Rostam katika tope jipya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam katika tope jipya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, May 15, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,376
  Likes Received: 5,663
  Trophy Points: 280
  • Aleta hasara kwa serikali
  • Akabidhi mahindi hewa

  Na Mwandishi Wetu
  MwanaHALISI ~ Maslahi ya Taifa Mbele


  TUHUMA mpya za ufisadi zimeibuka dhidi ya mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na kumzamisha katika tope jipya, MwanaHALISI limegundua.

  Tuhuma hizo zinahusu gharama za kutoa bandarini tani 4,677.82 za mahindi kazi iliyofanywa na Rostam Aziz.

  Kazi hiyo iligharimu Sh. 894,372,520 bila ya kuwapo mkataba kati ya Rostam na serikali.

  Tuhuma hizo zimebainishwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  CAG anasema fedha hizo zililipwa kwa Kampuni ya Tanzania Packages Manufacturers (1998) Ltd, kupitia akaunti Na. 1010400548400 iliyoko Benki ya Standard Chartered, na mhusika ni Rostam Aziz.

  Ofisi ya CAG anasema ununuzi huo wa mahindi tani 4,677.82 zenye thamani ya dola za Marekani 1,113,788.942 ni wa mashaka. Wakati huo dola moja ya Marekani ilikuwa Sh. 803.00. Rostam alizoa Sh. 894,372,520.

  “Hata hivyo, malipo haya yalifanyika bila kuwapo mkataba kati ya Rostam Aziz na serikali. Vilevile hapakuwapo nyaraka muhimu za kuingiza mahindi nchini, kama ilivyodokezwa katika aya ya 3.1.1 ya taarifa hii (ya CAG), hivyo kutia mashaka kama kweli mahindi haya yalinunuliwa toka nje ya nchi,” inasema taarifa.

  Taarifa hiyo ilikuwa inahusu utoaji wa zabuni na mikataba ya ununuzi wa tani 175,000 za mahindi kutoka nje ya nchi na msimamizi alikuwa Wizara ya Kilimo na Ushirika-Idara ya Usalama wa Chakula.

  Taarifa ya CAG ilikuwa ikipelekwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), na imesainiwa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, E.K.Shuli.

  Kwa mujibu wa aya hiyo, nyaraka muhimu za kuingiza mahindi ndani ya nchi, kama ilivyosainiwa chini ya kifungu 5.3 cha mkataba hazikuonyeshwa.

  Nyaraka hizo ambazo hazikuwasilishwa ni pamoja na nakala tano za Ankara (invoice) zinazoonyesha aina ya mali iliyoagizwa, kiasi, bei na thamani ya mali.

  Nyaraka nyingine ni nakala halisi za kuingiza mizigo nchini; nakala tano zenye orodha ya mali inayoingizwa nchini; cheti cha bima, cheti cha muuzaji mahindi kuthibitisha kuleta mali na cheti cha usafi wa mali.

  Cheti kingine kilichokosekana ni kile cha ukaguzi wa ubora wa mali kutoka kwa mkaguzi wa ubora (viwango) wa nchi ambayo mali hiyo imeagizwa au kununuliwa.

  “Kukosekana kwa nyaraka hizi muhimu za uingizaji mali nchini kunatia mashaka juu ya ubora wa mali iliyonunuliwa, na kama kweli mahindi yaliagizwa nje ya nchi na kampuni mbili,” inasema taarifa ya CAG.

  Mikataba ya ununuzi wa mahindi ilikuwa baina ya serikali na kampuni mbili za EECO Traders Ltd ya Uingereza, ambayo ilitakiwa kuingiza tani 25,000 zenye thamani ya dola za Marekani 4,187,500 na M/S Andre & CIE ya Afrika Kusini, ambayo ilitakiwa kuingiza tani 100,000 zenye thamani ya dola za Marekani 19,075,500.

  Majukumu ya mikataba hiyo miwili yalitekelezwa na Kampuni ya Tanzania Packages Manufacturers (1998) Ltd., na mhusika mkuu ni Rostam Aziz.

  Malipo ya kampuni zote mbili yalifanywa kwa kampuni hiyo na anayetajwa kupokea malipo ni Rostam yuleyule.

  Kubadilishwa kwa mfumo wa malipo kwa kampuni hiyo kulisababisha Barua ya Dhamana (LC) ya Sh. 2.995 bilioni iliyokuwa imefunguliwa katika NBC (1997) Ltd., tawi la City Drive kwa ajili ya EECO Traders Ltd., kuliingizia serikali hasara ya Sh. 29,329,728/25 ikiwa ni kamisheni ya benki kwa ajili ya kufungua LC hiyo.

  Taarifa ya CAG kwa Bunge inasema, “Kitendo cha Kampuni ya Tanzania Packages Manufacturers (1998) Ltd., kuchukua majukumu ya kutekeleza mikataba hii bila kibali cha maandishi cha serikali, kinaleta mashaka katika ununuzi huo wa mahindi.”

  Taarifa inasema kwa makosa hayo, serikali inapaswa kuidai EECO Traders Ltd., fidia ya hasara hiyo ya Sh. 29,329,728.82 iliyosababishwa na Rostam Aziz.

  Mbali na hasara hiyo, ukaguzi wa mikataba na nyaraka zilizohusika kupokelea mahindi ulionyesha kuwa tani 1,662.985 hazikupokelewa.

  Kufuatia kucheleweshwa kuletwa nchini kiasi hicho cha mahindi, wazabuni walipaswa kulipa fidia ya ucheleweshaji huo inayofikia jumla ya dola 745,993.

  Taarifa ya CAG inaitaka wizara ya kilimo na ushirika ithibitishe iwapo tani 1,662.985 za mahindi zilizochelewa kupokelewa ziliingizwa nchini baadaye na thamani yake ielezwe.

  “Wizara ithibitishe uhalali wa malipo haya kwa kuwasilisha mkataba wa ununuzi wa tani 4,677.82 za mahindi kati ya serikali na Rostam Aziz,” inasema taarifa ya CAG kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

  Tuhuma hizi zinakuja wakati serikali imetangaza kufunga mjadala juu ya tuhuma zinazomkabili Rostam na Mengi mengine yakitarajiwa kuibuliwa.
   
 2. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Mjadala wataufunga wao ila sisi tutauendeleza. More fire. Hit the mettle while it's hot. Wakuu inabidi hawa mafisadi wawekwe roho juu hivi hivi with non stop news of the wrongs they have done. Na ikifika kipindi tunahisi mijadala inapooza tunazindua ya nyuma ambayo haijamalizwa.
  The plan is not to let this ufisadi cases fade from the peoples mind untill election day. We need to keep it alive and interesting. Front page news!! So that by next year it will still be ammunition against the sharks.
  Lets wear them out!!! Sustained bombardment!!!!
  Tutashinda tu!!
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huyu RA kweli hasafishiki...the guy mission ni kutuibia tu hakuna lingine analolifanya Tanzania...benki account inamhusu lakini mkataba wa kuleta mahindi jina lake halimo...classic RA
   
 4. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145

  Swadaktaaaa, hiri rijamaaaa kila mahala palipo na feza chafu ukinusa vizuri utalikuta, hebu angalia Caspian inafanya kazi migodini kuchimba udongo lakini ili rikwepe kulipa mshahara kima cha chini wa kwenye migodi (Tsh 350,000/=) basi likaandikisha kuwa Caspian Viwanda na Biashara? halafu anajifanya anapenda wanainchi, Mzurumati mkubwa wa haki za wanainchi, na hao CCM wanazidi kumkumbatia wakati anazidi kuongeza mfarakano ndani ya chama chao kwa kuanza kuwapangia safu ya wabunge wa 2010 kwani tayari kesha anza kufadhili anaowataka yeye , Tusubiri tumbwiritumbwri wakati ukifika tutaona mgawanyiko wa Tarime Tanzania mzima[​IMG]
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Jana nilimwona white head ktk taarifda ya habari channel ten akiongea na wananchi wake kule monduli.
  anaonekana kijana bado jasiri wa kujibandua ngozi na kuwa kiumbe mwingine ila make ni ile ile....
   
 6. ChingaMzalendo

  ChingaMzalendo Senior Member

  #6
  May 15, 2009
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Fisadi apigwe mawe tumechoka naye. Walahi mtu, hichi ndo kilichobakia
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ni mara nyingi tu serikali imeomba mzabuni afanye kazi bila mkataba. Hii mara nyingi inatokana na kinachodaiwa kuwa ni umuhimu na uharaka wa kazi yenyewe. Anaechukua risk kubwa ni yule anaefanya kazi bila mkataba maana anaweza kurukwa mbeleni! Ila kama Rostam alilipwa fedha hizo bila ushahidi wowote wa kwamba mahindi yaliletwa, basi inabidi atueleze kulikoni! Yeye na wale wote waliohusika wapelekwe mbele ya sheria. Kama alileta hayo mahindi basi cha kuuliza ni alistahili kulipwa kiasi gani!

  Unfortunately katika nchi yetu kama wafanyabiashara wote watakataa kutoa huduma bila mkataba, tutakwama. Hasa hao walio mbali na Dar es Salaam. Mtindo wetu wa disbursement wa fedha una walakin mkubwa!

  Amandla........
   
 8. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Unajua Idd Amin alikuwa na akili nyingi kuliko Nyerere !!! sasa ndiyo nagundua, kumbe Amin aliona mbali sana kuliko Nyerere, hawa magabacholi hawafai hata kwa dawa!!. Nafikiri turudi tena tulikotoka na kuchukua uamuzi wa Idd Amin Dada.
   
 9. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Siyo kweli unachosema, Kinachofanyika siku zote mikataba inatolewa lakini mfanyabiashara yeyote anayefanya na serikali anajua hilo na huwa linaelezwa kwenye mkataba kuwa uwe tayari kulipwa baada ya kutoa huduma hata zaidi ya miezi mitatu. Kwa hiyo ukipata huo mkataba ni juu yako kuamua kama unakubali au no. Kwa hiyo mikataba inakuwepo labda masharti ndiyo tofauti.
   
 10. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Umefanya kazi kweli na serikali wewe? Unajua kinachofanyika kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha? Mimi sizungumzii theory bali practise.

  Mkataba unatakiwa usainiwe pamoja kati ya mshitiri na mzabuni mbele ya mashahidi wao! Kabla ya kufanyika hicho, hakuna cha mkataba. Mkataba hautakiwi kutumwa. Ukiona inafanyika hivyo ni kuwa pande zote zimeisharidhia kilichomo na kinachotafutwa na sahihi za wahusika na mashahidi wao. Kisheria kama mzabuni ataanza kutekeleza mkataba huo kabla ya hizo sahihi kuwepo atakuwa amefanya bila mkataba. Wengi wanafanya hivi. Na wako waliotekeleza maagizo na wakakataliwa kulipwa.Yapo. Yalitendeka.

  Amandla......
   
 11. M

  Msindima JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jamani huyu baba yukoje?mbona kila tuhuma ni yeye tu hivi haoni aibu,hata hiyo familia yake nahisi itakuwa ya ajabu ajabu,maana baba akishakua wa hivyo hata nyumbani ni hivyo hivyo.

  Karibu kila tenda anahusika,au yeye ndo raisi wetu?
   
 12. J

  Jafar JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Si amini karne bado serikali yetu inafanya biashara na watu binafsi bila ya mikataba. Hii ni risk kubwa kwa wote, kwa wafanya biashara na serikali pia.
  Pili, hivi hawa watu watatuchezea mpaka lini?
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Jamaa baada ya kutoa chake kikubwa ajili ya kumuweka madarakani........jk s asa anarudisha 10 times hakuna wa kumgusa hy ndio only asante yake atakayopata kabla jk hajatoka maana akitoka tuu...fadhila zitakuwa zime balance waanze kula mafao tuuu........kila deal jamaa yumo
   
 14. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #14
  May 15, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Fundimchundo ndugu yangu, ninachokwambia ndicho hicho nimefanya sana kazi hizo na hata sasa bado nazifanya humo humo sirikalini. Mkataba unakuwepo hata kama ni barua ya kukuita uje ufanye hiyo kazi ni mkataba tayari, huwezi kwenda kufanya kazi ya mamillion serikalini kwa kupigiwa simu tu. lazima upewe maandaishi. Hivyo Rostam anatakiwa ajibu kwa nini amefanya kazi na kulipwa bila mkataba !!!???
   
 15. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Na yanaendelea kutendeka mpaka leo....tatizo linakuja hapo kwenye malipo. Ilikuwaje RA kulipwa bila kutoa huduma aliyotakiwa kutoa; halafu bado hakuna mkataba..!!
   
 16. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ONCE FISADI ALWAYS FISADI.... Hang him to DEATH!
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Ni kweli, ila za arobaini zake zipo. Shida ni kuwa zinachukua muda mrefu kutimia na kadri muda unavyozidi kwenda, nyani wanamaliza mahindi. Kama ingewezekana basi tumalizane naye ili mambo yafikie ukomo. Hatuwezi kuendelea kumwongelea mtu mmoja kila siku. Labda sisi ndo wenye matatizo na jamaa tunamwonea tu.
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Barua ya kukuita si mkataba. Inapata uzito kama tu kuna barua ya mzabuni akikubali wito! Hata hapo, wajanja wanaweza kukuruka. Na kumbuka kuwa Dar es Salaam si mfano wa Tanzania nzima.

  Hapa wa kuwashika ni wale walioidhinisha alipwe bila mkataba. Wao ndio waeleze wali-base kwenye nini? Kama Rostam aliandika barua kudai alipwe, atakuwa amejiingiza mkenge. Lakini akiweza kuthibitisha kuwa kweli kazi aliifanya itakuwa vingine.

  Tumesahau kujiuliza nani ndiye anayetakiwa kutayarisha mkataba? Rostam au serikali? Hivi kama Rostam angeutayarisha na ikaja julikana si tungemsulubu zaidi? Kama mwenye wajibu wa kutayarisha mkataba ni serikali kwa nini alaumiwe Rostam kwa kukosekana mkataba! Jukumu la kuhakikisha kuwa taratibu zimefuatwa ni la watendaji wa serikali na wala si la Rostam.

  Amandla.......
   
 19. C

  Chuma JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bubu wenye JF kina nani?...unafikiri bila mimi na wewe n others kutakuwa na JF?

  Tatizo lako upo kama Mwanakjj anaamini kila analofanya yupo Sahihi. Hata kukubali kosa unashindwa...naona nawe ushaanza kupata blind follower...Mwafrika.

  Halafu zikijaa thread mnaanzisha thread ya kupongezana...? Kweli kama Huu ndio usomi wenu basi tuna kaz huko mbele ya safari.

  Mwafrika elewa kuwa mie na support at any cost Mafisadi wote papa na nyangumi waanikwe. na wale wanaojifunza ufisadi pia waanikwe....Ila wakati tunawalaumu viongozi kufanya recycling ya viongozi nyie mnachofanya n hicho hicho ktk mathread.
   
 20. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #20
  May 15, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hee hee hee heee heee heee,

  Rostam kapatikana na ufisadi mwingine? Lazima hapa kutakuwa na sababu ya msingi kabisa ya kumtetea Rostam. Fundi Mchundo atasema kuwa kuna typo error hapo (na hizo pesa sio nyingi kiasi hicho au ..) huku companero akisema kuwa huyo CAG ni mfuasi wa Mwanakijiji.
   
Loading...