Router gani nzuri kwa matumizi ya ofisi yenye watu zaidi ya 500

zigi 01

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
295
155
Habari za mida,

Naomba kusaidiwa router gani ni nzuri kwa matumizi ya taasisi ambayo inakuwa na watumiaji 500 kwa mara Moja wakiwa connected kwa wired na wireless?

Na kipi natakiwa kukiangalia kwenye hiyo router ili kujua idadi ya users inayoweza kuchukua?

NB: Sina utaalamu sana na router Nina basic knowledge tu ya kuzifanyia configuration!!
 
Kwa hizi router zetu za "consumer" si rahisi.

Watu 500 unaweza hata ukaweka private network, mkawekewa na mnara wenu.

Labda ufanye mesh uweke Router nyingi na Ap tofauti tofauti ili ku split load router moja wasiconect watu wengi.
 
Hakuna router inayoweza kubeba device 500 kwa wakati mmoja, hizi za kawaida hata 30-50 ni shida kwa sababu ya wifi inavyofanya kazi na uwezo mdogo wa processing.

Kwa watu wengi inabidi ufunge network yenye access point nyingi na zote zinaonekana kama moja, hii itahitaji utaalamu kiasi fulani na pro equipment, angalia kampuni kama Ubiquiti na UDM + AP zao. Pia fikiria utahitaji bandwidth kiasi gani ili watu 500 watumie net.
 
Mikrotik rb3011....bei $300...
 
Hapo nitafanya vipi hesabu ya kujua bandwidth inayohitajika?
 
Kwa hizi router zetu za "consumer" si rahisi.

Watu 500 unaweza hata ukaweka private network, mkawekewa na mnara wenu.

Labda ufanye mesh uweke Router nyingi na Ap tofauti tofauti ili ku split load router moja wasiconect watu wengi.
Kwa wastani kama Nina Tp link router Moja naweza kuhudumia client wangapi kwa muda mmoja?
 
Ulisha soma course ya CISCO angalau ya CCNA?
Kama una fanya sana kazi za networking fanya mpango usome hii kitu.
Kwa sasa sababu ya muda outsource kazi au ikishindikana mtafute mtu mjuzi mpoze kwa pesa yako.
 
Kwa wastani kama Nina Tp link router Moja naweza kuhudumia client wangapi kwa muda mmoja?
Tp link zipo nyingi na kila moja ipo na uwezo tofauti tofauti, ila wifi za kawaida 2.4Ghz tunaongelea bandwidth around 300mbps na hupati yote hio ipo on theory tu.

Wenyewe TP link wanashauri router za kawaida watu 25 na router za pro watu 50. Soma zaidi hapa

Na hapo tunaongelea watu wa kawaida huyu katuma WhatsApp, huyu anacheza game, huyu yupo insta, youtube, Tiktok etc.

Kwa mazingira ya office ambayo watu wanafanya video call, kuna voip, na mambo mengine serious utahitaji capacity ya maana, kifupi mkuu watu 500 including wired unahitaji kuajiri proffesional, ama tafuta isp ambaye atafanya hio kazi kama Simbanet.
 
Hapo nitafanya vipi hesabu ya kujua bandwidth inayohitajika?
Kwa kukadiria unaweza kugawanya, connection yako gawanya kwa idadi ya device ambazo zitakuwa zinafanya kazi kwa wakati mmoja, hayo ni makadirio tu kumbuka sio kila device itakuwa inafanya kazi zinazofanana.
 
Kwa wastani kama Nina Tp link router Moja naweza kuhudumia client wangapi kwa muda mmoja?
20-30 labda na kwa shida, tatizo sio router tu bali wifi yenyewe inavyofanya kazi, device kwenye wifi hazitumi data kwa pamoja bali zinapokezana kwa zamu moja baada ya nyingine ili kuepuka mgongano wa mawasiliano, zinatumia CSMA/CA.

Katika mpangilio huu wa kuepuka mgongano kama device ikifikiri kuna mgongano inabidi isubiri muda fulani kabla ya kurusha data upya, unapozidi kuongeza idadi ya device migongano inazidi hadi mnajikuta kila mtu anasubiri kila wakati na ufanisi unakuwa mdogo sana, ufanisi ukishuka sana device inagive up kutuma data.

Ndo maana inabidi utumie AcessPoint nyingi kila moja itabeba idadi fulani ya watu na ni channel independent zisizogongana pamoja ya kwamba watumiaji wataona jina moja la wifi.

Mbaya zaidi kama kuna watu 500 hata hao 20 hawatapata network kwa sababu wote 500 watajaribu kujiunga na kuua network kabisa.
 
Tp link zipo nyingi na kila moja ipo na uwezo tofauti tofauti, ila wifi za kawaida 2.4Ghz tunaongelea bandwidth around 300mbps na hupati yote hio ipo on theory tu.

Wenyewe TP link wanashauri router za kawaida watu 25 na router za pro watu 50. Soma zaidi hapa

Na hapo tunaongelea watu wa kawaida huyu katuma WhatsApp, huyu anacheza game, huyu yupo insta, youtube, Tiktok etc.

Kwa mazingira ya office ambayo watu wanafanya video call, kuna voip, na mambo mengine serious utahitaji capacity ya maana, kifupi mkuu watu 500 including wired unahitaji kuajiri proffesional, ama tafuta isp ambaye atafanya hio kazi kama Simbanet.
Well said. Hapo atufute ISP wakae mezani.
 
Habari za mida,

Naomba kusaidiwa router gani ni nzuri kwa matumizi ya taasisi ambayo inakuwa na watumiaji 500 kwa mara Moja wakiwa connected kwa wired na wireless?

Na kipi natakiwa kukiangalia kwenye hiyo router ili kujua idadi ya users inayoweza kuchukua?

NB: Sina utaalamu sana na router Nina basic knowledge tu ya kuzifanyia configuration!!
Kwa matumizi ya taasisi yenye watumiaji 500 wanaotumia mtandao kwa wired na wireless, ningependekeza router yenye nguvu na uwezo wa kusimamia idadi kubwa ya watumiaji kama hao. Router zenye uwezo wa kibiashara kama vile Cisco Catalyst series au Juniper MX series zinaweza kuwa chaguo nzuri. Pia, unaweza kutaka kuzingatia mifumo ya kusimamia mtandao kama vile Cisco Meraki au Ubiquiti UniFi, ambayo hutoa zana za usimamizi wa mtandao kwa urahisi. Kabla ya kufanya uamuzi, ni muhimu pia kuzingatia mahitaji maalum ya taasisi yako na bajeti yako.

#chatGPT
 
Kwa hizi router zetu za "consumer" si rahisi.

Watu 500 unaweza hata ukaweka private network, mkawekewa na mnara wenu.

Labda ufanye mesh uweke Router nyingi na Ap tofauti tofauti ili ku split load router moja wasiconect watu wengi.
Nje ya mada
1. Kama Adapter ya laptop imeungua baada ya umeme kuzidi. Kuna uwezekano wa laptop kuungua?
2. Kama imeungua kuna uwezekano wa laptop kutengenezwa na kupona?
3. Je, Hard disk inaweza kuwa nzima?
 
1. Uwezekano upo lakini kwa asilimia ndogo. Adapter kama imeungua,ina maana imekata umeme kuendelea kwenye laptop. Unless laptop yenyewe iwe na hitirafu kwenye board.
2. Kutenfeneza,inawezekana. Inategemea na tatizo lenyewe. Japo huku ni kibongobongo, ni nadra sana kupata repair ya uhakika.

3. Hard disk kama haijadondoka chini,kunyeshewa au kumwagiwa vimiminika,lazima iko poa
 
Back
Top Bottom