Rostam Aziz: Slaa ni mpotoshaji

Rostam Aziz: Slaa ni mpotoshaji

Radhia Sweety

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Posts
4,433
Reaction score
1,772
Amtaka Slaa kujitokeza hadharani kuthibitisha kauli zake. Akanusha kuisaidia CHADEMA. Asema Slaa ana historia ya uzushi.

Chanzo: Channel 10

======================


Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, amemvaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akimuita kuwa ni mtu mwongo, mbinafsi na mpotoshaji mkubwa.

Rostam alieleza hayo katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake jijini Dar es Salaam juzi, alipozungumza na vyombo vya habari kuelezea mambo kadhaa zikiwamo sababu za kujiondoa ndani ya Chadema.

Dk. Slaa alidai kuwa mwaka 2009 baada ya kutaja orodha ya mafisadi 11 nchini katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam, Rostam alimpigia simu na kumtishia maisha.

Dk. Slaa pia alidai juzi katika mkutano wake na vyombo vya habari uliorushwa na vituo vitatu vya runinga kuwa Rostam anaifadhili Chadema.

Katika taarifa yake jana, Rostam alisema: "Nilimsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa alipokuwa akizungumza katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

"Kwa mara nyingine kama ilivyo hulka yake miaka yote, Dk. Slaa kathibitisha pasipo na shaka kwamba yeye ni mbinafsi na mpotoshaji mkubwa."

"Nimesikitishwa na kushtushwa japo sikushangazwa hata kidogo na hatua ya Slaa ambaye sasa anaonekana kukubuhu kwa uzushi kutoa matamshi ya namna hiyo.

"Sijapata hata mara moja kuwa na mawasiliano na Dk Slaa wakati wowote. Madai yake kwamba eti nilimtisha ni ya kupuuzwa na yasiyo na msingi hata kidogo," alisema Rostam.

Rostam alieleza kuwa ni jambo lisiloingia akilini hata kidogo kwa watu wanaomfahamu Slaa kwamba anaweza kumtishia maisha na yeye akakaa kimya bila kuchukua hatua ya kwenda polisi na kumshitaki halafu anakaa na jambo hilo kwa miaka yote hadi juzi ndipo alisema hadharani.

"Ili kuthibitisha madai yake hayo, namtaka Dk. Slaa kujitokeza hadharani na kutoa ushahidi wa jambo hilo," alisema Rostam.

Huu ni uongo mwingine wa dhahiri. Namtaka Dk. Slaa kutoa ushahidi pia katika madai yake haya.

"Ni huyu huyu Dk. Slaa ambaye mwaka 2010 alizusha kwamba eti mimi, tukiwa na Rais Jakaya Kikwete na Edward Lowassa tulikutana katika hoteli ya La Kairo, Mwanza na kupanga njama za kumuibia kura zake za urais," alisema na kuongeza:

"Wakati Slaa akitoa madai hayo ya uongo, mimi nilithibitisha kwamba wakati huo nilikuwa Afrika Kusini na Rais Kikwete akiwa Lindi huku Lowassa akiwa Arusha. Ni wazi kwamba tusingeweza kukutana La Kairo kama alivyodai yeye."
Kwa mujibu wa Rostam, Dk. Slaa kuna wakati alimzushia hadi Rais Kikwete alipodai kwamba alisafiri kwa usiku mmoja kwenda China kumtoa mwanaye aliyekuwa amekamatwa na vyombo vya usalama, kisha kurejea Dar es Salaam usiku huo.

"Ni Slaa huyu huyu ambaye mwaka 2010 wakati wa kampeni alifikia hatua ya kuutangazia umma wa Watanzania kwamba kulikuwa na malori yaliyobeba kura za CCM ambazo zingesaidia ushindi wa wizi yaliyokamatwa Tunduma. Malori hayo yalipokaguliwa yalibainika kuwa na mizigo ya kawaida," aliongeza katika taarifa hiyo.
 
Zama zao zinapita wasitumie fursa kuwa watakimbilia nje na kuwa wakimbiza na kupewa ajira huko,watuache na Tanzania yetu kwa wale hata nchi jirani hatujafika ili tulete maendeleo yetu.Jamani hata vyama ni muda sasa zaidi ya miaka 60 wawe ni washauri tu wasipewe nafasi za uongozi.
 
Alhamdulilah lillah, Leo Rostam yuko na Chadema na Dr.Slaa yuko against Chadema. Haya sio Maigizo ni Siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Shikamoo Zitto uliesema tuwe tunaweka akiba ya Maneno na Tusiamini Wanasiasa hata kama ni wa Upinzani
 
Dah! yan mwaka huu, lakin je air time ya jana ni kweli amefadhiliwa na ccm au yey mwenyew kwa uchungu alionao kwa taifa?
 
Alhamdulilah lillah, Leo Rostam yuko na Chadema na Dr.Slaa yuko against Chadema. Haya sio Maigizo ni Siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Shikamoo Zitto uliesema tuwe tunaweka akiba ya Maneno na Tusiamini Wanasiasa hata kama ni wa Upinzani

Wapi kasema yuko Chadema?
 
Alhamdulilah lillah, Leo Rostam yuko na Chadema na Dr.Slaa yuko against Chadema. Haya sio Maigizo ni Siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Shikamoo Zitto uliesema tuwe tunaweka akiba ya Maneno na Tusiamini Wanasiasa hata kama ni wa Upinzani

Nani kakwambia Rostam yupo chadema acha uwongo,kaa na huyo yuda wako Zitto usitafute kick
 
Nakuomba chonde chonde Mtukufu Rais Mtarajiwa, Mh. Lowasa Edward Ngoyani, endelea kuwachoma hao ma-ccm, kwao umekuwa mwiba mkali. Wewe endelea na kampeni yako mkisaidiana na Sumaye, mpaka kieleweke.
Ninyi ndio mmekuwa ukombozi wa kweli kwa Mtanzania. Kura ni zenu na ushindi ni wenu. Mwaka huu Ikulu ipate mpsngsji mwingine
 
Back
Top Bottom