Royal Tour: Serikali itoe mchanganuo wa gharama

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,095
103,340
Nimefuatilia kwa mamlaka zote wanipe mchanganuo wa wa gharama za Royal Tour sijafanikiwa?

Naambiwa uko ngazi za juu. Nafikiri hili jambo lifanyike kwa uwazi na uwajibikaji isije kuwa kichaka cha kupiga kodi za wananchi.

Rais asituambie tu anafanya tour, atuambie bajeti ya tour ni pesa ngapi anategemea mapato/impacts ya kiasi gani kutokana na tour yake.

Kingine ni bunge lipi limepitisha matumizi ya hii tour, maana wakati wa bunge hatukusikia, tunakuja kusikia tu kama jambo la dharura? Tour ni dharura?

Walipa kodi tunahitaji kujua
 
Tozo za wanyonge zinavuja!😁😁😁
TVJd-1.jpg
 
Nimefuatilia kwa mamlaka zote wanipe mchanganuo wa wa gharama za Royal Tour sijafanikiwa?

Naambiwa uko ngazi za juu. Nafikiri hili jambo lifanyike kwa uwazi na uwajibikaji isije kuwa kichaka cha kupiga kodi za wananchi. Rais asituambie tu anafanya tour, atuambie bajeti ya tour ni pesa ngapi anategemea mapato/impacts ya kiasi gani kutokana na tour yake.

Kingine ni bunge lipi limepitisha matumizi ya hii tour, maana wakati wa bunge hatukusikia, tunakuja kusikia tu kama jambo la dharura? Tour ni dharura?

Walipa kodi tunahitaji kujua
Wafuasi wa Upinzani Ndo mana kila siku mnazidi kudharaulika.

Nimegundua wengi hamfuatilii mambo ya nchi yenu ila ndo wa kwanza kuja kulalamika mitandaoni.

Jibu la Maswali uliyouliza hapa ni kuwa siku Rais ametangaza kufanyika kwa hii program takribani miezi 3 au 4 iliyopita alisema wazi kuwa program hii haitatumia fedha za Serikali bali michango kutoka sekta binafsi.

Unavyosema Leo kuwa Bunge halikuwai kupitisha fedha za program hii unaonesha ni kwa jinsi gani sio tu hufuatilii mambo ya nchi yako bali wewe ni kilaza ulietukuka
 
Fedha za Sekta binafsi ndizo zinaendesha mipango ya maendeleo kwa TZ, Je ni mikopo au ni misaada? Kama kutakuwa na mafanikio serikali itapata mapato zaidi, je hao sekta binafsi watafaidikaje, sababu wametoa pesa zao + wanaendelea kulipa kodi.
 
No! anayo hoja ya msingi, wachangiaji toka secta binafsi ni kina nani? Wako wangapi? Wametoa kiasi gani? Wananufaikaje?

Isijekuwa Raisi wetu anafadhiliwa na hela chafu ikapelekea kuweka mfukoni na hao sponsors?
 
Huyu Dogo anajifanya mjuaji hawezi kujibu hizo hoja zako
 
No! anayo hoja ya msingi, wachangiaji toka secta binafsi ni kina nani? Wako wangapi? Wametoa kiasi gani? Wananufaikaje?

Isijekuwa Raisi wetu anafadhiliwa na hela chafu ikapelekea kuweka mfukoni na hao sponsors?
Kuna sheria inamtaka Rais kutaja watu anaowaomba wachangie shughuli fulani na kiasi walichotoa?

Wapi imeandikwa mtu akitoa mchango lazima anufaike?

Kama hayo ndo yalikuwa maswali yake Kwa nini hakuyaweka? Nini kimemfanya aulize Kama Bunge lilipitisha hizo fedha?
 
Kwa kuwa hii covid imetufungia sana ndani, wacha tujiliwaze na hizi tour za ndani.....ukitulia sana kwenye kiti miguu inajaa maji.
 
nasikia hela zote zinatoka kwa wenye kipindi na yeye anakatiwa chake kama stering tu,yaani galama zote yakiwemo mafuta,gali tu ndio zitatika ikule kwa maana wameunganisha kwa wakati mmoja Raisi yumo kwenye ziara na semtaim anafanya igizo.
 
Back
Top Bottom