia huo muarobaini wao usipatikane!!! Inshallah mwenyezi Mungu anaweza ingilia kati akaliponya hili Taifa toka kwa makucha ya hawa mafisadi!!
 
Huko nyuma katiba haikuruhusu lakini kumbuka katiba sio msahafu huweza kubadirika kadiri nchi inavyobadirika!!! Na yatu hivyo hivyo , generation ya kupigania uhuru sio generation ya leo; things change!!
Ni kweli mkuu, ila kwa Ccm hii...hata kama itabadilika, ujue utaletewa ile iliyopitishwa na bunge la katiba chini ya Mzee Sitta (RIP).
 
Sio rahisi tena kama unavyodhania damu inaweza mwagika watu wamechoka! Utaona hata kwenye huu uchaguzi wao ccm hakutakuwa salama!!
 
Wazo lilikuwa zuri, lakini mleta wazo katuzidi ujanja.

Unapotengeneza filamu ambayo ni andishi la kitaaluma na kibiashara,tulipaswa kutanguliza taaluma zaidi kuliko siasa.

Mwanasiasa anaweza kukumbwa na kashfa au dosari za kiuongozi na kupelekea kupoteza soko kusudiwa baada ya kususiwa kote ilikotangawzwa na kuvuma. Huo ndio utamaduni wa wazungu.

Tulipaswa pia kuzilenga taasisi kubwa zilizobobea katika taaluma hiyo Duniani kama vile National Geographic au Animal Planet ambazo tayari zinajiendesha kupitia Vituo vyao binafsi vya kurushia Documentary zao Dunia nzima. Na zinaangaliwa na mamilioni ya watu Duniani kila siku.

Huyu Peter Greenbag hana Impact kubwa Duniani kama ambavyo ametuingiza mkenge kumdhania. Unaweza kutafakari hilo kwa kujiuliza aina ya watu ambao wamehudhuria uzinduzi wake huko Marekani.

Pia jiulizeni kwamba,inakuwaje utengeneze filamu ya kukutangangaza kibiashara,halafu unaiingiza Sokoni Amazon kuiuza.

Badala ya wewe Mtangazaji wa biashara yako ndio uwalipe wao ili wakutangaze.eti wewe ndio unaliuza tangazo lako kwa wateja.

Lengo likiwa kujulikana zaidi na hivyo kuvutia wateja kuja kuyaona yale uliyoyatangaza kupitia filamu yako.

Unapoanza kwa kuiuza bila kujua kama ita hit kwenye mauzo au la! Hii inaleta maswali mengi kuliko majibu.

Pia ingekuwa vema Rais angeambatana na wataalamu wa fani ya utalii pamoja na wabobezi wa African Wildlife Management.
Ambao tungewaona bega kwa bega na Rais wetu,wakimsaidia kujibu maswali na kukidhi kiu ya waulizaji. Kwa kujikita zaidi kitaaluma na kitakwimu sahihi. Hususan kwenye hafla za uzinduzi.

Ambapo majibu yao ya kitaaluma yangeongeza chachu ya watu kuitamani zaidi filamu ili wajionee uzuri wa Tanzania.

Tofauti na kilichofanyika kwa kwenda kumpambanisha Rais wetu,ambaye kitaaluma sio fani yake.

Hapo tayari umemchezesha Bahati Nasibu rais na watanzania bila kujua wala kupenda.

Hapo ni wazi kwamba waandaaji wameutumia muda wa Rais kwa manufaa yao zaidi.

Boston ndio mji ambao ni kitovu cha utalii na taasisi za utalii na wadau wake nchini Marekani.hasa kuhusu utalii wa nje ya Marekani kama Afrika na kwingineko.
Kuliko New York au Los Angeles

Hivyo ingekuwa vema uzinduzi ule ukafanywa katika mji huo,kuliko kwenye jiji la New York ambalo halina sifa ya utalii zaidi ya kujaa watoto wa mjini.

Kwa nini hata hawakupata wazo la kuingia mkataba na mmojawapo wa wasanii maarufu nchini Marekani,ili waweze kurekodi pamoja na Rais wetu ili kuiongezea chachu na umaarufu kimataifa?

Rais Samia ni Maarufu Tanzania ndiyo.
Lakini hajawa maarufu kimataifa kwa kiwango cha kuwashawishi watu kumiminika kuinunua filamu yake kwa sasa.
Kama waandaaji na wapiga debe mnavyotaka kuiaminisha Dunia.

Will Smith ametengeneza filamu ndogo tu ya jinsi alivyotembelea Afrika na Tanzania ikiwemo na inaweza kuipiku kwa mbali sana hii ya kwetu.kulingana na jinsi inavyoshambuliwa huko Marekani kwa mauzo.

Tujaribu kidogo kumuangalia Kagame wa Rwanda jinsi anavyoitangaza nchi yake bila kuingiza sura yake hata kidogo na Rwanda inapaa kimataifa.

Madhara ya kumtumia Rais moja kwa moja,
Na kuihusisha serikali yake kwenye masuala ya matangazo hasa haya ya kitalii. Ni kwamba soko lake pia litategemea rekodi yake pamoja na serikali yake kiutawala.
Wazungu huwa wanapiga chini kila kitu pindi mhusika anapokumbwa na kashfa yoyote ile.

Nimalizie kwa kuitaka serikali isikie maombi ya watanzania kutaka watuweke wazi kuhusu gharama na umiliki wa filamu ya Tanzania Royal Tour.

Nimemaliza kuutumia uhuru wangu kikatiba.
View attachment 22003
S

Shida yako ni 1 tu

Ushamba!

Kwa taarifa yako Samia sio Rais wa 1 kufanya Royal Tour, wamefanya maraisi wengi sana kwa mtindo huo huo!

Acha ushamba na jaribu kufuatilia vitu ndo uje umwagike humu! Wabongo mjikite kuchambua mpira tu haya mambo mengine sio level yenu kwa uelewa wenu wa hapa na pale
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom