Ng'wanamangilingili
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 5,787
- 4,875
Huyo muongozaji ni mshindi wa tuzo za filamu, siyo mtu mdogo kwenye tasnia, huwezi rusha filamu BBC, CNN, Fox news...
You are less or not informed about Peter Greenberg
Huyo muongozaji ni mshindi wa tuzo za filamu, siyo mtu mdogo kwenye tasnia, huwezi rusha filamu BBC, CNN, Fox news...
'Movie' hii ni sehemu ya Kampeni ya kujijenga kuelekea 2025. Hawa watu wanaookotezwa kama hawa akina Rostam na hao akina Greenberg, ni mpango ule ule wa kujijenga wao na huyo anayewapa ulaji wa 'free range'.
Siku ya uzinduzi filam ilipata more than 3m viewers world wide.
Tuache ramli tusubiri matokeo.
At least, Mama Samia kajaribu kufanya kitu.
Kwa taarifa yako tu Wazungu wengi walijua Mlima Kilimanjaro uko Kenya hapo nyuma, Walijua Tanzanite inatoka Kenya na India n.k
Sasa tusipoitangaza Nchi tutaendelea kupigwa.
Raisi kaanza kwa kadri aliweza. Badae wataboresha zaidi. Sio Jambo la kubeza hata kidogo. Labda una lako Jambo.
Tatizo ni kwamba Sterling ni yule yule amerudi tena.Nakubaliana na wewe kuhusu observation hii; otherwise utaelezaje kuwepo wa Rostam Aziz huko Marekani wakati wa uzinduzi wa hii documentary ? Sio hivyo tu huyu Rostam Aziz ameonekana akitia saini makubaliano akiwepo Samia na balozi wetu wa huko Marekani sijui ni mikataba yake na biashara zake au ni mikataba ya nchi ya Tanzania? Kama ni mikataba ya nchi kwanini atie saini mfanya biashara na sio mawaziri wahusika na kama ni mikataba yake binafsi je kuwepo wa Rais kwenye utiaji saini huo unaashiria kuwekewa dramana na Serikali ya Tanzania kwenye hiyo mikataba? Hiyo gurantee inaweza kuwa na athari gani kwa nchi?
Samia hana budi kujifunza yale yaliyomtokea Zuma kula Afrika Kusini na uhusiano wake na wafanyabiashara wa kihindi wakina GUPTA!! Asije akajikuta kupitia huo uhusiano wake na so called PRIVARE sector akajichanganya na kukuta the STATE IS CAPTURED!!! Kikwete alikuwa muhanga wa STATE CAPTURE through HOME SHOPPING CENTRE lakini bahati yake kuwa wakati ule watu walikuwa hawana muamko na katiba haikuruhusu apelekwe mahakamani kwa ufisadi alioufanya!!! Hivyo Samia must be very careful where she treads with her solicitation of the private sector with Kikwete's counsel!
Kumbukeni pia kuwa huyu mfanyabiashara Rostam Azizi ndiye aliyekuwa architect wa wizi wa fedha kule BOT enzi ya marehemu Mkapa na gavana Balali!!!
Sidhani kama amefungua link kwenye post#33.Rejea post #33 na majibu yaliwekwa kutokana na maswali uliyouliza kutokana na post yako #1
Hivi mleta mada ushawahi kuiangalia Royal Tour film ya Rwanda? Je Kagame hakuwepo kwenye filamu? Tatizo lenu dada zetu wa siku hizi kila kitu mnakichukua kimipasho mipasho ilimradi na nyie muonekane kuwa mnajua kusuta.
Unaweza kukuta mleta mada ni raia wa nchi nyingine hivyo maendeleo yoyote kwa Tanzania ni sawa na msumali wa moto katikati ya makalio yake. Shem on you poor girl. JF imeingiliwa na mabinti wa mipasho na wanaharakati koko.
Maswali yako yote ni ya kipuuzi ndo maana wengi hatuoni sababu ya kuujibu upuuzi.Mimi ni Mtanzania njoo na majibu sahihi kwa maswali husika badala ya Porojo.
Unahamisha magoli.Rostam Aziz hahusiki lolote na Royal Tour Tanzania.Tatizo ni kwamba Sterling ni yule yule amerudi tena.
Kwa hiyo huyo Rostam huu ni msimu mpya wa mavuno.
Sasa hapa kati ya mleta mada na wewe ni nani mwajuma ndala ndefu kama sio wewe!!! Mtoto wakiume unachamba kuliko ata mange kimambiHivi mleta mada ushawahi kuiangalia Royal Tour film ya Rwanda? Je Kagame hakuwepo kwenye filamu? Tatizo lenu dada zetu wa siku hizi kila kitu mnakichukua kimipasho mipasho ilimradi na nyie muonekane kuwa mnajua kusuta.
Unaweza kukuta mleta mada ni raia wa nchi nyingine hivyo maendeleo yoyote kwa Tanzania ni sawa na msumali wa moto katikati ya makalio yake. Shem on you poor girl. JF imeingiliwa na mabinti wa mipasho na wanaharakati koko.
Sikuangalia uzinduzi,haihitaji mtu maarufu kuja kwenye uzinduzi,nasikia umepata views 3m...hayo ni mafanikio makubwa
Mkuu vema umeongea kitaaluma zaidi kuliko hawa wanaodhani kila jambo ni siasa tu.Viewers millioni 3 ndio Namba ya watalii wa Kuja kutembelea?
Unajua maana ya filamu na uhalisia? Hilo ni tangazo la biashara ama ni mkanda wa video?
Kwa ivo target ni viewers ama watalii kuja bongo? Au tunapata pesa per view?
What was the primary objective ya Royal Tour? Jina lenyewe haliaksi uhalisia.
PK had his mission kujisfisha kwa wazungu. Ukiingia NatioG, Animal Planet, Travel Channel, CGTN ect kuna coverage super sana za utalii wa Tanzania na ni huko hawa wanako relay. We had to boost a marketing stratagies na si advertisements.
Nina mengi ila hadi hapo najua utareply utumbo kwa sababu hutaki kupokea positive criticism.
Kidumu CC emu
Pamoja na mawazo yako mazuri ila kusema tumeingizwa mkenge hapana..Wazo lilikuwa zuri, lakini mleta wazo katuzidi ujanja.
Unapotengeneza filamu ambayo ni andishi la kitaaluma na kibiashara,tulipaswa kutanguliza taaluma zaidi kuliko siasa.
Mwanasiasa anaweza kukumbwa na kashfa au dosari za kiuongozi na kupelekea kupoteza soko kusudiwa baada ya kususiwa kote ilikotangawzwa na kuvuma. Huo ndio utamaduni wa wazungu.
Tulipaswa pia kuzilenga taasisi kubwa zilizobobea katika taaluma hiyo Duniani kama vile National Geographic au Animal Planet ambazo tayari zinajiendesha kupitia Vituo vyao binafsi vya kurushia Documentary zao Dunia nzima. Na zinaangaliwa na mamilioni ya watu Duniani kila siku.
Huyu Peter Greenbag hana Impact kubwa Duniani kama ambavyo ametuingiza mkenge kumdhania. Unaweza kutafakari hilo kwa kujiuliza aina ya watu ambao wamehudhuria uzinduzi wake huko Marekani.
Pia jiulizeni kwamba,inakuwaje utengeneze filamu ya kukutangangaza kibiashara,halafu unaiingiza Sokoni Amazon kuiuza.
Badala ya wewe Mtangazaji wa biashara yako ndio uwalipe wao ili wakutangaze.eti wewe ndio unaliuza tangazo lako kwa wateja.
Lengo likiwa kujulikana zaidi na hivyo kuvutia wateja kuja kuyaona yale uliyoyatangaza kupitia filamu yako.
Unapoanza kwa kuiuza bila kujua kama ita hit kwenye mauzo au la! Hii inaleta maswali mengi kuliko majibu.
Pia ingekuwa vema Rais angeambatana na wataalamu wa fani ya utalii pamoja na wabobezi wa African Wildlife Management.
Ambao tungewaona bega kwa bega na Rais wetu,wakimsaidia kujibu maswali na kukidhi kiu ya waulizaji. Kwa kujikita zaidi kitaaluma na kitakwimu sahihi. Hususan kwenye hafla za uzinduzi.
Ambapo majibu yao ya kitaaluma yangeongeza chachu ya watu kuitamani zaidi filamu ili wajionee uzuri wa Tanzania.
Tofauti na kilichofanyika kwa kwenda kumpambanisha Rais wetu,ambaye kitaaluma sio fani yake.
Hapo tayari umemchezesha Bahati Nasibu rais na watanzania bila kujua wala kupenda.
Hapo ni wazi kwamba waandaaji wameutumia muda wa Rais kwa manufaa yao zaidi.
Boston ndio mji ambao ni kitovu cha utalii na taasisi za utalii na wadau wake nchini Marekani.hasa kuhusu utalii wa nje ya Marekani kama Afrika na kwingineko.
Kuliko New York au Los Angeles
Hivyo ingekuwa vema uzinduzi ule ukafanywa katika mji huo,kuliko kwenye jiji la New York ambalo halina sifa ya utalii zaidi ya kujaa watoto wa mjini.
Kwa nini hata hawakupata wazo la kuingia mkataba na mmojawapo wa wasanii maarufu nchini Marekani,ili waweze kurekodi pamoja na Rais wetu ili kuiongezea chachu na umaarufu kimataifa?
Rais Samia ni Maarufu Tanzania ndiyo.
Lakini hajawa maarufu kimataifa kwa kiwango cha kuwashawishi watu kumiminika kuinunua filamu yake kwa sasa.
Kama waandaaji na wapiga debe mnavyotaka kuiaminisha Dunia.
Will Smith ametengeneza filamu ndogo tu ya jinsi alivyotembelea Afrika na Tanzania ikiwemo na inaweza kuipiku kwa mbali sana hii ya kwetu.kulingana na jinsi inavyoshambuliwa huko Marekani kwa mauzo.
Tujaribu kidogo kumuangalia Kagame wa Rwanda jinsi anavyoitangaza nchi yake bila kuingiza sura yake hata kidogo na Rwanda inapaa kimataifa.
Madhara ya kumtumia Rais moja kwa moja,
Na kuihusisha serikali yake kwenye masuala ya matangazo hasa haya ya kitalii. Ni kwamba soko lake pia litategemea rekodi yake pamoja na serikali yake kiutawala.
Wazungu huwa wanapiga chini kila kitu pindi mhusika anapokumbwa na kashfa yoyote ile.
Nimalizie kwa kuitaka serikali isikie maombi ya watanzania kutaka watuweke wazi kuhusu gharama na umiliki wa filamu ya Tanzania Royal Tour.
Nimemaliza kuutumia uhuru wangu kikatiba.
View attachment 2200347
Watoto wa kike kuteteana ni kawaida yenu. Kwahiyo sishangai kwa hili andiko lako hapa jukwaani.Sasa hapa kati ya mleta mada na wewe ni nani mwajuma ndala ndefu kama sio wewe!!! Mtoto wakiume unachamba kuliko ata mange kimambi
Neno moja: TUSUBIRI MATOKEOSiku ya uzinduzi filam ilipata more than 3m viewers world wide.
Tuache ramli tusubiri matokeo.
At least, Mama Samia kajaribu kufanya kitu.
Kwa taarifa yako tu Wazungu wengi walijua Mlima Kilimanjaro uko Kenya hapo nyuma, Walijua Tanzanite inatoka Kenya na India n.k
Sasa tusipoitangaza Nchi tutaendelea kupigwa.
Raisi kaanza kwa kadri aliweza. Badae wataboresha zaidi. Sio Jambo la kubeza hata kidogo. Labda una lako Jambo.