Rostam, Lowassa wafumwa kikaoni

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Rostam, Lowassa wafumwa kikaoni

  • Vyote vyafanyika ofisini kwa bw Edward Lowassa
  • Katibu Mkuu CCM, Makamba abainika alikuwepo
  • Vilifanyika Alhamisi wiki hii na vingine Jumatatu wiki hii kuanzia saa 4.00 asubuhi

Na Mwandishi Maalum,
Taifa Letu
April 3, 2009


Yule mfanyabiashara mwenye maadili yenye utata, Bw Rostam Aziz wiki hii amekuwa akifanya vikao kadhaa vya faragha na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Vikao hivyo ambavyo vinasadikiwa vinahusiana na sakata la kukwama kwa mara nyingine kwa jaribio la kutaka kuiuzia Tanesco mitambo chakavu ya Richmond, vimekuwa vilifanyika ofisini kwa Lowassa, Alpha Cleaners iliyoko eneo la viwanda Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba vikao hivyo vilimshirikisha pia Bw Yusuf Makamba.

Baadhi ya mashuhuda wameliambia gazeti hili kwamba vikao vya mikutano kati ya wakubwa hao vimeongezeka mno hasa kwa wiki hii ambapo baada ya gazeti hili kutonywa walipo vigogo hao lilivamia katika ofisi za Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na kumshuhudia Bwana Rostam Aziz akiingia sehemu hiyo ba gari la kifahari lenye namba za usajili T 347 AJL.

Uchunguzi wetu umebaini kwamba kikao cha kwanza baina ya Lowassa na Rostam kilifanyika Alhamisi wiki iliyopita lakini hapoakuwa na uhakika kama Bw Makamba alikuwepo.

Hata hivyo katika kikao ambacho kimefanyika juzi Jumatatu kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tano na dakika 45, makachero wa gazeti hili walimshuhudia Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akijumuika na Bw Rostam Aziz pamoja na Wziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa…………
 
Jamani, is that a crime for the people/friends to meet and discuss their interests of which u don know?
 
Si kosa marafiki kukutana ila kukutana kupanga namna ya kuihujumu nchi na wanaopinga ufisadi ni kosa,tafakari.
 
No issue here, shukuru kwamba umewaona, ni vikao vingapi wankutana na hauwaoni?
 
Maji ya shingo au ndo wanajipanga upya?
Hawa jamaa wakiamua wanaweza sasa inabidi kudhibiti mipango yao.
 
Maji ya shingo au ndo wanajipanga upya?
Hawa jamaa wakiamua wanaweza sasa inabidi kudhibiti mipango yao.
 
Ufisadi wot huanza na vikao kama hivyo! Kazi nzuri kijana tusubiri na makamba atakuja na lipi CCM.
 
Mipango yote iwe ya kifisadi au njema inapangwa thru vikao!!!! Kwa uhakika tupeni agenda za vikao hivyo. Tofauti na hapo tusianze ku create agenda zetu sisi wenyewe. Good day.
 
Ingekuwa wamekutana saa 4:00 usiku hapo ningekuwa interested but asubuhi tena ndani ya ofisi!! jamani................
 
Maji ya shingo au ndo wanajipanga upya?
Hawa jamaa wakiamua wanaweza sasa inabidi kudhibiti mipango yao.
__________________

Fidel80:

Jamaa hawa ni hatari sana -- hasa wanapofikwa na maji ya shingo ... wanaweza hata kupanga kumpindua JK!
 
Si kosa marafiki kukutana ila kukutana kupanga namna ya kuihujumu nchi na wanaopinga ufisadi ni kosa,tafakari.

Wewe unajuwa walicho zungumza hata useme ''kupanga namna ya kuihujumu nchi na wanaopinga ufisadi ni kosa'' huu ndio uzushi wenyewe!
 
' Kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiyari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na kuanzisha na kujiunga na vyama au mashirika yalilyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengine.'' Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania 1977 Ibara ya 20(1)
 
Whether normal meetings or not, but when refering to the fool business they did! extra care is needed on whatever they are doing, RA and EL are among dangerous peoples in this country, i believe YM is just looking for left outs!
 
Wewe unajuwa walicho zungumza hata useme ''kupanga namna ya kuihujumu nchi na wanaopinga ufisadi ni kosa'' huu ndio uzushi wenyewe!

Well,
Unajua mtuukisha umwa na nyoka kila ukiona mjusi lazima uruke maili mia!

Hawa watu walisha kaa vikao wakabaka uchumi wetu kupitia RICHMOND- DOWANS, KAGODA, n.k, Lazima mtu yeyote ukiwaona wamekaa kikao ujiulize leo watakuja na lipi!

Hawa wezi si wakuacha wakae wapange mipango yao ya kuzidi tuibia eti tunasingizia uhuru wa kukutana! Lazima tule nao sahani moja mguu kwa mguu mkono kwa mkono, tuwabane tena wajue tunafatilia nyendo zao zote na mipango yao ya kiwizi wizi ya kuhujumu uchumi wetu!

Yaani watanzania wote tuamke tule nao sahani moja kila wanako enda tunao mpaka wakose pa kutokea! Itakuwa ni ujinga eti tusiwafatilie ili hali tunajua ni wezi wetu! Tena inabidi tuwabane hata wakienda jificha offshore ka nzi ketu kawaanike ili wajue kwamba 'no longer at is'
 
TAARIFA za awali ni kuwa 'RA na EL wameamua kumshirikisha Baba January katika Dili yao ya kuwang'oa baadhi ya wabunge na kusimika watu wao, makamba maekubaliana nao na moja wapo ni kumshauri JK kumteua Waziri mmoja kuwa Balozi ili jimbo lake ligombewe na Mwenyekiti wa Wahindi mkoa mmoja, RA naye ni mwenyekiti wa Wahindi wa Dar'
 
TAARIFA za awali ni kuwa 'RA na EL wameamua kumshirikisha Baba January katika Dili yao ya kuwang'oa baadhi ya wabunge na kusimika watu wao, makamba maekubaliana nao na moja wapo ni kumshauri JK kumteua Waziri mmoja kuwa Balozi ili jimbo lake ligombewe na Mwenyekiti wa Wahindi mkoa mmoja, RA naye ni mwenyekiti wa Wahindi wa Dar'

Uwongo huu, Rostam si Muhindi for your information!
 
Kwa mwendo huu. Iko siku tutasoma magezetini....Rostam afumwa akielekea msalani..!!

Hawa watu wafuatiliwe kwa karibu kadiri itakavyowezekana. Ni watu hatari sio tu kwa AMANI na UTULIVU wa NCHI yetu, bali hata kwa UCHUMI na USTAWI wa watu wetu.
 
Back
Top Bottom