Rostam, Lowassa wafumwa kikaoni

Story ya thread hii si kamili. Nimelitafuta gazeti hilo na kuisoma story yote. Inavyoelekea makachero wa gazeti hilo walikuwa wanafuatilia ingia-toka ya ofisi hiyo ya EL hapo Alpha DryCleaners ambayo haiko mbali sana na ofisi za IPP, wachapishaji wa gazeti hilo la Taifa Letu.

Hizi ingia-toka za vigogo hawa ziliongezeka maradufu baada tu ya mpango wa tanesco kununua mitambo chakavu ya Dowans kukamwa na vikao hivyo vinaonekana ni crisis talks. Si kazi kubwa sana kuspeculate walikuwa wanaongea nini.

Mnadhani walikuwa wanaongea namna ya kuwapiga vita mafisadi?
 
Vyovyote vile kwa rangi yake na alivyo ni muhindi tu, awe mshiha au Mgoha wote ni wahindi, mbona unatetea mafisadi au umelipwa kwa kazi hiyo.

Upuuzi huo, huna hoja! una uhakika gani kuwa Rostam ni fisadi, mafisadi huwaoni mahakamani? unajuwa lakini maana ya ufisadi au unafata mkumbo tu.
 
Upuuzi huo, huna hoja! una uhakika gani kuwa Rostam ni fisadi, mafisadi huwaoni mahakamani? unajuwa lakini maana ya ufisadi au unafata mkumbo tu.

Dar es salaam na wewe acha upuuzi wako, na uache darasa lako hilo la kufundisha watu maana ya ufisadi!
 
Well,
Unajua mtuukisha umwa na nyoka kila ukiona mjusi lazima uruke maili mia!

Hawa watu walisha kaa vikao wakabaka uchumi wetu kupitia RICHMOND- DOWANS, KAGODA, n.k, Lazima mtu yeyote ukiwaona wamekaa kikao ujiulize leo watakuja na lipi!

Hawa wezi si wakuacha wakae wapange mipango yao ya kuzidi tuibia eti tunasingizia uhuru wa kukutana! Lazima tule nao sahani moja mguu kwa mguu mkono kwa mkono, tuwabane tena wajue tunafatilia nyendo zao zote na mipango yao ya kiwizi wizi ya kuhujumu uchumi wetu!

Yaani watanzania wote tuamke tule nao sahani moja kila wanako enda tunao mpaka wakose pa kutokea! Itakuwa ni ujinga eti tusiwafatilie ili hali tunajua ni wezi wetu! Tena inabidi tuwabane hata wakienda jificha offshore ka nzi ketu kawaanike ili wajue kwamba 'no longer at is'

Unajuwa kitu cha kushangaza ni kuwa, dhidi ya tuhuma zote mnazotowa kwa RA, hao wengine sijui, sijaona hata mmoja humu JF aliesema sasa nakwenda mahakamani kumfungulia mashtaka RA, mpaka nikatowa wazo humu, kwa mwenye nia na mwenye kuweza, atangaze JF apatiwe ushahidi au apatiwe ushauri wa vipi aanze kumfungulia kesi RA. Hivi maneno, kejeli, vijembe, matusi bila ya kutenda (action) inasaidia kweli? sidhani, kinacho washinda ni nini kufanya hivyo? au mnaogopa kuwa haya ni maneno tu na porojo za kijiweni na hamna ushahidi wa kosa lolote alilofanya na mkifanya action itawageukia?

RA kimyaaa, kapowa, anafanya vitu vyake taratibu na wala humsikii kusema sema hovyo, mie nasema siku zote, Mtikila alileta ngebe akaonyeshwa action ndogo tu, akaufyata.

Chuki na kero zenu zina agenda fulani, mimi naiita agenda ya siri. Lakini kwa ukweli ni kwamba, hamna hoja kabisa bali ni chuki binafsi za kibaguzi, ama kwa rangi yake au kwa dini yake au kwa fedha yake.
 
Kama ni kweli wamekutana, there is something bad they are planning agaisnt the people of Tanzania.Kikwete please be vigilant.

Rostam, Lowassa wafumwa kikaoni

  • Vyote vyafanyika ofisini kwa bw Edward Lowassa
  • Katibu Mkuu CCM, Makamba abainika alikuwepo
  • Vilifanyika Alhamisi wiki hii na vingine Jumatatu wiki hii kuanzia saa 4.00 asubuhi

Na Mwandishi Maalum,
Taifa Letu
April 3, 2009


Yule mfanyabiashara mwenye maadili yenye utata, Bw Rostam Aziz wiki hii amekuwa akifanya vikao kadhaa vya faragha na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Vikao hivyo ambavyo vinasadikiwa vinahusiana na sakata la kukwama kwa mara nyingine kwa jaribio la kutaka kuiuzia Tanesco mitambo chakavu ya Richmond, vimekuwa vilifanyika ofisini kwa Lowassa, Alpha Cleaners iliyoko eneo la viwanda Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba vikao hivyo vilimshirikisha pia Bw Yusuf Makamba.

Baadhi ya mashuhuda wameliambia gazeti hili kwamba vikao vya mikutano kati ya wakubwa hao vimeongezeka mno hasa kwa wiki hii ambapo baada ya gazeti hili kutonywa walipo vigogo hao lilivamia katika ofisi za Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na kumshuhudia Bwana Rostam Aziz akiingia sehemu hiyo ba gari la kifahari lenye namba za usajili T 347 AJL.

Uchunguzi wetu umebaini kwamba kikao cha kwanza baina ya Lowassa na Rostam kilifanyika Alhamisi wiki iliyopita lakini hapoakuwa na uhakika kama Bw Makamba alikuwepo.

Hata hivyo katika kikao ambacho kimefanyika juzi Jumatatu kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tano na dakika 45, makachero wa gazeti hili walimshuhudia Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akijumuika na Bw Rostam Aziz pamoja na Wziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa…………
 
Naona Rostam ni rafiki yako na inawezekana amekukatia kidogo!Pole.Lakini hata kama hatukwenda mahakamani, kelele zinasaidia kumnyima usingizi!
 
Hii timu ni ya hatari sana ,tusipoangalia 2110 SASA KAMA ANA WEZA kuendelea kupanga wakuu wa wilaya mkikosana umeula wa chuya hili linatakiwa kuangalia kwa macho ya ziada
 
Ingekuwa wamekutana saa 4:00 usiku hapo ningekuwa interested but asubuhi tena ndani ya ofisi!! jamani................

Ndiyo maana wamekutana saa 4:00 asubuhi ili watu kama mimi na wewe tusiwafikirie. Watanzania mpaka siku mafisadi watakapotunyonya macho ndiyo tutashtuka kwa sasa watapeta tu kwa vile bado tumelala..................!!!!!!!!!!!!!!
 
Upuuzi huo, huna hoja! una uhakika gani kuwa Rostam ni fisadi, mafisadi huwaoni mahakamani? unajuwa lakini maana ya ufisadi au unafata mkumbo tu.

Wewe Dar es Salaam tulishakujua siku nyingi na yawezekana kabisa wewe ni Rostam mwenyewe kama si houseboy wake. Watanzania si mabwege tena. Waziri mkuu alishasema kama Kagoda ya Rostam ikifikishwa mahakamani nchi hii itatikisika, kwa maana inawahusisha pia Mkapa na JK mwenyewe na CCM yote kwa ujumla na ndo maana Rostam hafikishwi mahakamani, elewa hilo. Huyu mtu (Rostam) ni fisadi la kupindukia tena jangili haswaaaaa.
 
HAOOOOOOO!wanajichanganya hoooooooo!VICHWA VINAWAUMAAAAA!WAMESHACHANGANIKIWAA
tuwazomeeeni,hahaha!
TUWACHEKENI,haoo!

SHIMO WAMETUCHIMBIA,wametumbukia wenyewe
 
Sioni hoja hapa, waache wakutane. Kwani wewe unapokutana na wenzako kijiweni ni lazima muwe mnapanga maovu? Kwani uhuru wa kukutana umeishaondolewa? Nimesoma hoja zote mlizoleta sebuleni sikuona la maana mnalopigia kelele zaidi tu ya hisia. Si afadhali wanakutana mchana kweupe, je wangekuwa wanakutana usiku si ndiyo ingekuwa balaa, mnasema lakini sijaona hoja kabisa.

Mzee DSM nakuunga mkono 100% kama kuna mtu mwenye ujasiri ajitokeze basi tumsaidie kumpeleka RA mahakamani kuliko kelele za chura zisizo mzuia tembo kunywa maji. Mimi siupendi kabisa UFISADI lakini napenda kuchukua hatua pale ninapoona ukweli upo. Leteni ukweli tushughulike.
 
Mzee Kibiongo,
Tuwe wakweli kukutana kwao na kukutana kijiweni kujadili Yanga na Al- Ahly NITOFAUTI SANA hoja ipo na makundi ni makubwa yanazidi siku hadi siku, Kuanguka kwa Lowassa na wenzake kuanzia Richmond hadi Dowans na wahusika wakuu ni hao wanaokutana na kuuza magazeti kila siku, hapa ipo hoja sana ya kujadili na kuleta amani katika nchi yetu,minayoelekea kwa watu wachache wanaoangalia masilahi binafsi badala ya masilahi ya Taifa.
 
Naona Rostam ni rafiki yako na inawezekana amekukatia kidogo!Pole.Lakini hata kama hatukwenda mahakamani, kelele zinasaidia kumnyima usingizi!

Mi investment aliyokuwa nayo Tanzania na nchi nyingi duniani inatosha kabisa kumnyima usingizi, na hizi za JF hata sijui kama ana time ya kuziona.
 
Mimi kuwa Rostam na Lowasa wamekutani sio jambo kubwa sana kwani tunahakika kuwa wanakutana na kuwasiliana mara nyingi sana ndani ya siku moja.

SWALI kubwa hapa ni kama kuna ukweli kuwa KATIBU mkuu wa CCM alikuwepo katika mkutano huo. Ieleweke kuwa Rostam na Lowasa siku zote tunawatuhumu tu, na serikali imekataa katakata kuwa fikisha mbele ya vyombo vya sheria, japokuwa tuhuma zao ziko wazi (Lowasa aliachia ngazi, kuna kagoda n.k).

CCM wamekuwa wakidai kama ni wizi na ufisadi umefanywa na mtu mmoja mmoja, sasa katika kikao hiki Makamba atakuwa amewakilisha CCM au amejiwakilisha yeye mwenyewe? Je, ni yale yale ya kujivua madaraka ya chama pale linapokuja swala la kuhujumu masilahi ya nchi.

Nadhani kama tukipata habari zaidi katika hili la kuwepo kwa MAKAMBA basi litaendelea kutoa mwanga zaidi kuwajua kama "ccm inahusika katika upotevu wa mali ya umma na pia itaongeza nguvu kwenye mjadala mzito unaoendelea kuwa serikali inaongozwa kwa remote na kundi la mafisadi walioko nje ya serikali".

Tujadili hili pia.
 
hao watatu wote maadili yao yana utata.kwa kifupi hiyo ni club ya mafisadi!historia ya makamba toka huko nyuma wakati wa TANU ni ya ovyo.kuna wakati mwl JKN alitaka kumfukuza uanachama akatetewa na marehemu sokoine.mzee Galus Obeid wa mwl Nyerere foundation anamfahamu vizuri bw yusuf.hao wawili hawahitaji mjadala.ipo siku watapigwa mawe na wadanganyika!
 
Mi investment aliyokuwa nayo Tanzania na nchi nyingi duniani inatosha kabisa kumnyima usingizi, na hizi za JF hata sijui kama ana time ya kuziona.

Hana time ya kuziona!!! Unataka kumzuga nani hapa jamvini!!!? Kila wakati uko hapa kufuatilia mijadala yote kuhusu ufisadi wako. Ujue tunakumulika na upumbavu wako uliofanya dhidi ya nchi yetu hautavumilika tena. Fisadi mkubwa wee!!!
 
wangekuwa wamekutana watu waadilifu katka jamii isingekuwa habari sana. labda katka mazingira fulani fulani.

lakin RA na EL hatuwachukulii hivyo hapa tz. tunawachukulia kama watu wenye nia na mipango mikubwa ya kuhujumu harakati zetu za kujiletea maendeleo. tunatafuta na kupata hela lakin wanatumia uhuni uhuni kuzichota. halafu mwishoni hela za kununulia vitabu mashuleni zinakuwa hamna. hospitali zinakuwa chache zikiwa na madawa kidogo. barabara zinakosa hela za kujengea etc.

mbaya ni kuwa wana access na kumiliki vyombo vya habari lakin wameshindwa kabisa kuvitumia kujitetea kwa tuhuma za ufisadi dhidi yao. wana waandishi wa habari wenye uwezo mkubwa na wanaoweza kuwasikiliza na kuandika vile watakavo lakin hawajaweza kuwatumia kuielewesha jamii ya watz kuwa wao hawahusiki na ufisadi

so? tuhuma dhidi yao sticks

na wakikutana tunaowatuhumu kuwa wezi wetu inakuwaje? easy. wanapanga 'dili' zingine

na mtaani kwetu vibaka wakikaa pamoja wanaongea tunafikiria hivyohivyo. tutaanzia wapi kufikiria kuwa wanapanga kuokoka?
 
Jamani naomba kujua Jana mchana Rostam amekula nini?

Saa sita mchana jana Lowassa alikuwa amevaa nguo gani?

Makamba Mzee, katibu wa CCM jana saa kumi alikuwa anaongea na nani?

Ni hayo tu.

Wabongo bwana!
 
Naona Rostam ni rafiki yako na inawezekana amekukatia kidogo!Pole.Lakini hata kama hatukwenda mahakamani, kelele zinasaidia kumnyima usingizi!

Nadhani hata yeye kama ameona tumemdhalilisha sana angemshauri RA akatushitaki au kumsaidia kwenda mahakamani. Te te te..kwi kwi kwiiiiiii!
 
Back
Top Bottom