Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 584
Pamoja na baadhi ya watu kuanza kuamini kwamba Rostam Aziz amepungua nguvu na kwamba sasa hana uwezo wa kupanga safu katika uchaguzi wa mwaka huu kama alivyofanya huko nyuma, UKWELI ni kwamba ana nguvu kubwa na viongozi wetu wa bara na visiwani, Rais Jakaya Kikwete na Rais Amani Abeid Karume, wanamtumia katika kufanikisha malengo yao na kwa maana hiyo kuendelea KULINDA MASLAHI YAO YA PEMBE TATU Z UFISADI (Naazima maneno ya Lula wa Raia Mwema).
Mutakumbuka suala la Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein kuwania Urais wa Zanzibar liliandikwa na gazeti la Mwananchi, na siku moja baadaaye zikachapishwa na gazeti la Rai katika toleo lake la wiki iliyopita kwa uzito mkubwa habari ambayo imerudiwa tena Rai la wiki hii lililoamua kutetea uamuzi wa Dk. Shein kwa nguvu zote na kuwabeza wanaompinga na kuwa ni "wabaya wake".
Tunakumbuka kwamba Rostam amekuwa akitamba (yaweza kuwa kweli) kwamba ndiye aliyemuweka Karume madarakani mwaka 2000 kwa kumdhibiti DK. Bilal asifurukute. Baadaye nguvu za Rostam na wenzake (kina Lowassa) ndiyo iliyoandaa mazingira ya Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005.
Kwa kifupi sasa Karume (Sina hakika kama JK anamuunga mkono kwa hili) ndiye anamtumia Rostam kumuingiza Dk. Shein Zanzibar ili yeye aje kuwa Makamu Bara lakini hata akikwama atakua na kinga maana Dk. Shein kihistoria si mtu wa maamuzi magumu ya kisiasa. Ni Mtendaji mzuri tu ambaye hakika atakua akifanya kazi kwa maelekezo ya hao waliomuweka. Si jambo zuri sana kulisema, lakini linahusu MUSTAKABALI NA USALAMA WA TAIFA LETU.
Hatari ya jambo hili ni kwamba hadi sasa msimamo wa JK haujaonekana wazi katika hili na kama Dk. Shein atakua ameingia katika mikono ya kina Rostam itakuwa ni UKURASA MWINGINE KWA SIASA ZA TANZANIA KUELEKEA 2015 na tujue fika kwamba huko tuendako LOWASSA ndiye Rais AJAYE 2015 huku ROSTAM na Kundi lake wakiendelea KUCHEZA NA UCHUMI WETU hadi hapo UKOMBOZI WA KWELI UTAKAPOWADIA.
TANZANIA UHURU WA KWELI BADO SAAANA