Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 35,826
- 47,146
Ccm wao kwa wao hupasuana sana tu, ila wakifika kwenye maslahi yao huwa wamoja.Utaona hata kwenye huu uchaguzi wao ccm hakutakuwa salama!!
Ccm wao kwa wao hupasuana sana tu, ila wakifika kwenye maslahi yao huwa wamoja.Utaona hata kwenye huu uchaguzi wao ccm hakutakuwa salama!!
You nailed it.Made my day and I humbly rest my case.S
Shida yako ni 1 tu
Ushamba!
Kwa taarifa yako Samia sio Rais wa 1 kufanya Royal Tour, wamefanya maraisi wengi sana kwa mtindo huo huo!
Acha ushamba na jaribu kufuatilia vitu ndo uje umwagike humu! Wabongo mjikite kuchambua mpira tu haya mambo mengine sio level yenu kwa uelewa wenu wa hapa na pale
Imani potofu japokuwa unaeleweka kwani Samia na JK wanao ukaribu wenye kutajirishana kupitia siasa.Chawa watakuja kusema kuwa humpendi Samia!!! Lazima mjifunze kufanya utafiti kabla ya kukurupuka na kufanya mambo ya kujitafutia umaarufu!! Hapo kuna watu wamepiga hela yao safi na kuipitisha kwenye foundation ya Mjomba wa Msoga!!! Ndio maana nae alitangulia kwenda kwenye uzinduzi ingawa walimficha kwenye picha zao!
Hakuna imani potofu hapo kutajirishana at the expense ya wananchi is nothing but UFISADI!! You are entitled to your beliefs though!!Imani potofu japokuwa unaeleweka kwani Samia na JK wanao ukaribu wenye kutajirishana kupitia siasa.
Time will tell!Ccm wao kwa wao hupasuana sana tu, ila wakifika kwenye maslahi yao huwa wamoja.
Viongozi wengi waliowika awamu ya 4 ndio wenye nguvu huko Ccm na nyadhifa nzuri serikalini, hivyo wamekamata mpini na wengine wameshika makali.Time will tell!
Duniani kazi nyepesi ni kukosoa na njia ya kufanikiwa ni kujaribu kwa kila nafasi inayopatikana mbele yetu.Wazo lilikuwa zuri, lakini mleta wazo katuzidi ujanja.
Unapotengeneza filamu ambayo ni andishi la kitaaluma na kibiashara,tulipaswa kutanguliza taaluma zaidi kuliko siasa.
Mwanasiasa anaweza kukumbwa na kashfa au dosari za kiuongozi na kupelekea kupoteza soko kusudiwa baada ya kususiwa kote ilikotangawzwa na kuvuma. Huo ndio utamaduni wa wazungu.
Tulipaswa pia kuzilenga taasisi kubwa zilizobobea katika taaluma hiyo Duniani kama vile National Geographic au Animal Planet ambazo tayari zinajiendesha kupitia Vituo vyao binafsi vya kurushia Documentary zao Dunia nzima. Na zinaangaliwa na mamilioni ya watu Duniani kila siku.
Huyu Peter Greenbag hana Impact kubwa Duniani kama ambavyo ametuingiza mkenge kumdhania. Unaweza kutafakari hilo kwa kujiuliza aina ya watu ambao wamehudhuria uzinduzi wake huko Marekani.
Pia jiulizeni kwamba,inakuwaje utengeneze filamu ya kukutangangaza kibiashara,halafu unaiingiza Sokoni Amazon kuiuza.
Badala ya wewe Mtangazaji wa biashara yako ndio uwalipe wao ili wakutangaze.eti wewe ndio unaliuza tangazo lako kwa wateja.
Lengo likiwa kujulikana zaidi na hivyo kuvutia wateja kuja kuyaona yale uliyoyatangaza kupitia filamu yako.
Unapoanza kwa kuiuza bila kujua kama ita hit kwenye mauzo au la! Hii inaleta maswali mengi kuliko majibu.
Pia ingekuwa vema Rais angeambatana na wataalamu wa fani ya utalii pamoja na wabobezi wa African Wildlife Management.
Ambao tungewaona bega kwa bega na Rais wetu,wakimsaidia kujibu maswali na kukidhi kiu ya waulizaji. Kwa kujikita zaidi kitaaluma na kitakwimu sahihi. Hususan kwenye hafla za uzinduzi.
Ambapo majibu yao ya kitaaluma yangeongeza chachu ya watu kuitamani zaidi filamu ili wajionee uzuri wa Tanzania.
Tofauti na kilichofanyika kwa kwenda kumpambanisha Rais wetu,ambaye kitaaluma sio fani yake.
Hapo tayari umemchezesha Bahati Nasibu rais na watanzania bila kujua wala kupenda.
Hapo ni wazi kwamba waandaaji wameutumia muda wa Rais kwa manufaa yao zaidi.
Boston ndio mji ambao ni kitovu cha utalii na taasisi za utalii na wadau wake nchini Marekani.hasa kuhusu utalii wa nje ya Marekani kama Afrika na kwingineko.
Kuliko New York au Los Angeles
Hivyo ingekuwa vema uzinduzi ule ukafanywa katika mji huo,kuliko kwenye jiji la New York ambalo halina sifa ya utalii zaidi ya kujaa watoto wa mjini.
Kwa nini hata hawakupata wazo la kuingia mkataba na mmojawapo wa wasanii maarufu nchini Marekani,ili waweze kurekodi pamoja na Rais wetu ili kuiongezea chachu na umaarufu kimataifa?
Rais Samia ni Maarufu Tanzania ndiyo.
Lakini hajawa maarufu kimataifa kwa kiwango cha kuwashawishi watu kumiminika kuinunua filamu yake kwa sasa.
Kama waandaaji na wapiga debe mnavyotaka kuiaminisha Dunia.
Will Smith ametengeneza filamu ndogo tu ya jinsi alivyotembelea Afrika na Tanzania ikiwemo na inaweza kuipiku kwa mbali sana hii ya kwetu.kulingana na jinsi inavyoshambuliwa huko Marekani kwa mauzo.
Tujaribu kidogo kumuangalia Kagame wa Rwanda jinsi anavyoitangaza nchi yake bila kuingiza sura yake hata kidogo na Rwanda inapaa kimataifa.
Madhara ya kumtumia Rais moja kwa moja,
Na kuihusisha serikali yake kwenye masuala ya matangazo hasa haya ya kitalii. Ni kwamba soko lake pia litategemea rekodi yake pamoja na serikali yake kiutawala.
Wazungu huwa wanapiga chini kila kitu pindi mhusika anapokumbwa na kashfa yoyote ile.
Nimalizie kwa kuitaka serikali isikie maombi ya watanzania kutaka watuweke wazi kuhusu gharama na umiliki wa filamu ya Tanzania Royal Tour.
Nimemaliza kuutumia uhuru wangu kikatiba.
View attachment 2200347
Viongozi wengi waliowika awamu ya 4 ndio wenye nguvu huko Ccm na nyadhifa nzuri serikalini, hivyo wamekamata mpini na wengine wameshika makali.
Sukuma gang hawana nguvu tena mkuu, wapo kimya tu huenda wamekubali wameshapoteza.Sukuma Gang nao wapo wanaangalia mchezo; hawa na wakwere wa Msoga hawawezi kula sahani moja lazima watamwagiana kitoweo!!
Masuala haya niliyouliza hayahusiani wala hayahitaji qualification ya film industry.Qualification sio vyeti ila vyeti vinaweza kuwa sehemu ya qualification. Basi tuseme leta personal profile yake kuhusu filamu na utalii.
Sukuma gang hawana nguvu tena mkuu, wapo kimya tu huenda wamekubali wameshapoteza.
Ila hao 'watoto wa mjini' ndio muda wao huu.
Kibiashara nikiwa na maana kuvutia soko la biashara ya utalii wa Tanzania kimataifa.Mwenzako amejenga hoja ya msingi wewe unaleta blaa blaa za kitoto hapa.
Leta link ya hayo majibu yako.Acha utoto,Rais kaongea mara nyingi na hata msemaji wa Serikali aneongea mara nyingi tuu kwamba pesa ni waliwachangisha wadau wa Utalii na ndio hasa walikuja na wazo..
Na kasema bil.11 zilipatikana ila wameshatumia bil.7
Sasa upotoshaji mwingine unamsukumo wa chuki binafsi kutoka kwenye kundi la wapuuzi wa Sukuma gang na Umoja Party yao.
Hao wananchi wanafaidika mpaka sisi tudhani kwamba wanakuwa wakitumiwa. Samia anafanya analoweza kwa uwezo wake. Kumpinga au kumuunga mkono ni uhuru binafsi wa kila mmoja wetu.Hakuna imani potofu hapo kutajirishana at the expense ya wananchi is nothing but UFISADI!! You are entitled to your beliefs though!!
Acheni uo wizi nyie sukuma gang. Kwa Nini hamkubali Kama Simba wa yuda alikufa?
Ukiwa salama nitakukong'ota makwenzi....hata kwenye huu uchaguzi wao ccm hakutakuwa salama!!
Hoja zako zipo wapi sasa!Mwenzako amejenga hoja ya msingi wewe unaleta blaa blaa za kitoto hapa.
Ndio maana marais wengine kama jirani yetu mmoja hakaribishi maoni maana utayumbishwa tu kila mtu na mtazamo wake jambo lenyewe moja tuHuyo muongozaji ni mshindi wa tuzo za filamu, siyo mtu mdogo kwenye tasnia, huwezi rusha filamu BBC, CNN, Fox news...