Rostam Aziz aandaa timu ya watetezi wa Dowans

Lostam atangaze siku hiyo ili ashuhudie ya Tunisia. Ajiandae kurudi Ilan kwao. It is not acceptable especially in this country . Hope he is wasting his money and time.Jf members big up and keep up to date. Iam sure even MR president knows about it and he is not happy of the on going situation.

Pole sana JK Mate. Have to find another way to replace all money used for the campain ,Althogh was'nt successful.
 
Wapiga debe wakuu (First Eleven) wa malipo ya kifisadi kwa Dowans ni hawa hapa:

1. Jakaya Kikwete
2. Mizengo Pinda
3. Frederick Werema
4. William Ngeleja
5. Mathias Chikawe
6. Edward Lowassa
7. Andrew Chenge
8. Mark Bomani
9. Anne Makinda
10. Zitto Kabwe
11. Rostam Aziz

Reserve Bench

1. Nimrod Mkono
2. Nazir Karamagi
3. Kingunge Ngombale-Mwiru
4. Sophia Simba
5. Emmanuel Nchimbi
6. Dr. Mohamed Gharib Bilal
7. Fisadi Media (Mtanzania/Rai, Tanzania Daima, Daily News, Jambo Leo)
 
Lisemwalo lipo, na kama halipo............ila sasa sarakasi zitakuwa kweli, lazima tuamke kuikomboa nchi yetu na hawa mahayawani
 
Kuna jitihada kuwaweka sawa kina Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF, Hamad Rashid wa CUF, Zitto Kabwe wa Chadema (kashanunuliwa siku nyingi na Rostam), John Shibuda wa Chadema, James Mbatia wa NCCR Mageuzi, John Cheyo wa UDP, Augustino Mrema wa TLP na Christopher Mtikila wa DP watoke hadharani kuunga mkono malipo kwa Dowans.

Hakuna kiongozi yeyote hata kama angekuwa Slaa ana uwezo wa kubadilisha watanzania uwezo wa kufikiri juu ya DOWANS. Atakayeshangilia kulipwa kwa Dowans atakwisha kisiasa. Mwendo ndiyo polepole.....oh I'm sorry...Polepole ndiyo mwendo.
 
It could be true. Tanzania Daima imekuwa ikitumiwa sana kuwakosha kina Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge na kuwaandika vibaya kina Samuel Sitta na Harisson Mwakyembe. Hii inatokana na ukweli kuwa mhariri wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, yuko kwenye payroll ya Edward Lowassa na Rostam Aziz.

nakubaliana nawe kwani gazeti la hivi karibuni la tanzania daima kulikuwa na makala ya Absalom Kibanda ikimponda mr six
 
Wasomi wamshukia Jaji Mark Bomani


*Ni kwa kutetea malipo kwa kampuni ya Dowans
*Wasema, kama hakurubuniwa, anazeeka vibaya


Na John Daniel (Majira)
SIKU moja baada ya aliyewahi kuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mark Bomani, kudai kuwa malipo ya sh. bilioni 94 kwa
Kampuni ya Dowans haikwepeki, wanazuoni nchini wamemshangaa Mzee huyo na kudai kuwa kama hakurubuniwa na wahusika wa kampuni hiyo basi anazeeka vibaya.

Wakizungumza na Majira jana wanazuoni hao walisema hawakutarajia kauli kama hiyo kutolewa na Jaji Bomani kwa kuwa ni moja kati ya watu wenye heshima ambao wangeweza kuisaidia serikali badala ya kutoa kauli zenye utata.

"Mimi nilifikiri kwamba Jaji Bomani angetoa ushauri kwa serikali kuwaeleza Watanzania nini kilichomo ndani ya kesi hiyo ya Dowans, hadi sasa wananchi hawajui ukweli kama Mkataba wa Richomnd ulikuwa halali au la, na kama haukuwa halali ndiyo hiyo ya Dowans au ni vitu viwili tofauti.

"Lakini pia kuna kampuni iliyowakilisha TANESCO kwenye kesi hiyo, wananchi wanataka kujua kama kampuni hiyo ina uhusiano wowote na Richmond iliyofutwa au sivyo," alisema Profesa Mwesiga Baregu.

Prof. Baregu ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza alilinganisha kauli ya Jaji Bomani na ile ya Mwanasheria Mkuu wa sasa, Jaji Frederick Werema ambayo pia ilipingwa vikali na Watanzania.

Alisema suala la malipo ya Dowans linagusa maslahi ya umma, hivyo ni lazima serikali ichukue taadhari kubwa kabla ya kuitekeleza ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa kina kwa wananchi na si kuharakisha malipo kama inavyoshauriwa na Jaji Bomani.

"Jaji Bomani angeshauri kwanza serikali kuwa wazi kwa wananchi kueleza nini kiini cha tatizo hilo, ni uzembe wa watendaji au udhaifu wa wanasheria kama inavyodaiwa, ieleze hatua zilizochukuliwa dhidi ya walioingiza taifa katika mkataba huo kabla ya kukubali malipo," alisisitiza Profsa Baregu.

Alionya kuwa iwapo serikali itaendelea na mfumo wa kufunika mambo muhimu yanayohitaji maelezo ya kina ili kuondoa mawazo potofu, wananchi watafikia hatua mbaya ya kukosa imani na serikali na kujenga chuki kwa viongozi.

Kwa upande wao wanafunzi wa mwaka wa tatu wa kitivo cha Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliozungumza na Majira kwa sharti la kutotajwa kwa ma hofu ya kushughulikiwa walisema wanadhani Jaji Bomani anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwa kauli yake ya jana.

"Sisi wanafunzi wa sheria Chuo Kikuu cha Dar es saalam hatukutegemea mwanasheria wa miaka mingi kama Jaji Bomani aongelee suala la Dowans ambalo liko kwenye mchakato wa mahakama, lengo lake nini kama si kuifluence mahakama?" aliohiji mwanafunzi mmoja katika ujunbe wao walioituma Majira.

"Ni aibu kuwa hata wazee kama Bomani wanarubuni na mafisadi kwa pesa na kuwasaliti wananchi masikini, amezeeka vibaya," iliongeza sehemu ya ujumbe huo.

Walisema walitegemea Jaji Bomani kuisaidia serikali kutafuta njia ya kurejea upya uamuzi huo katika kipengele cha uhalali wa mkataba kati ya Richmond na serikali ambayo ndio iliyorithiwa na Dowans.Walisema iwapo mkataba wa Richmond haukuwa halali ni vipi ikirithiwa na Dowans inakuwa halali, na kuitaka serikali kutoa ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo kwanza.Katika mazungumzo yake na gazeti hili jana, Jaji Bomani alitoa kauli ambayo haikutarajiwa na umma ya Watanzania kuitaka serikali kulipa Dowans kwa maelezo kuwa kutofanya hivyo kunaweza kuigarimu zaidi Taifa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam wiki hii, Jaji Bomani alisema ni vigumu Mahakama Kuu kutengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC Court) kama hakukuwa na kasoro zozote katika utoaji hukumu hiyo.

"Kwa kesi za usuluhishi kama hii hukumu hii inaweza kutenguliwa tu kama hao wapatanishi hawakuwa na sifa za kuwa wapatanishi kitu ambacho hapa hakiwezi kutumiwa kwa kuwa katika suala hili, hawa walikubaliwa na pande zote," alisema Jaji Bomani na kuongeza;

"Hukumu hii inaweza kutenguliwa tu kama ikidhihirika kwamba wamepewa rushwa kwa kutoa hukumu ya namna hiyo. Vinginevyo Mahakama Kuu haijihusishi na kuingilia kesi yenyewe.""Mimi kwa upande wangu kama nilivyokwisha kusema siku za nyuma jambo hili liishe ili mitambo hiyo itumike hapa nchini kuzalisha umeme tuondokane na hali ya mgawo na upungufu wa umeme na hilo ndilo jambo muhimu kwa uchumi wa nchi.
 
Hata wapeane mamilioni kutuibia, watanzania tumeamka watadanganyika na kuhongwa hao, lakini sio wananchi wote. Umoja wao na ufisadi wao utaangushwa tu. Walikuwepo wafalme wenye nguvu sana, walikuwepo viongozi kama Hitler lakini ilifika wakati wakaanguka kwa aibu. Wengine hawana Hata kumbukumbu, wala familia zao hazijulikani. Mali zao zimeliwa na wenye akili maana wao walikuwa WAPUMBAVU.
 
Nimepata taarifa leo kutoka kwa mtu aliye karibu na Rostam Aziz kuwa fisadi huyu aliyechonga dili zima la Richmond/Dowans sasa ameandaa timu ya viongozi mbali mbali wenye ushawishi kwenye jamii ambao wataibuka kwenye vyombo vya habari kuishinikiza serikali iwalipe Dowans.

Atatumia vyombo hivi kueneza propaganda yake: Tanzania Daima, Clouds FM, TBC1, Channel Ten, Mtanzania/Rai, Jambo Leo, Daily News, Habari Leo, Sauti Huru, etc.

Watu hawa wataibuka kuwapinga vikali Samuel Sitta na Harisson Mwakyembe na kutaka wafukuzwe kwenye uwaziri.

Pia wataitisha serikali kwa vitisho vya uwongo kuwa iwalipe Dowans haraka ama sivyo mali za Tanzania nje zitakamatwa, riba itaongezeka, eti Tanzania kamwe haiwezi kukwepa kuwalipa Dowans, wakati Mahakama Kuu ina uwezo kutupilia mbali hukumu ya ICC.

Wahariri wa vyombo hivyo tajwa vya habari wameshaandaliwa kutoa taarifa hizo prominently kwenye ukurasa wa mbele au kwenye vipindi maalumu vya TV na redio.

Watu hao mashuhuri wastaafu na wa sasa ni pamoja na wanasiasa, wanasheria, viongozi wa dini, waandishi wa habari, etc.

Tayari AG wa zamani, Jaji Mark Bomani, kashapewa mlungula na kuropoka hadharani kuunga mkono malipo haramu kwa Dowans.

Bomani has already been compromised na mafisadi. Wamemuweka pale Serengeti Breweries Limited kama mwenyekiti wa bodi na kumlipa senti zinazomfanya apoteze maadili. Serengeti Breweries inamilikiwa na mafisadi wa kihindi kina Mehta na wengine ambao waliiba pesa nyingi za Watanzania kupitia Benki Kuu (BoT).

Bomani kapewa rushwa na Rostam Aziz ili aibuke kutetea malipo kwa Dowans. Rostam sasa hivi anatoa pesa kwa watu ambao wanaonekana na influence kwenye jamii kushinikiza Dowans walipwe. Yupo radhi kutumia shilingi milioni 500 kugawa rushwa kwa viongozi hawa ili apate malipo ya shilingi bilioni 100.

Bado wataibuka viongozi wengine mashuhuri muda wowote sasa kuunga mkono malipo kwa Dowans ili kujaribu kuwachanganya wananchi.

Kuna jitihada kuwaweka sawa kina Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF, Hamad Rashid wa CUF, Zitto Kabwe wa Chadema (kashanunuliwa siku nyingi na Rostam), John Shibuda wa Chadema, James Mbatia wa NCCR Mageuzi, John Cheyo wa UDP, Augustino Mrema wa TLP na Christopher Mtikila wa DP watoke hadharani kuunga mkono malipo kwa Dowans.

Hapo tutajionea wazi jinsi viongozi wetu wanavyonunulika kirahisi kutokana na njaa kubwa waliyokuwa nayo na kukosa uzalendo kwa nchi yao wenyewe.

Stay tuned.... The Dowans circus is about to begin!

sio rahisi af toa Tanzania daima haliwezi huo upupu
 
Mbona wameanza tayari, magazeti ya leo wanasheria wanamuunga mkono yule mzeeeeeee, lakini hawakutaja majina yao
 
Back
Top Bottom